Mtunzi: ___
SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
“Sana, Sulee atasubiri sana kwako.”
“Mmmh! Ya kweli hayo?”
“Mimi nakwambia ndiyo maana nimeomba tuonane na wewe nje ya nyumbani kwako au nje ya hapa kazini kwangu.”
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
“Saa ngapi?”
“Sema wewe unataka saa ngapi?”
“Mimi jioni siwezi kutoka kwani nakuwa naandaa chakula cha mista mwenyewe, muda wangu ni asubuhi mpaka kwenye saa sitasita hivi.”
“Basi tukutane asubuhi hii.”
Walipanga kukutana kwenye gesti ya Kivumbi na Jasho nusu saa mbele ambapo Monica palepale aliingia bafuni kuoga na kuvaa. Kwa vile ilikuwa ahadi maalum, Monica alivaa sana siku hiyo.
Alipigilia gauni jepesi la kufika magotini na hivyo sehemu kubwa ya mapaja kuwa wazi. Hakuacha pafyumu kwa kujipulizia kwa wingi.
Midomo aliichora kwa rangi nyekundu huku nyusi akizipunguza kwa staili ya kukatia na kusiliba kwa wanja.
“Hapa naamini dokta ndiyo atazidi kukubali uzuri wangu. Si amesema mimi ni mzuri kuliko Sulee. Leo atajua mimi pia ni mzuri kuliko Kleopatra wa Misri.”
Alibeba kipochi cha begani kilichokuwa na kanga pea moja ndani yake, akachukua Bajaj hadi kwenye gesti hiyo ambapo dokta alishafika kama dakika kumi nyuma.
Alisimama nje ya gesti akamtumia meseji…
“Nipo nje.”
“Ingia namba kumi.”
***
Monica alishaingia chumbani na alikuwa amelala kwenye mapaja ya Dokta Kisarawe akimkunakuna mgongoni huku akizidi kumsifia sana…
“Baby wewe umeumbika bwana, kama hujui naomba ujue sasa.”
“Kweli dokta?”
“Kweli kabisa.”
Kule kushikwashikwa kulimpandisha mashamsham Monica, akaanza kuchaji. Hata kuhema kwake kulibadilika, pozi zilikuwa na kutegatega. Yeye mwenyewe akatoka kwenye miguu ya kwa dokta na kusimama, akajivua gauni, akabaki na kufuli tu, dokta akabahatika kuona uzuri wa mapaja ya mwanamke huyo.
Naye alikurupuka, akasimama, akavua suruali huku akichekacheka kama fisi aliyeona mbuzi akikatizia jirani yake kule porini.
“Lakini leo lazima dokta utumie kinga.”
“Khaa! Monica unataka mimba hutaki mimba? Kinga ya nini tena wakati unasema hujawahi kunasa ujauzito?”
“Ndiyo, lakini sitaki ujauzito wa kwako au mwanaume mwingine nje ya mume wangu.”
“Unaamini yeye anaweza kukuzalisha?”
“Si umenipa dawa!”
Dokta Kisarawe alikosa cha kuongeza, akabaki amemkodolea macho mwanamke huyo lakini kutoka moyoni hakupenda kutumia kondom kwake.
“Please my dear, twende uwanjani bila viatu,” alisema dokta huyo huku macho yake yakiwa yanakosa nguvu polepole.
“Hapana dokta, siwezi, tutumie viatu ili nisichomwe na miba. Kama ni miiba nataka ya mume wangu tu.”
“Nikwambie kitu Monica?”
“Niambie dokta.”
“Ujue raha ya mchezo kama huu ni kuingia uwanjani pekupeku, mguu kwa mguu, nyasi kwa nyasi,” hapo sasa Dokta Kisarawe alikuwa amemsogelea Monica na kumshika, akamvutia kwake…
“Noo dokta.”
“Please, nikubalie Monica,” dokta alisema huku akisogeza midomo yake kwenye sikio moja la mwanamke huyo na kumpumulia kwa karibu hali iliyomchanganya Monica ghafla…
“Aaa…dokta…”
“Nini tena Monica jamani?”
“Acha!”
“Kwani unaumia Monica?”
“Dokta bwana, unaniteke…”
“Mmm, polepole Monica wangu,” alisema dokta kwa sauti nene huku akizidi kumhemea, maskini Monica alikosa nguvu ghafla na kulegea.
“Do…do…dok…taaa.”
“Ee.”
“Kwa…kwa…ni…ni..?”
Dokta Kisarawe alimbeba Monica na kumpandisha kitandani, akamfuatia kwa haraka ili asimtoe kwenye ile hali ya msisimko.
Kuanzia hapo, Monica hakusema tena, alimwacha dokta huyo afanye kila alichotaka na yeye alikuwa tayari.
Miguno ilimtoka kinywani mrembo huyo kila pasi ya mpira ilipopigwa kwake, macho yalijaa giza jekundu huku mwili ukiwa mwepesi hasa sehemu ya katikati ambayo inaruhusu mwili kujimega sehemu moja na nyingine, hasa juu kwenda kifuani na chini kwenda magotini.
Wakiwa wazimawazima, wote walijikuta wakitangaza kila mmoja kujipatia pointi moja kwa mkwaju wa nguvu kuliko ule wa penati, wakatulia Monica akijikunjakunja kama samaki aliyerushwa nchi kavu kutoka majini na mvuvi mwenye utaalam wa hali ya juu.
“Iloo, lione kwanza,” Monica alimwambia Dokta Kisarawe huku akijua kwamba alizidiwa na kujikuta akishindwa kusimamia msimamo wake wa kucheza mechi na viatu, akakubali kucheza bila viatu.
“Umedhurika nini sasa mpenzi wangu Monica?” aliuliza dokta huku akichekacheka kimtindo.
“Madhara yapo. Je, nikinasa?”
“Hupendi kunasa?”
“Nilishasema nataka kwa mume wangu.”
“Huwezi kunasa, mi najua. Utanasa kwa mumeo tu.”
***
“Mambo Sulee?” Monica alimsalimia shoga yake huyo siku saba baada ya siku thelathini na moja za mwisho wa mwezi.
“Poa Monica, niambie.”
“Hivi unajua nimepita siku kama kumi na moja?”
“Kweli?”
“Eee.”
“Basi piga vigelegele Monica, tayari.”
“Inawezekana kweli?”
“Kabisa.”
***
Monica aliamua kwenda kwenye zahanati ya jirani na kwake ili akathibitishe kama kweli amenasa…
“Mh! Kama kweli atakuwa mume wangu tu. Siku ile si dokta alisema hakukuwa na uwezekano.”
Monica alipima haja ndogo, akasubiri majibu yake huku kiroho kikimdunda! Hakuwa amemwambia mume wake kuhusu kupitisha muda huo wote na mume naye siku hiyohiyo alikwenda kwenye hospitali moja kubwa kwa ajili ya kucheki mfumo wake wa uzazi kama upo sawa au la!
Wakati mumewe akiwa kwenye benchi akisubiri majibu, yeye alikuwa kwa dokta akipokea na alipanga asimwambie mkewe kwa majibu yoyote yale…
“Ndugu nani…katika maisha yako uliwahi kupata ajali ya gari hivi?” dokta alimuuliza mume wa Monica.
“Yeah! Mwaka elfu mbili na tatu.”
“Ulikuwa hujaoa?”
“Yah!”
“Sasa bwana sikiliza nikwambie, wewe mfumo wako wa uzazi ulivurugika baada ya ajali hiyo. Kwa hiyo huwezi kumpa mimba mwanamke.”
“Kweli dokta?”
“Ndiyo vipimo vinavyosema.”
***
“Mrembo majibu yako yapo sawa. Una ujauzito wa siku kumi na moja sasa. Hongera sana, mwambie mzee pia nampa hongera
ake,” daktari wa zahanati aliyokwenda Monica alimwambia.
“Kweli dokta?”
“Ndiyo kipimo kimesema hivyo mrembo. Wewe ni mjamzito.”
“Jamani, kweli Mungu mkubwa. Asante Mungu wangu. Mume wangu atafurahije?”
Monica alitoka akiwa na furaha iliyopitiliza, moja kwa moja hadi nyumbani, akafikia sebuleni ili ampigie simu mumewe na kumpa habari njema.
Simu ya mume wake iliita kwa muda bila kupokelewa, ikakatika akapiga tena…
“Khaa! Huyu vipi kwani? Simu hapokei, yuko wapi?”
Akajaribu kama mara tatu mpaka nne bila kupokelewa, akaamua kutuma meseji akiamini kwamba kama mumewe yuko mbali na simu, akiifikia atakutana na ujumbe wake mzuri…
“Baby, Mungu mkubwa mume wangu. Nimekwenda kupima nimeambiwa nina ujauzito. Da! Kweli Mungu hamtupi mja wake.”
Baada ya kutuma meseji hiyo, Monica alikaa nusu saa bila kujibiwa hali iliyompa wasiwasi, alianza kuhisi mumewe amepata matatizo makubwa mahali, akapiga tena simu, haikupokelewa.
“Mmh! Siyo kawaida,” alisema moyoni Monica lakini hakuchukua hatua yoyote. Ile furaha yake ikachanganyika na wasiwasi.
***
Mume wa Monica alikaa kwenye mgahawa mmoja na mume wa Sulee wakizungumza. Mume wa Monica alikuwa akimsimulia alichoambiwa na daktari baada ya kupima eneo la uzazi…
“Kwa hiyo ndiyo hivyo bwana, mimi sina uwezo wa kuzaa tena kwa mujibu wa yule daktari. Nimeumia, lakini nimeikubali hiyo hali, sina jinsi.”
“Da! Sasa shemeji yeye huko anakohangaika kwa Dokta Kisarawe ina maana anapoteza muda tu?”
“Kiukweli anapoteza muda ndugu yangu.”
Meseji nyingine iliingia kwenye simu ya mume wa Monica, mume wa Sulee akamshauri azisome…
“Kaka, kuna simu zimepigwa na meseji zimeingia, ungesoma hata meseji ujue nani, pengine madili ya hela.”
Mume wa Monicha aliivuta simu ilipokuwa, akaitumbulia macho…
“Shemeji yako amepiga mara kibao, halafu kuna meseji yake hapa, anasemaaa…baby, Mungu mkubwa mume wangu. Nimekwenda kupima nimeambiwa nina ujauzito… Da! Kweli Mungu hamtupi mja wake.”
Mume wa Sulee alishtuka kusikia hivyo, mume wa Monicha akaishiwa nguvu kabisa…
“Au dokta amekudanganya ndugu yangu, uko fiti!”
“Noo! Sidhani, huyu atakuwa na mimba ya mwanaume mwingine, kweli kabisa.”
“Hapana bwana, itakuwa yako.”
“Kaka, mimi nimemwamini dokta. Unajua nilishawahi kuwa na demu kabla ya Monica hakuwahi kunasa ujauzito wangu, lakini nilipomwacha tu, akaenda kunasa kwa jamaa mpya. Huoni kama ni kweli sina uwezo wa kuzalisha?”
“Mh! Shemeji anaweza kufanya hivyo?”
“Ndugu yangu, wanawake wanaweza. Tena unajua afadhali na mwanaume anayeweza kuzaa mtoto akamwacha kwa mama yake huko wapi sijui, lakini wao mtoto unalala naye kitandani lakini si wako.”
“Sasa unadhani iweje ili kubaini ukweli au uongo wake?”
“Itabidi nifanye uchunguzi.”
“Dah! Aisee, kama mimi nigundue mke wangu amebeba mimba ya mwanaume mwingine kwa kweli nadhani naweza kufanya jambo baya sana ulimwengu ukanishangaa.”
“Ni kweli. Lakini wewe mwenzangu si uwezo wa kuzaa unao kama hivi shemeji ni mjamzito na ulishawahi kumpa mimba yule mtoto wa mjumbe ukaitoa.”
“Eee, mimi ni mzima kaka, si Diana mtoto wa mjumbe tu, kuna demu anaitwa Maureen naye nilishampachika mimba ikatoka yenyewe,” alisema mume wa Sulee kama anayejitapa kwa mwenzake.
“Mimi bwana nitakwenda hadi kwenye DNA kutaka uhakika, niko tayari kutumia gharama yoyote ile lakini najua mwisho wa siku mtoto si wangu, naamini.”
“Mimi nitakuwa pamoja na wewe.”
Waliagana, kila mmoja akaelekea nyumbani kwake.
***
“Za kazi mume wangu?” Sulee alimsalimia mumewe.
“Nzuri tu.”
“Mbona kama haupo sawa?”
“Nitakuwa sawa kivipi wakati kumbe mnatusaliti?”
“Kivipi tena?”
“Monica amekwenda kupima akagundulika ana ujauzito…’
“Usiniambie, mbona hajania…”
“Sikiliza wewe, mbona unadandia kwa mbele.”
“Enhe?”
“Wakati yeye amekwenda kupima, mumewe naye alikwenda kupima, akabainika hawezi kumpa mimba mwanamke, sasa hiyo ya Monica ameipata wapi?”
“Mh! yamekuwa hayo?”
“Ndiyo maana yake. Nadhani hata hiyo ya kwako si yangu mke wangu.”
“Hamna my dear, mimba yako hii wala usiwe na wasiwasi,” Sulee alisema huku sura yake ikichora alama ya unyonge, alivuta picha kuhusu Monica akaamini hisia zake kwamba alitembea na Dokta Kisarawe ni za kweli.
“Lakini baby, unajua niliwahi kuhisi kwamba Monica anatembea na yule dokta aliyetupa dawa.”
“Dokta Kisarawe?”
“Ndiyo.”
“Kama ametembea naye yeye basi hata wewe umetembea naye maana ndiye uliyempeleka.”
“Wala, mimi hawezi.”
“Hawezi wewe mkali, mgumu, mjeuri au mwanaume mwenzake?”
“Hawezi tu.”
“Sikia Sulee…
Nakusikilia mume wangu.”
“Mimi si mjinga kama mume wa Monica, mimi mjanja sana.”
“Najua sana lakini siwezi kukusaliti mume wangu, amini.”
“Lakini si mlikuwa mnapelekana wote?”
“Ndiyo, lakini sijatembea na Dokta Kisarawe.”
“Je, nikigundua umetembea naye?”
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA