Mtunzi: ___
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
walikuwa wakinong’onezana
masikioni ili watu wengine wasisikie.
“hapana asee Roho yangu
imetua pale asee”
“sasa kaongee nae basi”
“poa subiri hapa hapa”
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
“Adams alivaa kiheshima sana
ilikuwa suti kwakuwa kulikuwa na joto sana alivua koti na kubakia na shati nyeupe na tai shingoni alipendeza sana.
“samahani kaka”
“bila samahani”
“Naomba nikae hapo ulipo
kaa nataka kuongea na huyu dada”
“ooh sawa kaa”
_______________________________________
Dada habari za kwako
nadhani una umwa maana naona
una mawazo sana muda wote naona umeinama chini”
“Matatizo kaka angu “
“pole sana, samahani kuna kitu nataka kuku uliza kidogo
naomba tukae pembeni kidogo”
“sawa labda wapi”
“kwenye kiti kile ile kama daktar ataita majina iwe lahisi kusikia”
“ok”
“Naitwa Adams j maryo jr.
Naishi Morogoro ni mfanya biashara”
“oh asante kuku fahamu”
“ok, nilikuona Muda wote upo
na hudhuni sana vp nini tatizo”
“Ni Afya yangu tu kaka:..
“Namba 11 ingia”
Ilikuwa sauti ya daktar
iliyo sikika hakuwa mwingine ni yule dada aliye kuwa akiongea na Adams aliinuka na kwenda.
“kaka ngoja niingie nisubiri”
“aliingia ndani kwa doktar..
Habari yako Dada”
“nzuri Doktar,Nipe majibu yangu
ilinijuwe kitakacho endelea katika Maisha yangu”
“Mbona una Haraka sana”
“Doktar ni umuhimu wangu
kujuwa”
“ok unaitwa Sulee siyo”
“ndiyo”
“ok Sasa mbona umekuja peke yako kupima”
“sina Mume wala mpenzi nipo mimi mwenyewe”
“Mh kwanini je mmeachana”
“ndiyo”
“kipindi gani tokea muachane”
“kama miezi 9 na siku kazaa”
“pole sana pole sana”
“doktar nina nini”
“hayo ni maisha yakawaida sana
leo wewe kesho mimi hupaswi kujutia Mungu ana kila sababu kwenye jambo lolote sawa sulee ona wewe ni mzuri sana lakini
leo hii una dosari katika maisha yako usikate tamaa kabisa Dada angu Mungu atakupa nguvu Na..
_______________________________________
Monica Alikuwa ana furaha
kubwa sana Moyoni kwakupata Mtoto japokuwa alikuwa akimkumbuka sana Mume wake
aliumia sana kwa kufikiria sana Jinsi Mumewe alivyo kuwa ana mjari na kumpenda
alijikuta akimuangalia Mtoto wake
huku machozi yakimtoka sana
alianza kumchukia Mtoto wake aliye fanana sana na Kisarawe
alitamani kumtupa au amtelekeze
yule mtoto kwa shangazi
lakini aliona Mtoto hana Hatia
kabisa alizidi kumtunza na kujitahidi kumpenda sana.
___________________________________
Mume wa Monica Aliamuwa kuwa mkulima katika kijiji cha mlali kilichopo mkoa wa Morogoro
alilima mazao lakini yalimgomea
kabisa alikuwa akivuna kidogo sana”Hii itakuwa Radhi ya mke wangu tu kuachana tu maisha yamekuwa magumu sana kila ninacho kifanya kwangu siyo
imekuwaje sijuwi niende kwa Mganga, lakini hapana hapana
siwezi kufanya hivyo kwakuwa huku kijijini hawajuwi kama tumeachana na mke wangu ngoja ni rudi dar nika mtafute mke wangu tujetuishi wote lakini anaweza kukubali kuja kuishi huku sijuwi”
Hayo yalikuwa Mawazo ya
Mume wake na Monica
aliyo kuwa aki waza
___________________________________
Nakushauri Usichoke kutafuta
sawa sulee”
“Doktar doktar sikuelewi”
Sulee aliulza kwa ukali kidogo
huku machozi yakilenga lenga
huku akitetemeka kwa uwoga na presha kupanda”
“hapana sule kuachika siyo mwisho wa kuto pendwa au kupenda utapata Mume bora
na aliye sahihi kwaku kazana kuomba Mungu atakuonyesha”
“doktar nime asirika tawezaje kukaa na Mtu asiye na virusi”
“nani kakwambia kuwa ume Asirika eeh”
“soma hivi hapa vyeti”
“mh Hapana sule vipimo vyetu havisemi hivyo upo salama kabisa
sulee”
“hapana doktar hostpital iyo siunaijuwa nikubwa sana
itadanganyaje hivyo”
“huwezi kujuwa wenda kuna sababu kama ulivyo niambia kuwa umeachika miezi9 naa, wenda ninjama ya mumeo”
“sasa unanishauri vp doktar”
“kapime hospital mbili tena
utapataje majibu”
“asante doktar”
“haya karibu tena”
Sulee alitoka nje hakuwa na kumbukumbukama kuna kijana
nje aliye kuwa na maongezi naye
alitoka huku akielekea mlango wakutokea nje kabisa
“sulee mbona hivyo
jamani”
“nisamehe sana Adams”
“ehee ina kuwaje maongezi yetu”
“ooh tuakae pale”
Kabla ya kukaa
doktar akasikika akisema namba 25 ingia” ilikuwa ninamba ya Adams j maryo jr.
“sulee ni namba yangu hiyo
je uta nisubiri niingie”
“sawa usichelewe sana”
“sawa”
“Pita tu”
“Habari yako doktar”
“salama tu ,wewe ni Adams”
“ndiyo”
“tatizo lako ni mchafuko wa Tumbo tu utaenda Dukani
uta chukuwa dawa hizi nilizo andika sawa”
“sawa kwaheri”
“pita huku “
ADAMS ALIPITA NJIA NYINGINE
NASIYO ILE ALIPO TOKEA SULEE
ADAMS ALICHUKUWA DAWA DUKANI NAKURUDI PALE ALIPO MUACHA DEREVA NA SULEE.
“vipi dereva yuko wapi yule dada
yuko wapi”
“kaondoka mda kidogo kaka”
“khaa sasa sijuwi tampataje
asee”
“kaacha namba yake ya simu
hii hapa”
“afadhari sana ,bac twende zetu
asee”
________________________________________
Sule hakutaka kurudi nyumbani
alienda hospital 3 tofauti kupima
tena mpaka saa3 usiku alikuwa akisubiria Majibu hospital zote3
Na majibu yote yalikuwa ni mamoja hana Virusi alikuwa na amani moyoni japokuwa aliambiwa arudi tena kupima baada ya miezi mi2/3
kiuwakika zaidi alirudi nyumbani
huku ana furaha sana.
“vp sulee mbona hivyo
una furaha”
“yani Mungu ashukuriwe
sina Virusi Monica”
“sasa iwe siri usimwambie shangazi sawa”
“mh kwa nini tena”
“utajuwa ukweli badae”
Monica alimwambia sulee vile
ili uadui usitokee kati yao na Shangazi yao
_______________________________________
miezi mi2 sulee alienda tena kupima alipata majibu tena kuwa hana virusi aliwaza sana ninani aliye fanya kitendo hicho cha kuambiwa ana h,i,v aliamuwa kwenda katika hospil ile aliyo ambiwa kuwa ana Virusi ilikumbana doktar yule
ajuwe ukweli.
Alipo fika alimkuta daktar wakike
“zakazi daktar”
“nzuri tu”
“nina shida”
“kiafya au kiofice
“kiofice”
“karibu”
“kuna siku nilikuja hapa kupima…
Kupima H.I.V. Na vyeti vya vipimo vyangu ni hivi hapa unaweza ukasoma.
“Yes inaonyesha umeasirika
Dada angu”
“ooh vizuri je nitarehe ngapi
hapo ina sema”
“eeeeeh eeeeeh ni 21/5/2014, mbona unaniuliza maswali sana”
“asante sana,uta juwa tyuu
usiwe na haraka, Je unaweza
kunisomea katika fairi la ofice hii alikuwepo nani tarehe iyo”
“aah kuna kazi nyingi zakufanya
sahizi niache nihudumie wagonjwa wengine”
Sulee aliingiza mkono
katika pochi yake nakutoka na
wekundu/pesa kazaa nakumpa yule dada/doktar akapokea
nakuweka katika Matiti yake.
“sasa naomba nisaidiye
kumjuwa ninani alikuwepo”
“ok subiri”
Baada ya dk5
Alisha pata jibu alikuwa ninani
“nimeona alikuwa ni
doktar john nimnene mweusi
ana nywele nyingi hivi”
“huyo huyo”
“sasa kafanyaje”
“habari ndefu sana wangu
angalia hivi vyeti nausome”
Doktar huyo alisoma
vyote vi nne alitoa pumzi
uphuuuu kisha akamtazama
kwa huzuni sana sulee kisha akainuka
nakumshika bega.
“sulee pole sana hiyo nikawaida yake huyo doktar hafai hata kwa dawa nakushauri fanya unavyo taka kufanya”
“ok nataka kujuwa ukweli tu
aliyemtuma afanye hivyo ninani”
“sawa”
Sulee alianza kufanya mipango:
alianzia Mahakamani
moja kwa moja kwakumshtaki
doktar john kwakumpa vipimo vyauwongo.
Kesi ilisumwa kort chemba
sulee hakutaka yawe makubwa
kwa doktar yeye alitaka ajuwe tu ninani alifanya vile tu.
Monica alikuwa akihisi kuwa ni Mume wangu ili tuachane, Lakini mbona alisema nisimwambie Shangazi kuhusu ilo suara.
Sulee alijiuliza moyoni
Doktar alibanwa sana mwisho akakubali kuwa alipewa pesa
na shangazi yake sulee adanganye majibu kuwa sulee ana ukimwi
ili aachane na Mumewe,(japo kuwa shangazi na sulee alikubaliana na Mume wa sule kuwa kama watakuwa wazima wote Mume wa sulee ange msamehe sulee)
“ok vizuri sana”
Kutokana na sifa za doktar huyo
kuwa mbaya anahusika na utoaji mimba NK. Mahakama iliamuwa kumfungia kazi kwa muda usiyo julikana.
Sulee ali Rudi nyumbani
huku akiwa na hasira sana
alikuwa ana hamu sana amkute shangazi yake
Lakini hakumkuta.
“kweli Monica doktar kakubali
kumbe shangazi ndiye kafanya tukio langu hilo eti kisa tuachane
na mume wangu, tulikubaliana
kama tutakuwa hatuna Virusi tungeendelea kukaa wote licha
yakuwa na mimba siyo yake”
“Sasa utafanyaje sulee”
“nataka kumchana live”
“Hapana Sulee kumbuka
hatuna pakwenda”
“potelea mbali liwalo na liwe
nimesha pagawa kasababisha kutoka kwa mimba yangu inauma sana nilikuwa nikikaa kwa Huzuni kama naumwa nilikonda kama
kweli na ngoma Monica siwezi kumsamehe Mimi”
“Sulee huoni kama ndiyo utakuwa
mwisho wetu wakukaa hapa”
“mmh popote mimi takwenda kukaa mimi”
“na mimi je”
“najuwa atanifukuza mimi
tu siyo wewe”
“hapana sulee atajuwa nime kwambia mimi hiyo siri”
“siri siri siri gani tena hiyo
Monica”
“kuwa wewe hauna ukimwi”
“mh mbona unanichanganya inamaana hata wewe ulikuwa ukijuwa kuwa mimi sina ukimwi
Monica mbona haukuniambia
mimi kwa nini kwa nini Monica
hukuniambia mapema
mpaka mimba yangu imetoka
Monicaaaaaa….
Hata wewe uliamua kuacha
kuniambia mapema mpaka
Mimba yangu imetoka aaaayi
M’baya sana wewe nakuchukia
wewe na shangazi wauwaji kabisa nyie nibora usingeniambia tu Mimba imesababisha niachike
leo hii inatoka/naipoteza kirahisi hivi hapana haiwezekani kabisa”
“Sulee Nimejuwa baada yakutoka
ndipo aliponiambia mimi kosa langu likowapi kukuambia au?
Kumbuka sulee Tatizo lako ndiyo langu nisingeweza kukuficha mimi wangu namimi naumia sana sulee shangazi aliniambia baada ujauzito wako kutoka”
“unaongea yana uhakika hayo”
“ndiyo”
“unaniakikishia vipi mimi nikuamini”
“Naapa mbele ya Mungu kuwa, haya nayo yasema mimi Monica niukweli mtupu”
“basi sawa” Sulee na Monica walikumbatiana
huku sulee akilia kwa uchungu sana:
Eeeh Mungu naomba unisamehe
kwa mambo yote niliyo mtendea Mume wangu popote alipo naomba umlinde naumpe Moyo wa kunikumbuka:
Alipokuwa akisari sulee simu yake ikawa ina ita Alipo itazama alikutana na namba iliyo ishia na 78 ilikuwa ningeni kwake akapokea.
“hallow nani mwenzangu”
“Adams j Maryo jr.
Upo wapi sahizi”
“oooh nipo home nw”
“ok upo na nani”
“nipo na ndugu yangu”
“poa sasa tutafanyaje sulee”
“kivipi”
“nilitamani tuonane
kama utakuwa una Muda”
“e eeeh yap ninao”
“asante Mimi nipo Mikocheni”
“swa kwahiyo”
“naomba tukutane Tegeta Africa sana”
“poa sasa hivi naja”
“ok nakusubiri”
Yalikuwa ni maongezi kati ya sulee na Adams wakipeana ahadi
yakuonana kwao, sulee Akajiremba safi akiwa mlangoni akitoka alikutana na shangazi yake.
“Afadhari sana tumekutana”
“kivipi sulee mbona kama una jazba vile”
“hujuwi eeh hujuwi”
“nijuwe nini mie”
“sikia wewe hivi unajiskiaje
mimba yangu ilivyo toka”
“mbona nikawaida tu”
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA