Mtunzi: ___
SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
“Kwa nini umenishawishi na kumsaliti mume wangu jamani dokta?” Monica akazidi kuhoji huku akitafuta nguo zake na kuanza kuvaa huku akijisonya.
“Sikiliza Monica, wote tumejikuta katika hali hiyo, hakuna wa kumlaumu hapa, sasa nakushangaa sana kama utaanza kunilaumu mimi wakati kama ni raha tumezipata wote…”
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
“Raha gani, raha gani dokta nakuuliza, au unataka nikujazie watu chumbani kwako?” alilalama Monica.
“Sasa kwa nini ufikie huko kote, halafu unaposema nilikushawishi nashindwa kuelewa, hadi naanza kukushawishi ulikuwa wapi?”
“Wewe ndiyo chanzo cha usaliti, kwani mimi nilikuambia naumwa huko, ulipoanza kushika sehemu ambazo hazihusiani na ugonjwa wangu nilikuambia kabisa kuwa dokta mi’ siumwi huko, lakini hukusikia, lengo lako lilikuwa nini…?”
“Unajua Monica hatupaswi kulaumiana sana kwa hili?” alisema Dokta Kisarawe huku akionesha uso wa huzuni japo moyoni alikuwa akifurahia na kujipongeza kwa kitendo cha kufanikisha kula tunda la mtoto mzuri kama Monica.
“Unasemaje wewe, hivi una akili kweli?” Monica aliendelea kung’aka chumbani humo.
Kutokana na maneno matamu na kuonesha heshima aliyokuwa akiyatoa Dokta Kisarawe, kwa kiasi fulani yalichangia kumlainisha Monica na kuanza kushuka taratibu.
“Sawa lakini siyo vizuri bwana”
“Sawa jamani, naomba tuchukulie kama bahati mbaya mama,” alisema Dokta Kisarawe.
Kitendo cha daktari huyo kutumia jina la mama wakati wa kumuita Monica, kilimfurahisha sana mrembo huyo kwani tangu aolewe hakuwahi kuitwa kwa jina hilo na mumewe.
“Poa, nimekuelewa, nimekuelewa baba;” Monica naye alijibu kwa sauti ya chini lakini alijikuta akimalizia kwa neno la baba hali iliyomshangaza na kumchanganya sana Dokta Kisarawe.
Kwa pamoja walivaa nguo zao huku kila mmoja akikumbuka utundu na utaalamu wa mwenzake.
“Ila twende mbele turudi nyuma, huyu dokta ni kiboko kwa mambo ya chumbani, sasa kama amenifanyia utundu wote huu kwenye eneo lisilokuwa na uhuru kama hili, vipi kama tukikutana ndani ya chumba tukiwa na muda wa kutosha, itakuwaje?” Monica aliwaza huku akimalizia kuvaa nguo yake ya ndani kabla ya kumalizia kwa zingine.
“Dah! Hata Mungu aliposema nitakufanyia msaidizi, aisee alikuwa akimaanisha huyu, mama yangu vile nakuambia…,” Dokta Kisarawe alijisemea kimoyomoyo huku akifunga mkanda wa suruali yake pana kiunoni.
“Sasa kwa hiyo kuhusu tiba dokta;?” Monica alimuuliza Dokta Kisarawe huku akimuangalia kwa macho ya; Ila unayaweza sana.’
“Aaah, kuhusu tiba inabidi uje baada ya siku mbili lakini kwa sasa nitakupa vidonge f’lani, sawa?” alijibu dokta huku akimuangalia Monica kwa jicho la hata hii si ni sehemu ya tiba?’
Baada ya muda waliagana na Dokta Kisarawe akampa Monica vidonge f’lani vya rangi nyekundu na kumpa maelekezo ya namna ya kuvitumia.
“Basi sawa, lakini dokta nitakushukuru mno kama nitapona na hatimaye kupata mtoto, ujue nina hamu sana ya kuitwa mama jamani;,” Monica alisema huku akimtolea macho Dokta Kisarawe hali iliyobadili kabisa hali ya mzunguko wa damu wa daktari huyo mwenye uchu wa warembo wazuri kama alivyokuwa Monica.
“Usijali Mamie, mimi ndiyo Dokta Kisarawe bwana, si umeona mfano kwa rafiki yako Sulee, naye alikuja hapa akiwa haamini kama wewe lakini kwa sasa ni mama kijacho…”
“Mmh! Sawa kama kweli basi mimi naenda bwana”
“Sawa, tutaonana”
Monica alifungua mlango na kuwakuta wateja wengine wakingojea huduma ya Dokta Kisarawe.
Walimtupia Monica macho ya chuki kwani kitendo cha kuitwa yeye kwanza na kuwaacha waliokuwa wametangulia kiliwakera na kuwaudhi vibaya mno.
“Muone kwanza, watu wengine wanajirahisi kwa madaktari wakidhani ndiyo njia pekee ya kutibu magonjwa yao sugu;,” yalikuwa mazungumzo ya akina mama wawili waliokuwa wamekaa kwenye benchi la kusubiri zamu huku wakimuangalia Monica kwa jicho baya.
Monica alimkuta rafiki yake Sulee amenuna bila kujua chanzo na sababu ya yeye kufanya hivyo. Moyoni akawaza huenda kilichomuudhi Sulee ni kitendo cha yeye kuchelewa chumbani kwa dokta.
Hali ilikuwa tofauti kabisa kwa upande wa Sulee, wivu wa mapenzi ya Dokta Kisarawe ulikuwa umemkaba hadi shingoni na sasa alikaribia kuzimia kwa hasira.
Kitendo cha kusikia meza na viti vikitoa sauti ya kusukumwa kila mara kilichangia kwa asilimia nyingi sana kwa Sulee kuamini kuwa ni lazima kwa vyovyote vile Monica atakuwa ametembea na Dokta Kisarawe jambo ambalo lilimuumiza kuliko ncha ya wembe kupita kwenye kidonda kibichi.
“Vipi rafiki yangu mbona unaonekana umenuna sana, pole kwa kuchelewa mwaya, “Monica alijibalaguza huku akimshika begani Sulee bila kujua hali mbaya ya wivu iliyokuwa ikimtesa mke huyo wa mtu.
“Ina maana kweli Monica unaweza kunifanyia hivyo;?” aliuliza Sulee kwa sauti ya kukwaruza.
“Nimefanya nini tena Sulee, si nimekuomba msamaha kwa kuchelewa jamani?”
“Si umetembea na Dokta Kisarawe wewe;,” alijibu Sulee kwa sauti ya juu na yenye hasira.
Je, nini kitatokea kuhusu penzi la Dokta Kisarawe na wawili hao?
“Mimi Sulee, una akili kweli au? Kwa nini unifikirie hivyo jamani?”
“Akili ninazo tena nyingi sana Monica. Sasa ile kukurukakara ya viti kutoa mlio ilikuwa nini? Ndiyo matibabu yenyewe?”
“Sasa je? Madokta we Sulee unawajua, wakimpima mwanamke mara wamshike makalio, mara watamani kumbusu, kama hukutumia akili yako unaweza kujikuta umemalizwa.”
“Mh! Mi siamini Monica.”
“Kwa nini huamini? Kwanza naomba nikuulize Sulee, umekuwa ukiniwekea wingu kuonana na dokta, kwani ni nani yako?”
Sulee alishtuka kwa swali hilo hasa alipokumbuka kwamba, mumewe na mume wa Monica ni marafiki na wao pia ni marafiki. Mambo yanaweza kufika mbali…
“Mi nimeuliwa tu, si nani wangu wala nini!”
“Sasa ni kwa nini umenitolea mimacho kwamba nimetembea na dokta kisa ulisikia viti vikilialia ndani?”
“Maana yangu usije ukamsaliti shemeji.”
“Mmmh! Au wewe siku ulipotembea naye mliliza viti? Sema ukweli Sulee.”
Ilibidi Sulee acheke ili kupoza mambo, akabalaguza kwa kuanzisha hoja nyingine kabisa nje ya hiyo.
Lakini Monica alishapata ujumbe, aliamini kuna kitu kati ya Sulee na Dokta Kisarawe…
“Amekupa dawa lakini?” aliuliza Sulee.
“Ndiyo, amesema nitumie hizo kisha niwasiliane naye.
Walifika kwanza nyumbani kwa Sulee, baadaye Monica akaenda nyumbani kwake.
Alifikia kwenye kiti akiwa amechoka sana kwa purukushani za Dokta Kisarawe…
“Lakini kama asingetumia nguvu walahi vile asingenipata, ana bahati sana, kidogo nimpigie kelele…
“Lakini lo! Dokta anayajua mambo yule, sijui ni dokta wa mapenzi au wa mwili. Kama ofisini kwake tena chapchapu ni vile. Je, tungekuwa chumbani?” Monica alijikuta akiwaza mengi sana kuhusu dokta na mazingira yote yaliyotokea. Ilikuwa mara yake ya kwanza kumsaliti mumewe na akahisi kuna tofauti kubwa kati ya mumewe na Dokta Kisarawe.
“Kwanza mume wangu hana pawa sana kama dokta. Halafu mume wangu utadhani hahemi, dokta anatoa mhemo mpaka unajua mwanaume yuko kazini,” alisema moyoni Monica.
***
Dokta Kisarawe alikaa kwenye kiti akimuwaza Monica…
“Huyu mwanamke ni mzuri sana kuliko wengine. Da! Bonge la mwanamke. Sijawahi kukutana na mwanamke mzuri kama huyu, ngozi nzuri, laini, hana kipele wala manundunundu kama wengine,” aliwaza moyoni daktari huyo ambaye inawezekana mpaka kwa Monica ni mwanamke wa mia mbili tangu aanze kutoa tiba.
***
Usiku wakiwa kitandani, mume wa Monica ndiye aliyeanza mazungumzo…
“Mke wangu, kwa dokta kuliendaje leo?”
Monica moyo ulimlipuka, alihisi aliulizwa swali lile kwa maana kwamba mumewe amesikia alitembea naye palepale kazini.
“Kwani vipi mume wangu?” Monica aliuliza kwa sauti ya chini.
“Ulikwenda hukwenda?”
“Nilikwenda dear.”
“Si ndiyo nakuuliza kulikuwaje?”
“Ooo, alinipa dawa akasema nitumie nikimaliza nirudi kumwambia.”
“Basi, tusubirie. Asubuhi unioneshe hizo dawa.”
“Sawa.”
***
Nyumbani kwa Sulee, mumewe alikuwa akilishikashika tumbo la Sulee akijifanya ndiyo anaulea ujauzito huo kwa mapenzi ya dhati…
“Natamani uzae hata leo mke wangu.”
Sulee alicheka huku moyoni akisema…
“Ungejua mtoto si wako, wala usingejipongeza, mwenzako mwenye nguvu za kusababisha mtoto ndiyo amehusika.”
***
Asubuhi, mume wa Monica akiwa ameshajiandaa kutoka kwenda kazini alikumbuka kitu, akamwita mkewe…
“Abee.”
“Nipe zile dawa.”
Monica alikwenda chumbani, akatoka na kipakti…
“Tena dokta alisema nikitaka kuzinywa lazima niwe nimekunywa chai ya kutosha,” alisema huku akimpa dawa hizo mumewe…
“Khaa! Mbona ni dawa mpya za mafua mke wangu, vipi kwani?”
“Dawa mpya za mafua?”
“Ndiyo. We hukumbuki siku zile mama alipokuja akawa anasumbuliwa na mafua nilinunua dawa hizi?”
“Mh! kweli? Kwani zile si zipo, ngoja nikazilete.”
Monica alikwenda kwenye bakuli kubwa la plastiki, akachakurachakura na kuona kipakti cha dawa hizo.
“Kweli mume wangu, si hizi hapa!”
“Si ndiyo sasa.”
“Mh! Ina maana Dokta Kisarawe kaniingiza mkenge siyo?”
“Haya, kumbe dokta mwenyewe anaitwa Kisarawe! Kisarawe si walaya ya mkoa wa Pwani, tangu lini likawa jina la mtu! Makubwa haya.”
Monica alifedheheka, akaanza kuhisi Sulee amemwingiza mkenge kwa kumpeleka kwa daktari feki na si yule aliyemsaidia yeye…
“Lakini kama ni feki, mbona pale nje palikuwa na wanawake wengine wengi tu tena wasiofahamiana na Sulee. Au..?” alishindwa kumalizia.
Baada ya dakika tano mumewe kuondoka, Monica alishika simu, akampigia simu Dokta Kisarawe…
“Dokta za leo, mimi Monica…”
“Ooo, Monica mpenzi, umeamkaje? Vipi, umenimisi my dear?” “Sikiliza Dokta Kisarawe…”
Enhe, nakusililiza baby.”
“Umenipa dawa gani?”
“Lini?”
“Jana.”
“Si za kusaidia kutunga mimba!”
“Mh! mbona ni dawa za mafua?”
“Sikiliza mpenzi wangu, mimi siwezi kukupa dawa sizo. We endelea kutumia hizo dawa halafu baada ya siku ishirini utaniambia matokeo,” alisema Dokta Kisarawe.
“Mh! Sijui, yangu macho.”
“Kwani uko wapi Monica mpenzi?”
“Nyumbani.”
“Unafanya nini?”
“Ndiyo nimeamka.”
“Naomba tuonane leo nje ya nyumbani kwako au nje ya hapa hospitalini kwangu.”
“Unataka nini tena? Jana si ulifanikiwa?”
“Nilifanikiwa lakini si kwa uhuru nilioutaka.”
“Uhuru gani? Kwani ulitaka uhuru au ulitaka kutimiza haja yako?”
“Haja na uhuru.”
“Kwanza nimegundua kitu, wewe na Sulee ni wapenzi, unabisha dokta?”
“Si kweli, kama mwenyewe Sulee amekwambia hivyo basi ujue ananitaka maana nilishawahi kuona dalili za kunitaka lakini nikampotezea, unajua lazima upende kilicho kizuri kama wewe.”
“Kwani mi mzuri dokta?” Monica alianza kulainika sasa, hata lugha aliyotumia iliashiria hivyo…
“Sana, Sulee atasubiri sana kwako.”
“Mmmh! Ya kweli hayo?”
“Mimi nakwambia ndiyo maana nimeomba tuonane na wewe nje ya nyumbani kwako au nje ya hapa kazini kwangu.”
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA