MUUZA CHIPS (79) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatatu, 12 Juni 2023

MUUZA CHIPS (79)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa

Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA SABINI NA TISA
ILIPOISHIA...
Ibrahim alifurahi sana kuskia kuwa kumepatikana mtoto wa kiume,.. Kana kwamba jasmini ndio kajifungua leo, lakini ndugu msomaji nadhani unakumbuka hii mimba ni yanani,.. Ila chidi hajui kuwa jasmini ana mimba yake, yeye chidi hajui kitu, lakini hio mimba au huyo mtoto ni wa chidi, lakini chidi hajui kitu..

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Pale pale wakiwa wanafurahia kupata kwa mtoto, mara sabra kaja kumvuta chidi pembeni kisha akamwambia chidi

"chidi, hongera kwa kupata mtoto, tena umefanana nae mtoto wako"

Chidi alikuwa hajaelewa mana mtoto wa kaka yako ni wako pia mana atakuita baba kama baba yake, lakini sabra yeye hakumaanisha hivyo, bali sabra anajua kuwa mtoto huyo ni wa chidi na sio mtoto wa Ibrahim kama inavyojulikana,..

"lazima nifanane nae, mana mimi ndio baba mdogo wake"

Sasa sabra akawazaa sijui amwambie ukweli kuwa huyo ni mtoto wake na sio mtoto wa kaka yake… Sabra alikuwa anataka kuharibu hali ya hewa iliotulia..

"chidi…huyo mtoto huko ndani ni mtoto wako,.. Ila ukichelewa kumchukuwa, atakuwa ni mtoto wa tarehe 7 mwezi wa 7"

Sabra aliongea hayo maneno lakini chidi hakuyaelewa…

"mbona sikuelewi sabra"

"utanielewa siku ikifika tarehe 7 mwezi wa 7"

Sabra aliondoka na kwenda wodi ya wazazi na kukaa na dada yake karibu,..

"tarehe 7 mwezi wa 7"

Aliongea sabra huku akimshika shika yule mtoto..

"sabra, hebu funga domo lako… Usiambiwe kitu basi wataka kila mtu ajue"

"dada,.. Leo ni tarehe 7 mwezi wa 4 sasa nani atajua tarehe 7 mwezi wa 7"

"hata kama ila naomba ukae kimya"

"jamani katoto kazuri kama baba yake mzazi… Ila tarehe 7 mwezi wa 7 sijui itakuaje"

Sasa huku nje chidi alikuwa ndio anaumiza kichwa kuhusiana na hio tarehe 7 mwezi wa 7, kuna nini kwenye hio tarehe,… Na leo ni tarehe 7 mwezi wa 4, hivyo kuna miezi mitatu mpaka ifike hio tarehe 7 mwezi wa 7….

Chidi alimfuata kaka yake na kutaka kumuuliza kuhusiana na hio tarehe..

"eti broo… Ivi unaijua hio tarehe 7 mwezi wa 7"

Aliuliza kijana chidi huku akisubiri majibu kutoka kwa kaka yake Ibrahim….

"hapana siijui, mana sijafika huko"

Lakini huku wodini sabra alikuwa akiusifia uzuri wa mtoto huyo…

"ivi dada, ni kweli hio tarehe utafanya hicho kitu"

"nitafanya kama nilivyo agizwa"

Katika maisha kuna njia nyingi za kuyafanikisha maisha,… Na sio kila mwenye maisha basi ana maisha, ila jua maisha yako ndio maisha, mana kuna wanaoishi kwa ajili ya maisha ya watu wengine, hivyo kuwa makini katika kutafuta maisha… Maisha yangu nayapenda sana kwasababu ndio maisha yangu ya kila siku na hayategemei maisha ya mtu,… Na ukiwa unaishi kwa tegemezi la maisha ya mtu basi jua katika maisha haya haya hutokuwa na amani hata kidogo…..

Tuje kwenye simulizi yetu…

Sabra na dada yake walionekana kuna kitu wanakijua katika maisha yao ila kwa sisi wasomaji bado hatujakijua kuwa ni kitu gani hicho,

"eti broo… Ivi unaijua hio tarehe 7 mwezi wa 7"

Aliuliza kijana chidi huku akisubiri majibu kutoka kwa kaka yake Ibrahim….

"hapana siijui, mana sijafika huko"

Lakini huku wodini sabra alikuwa akiusifia uzuri wa mtoto huyo…

"ivi dada, ni kweli hio tarehe utafanya hicho kitu"

"nitafanya kama nilivyo agizwa"

Alijibu jasmini tena kwa kujiamini sana, Sabra hakuwa na cha kumuuliza yena dada yake lakini alionekana kuchukia kwa kiasi fulani ila kwakuwa bado ni mdogo hawezi kuzuia uamuzi wa dada yake, mana katika familia yao ya kitajiri wapo wawili tu,..

Wakati huo huku nje kwa chidi alipigiwa simu na saida

"haloo"

"eee mambo chidi"

"safi hali yako"

"poa tu, sasa chidi… Mimi kuna kitu nataka tuongee"

"sawa ongea tu"

"no, no naomba tukutane mahari please"

"ok poa ngoja nifanye mpango tukutane"

Basi chidi pale pale alimuaga kaka yake kuwa anatoka kidogo wakati huo kaka mtu alikuwa na furaha sana kwa kuoata mtoto mana ndio kilio chake cha siku zote,…

Tukija huku hoteli kwa akina sarah, tunamuona mama sarah akiwa ofisini kwake na mtoto wake wakiwa wanapiga mahesabu ya siku hio, mana kwa sasa hoteli walishainunua toka mama huyo alipwe ile pesa na mama saida kwa ajili ya kumponyesha mtoto wake,… Hivyo hoteli ameshainunua tayari na sasa ipo chini yake,..

"ngoja nikamsalimie chidi wangu"

Aliongea mama sarah tena kwa bahati mbaya, na kujikuta sarah anamuuliza

"chidi wako??… Ina maana mama una mtoto mwingine, na kwanini ana jina la kiislamu"

Mama alijikuta anadondoshewa maswali ya hapa na pale kwa kuropoka kwake..

"sio mtoto wangu, ni mtoto wa rafiki yangu, ila nakapenda sana hako katoto"

Mama sarah alikuwa na njia nyingi sana za kumtoka mtu, huezi amini sarah keshaachwa kwenye mataa, haelewi kitu tena..

"kana miaka mingapi"

"mmmhhh kama kumi hivi au nane"

"mmmhhh haya mi nipo hapa"

Mama sarah aliondoka baada ya kumtoka mtoto wake kimaneno,..

Sasa tukija huku hoteli kubwa, kwa akina miriam,.. Miriam akiwa kakaa katika ofisi yake ya keshia alikuwa akiwaza mambo mengi sana katika kichwa chake,… Kama unakumbuka miezi kadhaa iliopita aliambiwa na mama yake kuwa aende Uingereza kimasomo kisa tu alikuwa na mahusiano na kijana chidi, lakini miriam alifanya ujanja wa kila aina mpaka safari ikafa,.. Na kijana chidi mpaka leo hajaacha kazi katika hoteli hio na mahusiano yao yanaendelea lakini ni kwa siri sana hata mama hajui kama chidi na miriam wanaendelea,..

"chidi mpenzi wangu, mbona leo umeondoka mapema hivyo hata sijakuona"

Aliongea mwanadada miriam huku akiwa na huzuni sana juu ya kijana chidi,.. Inaonekana chidi alikuja asubuhi kisha akaondoka na sasa keshazoeleka tabia yake ya kuja na kuondoka,..

Miriam alichukuwa simu na kumpigia chidi, lakini kumbe wakati huo anapiga simu mama yake ndio alikuwa anakuja pale kwenye ofisi ya miriam,..

"haloo chidi mambo baby"

Mama kasikia hayo maneno ikabidi atulie kimyaa ili amsikilize ataongea nini…

Tukija huku kwa saida akiwa ndio kwanza keshafika katika hoteli walioambizana wakutane, saida alikuwa tayari keshafika katika eneo la tukio,

Wakati huo huo kijana chidi akiwa njiani kuja hapo hotelini, alipokea simu ya mama sarah

"halooo boy mambo"

"safi mamy niambie"

"poa… Nimekumisi kweli yani"

"mmmhhh mamy si juzi tu kushinda jana"

"ni kweli, kwani hio juzi kuna kitu tulifanya"

"kweli, hatujafanya chochote"

"basi leo nipo kwako nakusubiria"

"ooohhh shit tayari umeshafika"

"ndio nipo nje hapa kwenye gari"

"duuuuuu nipo mbali kweli mamy"

"nakusubiria tu hivyo hivyo"

"ok poa"

Basi chidi alikata simu kisha akawa anaelekea hotelini…

Tukija huku hospitalini walipokuwa akina sabra na dada yake,.. Waliokiwa wamesharuhusiwa, Ibrahim akiwa ndio dereva tena alikuwa ni mtu mwenye furaha ya hali ya juu kwa kupata mtoto wa kiume,..

Walipofika nyumbani Ibrahim aliwaaga kuwa anakwenda kazini,… Hivyo Ibrahim aliondoka zake kwenda kazini mana ilikuwa bado mapema sana,

"dada… Si umwambie chidi tu ukweli kuwa ni mtoto wake"

"sabra, naomba tueshimiane sawa"

"lakini sura ya huyu mtoto na chidi, yaani vinaashiria kabisa"

"hata kama,.. Shida yangu sio mtoto kwa taarifa yako, we mshenzi nini"

"dadaaaaa.. Yani mi ni mshenzi"

"tena ukiendelea kunitibua nitakuziba vibao sasa hivi"

Jasmini alibadirika ghafla tena hakuwa mtu wa kawaida, pamoja na uzuri wake na umbo lake lote lenye kuvutia lakini kumbe ana roho mbaya kiasi kikubwa yaani sijui alikuwa na maana gani,..

Sabra hakutaka kuendelea kukaa karibu na dada yake mana wangelitibuana vilivyo,..

Tukija huku ofisini kwa akina Ibrahim, aliokuwa akiwachukuwa wafanyakazi wote ili wakafurahie siku ya kuzaliwa kwa mtoto wake,… Walichukua kosta nzima na kwenda katika hoteli ya Miras hoteli ili kufurahia maisha ya mtoto wake,.. Ofisi ilibaki na mlinzi peke yake, kana kwamba hata kama kuna mteja atakuja basi hatokuta mtu na hivyo ndivyo wanavyofanyaga akina Ibrahim,.. Kisa kampuni sio yakwake,… Lakini walipoondoka tu, Mlinzi kapiga simu kwa tajiri mwenye kampuni ambae ni jasmini

"boss, uliniambia wakiondoka nikuambie"

"enheee vipi wamekwenda wapi"

"sijui ila wameondoka wote kufurahia basdei ya mtoto wake"

"aanhaaaa sawa haina shida… Kuwa makini hapo sawa"

"sawa boss"

Sasa ndio tunaanza kuyaona makucha ya jasmini kumbe jasmini alikuwa ni upole wa bure, lakini ni mtu wa tofauti sana, na hii ni baada ya kujifungua mtoto huyo na ndio maana kaanza kubadilika,…

Wakati huo huo huku nyumba kwa jasmini alikuwa akimpigia simu mume wake ambae ni Ibrahim,.. Mana hawezi kutoka kutokana na uzazi aliokuwa nao hawezi kutoka…

"haloo mke wangu hali yako"

Aliongea Ibrahim lakini ilikuwa ni sauti ya pombe

"sikiliza ibra… Kuanzia hapo ulipo schana na kampuni yangu, fanya mambo yako binafsi"

Ibrahim pombe ilimuisha ghafla bila kutarajia,..

"unasemaje mke wangu"

"kampuni yangu sio ya kuchezea kiasi hicho"

"nimeichezea na nini tena… Ila mke wangu kwa utani wewe tu hujambo"

"sina utani.. Yaani hapo ulipo tu fanya mpango ujue pakwenda sina pesa za mchezo mimi"

Aliongea hivyo kisha akakata simu,.. Jasmini mwenyewe ndio huyo sasa, na sijui ni kwanini alikuwa mpole, yote tutayajua mbeleni….

Sasa tukija huku hotelini kwa akina miriam,.. Akiwa anaongea na kijana chidi

"halooo chidi mpenzi wangu mambo"

Aliongea miriam huku mama yake akimsikiliza kwa umakini

"poa niambie mamuu wangu"

"safi tu babuu…. Sasa mbona umeondoka mapema hivyo hata sijakuona babuu"

"no, nilikuwa hospitali"

"hospitali??… Kuna nini"

"aahhh ni shemeji yangu amejifungua sasa tulimpeleka hospitalini"

"ooohhh sasa si utakuja babuu"

"hapana… Kwa leo kuna ubize nipo nao mamuu"

"nimekumisi babuu"

"ngoja nitakupigia baadae"

"poa"

Ile anakata simu tu mama yake katokea, akiwa kasikia kila kitu kuhusu chidi na mtoto wake,..

"hivi Miriam mwanangu, kumbe bado unaendelea na huyo mjinga wako"

Aliongea mama yake Miriam huku akiwa anatetemeka haswa

"mama…. Kama ni huu utajiri wetu mimi basi lakini huezi kunichagulia sehemu ya kupenda.. Basi wacha niwe maskini kama yeye ili tuendane"

Miriam alichoka kuwa na mahusiano ya kujificha kwa muda wote huo na wakati anampenda sana mpenzi hivyo yupo tayari hata kuwa masikini ili tu aendane na chidi,…

"unasemaje we pumbavu… Yaani wewe ndio wa kuniambia maneno hayo mimi"

"mama, sina maana ya kukuvunjia heshima yako… Ila nimechoka kuishi kama mkimbizi katika mapenzi.. Kiukweli chidi ndio chaguo langu, na tena nataka anioe kabisa"

"funga domo lako mbwa wewe… Tena jiandae uende kusoma… Safari inaanza upya taka usitake utaenda tu"

Miriam alianza kulia kwa kitendo cha kuambiwa ajiandae safari ianze upyaa

"mama… Niachee"

"tena na huyo mwehu mwenzio staki kumuona hapa kazini kwangu"

Aliongea mama yake Miriam huku akiondoka kwa hasira nyingi sana

Sasa tukija huku hoteli flani hivi walipokubaliana wakutane kijana chidi na saida, saida akiwa kamsubiri chidi kwa muda mrefu sana,..

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni