MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (24)

0

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
TULIPOISHIA...
Alikuwa akimuona mwanae kama vile anamuona Sam, kwa jinsi anavyompenda mume wa DADA yake (Sam), ilitosha kabisa kufurahishwa na uufanano wa mwanae kwa Sam.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
“Bebiiii”
“Ma..ma…ma…ma”
Kitoto cha verity kilikuwa kinamfwata mama yake huku kinaita kwa kukatakata maneno huku kinamchekea mama yake
Verity nae alikuwa amejiachia mpaka jino la mwisho wakati mtoto wake anamshangilia, sura na muonekano wa Sam vilikuwa juu ya huyu mtoto.
“Bebiiiii…njoo bebiiiiii….waooooooooh”
Verity alimkumbatia mwanae.
“Bebiiii umefanana na baba yakoooooo, hadi raha”
Wakati Verity anamwambia mtoto hivi mtoto nae akaanza kutamka….
“Ba…ba….ba….ba….”
Gwakisa alikuwa amefika nyumbani anamuangalia mkewe ambaye anacheza na mtoto pasi na wao kumuona.

Alikuwa anafurahia jinsi mkewe anavyocheza na mtoto lakini ghafla alibadili mudi baada ya kusikia verity akimmwambia mtoto amefanana na Baba yake hadi raha.
Hapa Gwakisa alikuwa anajiuliza ni baba yupi huyo anayefanana na mtoto wakati yeye hafanani nae hata kidogo.
Ghafla meseji iliingia kwenye simu ya Verity ambaye aliichukua asome ile meseji
“Nina maongezi nawewe”
Verity aliisoma hii meseji kutoka kwa Sam, wakati anataka kuijibu alicheki pembeni na kukutana na sura ya Gwakisa akiwa ameegemea mlango.
“Baba mbona mkimyakimya”
“Kwni hapa si nyumbani kwangu”
“Haya karibu baba”
“TOTOOOOOOO…umemuona baba…njoo umsalimie”
Verity alikuwa anamvutia mtoto kwa baba yake (Gwakisa)
“Huyu mtoto nimefanana nae eenh?” gwakisa aliuliza
“Mh hata hujafanana nae sana, labda pua tu mimi ndio nimefanana nae” verity alijibu bila kujua kuwa anategwa.

“Si nimekusikia sasa hivi hapo unamwambia amefanana na baba yake hadi raha, alafu saivi unasema sijafanana nae ”
“Mh umenisikia sangapi, mimi sijasema hivyo”
Hapa Gwakisa alizidi kuchanganyikiwa?
“Hujasema hivyo wakati nimekusikia? Verity kuna nini kinaendelea”
“Aaaaah si ndio hiyo pua niliyokwambia umefanana nae”
“Yani Pua ndio useme nimefanana nae hadi raha?”
“Ndio, kwani mbona unauliza sana, una wasiwasi juu ya huyu mtoto”
“Sina wasiwasi wala usijali”
Tangia siku hiyo Gwakisa alikuwa amejenga picha mbaya sana kichwani mwake kuhusu Verity na Yule mtoto.
Kuna roho la mauaji lilikuwa limeanza kuisonga akili yake na lilikuwa linamtuma kufanya kitu kibaya.
……………………………
Rafiki alikuwa anawaza mengi sana kichwani mwake, kitendo kile alichokuwa anakiona kwa mme wake na mdogo wake kilikuwa kinampa wakati mgumu sana.
“Vipi una maongezi gani na Verity?”
“Kwani nimesema nina maongezi nae, yanini sasa?”
“Mme wangu…nimekuja mda tu na nimekuona unavyomuangalia mtoto wa mdogo wangu kwenye picha kisha ukamtumia verity meseji kuwa una maongezi nae, sasa unakataa nini?”
“AHHH kwahiyo unanichunguza? Unaanza kuniendesha kwasababu nimeambiwa nina matatizo si ndio?” sam alikuja juu.
“Usijali Sam, matatizo yako yanatibika ila unatakiwa uwe na subira, siwezi kukuendesha wewe ni mume wangu”
Ukweli ni kwamba Rafiki alikuwa amesoma saikolojia ya mume wake na kuona kuwa haiku sawa hakutaka kubishana nae na aliona njia nzuri ni kwenda nae polepole kwa kumbembeleza asijisikie vibaya.

Alimuendea pale alipo akamkumbatia na kuanza kumsugua sugua mgongoni ambapo Sam alianza kuwa normal na hata ile tempa ikawa imeshuka.
Rafiki alichukua simu ya Sam na kufungua picha za Yule mtoto na kuanza kumtania mme wake..
“Mh mume wangu umefanana na huyu mtoto?”
“Acha bhana sasa nifanane nae kwani ni ndugu yangu?”
“Lbda wewe ni baba yake?”
“Acha utani bhana, Verity si shemeji yangu, kwanza umeshaambiwa mimi nina matatizo”
“Sasa kama matatizo uliyapata baada ya kutungisha mimba, kwani si ulipigwa ukiwa tayarii ushatembea na Verity?”
Sam alipigwa na butwaa la mwaka kwani katika akili yake alikuwa hata siku moja hajawahi kudhani kuwa Rafiki anajua kuwa aliwahi kutembea na Verity. Alijua siri hii anaijua Verity na baba yake tu kumbe Rafiki alikuwa anajua kila kitu.
“Ahhhh….AHHHH acha utani bwana”
Sam alishikwa na kigugumizi kabisa na kushindwa kuongea jambo la maana.
“Tuachane nayo tuongelee yetu, ila chondechonde usije ukaharibu ndoa ya mdogo wangu”
Sam alitaka ajibu neon lakini Rafiki alimuwahi na kumnyonya mdomo na kuanza kufanya yao hadi walipochoka na kuamua kulala.
………………………………………….
Asubuhi na mapema Verity alichukua simu yake na kutaka kumpigia Sam, simu iliita kisha Sam akapokea
“Haloo”
“Mambo vip”
“Poa, umeniambia una mazungumzo na mimi”
“Ndio ni kuhusu huyo mtoto”
“Ana nini, si tulikubaliana hutamuulizia”
“Sawa Verity, hivi nikuulize kitu kimoja”
“Uliza… ”
“Mbona hospitali nimembiwa sina uwezo wa kuzaa alafu nawewe unaniambia mtoto ni wangu?”
Wakati Verity anataka ajibu alikutana na mumewe uso kwa uso akiwa anamuangalia
“Haloo, halooo, halooooo” Sam aliendelea bila kujua kuwa mwenzake yuko kimya kwasababu kataitika.
…………………………
Rafiki alitoka nje baada ya kumuona mumewe anaongea na simu kwa kujiibiza, aligundua kuwa Sam alikuwa anaongea na Verity.
Roho ilimuuma kiasi ambacho aliona anaweza asiweze kuvumilia…akiwa anawaza simu yake iliingia meseji, alipoifungua akakutana na meseji ya Dr Kelvin… “Nimekumiss mrembo”
Rafiki alifikiria ile meseji na kujikuta akivuta kumbukumbu nyuma na kisha akaishia kushusha pumzi kwa nguvu na kufuta ile meseji.
………………………
Gwakisa alikuwa anaemia mno moyoni, na Verity alionekana kabisa hajali….
Gwakisa aliingia kwenye kabati la nguo na kufungua chemba yake akaitazama Bastola yake kisha akaiweka vizuri, pepo la kuua lilikuwa limekaribia kabisa na vitendo, hakupenda kudharaulika…………

Maisha ndani ya Nairobi yalikuwa yakienda kwa kasi sana, Rafiki alikaa na mme wake kwa muda wa wiki moja huku Sam akijitahidi kumtembeza maeneo mazuri nay a starehe yaliyojazana kwenye jiji hili la Nairobi.
Rafiki alikuwa na furaha na aliionyesha usoni lakini ndani ya moyo wake alikuwa na kinyongo kinamtafuna.
Uhusiano kati ya Sam na Verity ulikuwa unamtesa sana, alijua baada ya ndoa kila kitu kitakuwa kimekaa sawa na Sam n verity watasahauliana lakini anashuhudia uhusiano ukiendelea kwa kupigiana simu na mawasiliano ya siri kuonyesha kuwa kuna jambo kati ya hawa watu wawili linaendelea.
Sam nae alikuwa anajaribu kuwaza kwanini Verity amemkatia simu ia alipokumbuka kuwa Verity ni mke wa mtu aliamua kuacha na kusubiri endapo Verity angemtafuta mwenyewe.
Siku ya siku ilifika Rfaiki akapakia kwenye ndege na safari ya kurudi dar es salaam ilikuwa imewadia. Kwa kuwa Dar es Salaam hadi Nairobi ilikuwa ni takribani lisaa limoja tu na dakika kadhaa haikumchukua muda mrefu sana Rafiki kufika.

Alifika na kuunganisha kwa basi lililokuwa linaenda Mbeya siku hiyo hiyo, akiwa ndani ya basi alikuwa akiwaza mambo mengi sana lakini mengi yakiwa yanaihusu ndoa yake.
Alikuwa anampenda sana mme wake na alitamani awe nae muda wote ili yale yanayowahusu wayajenge pamoja.
Alitamani sana awe na mtoto, alitamani amzalie mume wake ili atimize majukumu yake ya ndoa lakini ndio hivyo tena, wakati mwingine alijikuta akimchukia mdogo wake kwa kudhani kuwa huenda anamdharau kwakuwa yeye amezaa na Sam ikiwa yeye mwenye mume ameshindwa kumzalia mume wake.

Akiwa anawaza kumbukumbu zake zilienda mpaka kwa Dr Kelvin na kuamua kumtumia meseji kwani tangu alipotumiwa meseji na Dr huyo hakuwahi kuijibu.
“pole na kazi Dr. nadhani uko mzima”
Dr kelvin akiwa kazini kwake hakuamini kuona meseji kutoka kwa mwanamke ambaye toka aanze kazi ya udaktari huku akiwa na tabia ya kutembea na wagonjwa hakuwahi kukutana na mwanamke aina ya Rafiki. Alikuwa anavutiwa nae mno, alitamani sana alale nae hata mara mia moja ikiwezekana awe wake kabisa japo ni mke wa mtu tayari.
Kitendo cha kutumiwa ile sms kilimfanya auone ushindi ukikaribia mlangoni kwake.
Aliacha kila kitu na kuchukua simu kwa lengo la kumpigia kabisa Rafiki.
………………………………
Sam alikuwa kwenye kituo cha mafunzo ya kiusalama ambapo pamoja na mambo mengine lakini alikuwa anasomea masuala ya teknolojia na upelelezi jeshini.
Hizi ni kozi ambazo walikuwa wanasoma watu wachache ambao huwa wanalengwa kwa ajili ya vyeo vikubwa kwenye jeshi la Polisi.
Pamoja na uzuri wa hii kozi lakini Sam alikuwa anateswa na masharti ya dokta kwamba asifanye kazi ngumu sana hadi atibiwe tatizo lake la kutokutungisha mimba(infertility).
“Heeey…njoo hapa”
Sam aliitwa na kamanda wa mafunzo…
“Kwanini hujaenda mazoezini”
“Najisikia kuumwa mkuu”
“Pumbaaav….haya lala chini”
Sama alibidi alale, ahakukuwa na namna ya kujibishana na mkuu wake.

“Roll mpaka kuleeeee kwenye gereji”
Sam ilibiidi aanze kujibiringisha hapo chini mpaka akafika kwenye gereji ya hapa chuoni na kuamriwa ageuze tena.
Zoezi hilo lilipoisha alikuwa amechafuka kama aliyekuwa amezikwa.
“Miguu juu kichwa chini tembea na huu ukuta uende na kurudi”
Hili ni zoezi lingine ambalo Sam alikuwa analia nalo akiwa anazunguka kwenye ukuta kwa kutumia mikono huku miguu ikining’inia juu ya ukuta,
Mateso aliyokuwa anayapata alijiona wazi akiwa anaharibu masharti ya daktari, hakuwa na namna ilibidi aendelee na zoezi lake.

Alihenyeshwa kwa zaidi ya masaa mawili ndipo akaachiwa na kwenda kujumuika na wenzake.
Siku ya kesho yake aliamua kumfwata mkuu wa mafunzo na kumueleza matatizo yake akiambatanisha na vielelezo kutoka kwa daktari wa Kenyatta Hospital.
“Wewe Mtizedi shenzi sana…umewahi sikia askaria akililia kuzaa?” sam alikuwa anaambiwa maneno ambayo hakuyatarajia.
“Kwa kukupa tu taarifa, hawa wote hapa wanaowafundisha hakuna aliyepata zaa mtoto, hakuna aliyeoa bibi” askari huyu alikuwa akiongea lafudhi ya Kikenya akimwambia Sam kuwa eti sio lazima Askari azae.

“Wewe nenda fanya research yako alafu uniambie uliwahi ona komandoo wangapi wakizaa watoto?”
Sam kwa wakati mwingine alikutana na mtihani mwingine. Nikweli kuwa mazoezi yale magumu sana waliyokuwa wanapewa ilikuwa sio rahisi kuwa na uwezo wa kupata watoto, yalikuwa yanaharibusana mfumo wa uzazi wa awe mwanamume ama hata mwanamke.
Sam alijipa moyo kwamba whatever ili mradi tayari ana mtoto wake mmoja.
“Nitahakikisha namchukua mwanangu kutoka kwa Verity, sitajali chochote hata kama ni DNA tutapima, siwezi kupoteza damu yangu” sam alikuwa anawaza kimya kimya.
………………………………………
Verity alikuwa anashangazwa sana na mabadiliko ya mume wake Gwakisa, upendo uliongezeka mara dufu.
Kila siku jioni ilikuwa ni lazima watoke wakatembee wale na kunywa kwa furaha
Kila Gwakisa alipopata nafasi ya kutoka basi alikuwa anawaletea zawadi nyingi sana ikiwemo nguo na vitu vingine vingi tu vya kupendeza.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)