THE STRANGER (7)

0

SEHEMU YA SABA
TULIPOISHIA...
“nakuamini sana.’Aliibu Sam

“nakuomba geuka nyuma…nitahesabu mpaka tatu kisha utageuka na kuniangalia” alisema Jane na Sam bila kubisha akageuka nyuma na kumruhusu afanye anachokusudia kufanya.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Jane alihesabu kuanzia moja hadi tatu kama alivyomuahidi Sam kuwa atafanya hivyo.

Sam aligeuka na kushtuka alichokiona.

“JANE???.....WHY???”

Ulikua mshtuko mkubwa baada ya kumuona Jane kajichana na kisu maeneo ya shingooni. Damu zilianza kumtiririka taratibu .

“leo nitajua kama unanipenda au hunipendi…nipo tayari kwa lolote Sam”

Aliongea Jane na kumuangalia Sam ambae muda huo alishaanza kutetemeka na nguvu kumuisha. Midomo ya Sam ilitamani kuongea lakini ilishindwa kutokana na mitetemo aliyonayo muda huo. Macho yalianza kubadilika rangi na kufuatiwa na ngozi yoote kuwa ya kijani. Manyoya yakaaza kumtoka kwa kasi. Baada ya hapo muungurumo mkali ukasikika.

Jane muda wote huo alikuwa kasimama kijasiri akimshuhudia Sam anavyobadilika badilika. Hakuogopa wala kupatwa na hofu ya kutafunwa. Zaidi alitaka kukaa macho kushuhudia kila kitu akifanyacho Sam.

Sam alibadilika kabisa na kuwa mnyama wa ajabu. Alianza kuhangaika kwa kumzunguka Jane huku akiunguruma. Mara akaanza kujibamiza ukutani kwa nguvu. Alianza kujitupa tupa huku na huko katika kile chumba. Baada ya dakika kadhaa alikua amejiumiza vya kutosha na kuanza kutokwa na damu. Sam alijipangusa damu yake na kuilamba. Hapo hapo akabadilika na kuwa mtu tena. Lakini aliiumia vibaya hususani usoni.

Jane alishusha pumzi ndefu na kumsogelea mpenzi wake huyo. Alimpakata na kukilaza kichwa cha Sam kifuani kwake.

Mikiki ile ilimfanya Sam apoteze nguvu kabisa. Hivyo alikua kama mgonjwa pale chini. Alikua na njaa ya ajabu na hakuwa tayari kumla mpenzi wake.

“pole mpenzi wangu…nimeamini hata ukibadilika huwezi kunila na unanipenda kutoka moyoni.” Aliongea Jane na kumuangalia Sam aliyekuwa hoi pale chini.

Alijua kuwa Sam muda ule alikua na njaa sana. Hivyo alitafakari jinsi ya kupata chakula cha Sam usiku ule. Alikata shauri na kutoka nje. Alimkuta muhudumu aliyekuwa mapokezi peke yake akisinzia. Alimfuata na kumuamsha.

“samahani kaka, naomba msaada wako.” Aliongea Jane baada ya kumtikisa yule muhudumu aliyejawa na usingizi.

“shida gani dada.” Aliongea yule muhudumu kwa sauti kavu yenye usingizi.

“naomba uje chumbani kwetu.” Alingea Jane na kumuangalia yule muhudumu ambaye alikuwa anafikicha macho yake akijaribu kuuondoa usingizi.

“poa, nakuja “

Aliongea yule muhudumu na Jane akaondoka . haikupita hata dakika moja, yule muhudumu akawa amefika na kugonga kwenye chumba alichoelekezwa. Jane alifungua na kumruhusu yule muhudumu aingie ndani. Alipoingia tu, jane alichomoa kisu alichokificha kiunoni na kumchoma nacho yule muhudumu shingoni. Damu nyingi zilitoka na kumrukia Sam. Hapo hapo akapata nguvu na kurukia yule muhudumu na kuanza kufyonza damu yake kwa fujo.

*********************

Usingizi mkali uliompata Haiba ulikuja na ndoto juu ya Sam. Alijiona yupo karibu nae na wanakula raha katika maeneo mbali mbali ya sayari yao. Pia alivuta picha atakapopokelewa kishujaa atakaporudi na Sam. Kubwa zaidi aliona anafunga ndoa na Sam. Alishtuka kutoka usingizini na kukaa. Aliitafakari ile ndoto na kwenda kuchukua ule mkufu na kumuangalia Sam tena kwa umakini. Alijikuta moyo wake unasuuzika baada ya kumuona.

Alitoka na kwenda kuoga. Aliporudi alivaa nguo zake zilezile na kutoka mule hotelini.

Alitoka nje na kukodi tax iliyompeleka mpaka kariakoo. Alishuka na kuendelea kuangalia vitu mbali mbali ikiwemo msongamano wa watu wakiwa katika shughuli zao. Baada ya mwendo wa dakika kadhaa. Kwa mbaali alimuona mtu akiwa amekaa sehemu peke yake huku akiwa amejiinamia.

Alishawishika kumsogelea na kumshika begani.

“habari” alisalimia Haiba baada ya yule kaka kumuangalia. Alikua amejaa huzuni na macho yamemvimba kwa ajili ya kulia muda mrefu.

“salama tu”

Alijibu kiupole yule kaka na kufuta machozi yake.

“nini tatizo?” aliuliza Haiba na kumuangalia yule kaka usoni.

“we acha tu dada yangu.” Aliongea na kumuonyesha wazi kuwa yaliyomkuta ni mazito.

“niambie tu..labda naweza kukusaidia.” Alinga`ng`ania Haiba.

“dada yangu yaliyonikuta ni mazito mpaka natamani kuiaga dunia. Yaani najuta hata kwanini nimezaliwa.” Aliongea yule mvulana na kumuangalia Haiba.

“ yaani hapa nilipo nimefukuzwa kwenye nyumba niliyopanga na vitu vyangu vipo nje. Mke wangu kanikimbia na kaniachia watoto ambao mpaka sasa sijui nitaishi nao vipi. Sina kazi, kibanda changu kimebomolewa na mgambo na sina hata shilingi mfukoni mwangu. Sijui hata siku ya leo itaishaje maana hatujala na sijui nitawapa nini watoto wangu.” Aliongea yule kijana na kumuangalia Haiba aliyeonyesha wazi kuwa na nia ya kumsaidia.

“watoto wako wapi?” aliuliza haiba na kukaa karibu yake.

“kuna sehemu nimewaambia wanisubiri ili niwatafutie chakula.” Alijibu yule kijana.

Haiba alimwambie ampeleke mpaka kwa wale watoto. Yule kijana alimpeleka na kuwachukua wote na kurudi nao hotelini. Aliwanunulia vyakula walivyohitaji na kuhakikisha wameshiba.

Baada ya hapo, aliwapeleka shoping na kuwanunulia nguo wale watoto. Kisha akaenda kuwalipia kodi ya miezi yote waliyokuwa wanadaiwa na kuilipia kodi ya mwaka mzima.

Aliyafanya yote hayo na kumfanya yule kijana amshangae sana. Alijua yule hakuwa mtu wa kawaida, bali ni malaika aliyetumwa na mungu aje ayang`arishe maisha yake.

“unampenda sana mkeo?” aliuliza Haiba baada ya kumaliza kuingiza vitu ndani.

“yaani sikufichi dada yangu. Mi nampenda sana, hata yeye ananipenda sema tu kachoka maisha ya dhiki tunayoishi.” Aliongea yule kijana. Haiba alimuangalia kwa huruma na kumpooza.

“usijali, atarudi na mtaishi kama zamani.” Aliongea Haiba na kumshika yule kijana bega.

“hawezi kurudi. Nasikia amepata mwanaume mwingine mwenye hela na gari..atanikumbuka mimi kapuku?” aliongea yule kijana na kuonyesha ishara ya kukata tama.

“una picha yake?” aliuliza Haiba kuonyesha kuwa bado anaamini kuna uwezekano wa kumrudishia mpenzi wake.

“nina album nzima toka tunaoana” aliongea yule kijana na kuliendea kabati na kutoa album chakavu na kumletea Haiba.

“hizi hapa.” Aliongea yule kijana baada ya kumkabidhi Haiba.

Haiba aliitalii album nzima na kurudi kati na kuchagua picha moja.

“unaweza kuniruhusu niondoke nayo?” aliomba Haiba.

“hamna shida dada, yaani hata Album nzima ukitaka mi nitakupa.” Aliongea yule kijana. Haiba aliichukua ile picha na kuiingiza kwenye begi lake.

“naomba niwaache maana muda umeenda sana. Nitakuja kesho kuwaona.” Aliaga haiba na kutoa noti za elfu kumi tatu na kumkabidhi yule kijana.

“nashukuru sana dada yangu..mungu atakulipa kwa wema wako.” Aliongea yue kijana baada ya kuzipokea zile hela.

“halafu tumezunguka sana leo lakini hatukupata hata nafasi ya kuulizana majina.” Aliongea Haiba.

“kweli dada yangu, mimi naitwa Bakari.” Alijitambulisha yule kijana.

“naitwa Haiba.” Alijitambulisha kiufupi na kuondoka zake.

Alirudi hotelini na kukaa kitandani. Aliwaza aanzie wapi kuifanya kazi ya Bakari.

****************************

Baada ya ufanya mauaji yale ya kutisha, Sam na Jane waliamua kuondoka haraka na kutafuta nyumba nyingine ya kulala. Palipokucha walishauriana warudi Dar kwakua walikua wanakaribia kuishiwa hela walizokuwa nazo.

Walipanda treni na kurudi Dar. Walipofika maeneoo yao ya kujidai, walitafuta chumba kwa ajili ya mapumziko.

“nimeumiss sana mwili wako.” Aliongea Sam baada ya kumsogelea na Jane.

“realy?” aliuliza Jane na kuyarembua macho yake makubwa yaliyoongeza uzuri wake.

Sam hakujibu kitu zaidi ya kuonyesha vitendo. Alisomgelea na kumshika baadhi ya sehemu za mwili wa Jane. Alitumia dakika chache kumlainisha Jane. Maana kila alipotalii kulikua pana ashki kwa Jane.

Alitambua udhifu wa Jane kwakua ilikua ni mara ya pili kukutana nae kimwili. Walianza game na kumaliza kila mmoja akionyesha ufundi wake kwa mwenzie. Kila mmoja aliridhika kutoka rohoni na kuamua kulala.

Asubuhi ya siku ya pili yake, waliamka na Jane akaenda kupata kifungua kinywa. Baada ya kumaliza wakaamua kuondoa.

Walipokuwa barabarani, kwa mbaali walimuona mama yake Jane. Kabla hawajajificha, tayari mama yake Jane alishawaona.

“nyie mbwa, nisubirini hapo hapo.!” Aliongea mama yake Jane na kuanza kuwafata kwa spidi.

“mamaaaaaaaaaaa”

ilikua Sauti ya Jane ikipayuka kwa uchungu. Ni baada ya kushudia mama yake kugongwa na boda boda na kumrusha mbali na alipokuwepo.

Jane alianza kumkimbiza dereva wa boda boda aliyemgonga mama yake na kumuacha Sam akiwa pale . Alimkimbiza kwa muda bila mafanikio. Alirudi huku akilia. Alipofika pale alipokuwa mama yake, alipigwa na bumbuwazi.

“SAM??”

Alishindwa kuamini baada ya kumuona Sam kabadilika na tayari alishaanza kumnyonya mama yake Damu.

Sam alinyanyua sura na kumtazama Jane kwa kile alichokiona. Alinyanyuka na kurudi nyuma hatua kadhaa. Akageuka nyuma na kukimbia eneo lile.

Jane alimkimbilia mama yake aliyekuwa hoi pale chini.

“mamaaaa” aliita Jane huku akimtikisa mama yake aliyekuwa akipumua kwa shida huku damu zikimtoka kwa wingi kwa kua lile eneo lilikua tulivu, hakukua na mtu aliyemuona akipita maeneo yale. Alimuacha mama yake na kwenda barabarani na kuomba msaada.

“bado mzima?” aliuliza dereva wa gari alilolisimamisha Jane.

“ndio..naomba nisaidie kuokoa maisha ya mama yangu”.

Bila kuchelewa walimuingiza kwenye gari na kumuwahisha hospitali ya karibu. Walipofika walipokelewa na mama yake Jane alikimbizwa I C U. jane alikaa nje baada ya kutoruhusiwa kuingia ndani.

Baada ya masaa mawili, alitoka daktari aliyekuwa mule ICU.

“Vipi hali ya mgonjwa dokta.” Alinyanyuka Jane na kumsimamisha yule daktari.

“hakuna ndugu yeyote yule wa kiume aliyekuja?” aliuliza yule Daktari huku akikwepa kumuangalia usoni Jane.

“ni mimi pekee ndiye ninayeishi naye..ni mama yangu. Niambie tu daktari usinifiche.” Aliongea Jane huku akiwa na wasiwasi mkubwa.

“naomba uwe na kifua kwa hiki nitakachokueleza.” Aliongea daktari na kushusha kidogo miwani yake aliyovaa.

“pole binti. Tumejaribu kwa uwezo wetu wote, lakini hatukufanikiwa kuokoa maisha ya mama yako…tayari ameshafariki.” Aliongea daktari huku akijaribu kumpooza Jane.

“mamaa, mama yangu mie” alilia Jane kwa sauti kubwa. Daktari alijitahidi kumtuliza Jane lakini wapi. Lilikuwa swala gumu kuliamini na kulipokea kwa Jane.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)