Mtunzi: Omary John Mndambi
SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Walimkanda na maji ya moto pia kisha wakamfunga vizuri na kumpakia kwenye gari mpaka nje kwake kisha wao wakarudi na gari nyingine waliyoambatana nayo.
Jinsi gwakisa alivyoingia pale kwake kila mtu alishangaa, aliondoka bila taarifa na alipotafutwa hakupatikana alafu anarudi akiwa kwenye hali hii.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Baba yake Mkwe na Mama yake Mkwe walimuweka chini na kumuuliza kilichomkuta kule alikoenda na hapohapo Gwakisa akajua jinsi ya kupata uongo.
Aliwaeleza kuwa alipokuwa kwenye harakati za kumtafuta mtoto nae aliishia kutekwa na watu asiowajua wakampeleka sehemu yenye maficho kisha wakaanza kumtesa kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake.
Aliwaeleza kuwa wale watu walimwambia kuwa endapo ataendelea kumfwatilia Yule mtoto basi wataua familia nzima.
…………………………………………
Asubuhi na mapema Sam aliamka ili aende kwa Gwakisa waongee kuhusu ishu ya mtoto, alijiandaa vizuri kisha akatoka nje lakini pale alipomuacha mkewe hakumuona na wala hakuhangaika kumtafuta.
Aliondoka moja kwa moja kwa lengo la kumtafuta Gwakisa, kabla hajafika huko aliamua kumpigia kwanza simu.
Waliongea vizuri lakini Gwakisa akamwambia kuwa hangeweza kutoka nyumbani kwani hali yake sio nzuri hivyo aje nyumbani.
Sam hakusita, tena aliona ni vyema akimkuta Gwakisa akiwa na mke wake kwa pamoja…..
Sam alienda mpaka hapo kwa shemeji yake na kuingiza gari ndani ya uzio na kupaki….
Alikaribishwa ndani na kukaa sebuleni, baada ya muda kidogo alitokea Gwakisa akiwa anatembelea fimbo huku anachechemea, Sam alishtuka kuona vile akajua Gwakisa aanmuigizia.
“Karibu ndugu, habari za nyumbani?”
“Nzuri tu vipi hapa?”
“Hapa ndio hivyo ni matatizo tu, afadhali umerudi kutoka masomoni utasaidia maana mimi nimejitahidi kwa siku moja tu nimeishia kufanywa hivi”
“Kwani wamekufanyaje?”
“Ndugu yangu yani acha tu, wameniteka wakaanza kunipa kipigo si unaona nilivyovimba huku…wameniambia nikiendelea kufwatilia ishu za mtoto wangu wataniua kabisa”
Kwakuwa Sam alikuwa hamuamini Gwakisa alienda akamuangalia akagundua kuwa ni kweli kavimba ila bado hakutaka kuamini moja kwa moja, alijua anachezewa mchezo….
“Vipi shemeji yuko wapi?”
“Ngoja nimuite”
Aliitwa verity aliyekuwa huko chumbani kisha akaja pale walipokaa Sam na Mme wake, Verity alikuwa ana majonzi ila pia alikuwa hajiamini kutokana na hali halisi iliyokuwa pale….
“Kwanza kabisa nawapa pole kwa kupotelewa na mtoto katika mazingira kama haya”
“Asnte sana kaka roho inaniuma sana kwakweli nikimfikiria huyu mwanangu” alijibu Gwakisa.
“Ila mimi naumia zaidi kuliko wewe maana Yule mtoto ni wa kwangu” alisema Sam kitendo kilichomshitua Gwakisa na kumkata jicho Sam.
“Unasemaje wewe? Umeugua ukichaa sio?” Verity aling’aka kama mwendawazimu.
“Mimi sio kichaa, na hilo unalijua Shemeji Verity, na unajua kuwa Yule mtoto ni wangu na sio wa Gwakisa, Hebu leo mwambie mme wako ukweli ajue”
Gwakisa alimgeukia Verity na kumtazama kwa ishara kuwa anataka kusikia kutoka kwake
Verity alisimama wima na kuanza kuapia kwa Mungu wake…..
“Nakuapia mume wangu Gwakisa, Princess ni mwanao kabisa, usimsikilize huyu ni kichaa”
Gwakisa hakujibu chochote bali alibaki amemtolea macho Verity asiyejua kuwa Gwakisa ana ushahidi wa DNA kuwa mtoto sio wake isipokuwa baba halizi wa mtoto ndio alikuwa hajamjua bado…..
Gwakisa alifikiria cha kusema kutokana na uongo wa mkewe akashindwa afanye nini, akaishia kuguna tu.
Jambo moja ambalo aliamini ni lazima alifanya ni kulinda heshima yake, ya familia yake, ya mke wake nay a ndoa yake…
Japo alijua mkewe kakosea sana lakini mbele ya mwanaume mwenzake hakutaka aonekane dhaifu hata kidogo.
Mr Sam nimekusikiliza vizuri sana, nimekusikia vizuri mnooo ila nimegundua kitu kimoja…alisema Gwakisa.
“Kitu gani hicho” sam aliuliza
Gwakisa alichomjibu sam ni kwamba … “nimegundua kuwa huna akili kabisa”
“Unasemaje, mimi sina akili?”
“Huna hata kidogooo”
Sam alisimama wima akitaka ngumi zipigwe kwa kuona kuwa ametukanwa.
“Ndugu yangu Sam acha hasira za kijinga, unataka upigane namimi wakati unajua naumwa. Subiri nikipona ndio uanzishe vita, hapa ukinipiga wala huna haja ya kujisifu kuwa umenipiga”
Sam alikaa chini pale kwenye kochi huku Verity akimng’ang’aniza Sam aondoke pale nyumbani.
“Shemeji Sam nakuomba uondoke nyumbani kwangu la sivyo nitakuunguza hata na maji ya moto”
Sam aliamua kutulia kitendo kilichomp Gwakisa mwanya wa kuongea kidogo.
“Ndugu yangu tena mme Mwenzangu Sam labda nikuambie tu kuwa ungekuwa na akili ungeweka juhudi zooote kumtafuta kwanza mtoto ndio uanze kumdai kuwa ni wako”
“Mimi sio mjinga najua huyo mtoto mmemficha ili nisimchukue”
Gwakisa akiwa na hasira alimkata jicho kali Sam akamwambia nivile tu anaumwa lakini angempa disipilini ya kutosha na wala asingerudia kukanyaga hapo nyumbani kwake.
“Sam nashukuru sana kwa kunidhihirishia kuwa umekuwa ukitembea na mke wangu, ila nataka kukwambia kuwa mla vya wenzake na vyake huliwa, kampime mkeo ujauzito kwani inawezekana na mimi nimepanda mbegu zangu kwenye shamba lako”
Gwakisa alisema maneno hayo ili amuumize Sam kwa kile alichomfanyia bila kujua kuwa maneno hayo yalikuwa kama mwiba kwenye moyo wa Sam.
Sam alinyong’onyea akatahayari kwa yale aliyosikia, alioanisha mambo mengi mwisho akaamua kuondoka bila kuaga moja kwa moja kuelekea kwake.
Akiwa njiani kuelekea kwake alipokea simu ambayo ilimtaka afike ofisini mara moja.
Aligeuza gari na kuelekea ofisini ambapo alimkuta Bosi wake akiwa na RPC.
Kitendo cha Sam kufika pale akatiwa Pingu na kuwekwa mahabusu.
…………………………………………….
Kwenye mida ya saa tisa usiku RAfiki alikuwa akijihisi baridi kali mnooo, pamoja na baridi lakini alikuwa anahisi maumivu hasa kwenye maeneo ya mbavu zake.
Alijitahidi kufumbua macho yake akakutana na giza nene, taratibu alianza kukumbuka jambo moja baada ya jingine hadi alipofikia kukumbuka ugomvi wake na mmewe.
Hapohapo machozi yakaanza kummwagika, alinyanyuka taratibu ili afungue miango huku akichechemea.
Alipofika alianza kwa kutingisha grili lakini akakuta limefungwa kwa ndani, hakuamini kuwa mme wake ndie amekuwa katili kiasi kile.
Alirudi tena pale chini kwa kujikongija na kuendelea kulia sana, alilia akachoka na kuona sio suluhisho alisogea mpaka nyuma ya dirisha kilipo chumba chao cha kulala na kuanza kumuita mmewe lakini alisikia tu sauti ya kukoroma kwani ndio muda huo Sam nae usingizi ulikuwa umemkolea baada ya kuutafuta kwa muda mrefu.
Hakuamini kuwa pamoja na kumsubiria mme wake kwa muda mrefu kiasi hicho akitegemea mapenzi motomoto baada ya mume wake kumaliza mafunzo lakini kile ndicho alichokuwa anaambulia.
Alijuta sana kung’ang’ana kuolewa na Mwanamume kama Sam, alijutia ndoa lakini hakuwa na uwezo wa kurudisha mambo nyuma.
Alisubiria angalau kupambazuke ili aondoke pale nyumbani atafute sehemu yenye usalama…
Kweli masaa yalisogea kwa mwendo wa kinyonga na hatimaye kukaanza kupambazuka na watu pamoja na magari vikawa vinasikikika vikipita huko nje.
Aliamka kwa kujikongoja mpaka nje ya geti kisha akasubiria pikipiki akaisimamisha japo hakuwa na hela ila akapanda mpaka nyumbani kwa wazazi wake.
Wa kwanza kumuona alikuwa ni mama yake ambaye alimshangaa sana binti yake kwa jinsi alivyokuwa,
“Mwanangu umepatwa na nini”
“Nomba kwanza umlipe huyo bodaboda alafu nitakwambia”
Mama mtu alimshangaa binti yake anavyotembea kwa shida roho ikamuuma sana, alimwambia bodaboda amruhusu kisha akamshikilia bintiye na kumkongoja kwenda ndani kisha akamkalisha na kurudi kumlipa boda boda.
Aliporudi kwa binti yake alimhoji akasimuliwa mkasa mzima kitendo kilichomfanya ashike mdomo kwa kuhamaki kuwa yani Sam waliyemjua ndio kawa vilee?
Mama mtu hakuweza kuvumilia, alikimbilia chumbani kumsimulia mme wake ambaye nae alifadhaika sana kwa binti yake aliyempenda sana kufanyiwa yale.
Muafaka uliofikiwa ni Rafiki apelekwe hospitali huku taarifa zikiwa zinnafika ofisini kwa Sam ili hatua zichukuliwe kwa kitendo alichokifanya.
……………………………..
Dr Kelvin alikuwa anampigia sana Rafiki simu lakini alikua hampati, rafiki alizima simu yake na hata hivyo akawa ameiacha kule kwake wakati wa kuondoka baada ya ugomvi na mume wake.
Alishakata tamaa lakini kwa jinsi alivyokuwa na usongo na Rafiki alisema kuwa atamtafuta kivyovyote amtie mikononi mke huyu wa mtu.
Akiwa anaendelea na majukumu yake alipita korido ya mapokezi na kukuta mwanamke amejiinamia chini huku kashikiliwa na mama mmoja mtu mzima akashtuka kwani alimfananisha Yule binti.
Alisimama na kuwasalimia kwa lengo la kuwatambua vizuri, roho yake ililipuka baada ya kuuona uso wa Rafiki lakini ukiwa umevimba.
“Rafiki ni wewe? Mbona uko hivyo? Una matatizo gani?” dr Kelvin aliuliza maswali matatu kwa pamoja kabla hata la kwanza likiwa halijajibiwa.
Haraka haraka alifwatilia kila kitu na Rafiki akaanza kuhudumiwa kwa uharaka.
Kwakuwa yeye alikuwa daktari wa akina mama hakuweza kumhudumia Rafiki ila alihakikisha anampeleka kunakohusika na kwa madaktari anaowaamini ili ahudumiwe.
Huduma alizokuwa anapata Rafiki hata mama yake alikuwa anashangaa, mama yake aliambiwa apumzike tu kwani kila kitu kilikuwa kinafanywa na wauguzi waliokuwa wanapokea amri kwa madokta.
Tabia za madokta wa hii hospitali zilikuwa zinafanana sana kiasi kwamba ikiwa mmoja atawaambia wenzake kuwa huyu ni shemeji yenu muhudumieni vizuri basi atahudumiwa kwa ukaribu mno, na hiki ndicho kilichokuwa kinatokea kwa Rafiki.
Japo Dr Kelvin hakuwaambia kabisa uhusiano wake na Rafiki kwni ni mke wa mtu ila wale madaktari wenzake walihisi tu na wakawa wanamhudumia vizuri sana.
Rafiki alitibiwa na kupewa dawa huku akichomwa sindano za kuzuia maambukizi na maumivu pamoja na dawa za kupunguza uvimbe,
Hakuwa mgonjwa wa kulazwa ila aliandikiwa kulazwa,
Dr Kelvin siku hii alikuwa na furaha sana na alifanya kazi kwa amani mno huku kila mara akipita pale alipolazwa Rafiki.
Alikuwa akimletea vitu vidogo vidogo vya kula na vizawadi mbalimbali kiasi kwamba hata Rafiki mwenyewe akawa anajisikia ahueni.
Siku hii Dr Kelvin hakwenda kabisa kwenye hospitali nyingine ambazo annafanya kazi part time kwani alikuwa anataka akae na Rafiki zaidi pale hospitali.
Ilipofika usiku alienda kule alikolazwa akakaa kitandani na kuanza kumhoji Rafiki kuhusu mambo gani yaliyompata.
…………………………………..
Gwakisa alikaa siku mbili kisha akajisikia nafuu kidogo na kuanza kwenda kazini, ishu ya mtoto Princess ilikuwa imeshikiiwa na Jeshi la Wananchi kwani mtoto aliyepotea ni wa Bosi wao.
Lakini pia Jeshi la polisi lilikuwa limeikomalia kweli kweli kwani Yule mtoto alikuwa ni mjukuu wa RPC hivyo walihusianisha kupotea kwake na mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na visasi labda dhidi ya majeshi ya ulinzi na usalama.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)