Mtunzi: ___
SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Mara nyingi alipendelea sana kuvaa nguo za kubana na kusababisha mateso makubwa kwa wanaume wakware.
Miguu yake minene wastani, kila alipokuwa akikanyaga hatua moja, mzigo wa nyuma ulitingishika kiaina.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
“Sasa na mimi utanipeleka lini nikamuone huyo daktari…?”
“Wewe unapenda twende lini…,” Sulee alimuuliza Monica huku akiwa amemkazia macho.
“Hata sasa hivi, au unasemaje…?”
“Kwa leo itakuwa ngumu, maana inahitaji maandalizi…”
“Maandalizi gani Sulee jamani mimi nina shida, kama ni fedha ipo bwana…,” Monica alizungumza huku akizidi kuliangalia kwa umakini sana tumbo la Sulee.
“Kesho uje unipitie nyumbani jioni ya saa moja na nusu, sawa…?”
“Saa moja na nusu…?,” Monica alihoji kwa mshangao mkubwa.
Ee, saa moja jioni ndiyo, mbona unashituka Monica…?,” Sulee alihoji kwa sauti ya kishari f’lani hivi.
“Mmh!, nimeshangaa muda huo ni daktari gani anatoa huduma ya tiba kwa uzazi…!”
“Kha! Monica vipi kwani wanaojifungua huwa hawaendi kuzaa usiku…?”
“Umeshasema kujifungua, sasa mimi naenda kujifungua…?” alisema Monica huku akitingisha mguu mmoja na kulifanya wowowo lake litikisike kwa kitetemeshi cha kuvutia…
“Kama unataka tiba, utakuja nikupeleke na kama hutaki basi bwana nimeshaona una wasiwasi,” alisema Sulee akijiandaa kuondoka.
“Hapana shoga yangu, nitakuja bwana…”
“Oke, utanikuta ila usichelewe…”
“Sawa shoga yangu…”
Waliagana lakini moyoni Monica akabaki na maswali yasiyokuwa na majibu.
“Saa moja na nusu jioni tiba gani ya uzazi hiyo…?”
“Lakini kwani tiba huwa ina muda maalum, na mimi bwana…!”
“Lakini ngoja, sasa hiyo saa moja na nusu kuna kuwa na wagonjwa wengine…?”
“Ee, sasa si pale ni hospitalini…?”
“Mmh! Itajulikana hukohuko kesho…,” Monica alizidi kuwaza na kuwazua moyoni mwake.
Kesho yake Monica aliamka mapema asubuhi na kuanza kufanya kazi ndogondogo za pale nyumbani. Hamu kubwa ni kufika muda alioambiwa na Sulee wa kwenda kumuona Dokta Kisarawe.
Ilikuwa mara aingie jikoni, mara sebuleni wakati mwingine mara aguse hiki na kuacha kile. Lengo likiwa ni kusukuma muda.
Saa kumi na mbili kamili jioni, Monica alijiandaa vizuri. Akaingia bafuni na kujisafisha kwa umakini mno. Hata maeneo ambayo hakuwa ameyasugua kwa muda mrefu, siku hiyo aliyaosha kwa ustadi.
Kuanzia ndani ya kucha za miguuni, katikati ya vidole na kwingineko, ilimradi tu aonekane bomba zaidi.
“Hapa sasa ngoja nikajipigilie pamba za maana…,” Monica aliwaza wakati akimalizia kujifunga taulo kabla ya kutoka bafuni…
Aliingia chumbani kwake na kuanza kuchambua nguo zote alizozipenda. Kila aliyoijaribisha aliona kama haikumfaa kwa siku hiyo…
“Eehee, hii ndiyo nilikuwa naitaka sasa ngoja niitupie…,” alisema Monica na kuiweka pembeni nguo hiyo.
Lilikuwa gauni jekundu , lakini lilibana sana maeneo ya nyuma na kuufanya mzigo wa Monica ujitenge vizuri kila alipolivaa. Kwenda chini lilikomea chini kidogo ya magoti…
Alipojiridhisha, alifungua droo ya upande wa kitanda na kutoa pafyumu kali aina ya Red door, ambayo hutumiwa na wanawake wengi wa mjini ambao mambo yao yako bomba.
Akachukua sendozi za rangi nyeusi na kumechishia na mkoba wake, hakika alitokelezea kama wasemavyo vijana wa siku hizi.
Saa moja na nusu jioni, tayari Monica alikuwa sebuleni kwa Sulee akimsubiri waende kwa Dokta Kisarawe.
“Nimekuweka sana shoga yangu…?”
“Wala usijali, tayari…?”
“Eee, twende sasa…”
Waliongozana hadi kwa Dokta Kisarawe. Walipofika walikuta dokta huyo akimalizia kutoa maagizo fulani kwa mgonjwa mmoja.
Baada ya muda mfupi, Sulee alimpeleka Monica kwenye chumba cha daktari.
Dokta Kisarawe baada ya kumuona tu Monica, alishituka kwa uwazi na kuwafanya wote wauone mshituko huo.
“Ooh, karibuni sana…,” alisema Dokta Kisarawe huku akijiweka sawa kwenye kiti chake kirefu cha kuzunguka.
“Ahsante,” aliitikia Sulee kwa sauti ya uchangamfu.
Baada ya utambulisho, Dokta Kisarawe alimuomba Sulee awaache na Monica ili aweze kumsikiliza kwa umakini mkubwa.
Sulee alitoka nje na kukaa kwenye benchi, lakini moyo na akili yote vikabakia chumbani kwa Dokta Kisarawe na Monica.
Kilipita kimya kidogo bila kusikia sauti yoyote achilia mbali minong’ono…
Akaendelea kukaa huku akijiuliza maswali.
“Sasa mbona sisikii wakiongea…?”
“Au…mh!…,” Sulee hakumalizi sentensi yake na kuishia kuguna.
Kimya kikazidi kupita. Giza nalo likazidi kutanda, lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kumsubiri Monica aliyekuwa akipata tiba maalum.
Kuna wakati alitamani avamie ndani ili kuona kilichokuwa kinaendelea kati ya Dokta Kisarawe na rafiki yake Monica, maana tayari alishaanza kuhisi wivu f’lani hivi hasa akikumbuka jinsi yeye alivyoanzisha uhusiano na Dokta Kisarawe.
Wakati akiwaza hili na lile, ghafla alishituka baada ya kusikia kitu kama meza au kitanda kikilia kuashiria kama kuna mtu anakisogeza.
Akanyanyuka alipokuwa amekaa na kwenda hadi mlangoni.
Kwa kutumia tundu la komeo la mlangoni, Sulee alichungulia ndani.
“Duh! Yaani kweli…?” Sulee alitamka maneno hayo baada ya kuona kwa ndani.
Akarudi na kukaa tena kwenye benchi kama zamani, lakini akawa hatulii sehemu moja…
Kila mara alikuwa akiinuka kukaa, mara asogee mbele na nyuma, hakika wivu ulikuwa ukimpeleka vibaya…
“Haiwezekani, huyu Dokta Kisarawe anaweza kutuchanganya na rafiki yangu kweli? Hapana haiwezekani…,” Sulee akawa anawaza moyoni.
Baada ya muda mfupi, kilisikika kimya kutoka chumbani kwa Dokta Kisarawe. Baadaye akatoka Monica lakini uso wake ulikuwa haueleweki.
Kwa mbali alionekana mchovu kwa shughuli fulani lakini pia wakati mwingine alionesha uso wa uchangamfu na kuzidi kumchanganya zaidi Sulee.
“Vipi…,” Sulee alimuuliza Monica wakati wakiongoza njia ya kurudi nyumbani.
“Safi tu…”
“Umeonana na dokta…?”
“Sijaonana naye…,” Monica alimjibu Sulee huku akimkazia macho.
“Hujamuona…!?,” Sulee akauliza kwa sauti ya mshangao mkubwa.
“Sulee bwana, sasa wewe unajua kabisa niliingia ndani kwa dokta tena wewe ndiye uliyenipeleka, sasa unaponiuliza kama nimemuona dokta ulitaka nikujibuje? Basi sijamuona…,” Monica alijibu huku akimtazama Sulee kwa jicho la ‘Uwe unafikiri kabla ya kuuliza swali’.
Sulee akakaa kimya na kumuangalia Monica kama anayesema ‘Leo umeniweza’.
Wakaendelea na safari yao, lakini Sulee hakuwa amejiridhisha na majibu ya Monica hivyo akaendelea kumdadisi zaidi kujua kilichoendelea kati yake na Dokta Kisarawe.
“Oke, kasemaje…?”
“Amenipima na kunipa dawa hizi, lakini ameniambia nirudi baada ya siku mbili…,” Monica alimjibu Sulee na kumuonesha dawa ambazo alikuwa amepewa na Dokta Kisarawe.
Moyoni Sulee alijisikia wivu zaidi kwani hata yeye mara ya kwanza kuonana na Dokta Kisarawe alipimwa na kisha kupewa dawa na kuambiwa arudi baada ya siku mbili.
Hisia za Dokta Kisarawe kufanya kama alivyomfanyia yeye zikazidi kumgubika moyoni.
“Siku ya kurudi utaniambia ili twende wote, sawa…?”
“Sawa…,” Monica alijibu kwa mkato na sauti ya chini mno.
“Mbona kama umeishiwa na raha Monica…?”
“Hamna, mbona niko kawaida tu Sulee…”
“Au umeambiwa nini na Dokta Kisarawe…?”
“Hakuna kitu Sulee, niko sawa…”
Waliendelea na mazungumzo ya hapa na pale, lakini Monica alionesha wazi kuwa hakuwa sawa kabisa, jambo ambalo lilizidi kumuweka njia panda Sulee.
Baadaye waliagana na kila mmoja kwenda nyumbani kwake kwani tayari ilishakuwa usiku wa saa tatu kama na robo hivi…
Monica akiwa njiani, alianza kuwaza mambo mengi sana, lakini kubwa ni kwa nini Sulee aendelee kung’ang’ania kwenda naye mara ya pili wakati alishamuelekeza.
“Aah wapi, naenda peke yangu, si ameshanionesha…?” Monica akaendelea kuwaza na kufikia uamuzi wa kutokwenda na Sulee mara ya pili.
***
Baada ya siku mbili, Monica aliamua kwenda kwa Dokta Sulee peke yake bila kumtaarifu Sulee…
Baada ya kutimu saa moja na nusu karibia saa mbili, Sulee akazidi kushangaa kwa nini Monica hakumpitia kama walivyokubaliana.
“Huyu mbona hajafika hadi sasa hivi, au kaghairi…?” Sulee alizidi kuwaza baada ya kuona muda unazidi kusonga mbele bila kumuona rafiki yake Monica.
Akachukua simu na kujaribu kumpigia ili amuulize kama alikuwa ameghairi kwenda kwa dokta.
Simu ya Monica iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa licha ya Sulee kurudia tena zaidi ya mara tano. Akazidi kuchanganyikiwa.
Akampigia Dokta Kisarawe, naye akawa hapokei. Akaamua kumpigia mume wake na Monica ili kujiridhisha. Mume wake Monica alimwambia Sulee kuwa rafiki yake huyo alikuwa ameenda kwa dokta.
Sulee akatulia. Baada ya kupita saa nzima, simu ya Sulee iliita na alipoitazama, alikuwa ni mumewe Monica akimtaarifu kuwa Monica amepokea na kumueleza kuwa anajiandaa kurudi. Sulee hakujibu kitu zaidi ya kulala.
Kesho yake, aliamua kwenda kimyakimya nyumbani kwa Monica. Baada ya kuzungumza, walikubaliana kwenda pamoja siku hiyo huku Sulee akimlaumu kwa kumuacha jana yake.
“Nilichelewa nikaona nitakusumbua shoga yangu,” alijibu Monica lakini akikimbiza macho yake chini kwa aibu f’lani hivi.
Ilipotimu jioni, waliongozana pamoja hadi kwa Dokta Kisarawe, walikuta wagonjwa wengine wamepanga foleni.
Mlango ukafunguliwa na Dokta Kisarawe akatoka, alipowaona haraka akamuita Monica na kuwaacha wagonjwa wengine, akafunga mlango. Sulee kuona vile, akasogea hadi mlangoni na kuanza kuchungulia tena.
Kwa mbali akaanza kusikia tena vitu vikisogezwa. Mara kikatokea kimya cha ajabu.
Baadaye kidogo, Sulee alisikia sauti ya kulalamika ya Monica akisema
Dokta mimi siumwi huko jamaniiii, mmh!.
Moyo ukazidi kumwenda kasi Sulee, alijua kilichokuwa kikiendelea kati ya Monica na Dokta Kisarawe.
“Yaani kweli Kisarawe anaweza kunifanyia hivi…?.,” Sulee alijikuta akisema kwa sauti na kuwafanya baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamekaa kwenye benchi wamwangalie kwa jicho la kumshangaa kutokana na sauti yake.
“Haiwezekani, nasema haiwezekani hapa ni lazima nifanye kitu…,” akazidi kuwaza huku akiwafikiria njia ya kuzuia kilichokuwa kikiendelea kati ya Monica na Dokta Kisarawe.
Kitendo cha Dokta Kisarawe kumuita Monica aliyefika mwishoni na kuwatangulia baadhi ya wagonjwa kilileta kero kwa baadhi ya wagonjwa na kuanza kumjadili kwa tabia yake hiyo.
“Mh, ina maana huyu dokta hajaona kama kuna wagonjwa wengine hapa tuliowahi…?” alihoji kwa sauti ya juu mama mmoja aliyekuwa amekaa kwenye benchi la wagonjwa.
“Shangaa, halafu kila akiingia na mwanamke ni lazima afunge mlango,” alishadadia mwanamke aliyekuwa ameketi jirani kabisa na Sulee.
Mjadala juu ya tabia ya Dokta Kisarawe ulizidi kupamba moto baina ya wale wanawake waliochukizwa hasa kwa kitendo chake cha kumuita Monica licha ya kuwakuta baadhi yao wakiendelea kusubiri zamu yao ifike.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA