Mtunzi: Hussein O. Molito
SEHEMU YA TANO
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Kiza kilipochukua nafasi yake, akaona ndio muda sahihi wa kuondoka. Alikusanya vitu vyenye umuhimu kwake na vinavyobebeka kwa maramoja na kutoka nje. Aliviacha vitu vingi vya thamani. Hakutaka hata kufuatilia magari ya yule mama ambaye aliyasaini kwa jina lake kama mrithi wa yule mama.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Vyote hakuona umuhimu wake.
Alitoka nje na kukiangalia chumba cha Jane kisha akaanza kuchapa mwendo kuelekea kusikojulikana.
Wazo la kuhama jiji lilimjia kutokana na kuwa gumzo sana hapa Dar. Safari yake ilimfikisha kwenye stesheni ya treni. Huko aliangalia treni zinazosafiri muda huo na kukuta treni ielekeayo Mang`ula ikisubiri masaa kadhaa ianze safari. Alibahatika kupata tiketi na kuingia ndani ya treni na kujituliza.
Muda ulipofika, treni ilipiga honi mara tatu kuashiria kuwa safari inaanza. Taratibu wakaguzi waliingia na kukagua tiketi.
Treni ilianza safari huku watu kadhaa waliokuwa chini wakwapungia mikono ndugu zao waliokuwa wanasafiri na kuwaombea dua.
Treni ilianza safari kwa mwendo wa kinyonga, lakini kila dakika iliyokuja mbele liliongeza spidi.
Wakati huo Sam alikua anaagalia nje tu bila kupepesa macho, lakini fikira na mawazo yake vilikuwa mbaali sana. Alipawaza pia aendapo maana hakuwahi kufika wala kupasikia. Alijua kuwa huko anaenda kuanza maisha mapya.
Masaa yalikatika kwa kasi. Na ilipofikia muda wa watu kula chakula cha mchana, Sam alipitiwa na usingizi mzito ambao alishindwa kuumiliki kama alivyotaka yeye kukaa macho wakati wote kwa usalama wake.
************************
Zoezi la kutafuta mtu mwenye damu inayolingana na watu waishio kwenye sayari ya tatu liliendelea kwa watoto wadogo. Lakini dalili za mafanikia haikuwapo hata kidogo. Hali hiyo ilimnyima raha mfalme. Alijua kuwa itakuwa aibu kwa mfalme kushindwa kumuachia kiti mwanae na ufalme kwenda katika ukoo mwingine.
Gaments za watu wa jamii ya Baikiri zipo tofauti na sisi hapa duniani. Wao walikua wanauwezo wa kuzaa watoto wawili tu. Na huwa inategemea unaanza wa kiume au wa kike. Kwakua mfale alishazaa mtoto wa kiume. Alijua kuwa mtoto atakayezaliwa atakuwa wakike ambaye ni mwiko kuongoza cheo chochote katika jamii yao. Pia toka watu wa jami hiyo walipobuni maswala ya utawala, ni ukoo wao tu ndio walirithishana mpaka alipofikia yeye. Ni wafalme zaidi ya arobaini walishapita mpaka yeye kuwa mfalme. Kwa hiyo kama asingempata mtoto wake, ni dhahiri atakuwa ameuzalilisha ukoo wao.
“mama , mimi nina uhakika kabisa nina damu Group O.”aliongea binti mmoja akiwa nyumbani kwao.
“weee..usirudie tene kusema hivyo. Wanaume wote wamepimwa na hakuna mwenye damu hiyo, wewe mwanamke utaipata wapi??....tena ukome kuongea maneno hayo” aliongea mama yake ni kumfanya yule binti atulie.
Lakini kabla hawajafanya lolote, kikosi cha maaskari karibia kumi wakiongozwa na msemaji mkuu wa jamii ya Baikiri kiliingia bila hodi na kuwafanya yule binti na mama yake kupatwa na hofu. Hawajawahi kufanyiwa vile hata siku moja.
“ni yupi kati ya wale ulimsikia akisema ana damu Group O??” aliuliza msemaji kumuuliza mmoja wa maaskari waliokuwa doria maeneo yale.
“ni sauti ya huyu binti hapa ndio niliisikia mkuu” alijibu yule afande kwa ukakamavu.
“haya mchukueni…na kama anatania basi nikatieni kichwa chake na kukileta ofisini kwangu.”
Hiyo amri iilitolewa na mara moja bila kujiuliza mara mbili. Wale maafande walimfata yule binti na kumbeba juju na kuondoka naye. Mama mtu alibaki analia na hajui nini afanye kumsaidia mtoto wake.
Walimchukua na kuelekea kwenye vipimo. Msemaji mkuu alikaa ofisini lakini aliona majibu yanachelewa. Wakati anatoka ili akaulize ni nini kinachoendelea. Mlangoni akagongnana na askari mmoja wapo akiwa anakimbia kulekea ofisini kwake.
Huku akihema kwa nguvu kiasi cha kushindwa kuongea kutokana na mbio alizotimua. Msemaji alimtuliza na kumwambia ampe taarifa.
“mkuu….yule binti…ana..ana damu..Group O!” aliongea maneno yale na kumfanya msemaji kutoka mbio nay eye kuelekea katia chumba cha vipimo. Huko alijikuta amejaa furaha baada ya kugundua kuwa ni kweli yule binti alikua na damu hiyo. Kwa furaha ya ajabu aliamuru yule binti aletwa kwake.
Maaskari waliomuweka chini ya ulinzi yule binti, walimtoa na kumruhusu aende kwa msemaji mkuu.
Huko msemaji alimkumbatia na kuwaamuru maaskari wake wampatie chakula anachokitaka yule binti nay eye akaanza safari ya kumpelekea taarifa zile nzuri mfalme.
Alipofika alingia na kumkuta mfalme akiwa amejiinamia kwa mawazo.
“nahitaji kuwa peke yangu kwa sasa msemaji mkuu” aliongea mfalme baada ya msemaji kuingia ndani.
“sawa mtukufu mfalme, lakini nina habari njema.” Aliongea msemaji na kumfanya mfalme Josh kunyanyua kichwa chake na kukaa sawa.
“amepatikana mtu mwenye damu Group O????” aliuliza kwa hamaki mfalme.
“ndio mkuu…lakini mtu mwenyewe ni mwanamke. Pia ni mtoto sana.” Aliongea msemaji na kumuangalia mfalme ambaye muda wote alikuwa hawataki wanawake washirikishwe katika jambo lolote. Daima aliamini mwanamke hana faida kwake na aliwadharau kwa kila kitu. Kuanzia maumbile mpaka akili. Hata malikia mwenyewe hakua na usemi wala ushauri wowote kwa mfalme.
“haina shida…mlete sasa hivi nimuone.” Aliongea mfalme na kutabasamu.
Hakika lile tabasamu liliongezeka maradufu baada ya kumuona yule binti akiletwa mule ndani.
“ heshima yako mtukufu mfalme Josh” alisalimia yule binti na kuinama kuashiria kumuheshimu mfalme.
“unaitwa nani binti yangu.?” Aliuliza mfalme Josh bila kuitikia salamu na kuonyesha furaha yake wazi bila kificho.
“naitwa HAIBA” alijibu yule msichana na kuinamisha sura yake chini.
“Haiba…umenifanya niamini kuwa si kila kitu mwanaume anaweza kufanya…wewe ni shujaa wangu wa kwanza wa kike. Upo tayari kufanya kazi yangu??” aliuliza mfalme na kumuangalia Haiba kwa umakini mkubwa..
“hata leo hii nipo tayari mfalme.” Alijibu Haiba kishujaa na kwa kujiamini vya kutosha.
.
Ujasiri wa Haiba ulizidi kumtoa hofu mfalme Josh kuwa kazi yake inaweza kufanikiwa kwa asilimia zote.
Kesho yake uliitwa mkutano kwa wakazi woote wa Baikiri. Watu wote walihudhuria na kukaa katika nafasi waliyoitumia kwa ajili ya mikutano mikubwa.
Wengi wao hawakujua walichoitiwa na mfalme, hivyo waliwahi mapema kwakua walijawa na dukuduku la kutaka kujua jambo lililowakusanya pale.
Muda ulipofika, mfalme alipanda na kumtabulsha Haiba kuwa ndiye shujaa wa jamii yao kwa kuwa na damu Group O peke yake. Pia aliwaambia kuwa safari ya kuelekea duniani itaanza kesho yake asubuhi. Baada ya hapo aliwaruhusu watu warudi makwao.
Hakika waliishiwa nguvu na kuona maajabu kwa mfalme kukubali kazi yake kufanywa na mwanamke.
“kwa heri mama” hayo maneno aliyaongea Haiba baada ya kumkumbatia mama yake. Huku wote wakiwa wanalia. Waliachiana mikono na Haiba akapanda chombo maalumu kwa ajili ya kuja huku duniani kumtafuta mtoto wa mfalme Josh-
Chombo hicho chenye spidi zaidi ya rocket, kilizidi kuambaa sayari kadhaa na kuifikia dunia kwa kasi ya ajabu.
Kilisoma alama za mtoto wa mfalme alipodondokea. Na majibu yakaja kuwa alidondoka Tanzania katika jiji la Dar-es-salaam.
Kwa muongozo huo. Ndipo chombo hicho kikatua maeneo ya karibu na club maisha. Kwa kua ilikua ni usiku na pilika pilika hazikuwapo, hakuna aliyekiona chombo hicho wakati kinamshusha mrembo huyo.
Kwa haraka chombo kilipaa na kupotelea hewani baada ya kumshusha Haiba.
Mazingira na hewa ya huku vilikuwa kivutio kikubwa kwa Haiba. Moja kwa moja akaaza kusogea sehemu zenye kelele alizokua akizisikia.
Alivuka barabara kwa madaha bila kuangalia magari. Sana sana aliyashangaa tu na kutabasamu peke yake. Kila aliyemuona hakuridhika kumuangalia mara moja. Maana alikua na uzuri wa kutisha. Nywele zake zilikua ndefu mpaka kwenye makalio. Pia zilikua nyeusi kupindukia. Pia alikua na weupe unaong`aa kama mwarabu lakini shape yake ilikua ya kibantu. Kiuno number 6 na hipsi zilizojichonga kama glass ya wine. Vijisima vidogo masavuni vilionekana dhahiri pale alipokuwa akitabasamu. Hakika alikuwa wa pekee. Hata nguo alizo vaa zilinakshiwa na ngozi inayofanana na nyoka lakini yenyewe ilikuwa inangaa bila kutoa muwako.
Safari yake ilimpelekea kufika disco na kuingia ndani bila kudaiwa tiketi kutokana na alivyowapagawisha watu wa geti kuu.
Aliingia ndani na kuanza kutalii. Huku akiwa anatikisa kichwa kwa mdundo na nyimbo nzuri anazoendelea kuzisikia akiwa humo.
Alitafuta siti na kukaa. Ndani kulikua na wahudumu wakizunguka na kugawa vinywaji. Aliangalia watu na kuwaona wanakunywa. Na yeye akachukua kimoja na kuanza kunywa. Alivutiwa na ladha yake na kuagiza kingine. Alifanya hivyo mara kadhaa mpaka alipoanza kulewa
Aliangalia watu waliokuwa kwenye Dancing floo wakiwa wanacheza wawili wawili. Alinyanyuka na kumfuata kijana mmoja aliyekuwa pembeni yake na kuchukua bila kumuomba na kwenda naye kujumuika na wengine na kucheza naye.
Huyo kijana alijiona ana bahati ya pekee. Maana msichana mrembo kama huyo kumzimikia na kumtaka acheze naye, alijiona ana bahati sana. Basi bila kusita aliingia kati na kucheza kwa juhudi zake zote huku akijaribu kumchombeza kwa maneno.
“naitwa Abby, sijui mwenzangu unaitwa nani?” aliongea yule mvulana kwa sauti kidogo kutokana na mziki mnene unaoendelea kukita spika za ukumbi huo.
Haiba hakua anaelewa Kiswahili kutokana na lugha yao wanayoongea. Ila alikua na kifaa maalumu alichowekewa. Kilikua kinatafsiri kwa haraka na kwa muda huo huo kilikua kinatoa sauti ya Haiba kwa Kiswahili pindi atakapojibu.
“naitwa Haiba”alijibu na kuendelea kucheza. Abby alitumia ujuzi mwingi kwa kumgeuza na kumzungusha Haiba na kumkumbatia bila Haiba kusema lolote wala kumkataza. Alitabasamu na kuuliza.
“umechoka?”
“bado” alijibu Haiba huku akitabasamu.
Harufu nzuri ya marashi ilizidi kumchanganya Abby na kutamani aondoke naye. Alijiamini kuwa huyo binti kalewa hivyo hata kwa nguvu angeweza kutimiza haja zake.
Baada ya kucheza nyimbo kadhaa, Haiba na Abby waliketi na kuendelea kukata mtungi. Baadae walitoka mle ukumbini . Abby alimuingiza kwenye gari na kwenda naye hotelini. Alilipia chumba na kuingia na Haiba. Wakati huo Haiba alikua hajitambui sawa sawa kwa kilevi alichozidishiwa na Abby.
Abby alimlaza Haiba kitandani nay eye akatoka nje ya ile hotel na kuagiza chakula. Yeye hakua amekunywa sana. Alitambua kila kitu anachokitenda. Alirudi taratibu na kuanza kula huku akiutathmini mwili mchanga wa haiba.
Miaka yake ni kumi na sita. Lakini huku duniani alifanana na mabinti wa miaka ishirini na mbili.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)