Mtunzi: Hussein O. Molito
SEHEMU YA NNE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
“Poa” alijibu na safari ya kutafuta lodge iliyokuwa karibu na hapo ilianza.
Baada ya mwendo wa dakika kadhaa, walipata lodge nzuri na kuchagua chumba. Waliingia ndani na kukaa kitandani.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Wote waliangaliana na kila mmoja alikuwa na ishara zote za kuchoka. Jane alilala fofofo na kumuacha Sam akimuangalia na kumtathmini. Hakika Jane alikuwa na uzuri wa asili. Kwa mara ya kwanza Sam alipata muda wa kukaa na msichana karibu vile. Alimuangalia kwa muda na kuamua kulala.
Iliwachukua masaa matatu na kuamka. Walitoka nje na kupata chai kisha wakarudi ndani. Kila mmoja akaingia bafuni na kuoga. Baada ya hapo walitoka na kuangaliana kwa muda na wote wakatabasamu kwa pamoja. Jane ndiye aliyekuwa wakwanza kupata ujasiri wa kumsogelea Sam mpaka aliposimama, alimkumbatia na kuanza kumshika na kumtomasa kila kona ya mwili wake. Lile tendo liliamsha kila hisia na mshawasha wa kufanya mapenzi.
Walijikuta mataulo yakiwadondoka na wakaingia kwenye sita kwa sita kwa style za aina yake. Hakika walikipata kile walichokikosa siku ile.
******************
“Umetoka wapi Sam?” hilo ndilo swali alilokutana nalo baada ya kumsalimia mama yake.
“Nilitoka alfajiri sana na kwenda beach kufanya mazoezi.” Aliongea Sam na kuliendea friji na kuchukua chupa iliyokuwa na damu ndani yake na kuaza kuiywa huku akijifanya hana hatia yoyote.
“Toka lini umeanza mazoezi?” aliuliza mama yake kwa mshangao mkuu.
“Leo mama..naboreka sana ninapokaa ndani peke yangu masaa yote…kwani wasi wasi wako ni nini mama?..maana kama ni chakula ni hiki unanipatia na kinanifanya nisiwe tofauti na wengine. Kuwa na amani mama yangu.” Aliongea Sam na kumfata mama yake na kumkumbatia. Alitambua jinsi gani mama yake huyo anavyofarijika aitwapo mama na kukumbatiwa na yeye. Mpaka hapo aliimaliza hiyo kesi na kwenda kulala chumbani kwake. Yeye mchana ni kama usiku kwa vile usingizi wake ulivyogeuka. Hupata ladha ya usingizi wa usiku alalapo mchana kuliko usiku wenyewe.
Mapenzi yaliwachanganya wawili hawa na kila mmoja aliutumia usiku kama njia za kujiiba bila kugundulika na mzazi wake.
Siku hiyo wakati wanarudi kutoka sehemu waliyoamua kwenda kujirusha., njiani walikutana na majamaa watatu. Walikuwa wamevaa kininja. Kufumba na kufumbua walijikuta wamezungukwa na kuamuriwa watoe kila walichokuwa nacho.
Wakati Sam akiduwaa na Jane akitetemeka kwa woga. Ngumi kali ya tumbo ilitua sawia kwa Sam iliyomfanya ainame kwa muda. Akashushiwa kipepsi kilichompeleka mpaka chini.
“kama hawana kitu, mchukue huyu msichana akatuburudishe.” Aliongea mmoja wao na wengine wakatii amri na kumnyanyua Jane na kuanza kuzama nae vichakani.
Kelele za kuomba msaada zilitua vizuri katika masikio ya Sam. Hata hivyo alijikuta hana nguvu miguuni na mara akaanza kutetemeka mwili mzima. Mara akaanza kuwa wakijani na manyoya yakaanza kutoka kwa spidi ya ajabu. Mara akabadilika umbo zima na kuanza kuunguruma kwa nguvu.
Wakiwa wanazidi kutokomea kichakani, ule muungurumu uliwashtusha na kuamua kusimama kuangalia unatokea wapi. Maana haukufanana na mnyama yeyote. Pia Dar kutokea mnyama anayeunguruma kama hivyo ni maajabu. Wakati wamezubaa. Walisikia vishindo vya nyayo vikija kwa nguvu upande wao. Ile kugeuka nyuma tu. Wakakutana na mziki wa Sam.
Jane alishindwa kuangalia jinsi mpenzi wake alivyobadilika na kuwa vile. Alitamani kukimbia, lakini kwa kitete alidondoka na kuanguka chini. Aliyafumba macho yake asiendelee kuangalia mauaji yale ya kutisha.
Dakika ishirini baadae, hali ilikuwa shwari na hakuna kilichosikika tena.
Jane akiwa anatetemeka kwa woga huku akiwa ameyafumba macho yake. Alishtushwa na mkono wa Sam ukiwa umemgusa. Alipiga kelele maana alijua ni zamu yake kuliwa.
Alipofumbua macho alimuona Sam akiwa amelowana damu shati lake lote na mdomoni.
“naomba uniache.” Aliongea Jane huku akirudi nyuma kwa woga.
“kwa nini Jane?” aliuliza Sam kwa sauti ya upole. Kama si yeye aliyekuwa kiumbe cha ajabu na aliyefanya mauaji ya kutisha dakika kadhaa zilizopita. Sauti hiyo isiyokuwa na hatia, haikumshawishi Jane kumuamini hata kidogo. Ndio kwanza alijikongoja na kuondoka eneo hilo huku akichechemea. Sam aliamua kumuhimiza abaki ili amsimulie kila kitu. Lakini Jane hakutaka kusikia chochote kutoka kwake. Sam alijikuta akianza kulia na kupiga mateke makopo yaliyokuwa karibu yake. Hakika hakuipenda ile hali hata kidogo. Alitamani awe kama sisi, tatizo haiwezekani tena. Ndivyo alivyoumbwa.
Alilaani na kuamua kukaa chini kwa muda.
Jane wakati huo ailshaondoka na kurudi kwao. Hakika alijawa hofu ambayo hajawahi kuwa nayo toka anazaliwa. Alishindwa kuamini kuwa Sam licha ya kuwa alikua na miujiza, kumbe pia huweza kubadilika na kuwa mnyama wa ajabu na kufikia hatua ya kula watu.
Mawazo ya kile alichokiona kilimkosesha usingizi Jane. Alimshukuru mungu kwa kumuacha yeye salama na kumuonyesha kuwa mtu aliyeanzisha naye mahusiano kuwa si mtu bali ni myama mla watu.
Aliunganisha tukio hilo na matukio mbalimbali yatangazwayo kwenye vituo mbalimbali vya matangazo juu ya mauaji ya ajabu yafanyikayo na kiumbe asiyefahamika. Hata maabara za nje ya nchi hii zilishindwa kusoma alama za vidole vya kiumbe huyo.
Hapo aliamini kiumbe atafutwaye na serikali ya Tanzania kwa udi na uvumba ni Sam.
Alishusha pumzi ndeefu na kujaribu kuuvuta usungizi lakini wapi. Hakupata hata lepe la usingizi.
***********************
Palipokaribia kukucha, Sam alinyanyuka na kuanza safari ya kurudi nyumbani. Aliijutia siku ile , maana alijua wazi kuwa Jane kagundua kila kitu. Hivyo usalama wao ulikuwa mdogo yeye na mama yake. Alijiona mkosaji kwa kutomsikiliza mama yake. Aliamini kuwa mama yake alimpenda na alikuwa anaona mbali. Aliujua umuhimu wa kumsikiliza mzazi.
Maana laiti kama angelimsikiliza yasingelitokea yote yale. Hakika njia nzima aliijutia siku ile na kuulaumu moyo wake kwa kuuendekeza kuwa na yule msichana kimapenzi na kutokuwa tayari kufuata maagizo ya mama yake.
Aliamua kupitia mlangoni ili mama yake amuone alivyo na amuombe msamaha. Cha ajabu hakumuona sebuleni wala alipobisha hodi mlangoni kwa mama yake hakuitikiwa. Alijua kuwa mama yake atakua anamtafuta. Aliamua kuwenda kuoga na kubadilsha nguo. Kisha akakaa sebuleni kumsubiri.
Saa nzima ilikatika bila mama yake kurudi. Alipata wasiwasi mkubwa, maana si kawaida ya mama yake. Alijilaumu tena kwa kutokuwa nyumbani. Wazo la kumtafuta na yeye ndio lilichukua nafasi kubwa kwenye ubongo wake.
Aliamua kutoka nje na kuanza kumafuta mamayake.
Katika sayari ya Mars. Huko kulikuwa na mkutano mkubwa wa viongozi wa sayari hiyo juu ya upotevu wa mtoto wa mfalme Josh waliyempoteza Duniani wiki moja iliyopita walipokuwa katika matembezi na utalii.
Ilikuwa huzuni kubwa katika jamii ya viumbe waishio kaatika sayari hiyo. Walikuwa wanampenda sana mfalme wao. Hawakutaka mfalme wao awe na huzuni. Pia walipenda kufanya kitu chochote ambacho mfalme wao aliagiza. Taarifa hizo ziliwanyong’onyesha na kuwakosesha raha kabisa.
“Hakuna mtu asiye fahamu kuwa jamii yetu ya Baikiri imepata pigo kwa kumpoteza mtotowa kiume wiki iliyopita wakati mfalme na malikia walipokuwa safarini sayari ya tatu. Basi tuna tangaza kwa yeyote mwenye damu group O. basi aje ili apewe kazi ya kumtafuta mtoto huyo.” Aliongea msemaji mkuu wa jamii hiyo kwa lugha yao.
Baada ya kuongea machache. Walijitokeza vijana na wakapimwa damu zao. Walitaka waliokuwa na damu Group O kwakua ndiyo pekee wanaoweza kuishi duniani na kuvuta pumzi ya huku. Ni viumbe wachache wanaofanana na binaadamu wanaokuwa na damu Group O katika jamii yao. Waliouwa na Damu hiyo sana sana walikua ni ndege na samaki wa jami hiyo. Hilo zoezi lilifeli kwa kiasi kikubwa na kuwaumiza vichwa viongozi wa jamii ya Baikiri.
Walikata tamaa ya kumpta mtoto huyo na hawakuwa na njia nyingine ya kufanya.
“mfalme, zoezi limeshindikana.” Aliongea msemaji wao ambaye alikuwa anasimamia zoezi zima la upimaji damu.
“haliwezi kushindikana…ina maana mimi nimpoteze mtoto wangu wa pekee kwa kuwa njia hiyo imeshindikana. Nipo tayari hata kuingia na vyombo huko sayari ya tatu na kama vita tupigane. Ilimradi nimpate mwanangu.” Aliongea mfalme kwa jazba. Na msemaji hakuwa na kauli wala kupinga chochote kile.
“kuna watoto wadogo bado wanaendelea na upimaji…labda wakiisha hao tutaangalia. Kama kuivamia dunia au laa.” Aliongeza msemaji na mfalme Josh aliitikia kwa kutingisha kichwa. Msemaji alitoka na kwenda kuendelea kusimamia upimaji.
************************
Baada ya mwendo wa dakika zipatazo ishirini, Sam aliona watu wengi wakiwa wamekusanyika sehemu moja. Wengine wakiwa wameshika vichwa na wengine wakikimbilia eneo la tukio. Mara defender za polisi ziliwasili kuona ni kitu gani kilichotokea. Sam alisogea eneo la tukio na kuwapangua watu kadhaa ili apate kuona kilichojiri maeneo yale.
Hakuweza kuamini kilichotokea. Ilikua ni zaidi pigo lililopiga sawia katika moyo wake. Hakuweza kuangalia tena kwa mara ya pili. Alichoamua ni kukimbia mbio na kurudi nyumbani kwao huku analia. Alilia kwa uchungu huku akiomba msamaha kwa mama yake. Alijitupa na kujiona ana hatia kwa kile kilichotokea. Hakika ilimuuma kumpoteza mama yake wa pekee. Hatimaye mama yake ndiye aliyepoteza maisha kwa ajali ya gari.
Baada ya mwili wa marehemu kutangazwa kila mahali, hakuna ndugu aliyejitokeza. Hivyo akazikwa na kiserikali.
Sam alikaa siku tatu nje ya nyumba waliyopanga. Hata hivyo hiyo siku alitakiwa apate damu. Alienda sehemu na kutega. Alipita mwana mazoezi mida ya saa kumi alfajiri.
Huyo alikua halali ya Sam. Aliporejea katika hali yake ya kawaida, alikaa na kumuwaza mama yake aliyekuwa akimletea damu bila kufanya kazi yoyote.
Siku hiyo alirudi nyumbani kwao mapema na kumkuta Jane nje. Alimuangalia na Jane akaangalia pembeni. Aliamua kumpita na kwenda chumbani kwake. Huko alienda kupanga nguo zake kwenye begi. Alijua kukaa karibu na Jane ni kuhatarisha maisha yake. Alisubiri usiku uingie ndio aanze safari ambayo hata yeye hakuifahamu. Kwa sasa Sam aliona hana umuhimu wa kuendelea kuwa mtu tena maana hakukua na faida. Mama yake mpenzi amekufa na mpenzi wake hamtaki tena.
Kiza kilipochukua nafasi yake, akaona ndio muda sahihi wa kuondoka. Alikusanya vitu vyenye umuhimu kwake na vinavyobebeka kwa maramoja na kutoka nje. Aliviacha vitu vingi vya thamani. Hakutaka hata kufuatilia magari ya yule mama ambaye aliyasaini kwa jina lake kama mrithi wa yule mama.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)