MUUZA CHIPS (53)

0
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA HAMSINI NA TATU
ILIPOISHIA...
sasa hivi sarah anaisikilizia tu kwa mbalii na vile chidi kajaaliwa katika sehemu hio, na licha ya kujaaliwa pia anajua kuitumia vizuri, mana kuna mijanaume mingine imejaaliwa lakini hawawezi kutumia umbile hilo,… Maskini sarah alikuwa akilia kwa utamu aliokuwa anaupa mana jana yalikuwa ni maumivu kwasababu anaanza,…. Lakini chidi hakuitupia yote, ila mtoto wa kike kilio hakimuishi…

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Tukija huku kwa Ibrahim akiwa na mke wake mezani,

"mbona hapokei simu"

Aliongea Ibrahim huku akiiangalia simu yake,

"mi sijui, na hata mimi hapokei"

"au atakuwa sehemu mbaya ndio mana hapokei"

Aliongea Ibrahim lakini sio kweli, chidi alifanya makusudi kutopokea simu za watu hao,…

"baadae nitajaribu tena, najua hanishindi yule ni shemeji yangu"

Aliongea jasmine huku akiendelea kunywa chai,…

"ok we endelea kumpigia akikubali tukutane we nipigie nitatoka ofisini nije tuongee nae"

"sawa mume wangu"

Tukija huku kwa kijana chidi na sarah, chidi akiwa anamshuhulikia mtoto wa watu vizuri sana, yaani hata huruma chidi hana,…

Dakika chache mbele walimaliza lakini katoto hata kutembea kanaona uvivu,.. Chidi alimbeba mpaka bafuni wakaoga wote na kumaliza,..

"chidi ivi chupi yangu ipo wapi"

"ooohhhh shit unakumbuka jana tuliiacha kwenye maji"

"jamani chidi,… Sasa nitaendaje nyumbani mimi"

"tuifue tuianike hapa hapa utakuja kuichukuwa kesho"

"Mungu wangu chidi jamni"

"nini kwani"

"nitatetemesha sana chidi"

"wauweeeeee"

"no buana watu wataniona malaya"

"kwani usipovaa chupi unakuwaje"

"hhhmmm na kile kigauni changu,.. Nitatingisha sana kile kigauni ni chepesi sana"

"basi vaa mbichi hivyo hivyo"

"No, siwezi"

"sasa wataka nini"

"nipe boxer yako"

"aaahhhhhh sasa boxer yangu itakuenea wapi na umbo lote hilo"

"chidi, we nipe tu hivyo hivyo… Ilimradi nisitetemeshe sana"

"hhmmmm sawa, wewe tu"

Basi waliifua ile nguo walioiacha kwenye maji toka jana kisha wakatoka huko bafuni,… Kila mmoja alivaa nguo zake na sarah alivaa boxer ya chidi ili asisumbue sana huko mtaani mana anaheshimika sana,…

Sasa tukija huku hotelini kwa akina mama sarah, mama mwenye akili nyingi za kimaisha, huyu mama angelikuwa mchaga basi ingekuwa poa sana,… Sema kabila lake ni tofauti na wachaga na haiviendani na vitendo vyake, yaani mama anawaza pesa tu wakati wote..

Sasa akiwa hapo ofisini kwake, mama sarah huyo

Ghafla simu yake ikaita, lakini namba hio hakuisevu ilikuwa ni namba yenyewe, ila kuipokea kwake kulikuwa ni kwa wasiwasi sana,…

Mama sarah alikuwa ofisini kwake lakini bado alifunga milango la kuteremsha mapazia ili tu asionekane…

"haloo mama saida habari yako"

Aliongea mama sarah tena bila wasiwasi wowote sema hakutaka asikiwe na mtu,.

"salama habari yako Grace"

Alikuwa ni mwanamke na anaitwa mama saida,…

"safi tu.."

"vipi, mbona hunipi majibu ya huyo kijana wako"

"aaahhhhhhh utanisamehe mama sai"

"vipi?, Umeshindwa na kazi?????"

Kiukweli hii simulizi ni ya kijanja sana, na ni simulizi ambayo inahitaji umakini wa hali ya juu mno,.. Yaani usipokuwa makini katika kuisoma basi utajikuta huielewi hata kidogo, mana huu ndio uandishi wangu mpya, kama muvi vile kumbe ni simulizi…

Sasa huku kwa mama sarah aliokuwa na wasiwasi wa kuonewa na baadhi ya wahudumu baada ya kupigiwa simu na mwanamke mwenzie, mama sarah alionekana kumheshimu sana mwanamke huyo japo hatujui chanzo chake,… Mama sarah yupo kifaida zaidi yaani hataki mchezo na pesa japo anazimaliza kwa kijana chidi,..

"haloo mama saida habari yako"

Aliongea mama sarah tena bila wasiwasi wowote sema hakutaka asikiwe na mtu,.

"salama habari yako Grace"

Alikuwa ni mwanamke na anaitwa mama saida,…

"safi tu.."

"vipi, mbona hunipi majibu ya huyo kijana wako"

"aaahhhhhhh utanisamehe mama sai"

"vipi?, Umeshindwa na kazi?????"

"hapana mama saida, bado naendelea na kazi yako"

"si ulisema leo jana utafanikisha sasa kwanini bado"

"nipe nafasi ya mwisho, nikishindwa tutajua cha kufanya"

"sawa, nakuamini mama sarah"

"ahsante kwa kuniamini"

Mama sarah alikata simu huku akipumua kwa nguvu, kana kwamba kazi alioipewa anaiqeza vizuri sana ila sema hio kazi yenyewe inamuathiri mpenzi wake, hivyo roho inamuuma kufanya hivyo, ila akiangalia kuna pesa mbele basi anakuwa Mwepesi sana kuifanya kazi hiyo,

Mama sarah akiwa hapo ofisini kwake tusijue kile anachokiwaza kwa muda huo, lakini kuna kitu alikikumbuka kutoka kwa mama saida,..

"nitakupa kiasi cha Tsh Bilioni moja, pale utakaponiletea mbegu za kiume tena nataka za mwanaume rijali haswa"

Mama sarah alikumbuka kauli hio kutoka kwa mama saida,.. Sasa hapa naona kama nachanganyikiwa, mana kule nyuma mama sarah alitupa kumbukumbu ya yeye aliooenda kwa mganga ili amfunge chidi awe peke yake,.. Afu na hapa kumbe katumwa na mtu mwingine tofauti na uhitaji wake yeye mwenyewe,…..

Mama sarah alinyanyua simu yake na kumpigia chidi ili wakutane ampeleke kazini akaanze kazi

Tukija huku kwa akina chidi tunawakuta wawili hao wakiwa tayari kwa kutoka,

"chidi… "

"sema mamy"

"nakupenda chidi wangu"

"mi pia.., afu sarah we mtamu eti"

"muongo chidiii"

"kweliiii"

Basi chidi alipanda katika gari ya sarah, lakini ghafla simu ya chidi ikaita, kuangalia alikuwa ni mama sarah wake,..

"haloo mamy"

"eeehh naomba tukutane pale stendi sawa"

"sawa mamy"

Chidi alikata simu huku akimwambia sarah kuwa,

"nipeleke hapo stendi"

"poa haina shida"

Basi chidi alifikishwa stendi kisha sarah akaondoka zake, chidi akaanza kumtafuta mama kwa simu mpaka akampata,.. Chidi akapanda katika gari ya mama sarah na kupelekwa katika hoteli ya akina miriam ambayo inakwenda kwa jina la MIRAS HOTELI (Miriam Agnes Hoteli) wamiliki wa hoteli hizo huwa wanapenda kuandika majina ya watoto wao au pamoja na yakwao,.. Mana hata ile ya akina sarah inakwenda kuitwa SARADISE HOTELI badala ya PARADISE HOTELI jina la zamani.. Chidi alikuwa katika furaha ya hali ya juu mno kwakuwa anakwenda kupewa kazi japo hajui ni hoteli gani lakini anakwenda tu kufanya kazi ya kukaanga CHIPSI,.. Mana hapendi kukaa bila kazi

Wakati huo na sarah nae anaelekea kazini huku mama yake anakwenda miras hoteli ili kumkabidhi chidi kwa ajili ya kazi,.. Na mama sarah alipenda sana kijana chidi afanye kazi katika hoteli yake lakini, kutokana na hofu ya mtoto wake kupenda wanaume mahensam hivyo alihisi huenda wakapendana afu akajikuta analiwa yeye na mtoto wake, kitu ambacho hakitokuwa kizuri katika familia, lakini hayo ni mawazo yake, lakini anachokiwaza ndicho kinachofanyika kwa wakati huo…

Mama sarah na chidi wanakutana na mama miriam katika ofisini maalumu kwa ajili ya kukabidhiwa kikazi

"heeee mama miri habari yako"

"salama tu,.. Naona leo umenitembelea"

"ndio… Kuna siku ulikuwa unalilia mkaanga chipsi,.. Nadhani kilio chako kimefika mwisho"

"we acha tu mama sarah, hoteli kubwaa yenye hadhi ya juu, lakini chipsi haziwi nzuri"

"sasa huyu ni Profesional wa kukaanga chipsi"

"unaongea kweli au unatania mama sarah"

"kweli, huyu kijana nilitamani sana akae pale kwangu, lakini sema kuna mmoja ninae afu pia hii hoteli ina hadhi ya juu, hivyo kwa upande wa chipsi we mwachie huyu kijana"

"nitashukuru sana,….. Kijana habari yako"

"salama mamy shkamoo"

"marahaba ujambo"

Chidi alikuwa akijitambulisha kwa boss wake mpya, ambae ni mama miriam,..

"sijambo"

"aaaassh sasa kuhusiana na mshahara nadhani nitajua nimlipe vipi baada ya mwezi huu kuisha,.. Ili nione pishi lake la chipsi lilivyo"

"sawa,.. Ni wewe tu, ila ujue huyu ni Profesional wa chipsi hivyo nadhani utajua ni jinsi gani utamlipa"

Mama sarah aliongea ili kumpigia debe kijana chidi alipwe mshahara mnono,..

Mama miriam alimpokea kijana chidi kwa mikono yote miwili kwasababu alikuwa ana shida na mtu kama huyo kwa ajili ya kuleta ushindani wa kibiashara na hoteli zingine,…

"lakini si umempa masharti ninayotaka mimi"

Mama miriam alimuuliza mama sarah kuwa amempa chidi masharti ya kuwepo hapa hotelini,

"nadhani anaelewa…. Chidi?? Hapa kwenye hii hoteli, haruhusiwi kuangalia wateja, haruhusiwi kupendana na mteja au muhudumu yeyote yule kuanzia ngazi ya juu mpaka ya mwisho,.. Yaani ni wewe na kazi tu"

Aliongea mama sarah huku akisisitiza sana

"ndio kijana,… Hapa kunaingia wateja wa kila lika, hivyo kuwa makini na macho yako na nafsi yako,… Alafu cha mwisho haruhusiwi kutoka nje kwenye halaiki ya watu, wewe utaishia jikoni tu.. Ukitoka nje ni kwa dharura tu"

Aliongea mama miriam huku akiwa siriasi kweli na hakuwa na utani,… Mama sarah alimuaga Agnes kisha huyoo akaondoka zake… Lakini alipotoka hapo alipigiwa simu na mama saida kuwa wakutane…

Huku hotelini chidi aliingizwa huko jikoni na kukutana na watu wengi sana,.. Ila alishangaa kukutana na saidi huko ndani, kama unamkumbuka saidi ni rafiki yake sana toka akiwa kule kwa kaka yake, na alikuwa akimwachia chipsi kisha yeye anafanya mambo yake, kama unakumbuka kule nyuma chidi na saidi ni marafiki wakubwa tu sema walipoteana kipindi chidi ana matatizo ya kufukuzwa na kaka yake..

"vijana,… Huyu kijana ndio atawaelekeza jinsi ya kupika chipsi vizuri, hivyo mutamsikiliza ila mtakuwa nae huku jikoni, na mtakuwa nae kwenye mapishi, naomba muheshimiene jamni sawa"

"sawa boss"

Mama Miriam alikwenda kumtambulisha kijana chidi kwa wapikaji chipsi wenzie, kwahio mpaka hapo kijana chidi ana cheo, mana kwanza kaletwa na boss afu pili ni mtaalamu wa chipsi vibaya mno..

Tukija huku kwa mama saida na mama sarah, wakiwa wapo nyumbani kwa mama saida, yaani mama sarah ndio alikwenda kwa mama saida,…

"naona kazi inakuwa ngumu mama sarah eti ee"

Aliongea mama saida lakini ni kwa kawaida tu

"kiukweli kazi ni ngumu, lakini nahitaji kurudi kwa mganga ili nijue natumia njia gani nyingine"

"fanya juu chini mama sarah,.. Kijana wangu anazidi kukua tu"

"usijali,.. Kijana wako atapona tu, yaani huyo kijana nilienae ana nguvu za kiume haswa, yaani huyo mtoto ukimtajia hata chupi tu, anakuambia anateseka sana"

"weeeeeeeee….. Yaani akiskia tu kutajwa kwa chupi anateseka"

"yaani tena sio kidogo… Huyo mtoto ni rijali haswa"

"ni mzaliwa wa wapi huyo"

"mtanga,… Msambaa flani hivi hensam hensam hivi"

"aahhhh basi, kama ni mtanga basi nakuamini shost"

"ok, basi mimi wacha nirudi nyumbani"

"sawa ila hakikisha hukosei mama sarah"

"usijali mama saida lazima lengo lako litimie"

Mama sarah aliondoka zake na kumwacha mama saida katika jumba lake la kitajiri kuliko hata mama sarah au hata mama Miriam,… Huyu mama saida ni tajiri mkubwa tena mkubwa wa haswa

SASA HAPA WACHA TUUJUE UKWELI HALISI JUU YA WAWILI HAWA, MANA ULE UKWELI WA MWANZO NADHANI ULIKUWA NI UONGO… SASA HEBU TURUDI NYUMA KWENYE MAELEWANO YAO YALIKUWAJE

Sasa tukiwa tumerudisha siku nyuma, kama kumbukumbu jinsi ilivyotokea

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)