DOKTA SIUMWI HUKO (3)

0
Mtunzi: ___

SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...

Sulee alirudi hadi alipokuwa ameketi awali, nakuanza kujiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu.
“Hivi, wanaweza kuwa wanafahamiana kweli…?”
“Kha, lakini nami bwana, sasa kama hawafahamiana wanawezaje kucheka na kugongesheana mikono namna hiyo…?”

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
“Kwa vyovyote vile watakuwa wanafahamiana tu, ngoja nifuatilie sana…!
“Sasa kama wanafahamiana, kuna uwezekano huyu dokta kuwa anatuchanganya...?”
“Yawezekana…”
“Lakini ni sisi wanawake yawezekana ndiyo tunajichanganya…,” Sulee aliendelea kujisemea juu ya hali aliyoiona kwa siku hiyo.
“Ina maana kila mwanamke mwenye ugonjwa kama wangu, ni lazima atembee na huyu dokta ndiyo apone…?”
“Sasa kama ni hivyo atakuwa ametembea na wangapi?”
“Kama ndiyo mtindo wake, kwa nini sisi wanawake tusishituke ?”
“Kuna uwezekano wanawake wengi wanajua, lakini nani wa kuvujisha siri kama anapokea dozi ya maana ya Dokta Kisarawe…? Halafu sasa unakuta wengi wao ni wake za watu, lakini sisi wanawake bwana…!

“Sisi wanawake siyo, wewe tufuatilie sana, siyo kwa sababu haiwezekani wote hawa tutembee na mtu mmoja na siri isijulikane…,” maswali yakazidi kumchanganya Sulee mahali alipokuwa amekaa.
Lakini kwa wakati wote huo akiwa amekaa kwenye ile foleni, macho yake hayakuwa yanabanduka kwenye mlango wa ofisi ya Dokta Kisarawe…
“Lakini mimi naye bwana, sasa nimethibitishaje kuwa ni wapenzi labda huenda wanafahamiana tu na umepita muda mrefu bila kuonana?”
“Lakini, kufahamiana gani huko wanacheka hadi kugonganisha mikono kwa sana…?”
“Sasa kwani kugongeana mikono kuna maanisha nini…?,” Sulee akazidi kujihoji na kujijibu mwenyewe, hali ilishaanza kuwa tete ndani yake. Moyo haukuwa na amani tena na kidonda cha wivu kilishaanza kumnyemelea.

“Yaani kweli mambo anayonifanyia Dokta Kisarawe, anaweza kumfanyia mwanamke mwingine kweli?”
“Eee, inawezekana kwani kama aliweza kwako ni kivipi asiwafanyie wengine…,” ilisikika sauti ikimjibu kutoka upande wa pili wa moyo wake.
“Ila kweli, hilo nalo neno.”
Sulee aliendelea kujihoji na kujijibu mwenyewe. Hali haikuwa hali. Dokta Kisarawe alikuwa amemuingia moyoni mwake, sasa alikuwa haambiliki wala kusikia chochote juu yake.
“Haya mapenzi bwanaaa, hayana maana….,” wimbo wa Diamond ulisikika masikioni mwake baada ya kushindwa kuhimili vishindo vya maumivu ya wivu wa mapenzi.

Muda mfupi baadaye, Sulee aliamua kusogea tena karibu kabisa na mlango wa ofisi ya Dokta Kisarawe. Lengo la safari hii ni kusikia nini kilikuwa kikiendelea ofisini humo.
Sulee alishituka baada ya kusikia sauti za kunong’ona kwa chini sana tofauti na awali ambapo Dokta Kisarawe na mteja wake walikuwa wakizungumza kwa sauti ya juu.
Safari hii alisikia watu wakibusiana, moyo ukazidi kumuuma…

Akajishika kifuani kwa upande wa kushoto ulipo moyo, mapigo yakazidi kumuenda mbio.
Dakika mbili baadaye, alianza kusikia miguno na sauti ya meza na kiti vikisogea…Moyo ukazidi kumuuma kuliko kawaida.
“Kuchiii…..kwaguuu…vegeeee….vegeeee…..vigi…vigiiiii….,” milio ya kiti na meza viliendelea kusikika na kuzidi kumpa maswali mengi sana Sulee…
Mbali na milio ya samani hizo, miguno na mihemo ya chini ikazidi kusikika, kila dalili ya watu kula mua ikawa inajionesha wazi…

Sulee akashindwa kuvumilia, akarudi kwenye kiti. Dakika tano baadaye yule mwanamke akatoka. Dokta Kisarawe naye akatoka nje na kumuita mwanamke mwingine. Lakini wakati akimuita mtu mwingine, macho yake na ya Sulee yalikutana lakini hakuonesha dalili yoyote ya kumchangamkia (Sulee). Hali hiyo ikazidi kumchanganya kabisa Sulee.
Kuna kipindi akataka kuondoka lakini akazidi kujipa moyo na kuendelea kusubiri aone hatma ya mchezo wa siku hiyo.

“Kha, au kuna kitu nimemkosea ndiyo maana kachukia namna hii, au niondoke? Lakini nikiondoka wakati nimeshafika hapa itakuwa si busara. Ngoja niangalie mwisho wa hii sinema…,” akawaza moyoni Sulee.
Hatimaye wote wakaisha na kubaki kwenye benchi peke yake. Akadhani sasa zamu yake imewadia. Lakini alishangaa kumuona Dokta Kisarawe akitoka huku akifunga mlango wa ofisi yake kwa ufunguo.
Kuona hivyo, Sulee akahamaki na kumuuliza kulikoni iwe hivyo na vipi kuhusu tiba yake kwa siku hiyo?

“Haa, sasa Dokta mbona unaondoka vipi kuhusu mimi jamani…?
“Kuhusu wewe nini tena…”
“Si tiba yangu…”
“Ipi…”
“Ya siku zote, ina maana umesahau kabisa…?”
“Hebu acha maneno yako wewe…,” alijibu Dokta Kisarawe huku akimalizia kufunga kufuli la mlango.
 “Kuhusu wewe nini tena…”
“Si tiba yangu…”
“Ipi…?”
“Ya siku zote, ina maana umesahau kabisa…?”
“Hebu acha maneno yako wewe…,”
“Kha, dokta mbona sikuelewi…?”
“Hunielewi kivipi wewe….?”
“Si hivyo, ina maana kweli juhui kilichonileta…?”
“Sasa kama ningekuwa sijui si ningekuuliza…?”
“Sikiliza, nina mazungumzo na wewe nje ya mazingira haya ya kazi, ndiyo maaana sikutaka kukuita toka mwanzo.
“Hapo sawa, kwa hiyo tunaelekea wapi…?”
“Wewe tulia, si uko na mimi sasa wasiwasi wako nini…?
Ikabidi atulie.

“ngoja nione mwisho wa safari hii…,” akawaza moyoni huku akiegemea kwa nyuma.
Safari ikaendelea, mbele kidogo dereva alianza kupunguza mwendo, Sulee alipochungulia kupitia kioo, akasoma bango lililoandikwa Utulivu Gest House.
Moyo ukamlipuka, akajua nikilichokuwa kinaendelea.
Baada ya kuteremka, dokta alimlipa dereva pesa yake na kumruhusu aondoke zake lakini akamwambia angempigia simu baaadaye kwa ajili ya kwenda kuwapokea. Alionekana kuwa ni mtu wake wa karibu sana, ndiyo maana Dokta Kisarawe alikuwa anamuamini kwa kiasi kikubwa namna hiyo.
Wakazama hadi mapokezi ambapo baada ya kukamilisha taratibu zote, wakapewa chumba.
Walipoingia tu, Dokta akaanzisha mazungumzo.

“Umeona mwisho wa safari yetu…?”
“Nimeona, umeshinda bwana…”
“Ulikuw ana wasiwasiii….?”
“Mmh…”

Dokta Kisarawe alimwambia Sulee kuwa alikuwa mjamzito jambo lililomshangaza sana Sulee.
“Unasema kweli dokta…?”
“Wewe niamini mimi…”
“Kweli…?”
“Ili uhakikishe, naomba kesho ukapime kwa daktari mwingine halafu uje uniambie.”
Waliongea mengi lakini mwisho wa siku wakaelekea kwenye uwanja wa fundi seremala ambapo shughuli ilikuwa pevu, Sulee alijiachia na kutamka maneno yote aliyoyajua. Hatimaye walifika pamoja mwisho wa safari yao.

Baada ya shughuli hiyo, Sulee aliingia bafuni kujiweka sawa, na kisha kutoka ambapo alichukua usafiri hadi nyumbani kwake.
“Mbona leo umechelewa sana kurudi…?,” Mumewe Sulee, Masofa alimuuliza akiwa amekunja ndita.
Ilikuwa ni kama saa mbili na dakika kumi usiku kwa wakati huo.
“Watu walikuwa wengi sana, halafu nina habari njema sana mume wangu…”
“Habari gani hiyo…?”
“Nina mimba…”
“Amekupima…?”
“Sasa asingenipima ningejuaje…?”
“Ok, mimi siamini labda twende kwa daktari mwingine…”
“Sawa…”
Waliongoz
ana hadi kwenye zahanati ya jirani, na kumkuta daktari akiwa peke yake.
“Karibuni jamani”
“Ahsante…”
Walieleza shida zao, taratibu zikafanyika na baada ya dakika ishirini, waliitwa na daktari huyo.

Jamani sasa naomba muwe tayari kwa ajili ya kupata majibu yenu…,” yule daktari akafungua uwanja wa mazungumzo.
“Sawa daktari, tuko tayari…,” mumewe Sulee Mr. Masofa alijibu kwa sauti ya unyenyekevu na wasiwasi mkubwa.
“Hongereni sana…”

Aliposema maneno hayo, akatulia na kuwaangalia kwa zamu.
“Mkeo ana ujauzito wa mwezi mmoja, hongereni sana…,” yule daktari alirudia tena na kuwapa mikono ya furaha kwa pamoja.
“Jamani mke wangu, kumbe ni kweli, hongera sana…,” Masofa alisema huku akimkumbatia kwa furaha kubwa mkewe.
“Ahsante sana mume wangu, hata mimi sikuamini nilipojua…”
Waliendelea kufurahia kwa muda mrefu kabla ya kuagana na daktari.
Walipofika nyumbani, furaha iliendelea, kila mmoja wao akijitahidi kuonesha upendo wa hali ya juu kwa mwenziye.

“Mume wangu Mungu ni mkubwa sana…”
“Kweli kabisa mke wangu…”
“Kwa jinsi tulivyohangaika kutafuta mtoto, hakika Mungu yupo mume wangu…”
“Uko sahihi kabisa mke wangu, tumshukuru kwa pamoja.”
Furaha iliendelea kati ya Sulee na mumewe Masofa. Usiku mzima waliendelea kubadilishana mawazo ya hapa na pale ili mradi tu kukamilisha furaha hiyo.

Siku iliyofuata, mumewe Sulee alidamka mapema na kuwahi kibaruani akiwa mwenye furaha tele.
Sulee aliendelea kuchapa usingizi huku akimfikiria sana Dokta Kisarawe. Mapenzi yake juu ya dokata huyo yaliendelea kushamiri hasa kwa kitendo cha yeye kunasa ujauzito.
“Ina maana hapa mwenye matatizo ya uzazi ni huyu mume wangu Masofa…,” Sulee alianza kujisemea muda mfupi baada ya kuamka na kuketi kitandani.

“Kweli kabisa, ni lazima atakuwa ni huyuhuyu, kwa sababu kama ningekuwa ni mimi nisingeweza kunasa hii mimba,” mawazo hayo yakaendelea kujirudia kila mara akilini mwake.
Aliamka na kuanza kufanya usafi wa ndani baadaye akaenda kuoga. Alipomaliza akabandika chai jikoni huku akiendelea na ufuaji wa nguo chache zilizokuwa chafu.
Akamaliza kazi zote na kuanza kunywa chai huku akiwa ndani ya khanga moja iliyolichora thabiti umbo lake la namba nane.

Baada ya kunywa chai, aliingia ndani na kubadili nguo ambapo alivaa viwalo vikali vilivyomtoa sana.
Akaamua kwenda kwa rafiki yake mmoja aitwaye Monica aliyekuwa na tatizo la kutozaa kama alilokuwa nalo yeye.
“Hodi jamani hapa, hodi jamani…,” Sulee alibisha hodi kwa mbwembwe na uchangamfu wa hali ya juu.
“Mm! Karibu sana jamani…,” aliitikia Monicha huku akimshangaa Sulee kwa jinsi alivyokuwa amechangamka.
“Mzima shoga yangu…?”
“Mzima sijui wewe…?”
“Salama…”
“Karibu, naona una furaha kubwa kulikoni…?”
“Tayari shoga yangu, tayariii…”
“Tayari nini tena, mbona sikuelewi…!”
“Nimenasa…”
“Umenasa…?”
“Eee, nimenasa…”
“Umenasa nini Sulee, mbona sikuelewi?”
“Mwenzio nina mimba Monica…”
“Hamna, acha utani wako bwana…”
“Siyo utani Monica, nina mimba…”

Waliendelea kuzungumza mengi huku Monica akishangaa ni kwa namna gani ameweza kupata ujauzito wakati wote kwa pamoja walisumbuliwa na tatizo moja la kutopata ujauzito. Kwa upande wa Monica tayari alikuwa amekata tamaa.
“Umepata wapi hiyo tiba mwenzangu…?”
“Kuna daktari mmoja mtaalamu sana, yaani ameponesha wengi.”
Sulee aliendelea kummwagia sifa Dokta Kisarawe.

Kwa muonekano, Monica alikuwa mwanamke mrembo mno kupita Sulee. Alikuwa mweupe, mrefu mnene kiasi huku nyuma akiwa ‘amejazia mzigo wa maana.’
Mwili wake ulinakishiwa kwa vinyweleo nadhifu vilivyolala, pua nyembamba ndefu wastani huku maeneo ya kifuani yakiwa yamepambwa kwa ‘nido’ ndogo kiasi zilizochongoka.
Mara nyingi alipendelea sana kuvaa nguo za kubana na kusababisha mateso makubwa kwa wanaume wakware.
Miguu yake minene wastani, kila alipokuwa akikanyaga hatua moja, mzigo wa nyuma ulitingishika kiaina.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)