Mtunzi: ___
SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Mara, mume wa Sulee alimpigia
mke wake…
“Enheee, Sulee hebu njoo hapa Kinondoni Mkwajuni haraka sana, chukua Bajaj,” alisema mwanaume huyo.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
“Kuna nini tena?”
“Nimesema njoo, utajua hapahapa.”
Sulee kwa sababu alikuwa amevaa gauni, alichofanya ni kubeba khanga moja tu, akatoka mbio na kuchukua Bajaj mpaka Mkwajuni. Alimpigia simu mumewe, akamwambia alipo. Ile anafika tu na kumwona mume wa shoga yake Monica akahisi kitu tayari kuhusu Monica mwenyewe…
“Hapana lazima Monica amefanya kitu,” alisema moyoni lakini alishindwa kumpigia kwa sababu tayari alikuwa mbele ya wanaume hao walioonesha sura za kuchukia…
“Kuna nini kwani? Eti shemu kuna nini?”
“Ingia kwanza ndani ya gari,” mume wake alimwambia akiwa ameshamfungulia mlango…
“Rafiki yako ameingia gesti ile…”alisema mume wa Monica.
“Na nani? Ameingia na mwanaume gani?”
“Hatujajua, lakini tumemwona yule Dokta Kisarawe naye akiingia,” alisema mume wa Sulee…
“Mungu wangu, ina maana Dokta Kisarawe ndiyo wa kwake siku hizi siyo?”
“Hatujathibitisha.”
“Sasa kwa nini msiende?”
“Tumeona hakuna haja ya kwenda shemu, ila tukae hapa mpaka watoke ndipo na sisi tujitokeze,” alisisitiza mume wa Monica.
“Mh! Makubwa,” alichoka kabisa Sulee. Moyoni alikuwa na mambo mawili, kwanza shoga yake kuingia kwenye mkenge huo, pili ni wivu wa dokta kutembea na Monica jambo ambalo aliwahi kulihisi lakini akakosa ushahidi wa moja kwa moja.
“Lakini mkuu je kama shemeji atatoka peke yake na Dokta Kisarawe naye peke yake itakuwaje?” alihoji mume wa Sulee hoja ambayo ni ya kweli kwani kama angeanza kutoka mmoja wao, mfano dokta wangemuingizaje kwenye tuhuma za kumfumania?
“We sikiliza, hata kama itakuwa hivyo bado ni tatizo, ishu hapa ni yeye kuja gesti, iwe na dokta iwe na mwanaume mwingine lakini hoja ni moja tu, sijapenda. Halafu ananidanganya kwamba yuko nyumbani,” alilalamika mume wa Monica.
Nusu saa ilikatika, hakukuwa na mtu yeyote aliyetoka ndani achilia mbali Dokta Kisarawe na Monica. Sulee akashauri…
“Mimi shemeji nashauri kwamba, kama inawezekana mimi niende kuingia, nikaulizie…”
“Hapana,” alikataa mume wa Sulee, akataka uendelee utaratibu uleule kwani ufafanuzi ulikuwa tayari kwamba, awe amenaswa laivu au la, ishu ni yeye kuingia katika gesti hiyo.
Dakika sitini zilionesha kwenye saa zao za kwenye simu na mkononi, walitoka watu wawili, mwanamke na mwanaume lakini wakiwa wamepishana kwa dakika kama tatu hivi. Aliyeanza ni mwanaume.
“Loo! Shemeji naona shoga yako kaamua kumkinaisha Dokta Kisarawe, lisaa limoja sasa,” alisema mume wa Monica…
“We acha tu, mi mwenyewe nashangaa, muda wote huu?”
“Ungekuwa wewe ungetumia dakika ngapi?” Sulee aliulizwa na mume wake lakini kicheko cha mume wa Monica kukalifanya swali hilo kuwa jepesi zaidi.
“Mimi sina mpango huo kwanza, sijui yeye ametolea wapi haya mawazo,” alijibu Sulee.
Mume wake akaendelea…
“Nimekuuliza kwa sababu umesema unamshangaa yeye kutumia muda mrefu hivi, ndiyo maana nikataka kujua ungekuwa wewe ungetumia muda gani?”
Kabla jibu halijapatikana, ndani ya gesti hiyo alitokea mwanaume mmoja, si Dokta Kisarawe. Alikuwa akifunga vifungo vya shati vizuri huku uso ukionekana kuwa na jasho kwa kazi ya chumbani.
“Jamani, inawezekana yule mwanaume ndiyo alikuwa na Monica chumbani?” alisema kwa mshtuko mume wa Sulee…
“Haa! Halafu namfahamu, ni jirani yangu bwana. Anaitwa baba Anode, atakuwa yeye,” alisema mume wa Monica huku akianza kufungua mlango ili atoke, tayari alikuwa amekasirika kuona kumbe anayemwibia ni jirani yake.
Kabla hajatoka, msichana mmoja naye wa nyumba ya jirani na mume wa Monica alitoka kwenye gesti hiyo hivyo kutoa picha kwamba, alikuwa na baba Anode.
“Yule msichana anaitwa Mwasiti, ina maana anatembea na baba Anode?” alihoji mume wa Monica akionekana kushangaa sana.
Tena ili kudhihirisha kwamba kweli walikuwa wote gesti, Mwasiti alikazana na kumfikia baba Anode ambapo walishikana mikono na kutembea kwa maringo kama wapo fungate.
Baada yakuona kimya hawatoki Mume wa Monica na mume wa sulee waliamuwa kuingia ndani nakuwakuta Monica na dokta wakiwa chumbani
Monica kumwona mumewe akadondoka chini
nakupoteza fahamu kwa presha aliyo kuwa nayo.
Wanasema anayefumaniwa hupoteza nguvu hata kama ni baunsa uwa mdhembe, mume wa Sulee licha ya wembamba wake lakini aliweza kumkwida Dokta Kisarawe na kumtembeza hadi lipokuwa Sulee,
Monica alikuwa hajazinduka.Dokta Kisarawe akawekwa chini akae pembeni ya Monica huku kazi ya kumpepea Monica ikiendelea ili azinduke… “Katika hali kama hii shemeji halafu mwanamke aje kuniambia eti mimba ni yangu inawezekana kweli?” Mume wa Monica alimwambia Sulee…
“Kweli lakini shemeji. Inauma sana!” Dokta Kisarawe aliinua uso na kumwangalia Sulee kwa sura inayosema…
“Hata wewe unaongea maneno kama hayo wakati mimba yako pia ni yangu?”“Unaniangalia nini, kwenda huko?” Sulee alimkandia daktari huyo kwani alijua kwa pale hakuwa na ujanja wa kumfanya chochote wala kutoboa siri. Atoboe siri ale mkong’oto! Katika hali isiyotarajiwa, mume wa Monica alimvaa Dokta Kisarawe kwa kumpiga teke la tumbo na mangumi ya kichwani hadi naye akaanguka na kupoteza fahamu…
“Siwezi kumlegezea mtu kama huyu, ameharibu ndoa yangu,” alisema mume wa Monica huku akitaka kumwongezea kipigo lakini mume wa Sulee akazuia. Watu walianza kujaa eneo la tukio. “Jamani kuna nini kwani?” Walihoji watu huku wengine wakiwa tayari wameokota mawe kutaka kumpiga Dokta Kisarawe. “Ha! Jamani huyu si Dokta Kisarawe?” Mwanamke mmoja aliuliza kwa mshangao mkubwa.
“Ni yeye bwana,” mwenzake alijibu halafu akaendelea kusema…
“Halafu mi nilijua tu jamani kwamba iko siku moja dokta atafumaniwa. Kutibu gani wagonjwa kila siku uko na wake za watu?” “Mimi mwenyewe siyo siri niliacha kwenda kwake baada ya kunitongoza kila nikifika. Wengine dokta hatujaumbwa hivyo. Wewe kila mwanamke unadhani anaweza kukukubali?”
Mazungumzo ya wanawake hao wawili yalitoa mwanga mpya kabisa kwa akina Sulee, mume wa Monica akasema anataka kummaliza dokta kwa kumpiga risasi… “Noo…nooo, usifanye hivyo,” mume wa Sulee akamzuia.
Alipoona amezuiwa kwa tendo hilo, mume wa Monica akaomba watu watawanyike ili abaki yeye, Sulee na mume wake. Watu walitii, wakaondoka lakini wengi walionekana kumkandia daktari huyo. Wapo waliodai wamewahi kusikia kwamba kuna daktari anapenda ngono na wake za watu. Wakati huo Monica alishaamka. Sasa walibaki sita tu, wakamuomba dereva wa teksi aondoke akakae mahali ili wao waingie ndani ya gari. Walimbeba Monica hadi ndani ya gari, wakamwingiza na Dokta Kisarawe. Walikaa wote wakaenea… “Dokta,” alianza kwa kuita mume wa Monica…
“Naam.” “Ni kwa nini unatembea na mke wangu tena mpaka umempa mimba?”
Dokta Kisarawe aliangalia chini tu. Alijua ukweli wa madai ya mwanaume huyo…
“Monica,” mumewe alimwita…
“Bee.” “Ni kwa nini uliamua kunisaliti kwa kutembea nje ya ndoa hadi kupata mimba?”
“Nisamehe mume wangu ni shetani tu.”
“Sawa, labda nikuulize kitu kingine. Ni kwa nini uliamua kusema mimi ndiye mwenye mimba?”
Monica alibaki kimya, akaulizwa tena pia akabaki kimya. Kidogo mume wake amchape makofi…
“Si nakuuliza wewe mbwa.” “Monica si useme tu ukweli, kama kusamehewa usamehewe, unakatakata maneno ya nini?” Alisema Sulee, Monica akakasirika sana na kusema…
“Jamani, haya yote sababu kubwa ni Sulee.” “Ha! We Monica mwogope Mungu, sababu kubwa ni mimi kivipi?
“We si ndiyo ulinipeleka!”
“Halafu nikakutongozea kwa dokta?”
“Unajua mwenyewe.” “Sikia Monica, sidhani kama mimi ni mjinga kiasi hicho. Wewe mzigo wote huu ni wako, hakuna ubishi. Unapotaka kumsukumia mwenzako ni kutapatapa tu.”
“Mwambie shemeji, nahisi kama anataka tufe wote.” “Siyo nataka tufe wote, kwani na wewe si una mimba ya Dokta Kisarawe.”
Mambo yaliharibika! Monica alisema kauli nzito na mbaya, ni kama alichochea kuni kwenye moto wa kuni ulioanza kuzimika. “Unaona Sulee…unaona? Sikukwambia mimi kwamba nahisi hata wewe hiyo mimba ni ya Dokta Kisarawe?” Mume wake alikuja juu.
“Jamani maneno ya Monica si ya kuyaunga mkono, amechanganyakiwa huyu mume wangu,” alijitetea Sulee, msala ulishamwangukia. Mume wake alimvaa mume wa Monica na kumnyang’anya bastola, akamwelekezea mke wake, lakini mume wa Monica akamuwahi na kumpiga mkono, ikaanguka chini. Kuona hivyo, mume wa Sulee alitoka ndani ya gari, akaenda kuokota jiwe kubwa akawa anakwenda nalo kwenye gari ili ampige nalo mke wake. Yeye hakuonekana kuwa na haja na Dokta Kisarawe…
“Naua mimi, naua nasema,” alilirusha jiwe hilo likatua kwenye mlango jambo ambalo mle ndani hakuna aliyetegemea… “Mume wangu jamani siyo kweli,” alisema Sulee akianza kulia. Tayari gari sehemu ya mlango ilikuwa nyang’anyang’a kwa lile jiwe na mwenye gari alikwenda mbali kidogo kwa vile..
kwa vile mahali aliposimamisha gari hakukuwa na njia nyingine ya kutokea zaidi ya ile aliyoelekea yeye kwa miguu… “Mtasha mbona umekuwa mstari wa mbele sana kunizuia mimi nisifafanye uhalifu, inakuwaje wewe unashindwa kujizuia?” Mume wa Monica alisema akimwita mwenzake huyo kwa jina lake la utani.
Mara, mwenye gari alitokea
Alishtuka kuona gari lake limeharibika sehemu ya mlango huku timbwili likiendelea…
“Jamani vipi tena?” aliuliza kwa mshangao mkubwa.
Majibu aliyoyapata yalimfanya ajutie lakini akaahidiwa kulipwa fedha ili kwenda kutengeneza gari hilo japokuwa alikubali lakini kwa shingo upande.
Baada ya utulivu kurejea lakini huku wanaume wote wakiwa na hasira ya wivu, waliamua kwenda polisi ambapo Dokta Kisarawe aliwekwa ndani ili kupisha uchunguzi wa madai ya wanaume hao kwamba ametembea na wake zao na kuwapa ujauzito.
Baada ya kuandikisha maelezo, walirudi nyumbani. Wote walifikia nyumbani kwa Mtasha, mume wa Sulee ambapo kikao kilikaa na misimamo ilitolewa…
“Mimi bwana kwa upande wangu nasema wazi kwamba sina haja ya kuwa na mke kama huyu,” alisema mume wa Monica huku akimwangalia mkewe kwa macho yaliyojaa uchungu…
“Hata mimi, Sulee nakuandikia talaka zako tatu sasa hivi,” alikuja juu Mtasha na kutaka kumpiga tena mke wake kwa hasira…
“Sasa Mtasha si umeshasema unamwandikia talaka si ufanye hivyo, achana na kumpiga bwana,” alisema mume wa Monica.
Wanawake hao wawili waliangua kilio huku kila mmoja akimlaumu mwenzake kwamba alimsababishia lakini lawama za Monica kwa Sulee zilikuwa za kweli kwani yeye alipelekwa na shoga yake huyo ambaye alikuwa akiijua tabia chafu ya Dokta Kisarawe…
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA