MUUZA CHIPS (64)
Sehemu ya Sitini na Nne, mama yake chidi, baba yake chidi, babu yake chidi, ambae ndio babu, babu yake na, chidi lakini sio, dereva ageuke nyuma
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: MoonBoy
SEHEMU YA SITINI NA NNE
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
"basi turudini, mana kitu muhimu tumeshakikosa"
Aliongea mama saida huku akimpoza mwanae tu kuwa atapona tu,.. Ridhiwani aliwasha gari hio japo ilipondeka sana lakini iliwaka na kuondoka zao kurudi mjini Arusha,…
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
"lakini mama saida nipe muda tena, mana hata mimi imeniuma kwa kutoa pesa yangu buree"
"mimi nitakulipa hizo pesa zako zote lakini hebu jaribu tena"
"sawa,.. Ila naomba tusifanye kwa huyo kijana tena"
"kwanini isiwe hivyo"
"yule mtoto anaonekana ana mungu, mana hata wakati namvalisha ile kondomu, nywele zake zilisisimkwa, kana kwamba kapewa ishara tu kuwa hapo alipo kuna kitu kibaya.. Mimi nilifahamu lakini yeye hakujua kama ni ile kondomu niliomvalisha"
"wewe mama sarah, mambo ya yeye na mungu wake mwachie yeye,.. We fanya kazi yako tu"
"hhmmm sawa nitajaribu tena.. Lakini jua natumia pesa ivo"
"kwenye Bilioni moja nitakuongezea Milioni 500 kwa ajili ya hizo pesa zako unazompa"
"sawa nitajaribu, mana hio ya mara ya kwanza tu yenyewe ilikuwa ni mbinde"
"au mama sarah… Mimi nimepata wazo jipyaaaaa"
Mama saida alionekana kupata wazo juu ya jambo lao hilo la kumsaidia Ridhiwani,
"wazo gani hilo mama saida"
"we twende tukaliongelee nyumbani"
Basi ridhiwani aliendelea kuendesha gari kwa kurudi Arusha, ili kuanza kazi upyaaa
Tukija huku kwa kijana chidi akiwa yupo kitandani kwake, akiwa kazimwaga pesa hizo kitandani, huku akizilalia kwa furaha ya ajabu, mana hajawahi kupata pesa kama hio toka kuzaliwa kwake… Sasa wakati anaendelea kucheza na pesa hizo mara sms ikaingia katika simu yake
"best, bado upo bize"
Alikuwa ni miriam aliokosea namba ila kwa sisi wasomaji tunajua kuwa huyo ni miriam yule yule boss wake, sasa kaja kwa njia ya kama miriam mwingine,..
"ndio nipo bize subiri"
"heeeee kwani unafanya nini"
"Hayakuusu bwana we subiri kwanza.. Afu ukiendelea kuchati na mimi naweza kukublock eti"
"mmmhh sorry,.. Nitasubiria basi"
Maskini chidi hajui kama huyo anaemtolea nje ni boss wake wa kazini, yaani laiti angelijua sijui ingekuwaje…
Chidi aliendelea kuzifurahia pesa hizo huku akizirusha juu kama vile anagawa sadaka,…
"kumbe side alichoniambia ni cha kweli ee… Aaahhhh sasa watanikoma wale matajiri wote wanaojipendekeza kwangu, afu hata sarah namlia taimingi mana anaonekana yumo katika wale waliomo"
Chidi alijiongelea mwenyewe huku akiweka pesa zake hizo katika begi
"kweli mjini shule, nguvu peleka kwenu… Sasa hapa nimefunguliwa, afu hata shemeji pia akizingua namchuna, yaani sibagui wala sichagui, yeyote yule yupo usoni kwangu ni hela tu"
Sasa tukija huku kijijini kwa wazazi wa kijana chidi, waliokuwa wametulia ndani huku wakiwaza tukioa ambalo mama mtu kaliota usiku wa kuamkia leo,…
"baba Rashidi, mimi nilikuwambia nilichoota ni cha kweli wewe umebisha"
"aaaahhh mi najuaga ndoto ni ndoto tu mke wangu"
"sawa ndoto ni ndoto, lakini sio zote ni ndoto bali zingine ni maono yajayo unaonyeshwa kupitia ndoto"
"sawa mke wangu,… Lakini si tayari tumeshalisuruhisha"
"hapana, yaani hapa sina amani kabisa mpaka baba aniambie kama limefanikiwa au vipi"
Aliongea mama yake chidi, kana kwamba kuna kitu wamefanya watu hawa,…
Sasa wakiwa wapo hapo nyumbani, mara ghafla simu iliita, kuangalia jina alikuwa ni baba yake na mama yake chidi, yaani babu yake chidi
"haloo mzee"
"aaahhh mwanangu,… mjukuu wangu alikuwa anapotea"
Aliongea babu yake chidi huku mama yake chidi akiwa anasikiliza kwa makini sana,..
"baba.. Lakini si umeshamseidia"
"aaahhh tayari, na kile kitu tumeshakitokomeza mbali"
"nashukuru mzee wangu"
Huyo mzee, ni babu yake chidi lakini sio babu yake mzaa mama bali, babu yake chidi mzaa mama na huyu mzee, wamezaliwa tumbo moja, hivyo ni babu yake tu, mana wamezaliwa na babu yake mzazi…
Sasa Kumbe wazazi wake na kijana chidi walionekana kuwa kuna kitu wamekifanya juu ya mtoto wao,… Sasa cha ajabu na cha kushangaza, kumbe ile jana walipokuwa wanataka kumwambia chidi na wakaogopa kumbe hawakuishia pake… Sasa twende sawa ili ujue walifanya nini wazazi hawa…..
Sasa tuanzie siku ile walipokuwa wanaongea na mtoto wao chidi, yaani ile siku kabla ya kuvaa kondomu ambapo mama yake alitamani kusema lakini alishindwa, kutokana na heshma ya mama na mtoto… Sasa siku ile ilikuwa hivi…
Baba alikuwa akimcheka mke wake kwa kigugumizi alichokipata kuongea na mtoto wao
"sasa unacheka nini baba chidi,.. We unadhani ni jambo dogo hilo"
"unajua mama chidi wewe huna akili wewe,.. Mimi ndio ningeliweza kuongea nae yule mtoto, sasa wewe ukanipokonya simu, haya ona sasa kusudio lako limeshindikana"
"lakini baba chidi mimi sikubali, lazima nilifuatilie hili jambo"
"lakini mama chidi una uhakika na ndoto yako"
"sina uhakika sana lakini sio vizuri kama tutapuuzia baba chidi"
"ok sawa,.. Ila kwani wataka tufanye nini kwenye swala kama hilo"
"twende kwa babu yake mzee juma ili tujue"
"aahhhhhhh ona sasa umeshalifanya jambo liwe la kishirikina tena"
"kama hutaki naenda mwenyewe"
"basi ngoja nikusindikize mke wangu"
"twende sasa"
Wazazi wake na kijana chidi walikuwa wakipendana sana, tena walikuwa wakimpenda pia na mtoto wao… Kama kawaida kama unavyojua kijijini usafiri ni baiskeli na baba yake chidi alikuwa nayo baisikeli ya zamani kweli,… Basi mzee alimpakia mke wake kisha haooo wanaelekea kwa babu yake na chidi ambae ni mganga wa kienyeji na anaweza kumuona mtu kupitia moja ya nguo yake,…
Walipofika kwa mzee juma ambae ndio babu yake na kijana chidi…
Baba yake chidi ndio alitangulia kwenda kutoa maelezo, mana ni vigumu huyu mama kumweleza baba yake matatizo ya mjukuu wake, hivyo baba yake chidi akaenda kuongea na baba mkwe wake,.. Waliongea kwa muda mrefu na hatmae walimaliza, hapo mama akaruhusiwa kuingia ndani mana alikuwa nje ili mazungumzo yanapoongelewa asisikie mbele ya baba yake mkubwa,..
"mumekuja na nguo yake yeyote ile"
"ndio baba kuna tisheti yake hii hapa"
Basi mzee juma aliichukuwa ile tisheti na kuisomea mambo yake kisha akaichovya kwenye maji yenye dawa zake mwenyewe anazozijua…
Baada ya hapo aliipiga ile tisheti kwenye kioo chake kinachotumika kama tv, wanaiita TV asilia… Lakini mganga huyo ambae ndio babu wa chidi, alipopiga ile lamli yake pale kwenye kioo, alishangaa kuona kuna pande mbili badala ya moja…
Moja wamemuona chidi akiwa benki.. Ndio pale chidi alipoenda kuchukuwa pesa ile shilingi milioni miamoja,… Alafu upande mwingine wanaona majani yanatembea kwa spidi maana yake ni kwamba kuna gari iliokuwa ikitembea kwa spidi kali mno… Sasa unajua kwanini waliiona hio gari, ni kwasababu kule kwenye gari kuna kondomu afu ndani ya kondomu kuna damu ya kijanja chidi, hivyo ndio maana kioo chake kimemuonyesha sehemu mbili tofauti…
"hiii gari inaenda wapi, afu yeye mbona kama yupo benki huyu hapa"
"baba… Angalia vizuri hio gari"
Babu akafanya mambo yake pale… Alipogundua ikabidi amwambie yule mwanamke atoke, ambae ni mama yake chidi… Afu baba yake chidi ndio akabaki sasa
"mzee mwenzangu… Hapa kwenye huu mkoba wa huyu mwanamke, kuna kitu kinachohusiana na mjukuu wangu"
Aliingea mzee juma huku akimuonyesha baba chidi, wakati huo mama yake chidi yupo nje ya nyumba hio, moyo ulikuwa ukimuenda mbio…. JAMANI UPENDO WA MAMA NI KITU KINGINE, NA USIKIFANANISHE NA JAMBO LOLOTE LILE,…
"itakuwa ndio hicho nilichokwambia mzee jumaa"
"sasa… Hapa hawafiki mbali"
Mzee juma alisema hivyo huku akichukuwa tunguli zake, na kuchanganya madawa yake mwenyewe ambayo hayajulikani,… Alichana vitambaa vingi na kutengeneza midoli mitano mfano wa watu.. Kisha ile midoli akaiwekea dawa kwa ndani, na kuanza kuisomea.. Lakini katika hio midoli kuna mmoja ni kama mzee kamtengenezea fimbo kabisa… Mzee juma alianza kusima mambo yake, kichina sio kichina kikorea sio kikorea, sijui ni lugha gani aliokuwa akiiongea mganga huyo ambae ni baba wa mama yake chidi, lakini sio wa kumzaa, Ni baba yake mkubwa…
Sasa mzee juma baada ya kuongea hayo mambo yake,… Baba yake chidi alishangaa kuona watu wapo mbele yao, kana kwamba ile midoli ndio imegeuka kuwa watu…. Baada ya kugeuka kuwa watu, papo hapo akawatuma katika njia ya moshi katika gari inayokwenda spidi ya ajabu,….
"nawatuma katika hii barabara…. Mnaiona hii gari hapa"
Aliwauliza hao vinyamkela vyake ambavyo kavitengeneza sasa hivi tu
"ndio tumeiona"
"nendeni… Mkaisababishie ajali hii gari, lakini asiumie mtu wala asife mtu, hakikisheni mnawakinga asiumie mtu hata mmoja"
"sawa mkuuu"
"mkishaisababishia ajali, watu hao muwazimishe… Afu unaona huu mkoba mwekundu hapa"
"ndio"
"huu mkoba una kondomu yenye mbegu za kiume…. Hivyo naomba mchukue hio tu basi"
"tumekuelewa mkuu"
"mkishaipata hio kondomu, ileteni tuiteketeze isije ikavutwa na wenzetu, tukamkosa mjuu wetu… Haya nendeni haraka sana"
Alioosema tu hivyo wale vinyamkela walitoka kama upepo vile,… Sasa hapo mama chidi akaingia ndani japo kuna baadhi ya maneno aliyasikia
"mwanangu punguza presha, hilo limekwisha"
"ahsante baba"
"tena mumefanya vizuri sana kutopuuza ndoto hio,… Bila hivyo, mjukuu wangu angeitwa tu rashidi lakini asingelikuwa na lolote lile"
"Tunashukuru sana baba…. Ila baba, baada ya kufanya hivyo hatuwezi kumkinga na kinga yeyote ile"
"aahhh kiukweli hatuwezi ni mpaka aje yeye, ila kumpa kinga kwa mbali haiwezekani"
"sawa, itabidi tumuite aje umkinge mjukuu wako"
"hakuna shida… Sasa nyie mnaweza kwenda tu nyumbani, nitawajulisha kile kilichotokea"
"sawa mzee, Tunashukuru mzee wangu"
Basi wazazi wa kijana chidi walipanda baiskeli yao kisha haooo wakarudi zao nyumbani…..
Sasa tukija huku njia ya moshi kwa akina mama sarah wakiwa ndani ya gari wanaongea, kwa furaha kubwa sana mana wanakwenda kumaliza tatizo la ridhiwani ambae amezaliwa akiwa hana nguvu za kiume…
Katika kichaka kimoja hivi mbele kabisa, walionekana wale vinyamkela waliotumwa na mzee juma
"sasa hapa tunafanyeje jamani"
"mbona ni kazi rahisi tu, kwa hio spidi yao wanayokuja nayo ni kazi rahisi sana"
"sasa, hebu wewe nenda pale ndani ya gari puliza upepo wa kuwafanya wacheke sana… Ili huyu dereva aangalie nyuma… Na akiangalia nyuma, hapo hapo huyu bibi kizee avuke,.. Afu sisi tutaizungusha hio gari pasina kuumia mtu"
Walipanga mipando yao, kisha wakaanza kugawana kila kinyamkela kiende katika nafasi yake,… Vinyamkela hivyo tayari vilishapangilia mambo yao… Na yule mmoja alienda kwenye gari na kupuliza sumu ya umbea… Yaani waanze kuonge umbea umbea ili vicheko viwe vingi mpaka yule dereva ageuke nyuma… Hivyo kinachotafutwa ni dereva ageuke nyuma kwa utamu wa vicheko vya mama zake…. Baina ya mama sarah na mama saida…..
INAENDELEA...
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni