MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (28)

0

SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE
TULIPOISHIA...
Waliendelea mpaka mpakani na Kongo wakakutana na watu wengine waliowakabidhi mzigo na kurudi nao mpaka Mbeya mjini kisha wakaagana kwa lengo kila mtu aende kwake baada ya kufikisha mzigo panapotakiwa.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
‘ngoja kidogo Gwakisa’

Gwakisa alitulia asikilize anachoambiwa lakini cha ajabu alifwatwa mdomoni na kupewa denda ambalo liliibua tena hisia zake ambapo alianza kupitisha mikono yake kwenye maziwa ya Yule dada.

“Subiri wewe hapa njiani ” aliambiwa Gwakisa na kutoa mikono yako,
“Nenda kwako lakini utakachokutana nacho usishtuke, kama utakuwa na maswali utaniuliza siku tukikutana ila usishtuke kila kitu ni salama tu na hakuna kibaya”

Gwakisa alianza kuogopa lakini akiwa anawaza Tayri Yule dada alishashuka na kutokomea zake.

Kwa hofu Gwakisa aliendesha Gari mpaka kwake na kukuta kumefungwa na hakuna mtu.

Alichukua simu yake ampigie mkewe lakini aligundua kuwa simu yake ilikuwa imezimwa, alijua kabisa walioizima ni wale jamaa kule alikotoka.

Aliiwasha na kumtafuta mke wake ambapo alipokelewa na kilio kikali.
“Nini wewe unalia nini” aliuliza Gwakisa
“Mtoto wetu amepotea mume wangu uuuuuwiiiii, mamamamaaaaaaaaaa, mamaaaa mimi mwanangu jamaniiiiii” alikuwa analia Verity

Hapo hapo Gwakisa aliwahi kituo cha Polisi ambapo alimkuta mke wake akiwa na wazazi wake wakiwa wanatoa maelezo pale na tayari taarifa zilishasambazwa kila sehemu kwenye vituo mbalimbali ili utafutwaji uanze wakifwatia maelezo ya wahusika anaowashuku Verity.

Gwakisa hakuelewa afanye nini kwani akili yake ilishawawaza wale jamaa zake lakini akawa anashindwa kuelewa kuwa ni kwanini wamchukue Yule mtoto, yeye anahusiana nini….

Akili yake ilimpa mawazo kwamba huenda wale watu ni washirikina na wanataka wakamtoe Yule mtoto kafara.
Roho ilikuwa inamuuma sana, japo Yule mtoto sio wake lakini alikuwa hana mpango wa kumdhuru, mpango wake ulikuwa ni mwingine kabisa na sio kumdhuru.

Roho ya kibinadamu na kiulezi ilikuwa inamuuma sana, alimfwata mke wake na kumnyanyua pale chini akasogea kando na kumwambia….

“Usilie mke wangu, nitapambana na mtu yeyote mpaka mtoto apatikane.”

……………………………..

Sam alikuwa njiani kurudi Tanzania kwa kutumia usafiri wa anga, ndani ya lisaa limoja tayari alikuwa Dar es salaam na mawazo yake yote yalikuwa kwa mwanae.
Alipanga kuwa akifika tu ni lazima amchukue mtoto wake.

Siku hiyo hiyo kwakuwa alishakata tiketi online aliunganisha ndege na kutua uwanja wa Songwe Mbeya kwa Ndege.
Alipofika breki ya kwanza ilikuwa kwa Gwakisa na Verity ambapo alitaka amuone mwanae na waweke kila kitu wazi.

Alipanga kuwa endapo wakikataa tu ataomba vipimo vya DNA vifanyike.
Alipofika pale alishtushwa na uwepo wa gari la RPC pamoja na magari mengine yakiwemo yenye namba za Jeshi.
Kwakuwa simu yake mda wote ilikuwa imezimwa kwa ajili ya safari za kwenye ndege akawa hakupata taarifa yeyote kuhusu kilichokuwa kinaendelea na mke wake alishampigia simu mara kibao bila kumpata.

Alipofika pale alilakiwa na wakwe zake huku akisikia kilio cha Verity ambaye anamtaja mwanae .

Sam alishindwa kuelewa haraka lakini picha aliyoipata ni huenda Princess amefariki. Mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda kwa kasi sana.
“Kuna nini kwani”

“Alimuuliza Mama yake Mkwe”
“Mtoto wa Verity amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha”

Sam alisogea kando akawaza, kisha akaibuka haraka mpaka kule ndani alikokuwa anafarijiwa Verity….

“Nisikilize Vizuri Verity, ujanja wenu nimeshaujua, mimi ni askari by Profesheni, mmeamua kumficha mtoto wangu nisimchukue lakini mtamtoa tu huko aliko”

Maneno ya Sam yalimshitua kila mtu na wala hakuwa na muda wa kubaki hapo, aliondoka mpaka kwake ambapo alikuta kuko kimya kwani Rafiki alikuwa kwenye harakati za kusaidia kumtafuta mtoto wa mdogo wake.

……………………………….
Gwakisa aliwahi kule kwa wale jamaa zake na aliingia kama mbogo. Alikuwa anarusha ngumi nzito na mateke huku akihoji aliko mwanae.

Ghafla mijitu minkubwa ilijitokeza mbele yake na kumkamata huku ikimpa kichapo kilichomkalisha chini hawezi hata kuamka.

Ghafla mbele yake alitokeza Yule dada askari na kuuliza kwanini Yule Gwakisa yuko kwenye hali ile….

“Kaja hapa analeta tabu anaulizia sijui mwanae sijui vitu gani tumempa adabu kidogo atulie”

“Okeeeey, wewe bwege unapaswa kuwa na heshima hapa ni ikulu hupaswi kuleta fujo”

Yule dada alimkamata Gwakisa kichwani huku akimuangalia usoni akiwa kapiga magoti.

“Wakuu huyu nimempa mtego kidogo tu, mwanae ninae”

Gwakisa kusikia vile alishtuka kisha akaambiwa “nifwate huku”

Pamoja na Gwakisa kuambiwa nifwate na Yule dada hakuwa na uwezo huo kwani alipigwa kwenye viungo vya miguu, hivyo ilibidi apelekwe na wale mabaunsa.
Alipofika alilazwa kitandani kisha Yule dada akaanza kumpa maneno….

“Huwezi kulea mtoto ambae sio wako, hiyo ni fedheha kubwa wewe kijana, nimeamua kukusaidia hatua za kuchukua, Yule mtoto kwa sasa yupo sehemu salama na utamuona, ataenda kukaa mbali na atasoma huko huko wakati wewe unatafuta wako mwenyewe, tena nitakuzalia mimi…..”

Gwakisa alijiuliza sana kwamba imekuwaje hadi Yule dada akajua kuwa Yule mtoto sio wake.

Alitamani amuulize lakini akakwama namna ya kuuliza akabaki anajiuliza tu bila ya majibu.

“Au unakataaa kuwa mtoto hujachakachuliwa?”

“Kwanza yuko wapi?”

“Utamuona muda ukifika wala usijali”

“Nisijali vipi, hivi mnadhani familia yangu itatulia ikiwa mtoto hayupo?”

“Itatulia tu wala usijali”

“Hivi ninyi mnaofanya hivi mngependa ikiwa nanyie mngekuwa mnafanyiwa hivi”

“Unadhani kuna jambo zuri lisilo na maumivu?”

“Basi mimi siyataki haya maumivu na hilo jambo lenu zuri silitaki pia”

Yule dada alimuangalia Gwakisa kwa dakika chache kisha akamwambia….
“Kama wewe hulitaki tambua kuwa sisi tunakutaka kwenye mambo yetu, alafu pia kumbuka kuwa umesaini mkataba.”

…………………………………
Sam hasira alizokuwa nazo zilikuwa hazielezeki, alijua kuwa kuna mchezo anafanyiwa ili asimpate mwanae, alijipanga kwa mambo mengi ila la kwanza ilikuwa ni kumtafuta Gwakisa.
Alirudi kule alikotoka kwa mara nyingine ili amtafute Gwakisa.

Safari hii alienda kisataarabu sana ambapo aliegesha gari getini kisha akazama ndani.
Alimfwata kijana mmoja ambaye alimjua ni wa karibu nah ii familia, alimshika began a kumvuta kando kidogo.

“Dogo hivi huyu baba wa hii familia yeye yuko wapi”
“Yani huyu aliyepotelewa na mtoto?”
“Ndio huyo huyo” sam aliitikia kwa sitaki nataka
“alitoka hapa mda mrefu, nadhani yuko kwenye harakati zake za kumtafuta mwanae”
Sam alijua moja kwa moja kuwa Gwakisa yuko sehemu na sehemu alipo itakuwa ni kwenye vyombo vya usalama wanazuga tu.

Sam aliridhia kuwa kila kitu kwa siku hiyo kisimame mpaka kesho yake.
Alienda kwake akamkuta mkewe ambaye alikuwa amenuna si kawaida.

“Sam hivi kweli yani wewe ni mume wangu lakini unarudi safari hata kunitaarifu”

“Please sitaki usumbufu rafiki niache nipumzike”

“Hivi wewe mwanaume una matatizo gani lakini, najuta kuolewa nawewe”

Ile Rafiki anamalizia herufi ya mwisho tu ….. ‘paaaaaaa,paaaaaaa,paaaaaaa’

Yalikuwa ni makofi matatu mubashara yaliyokuwa yanatua kwenye shavu la Rafiki, kofi moja lilipotaka kumdondosha chini alizuiwa na kofi la upande mwingine, alipotaka kuanguka upande mwingine kofi la shavu jingine lilimbadilisha mwelekeo na kuangukia upande mwingine huku akiachia ukelele mmoja tu kisha akatulia kimya.

Yalikuwa ni makofi matatu yaliyotua kwenye mashavu mawili kwa mtiririko yakamzimisha mtoto huyu wa RPC kimya kabisa pale chini.

Sam alikuwa na hasira nyingi mno na kuanza kuropoka….

“sitaki usengeeee, nasema usenge sitaki, baba yako alinipiga mpaka nimekuwa mgumba alafu unanipandishia sauti….kufaaaaaa”

Sam alikuwa mbogo sana na alikuwa akiongea peke yake…..

“Mimi nimehaso, nimehaso kupata haya maisha nimepitia mambo elfu kidogo, mimi ni mhuni tuuuuu, nitaua mtu yeyote lakini mwanangu nitamchukua tu”
“Mwambie mdogo wako lazima mtoto wangu amtoeeeee”

Sam aliongea bila kujibiwa na mtu kwani mkewe alikuwa pale chini hajitambui lakini wala hakujali na cha ajabu zaidi akamsindikiza na teke la mgongoni.
Aliingia chumbani kwake akabadilisha nguo akaoga na kuvaa zingine, akiwa anataka kulala akakumbuka kuwa kule nje aliacha mtu.

Alitoka akamkuta mkewe kalala pale pale alipomuacha na wala hatikisiki. Alimgeuza akamtikisa lakini wala hakuonyesha kujielewa kwa lolote.
Sam wala hakujali na ndio hasira zilimzidi, alimburuza mpaka nje kwenye korido akamuacha humo kisha yeye akafunga milango na kuingia ndani kulala.

Alipanda kitandani akawa anapanga mipango yake lakini ikawa haipangiki, aliamua kuwa kesho yake adamkie kwa Gwakisa wamalizane kuhusu mtoto.
Alijaribu kuutafuta usingizi sasa ili apumzike. Kila alipojaribu hakuupata, usingizi ulikuwa mbali nayeye kabisa.
Alijitahidi kutulia labda utakuja lakini masaa yalikuwa yanakatika tu bila kusikia lolote.

Aliamka na kujimwagia maji bafuni akijua huenda usingizi utakuja lakini wapi, hakuambulia chochote,
Alijifunika gubigubi na kulala huku kafumba macho lakini alipotaka tu kupitiwa na usingizi alijiwa na ndoto iliyomtisha ikabidi aamke kwa kukurupuka.

Alianza kuwaza hatua moja hadi nyingine kuanzia alipokutana na mkewe akajikuta akianza kuingiwa na roho ya huruma na woga.

Kwanza aliogopa akijua huenda ameua lakini pia alimuonea huruma mkewe kwani alijua kuwa mkewe anampenda sana.
Taratibu alijikongoja mpaka sebuleni akakusanya funguo ili aanza kufungua milango akamuangalie mkewe kule nje alikomuacha.

Alipotaka tu kufungua mlango roho ya ukatili ilimjia tena na kujikuta akijilaumu kwa zile huruma anazoanza kuwa nazo.
Alirudi haraka mpaka ndani chumbani na kupanda kitandani kisha akalala zake.

…………………………….
Gwakisa alikuwa kawekwa mtu kati hafurukuti na kila alichokuwa anauliza alipewa majibu yasiyo na matumaini.
Aliikumbuka mikataba aliyosaini akaona hana uwezo wa kuwakwepa hawa watu hivyo ikambidi akubaliane na kila kitu.
“Basi nae naomba niende nyumbani”
“Mkandeni hiyo miguu yake mumpeleke kwake asije akaachika” Yule dada askari alitoa amri.

Wale jamaa walichukua dawa ya kupulizia ambayo humaliza maumivu na kumpulizia huku wakimpaka nyingine kwenye magoti na kwenye viungio vya mikono.

Walimkanda na maji ya moto pia kisha wakamfunga vizuri na kumpakia kwenye gari mpaka nje kwake kisha wao wakarudi na gari nyingine waliyoambatana nayo.
Jinsi gwakisa alivyoingia pale kwake kila mtu alishangaa, aliondoka bila taarifa na alipotafutwa hakupatikana alafu anarudi akiwa kwenye hali hii.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)