MUUZA CHIPS (87)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: MoonBoy
SEHEMU YA THEMANINI NA SABA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Yaani chidi bado haamini kama hii ishu inakuwa kweli kama jinsi ilivyo, na hakuwa na budi kukubaliana navyo,.. yaani chidi kila akitembea anahisi jela ipo mbele…. Hapo alipo mkononi ana ATM CARD ya miriam, anaijua hii akaunti ina pesa nyingi sana, yaani ina kama milioni 600 hivi, mana anakumbuka siku ya mwisho alipewa hii kadi ili akatoe pesa ya kutuma nyumbani baada ya kusikika wazazi wake wanaumwa, lakini hakuwa yeye ila bingo lilimdondokea siku ile…
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
Sasa tukija huki Dar es Salaam kwa mr Jackson na salma, waliokuwa wakigombana kwa ajili ya siku ya ndoa
"umenitoa kwa mume wangu ili unioe, lakini ona sasa mpaka leo mwaka unaisha huu sioni cha ndoa.. Ilifikia mahari pazuri tuka andaa kila kitu lakini ikaahirishwa.. Ivi una nini lakini Jackson"
Aliongea salma yule mke wa chidi wa kule kijijini, ukumbuke ana mtoto nae mmoja hivyo,.. Sasa wakati huo Jackson alikuwa kimya katulia tu
"sikiliza salma, harusi yetu iliahirishwa kwasababu baba yangu alikuwa anaumwa, kungelikuwa na raha gani ya harusi na wakati baba yupo kitandani,.. Rafiki zake kitoka arusha, mbea, Mwanza, na sehemu nyingi walikuja kwa ajili ya harusi yetu, sasa tufunge ndoa na wakati baba anaumwa"
"sawa, lakini toka baba apone, ni miezi mingapi imepita"
"najua ni mingi sana"
"sasa kwanini hatufungi ndoa,… Jackson kumbuka nimeacha mtoto wangu na mume wangu kwa ajili yako eti"
Sasa wakati anaongea hivyo kumbe familia ya Jackson ilikuwa inasikia, na waliokuwa wakisikiliza ni mama yake na Jackson na dada zake, mana akina Jackson walikuwa chumbani kwao, hivyo walishangaa kusikia miriam alikuwa na mtoto, tena mbaya zaidi kumbe alishaolewa kwa ndoa
"ina maana huyu fedhuli kumbe ana mtoto,.."
Alikuwa ni mama mtu akimwambia mtoto wake wa kike
"mimi hata sijui ndio najua leo"
Salma alikuwa ni mschana mzuri na mrembo sana, hivyo pasina kukuambia kuwa ana mtoto, huezi mjua mana ana umbo lisilo onyesha kama yeye ni mama wa mtoto mmoja,..
"hapana, mwanangu hawezi kuoana na mzee kiasi hicho"
"lakini mama… Wao wamependana,.. Na hata Jackson anajua kuwa huyo mdada ana mtoto"
"hata kama,… Janet? Jackson ni mdogo wako lakini sio haki aoe mwanamke aliokwisha zaa"
"mamaaaaaa…."
"nini…. Ina mana wewe tukutafutie mbaba mtu mzima tukuozeshe"
"sawa kama atakuwa anavutia na tupendane tu"
"nyooooooooooo… Sasa nasema hivi mimi sitaki mkwe aliokwisha zaa"
Mama alikuja juu baada ya kusikia kuwa miriam aliacha mtoto huko kijijini,… Lakini Jackson licha ya kusema kuwa harusi iliahirishwa kwa kuumwa kwa baba yake, pia hakuwa upande wa salma, yeye alikuwa akimpenda mschana mwingine…
"kwahio Jackson.. Utanioa au hunioi"
"ngoja kwanza basiiii"
Jackson alitoka na kukutana na rafiki yake aitwaye jems,…
"woooza jema jems nambie mkali wangu"
Alisalimia Jackson huku wakipeana mikono
"ebana poa.. Nambie bwana jack"
"safi tu.. Leo bata wapi"
Aliuliza Jackson huku wakiendelea kukumbatiana, mambo ya salamu za kizungu
"Maisha Club pale kuna bonge la shoo, watoto wengi kinoma"
"aaahhhhhhh wachaaaa"
"nikutonye na pengine"
"Enheeeee"
"Mnazi mmoja… Kuna party ya maana… Manzese yenyewe kuna party nyingine ya ahatari"
Aliongea jems huku wakijisifu kwa kula bada jijini hapo,..
"tuchague pakwenda sasa jems"
"ahhhhhh lakini we Jackson una demu wako wewe utatoka nae nini"
"aaahhhhhhh uyo mchafu kuoga nani atoke nae"
"eehhhh mchafu kuoga tena?… Mbona umeishi nae muda mrefu ivo"
"waapi.. Nalifariji tu apo ili asijione mbaya,.. Hana lolote mtu mwenyewe keshazalishwa uko kijijini, afu anataka nimuoe"
"lakini Jackson we mnafki wewe…"
"unafki wangu nini sasa na wewe jems"
"si ulitakaga kumuoa wewe, afu mpaka kadi zikaandaliwa kila kitu nini"
"aahhhhh… Sikia sasa ishu yenyewe, ile harusi alijua anaolewa yeye… Lakini nilikuwa namuoa yule demu wangu wa mbezi beach,… Sema tu kuumwa kwa dingi ndio maana imeahirishwa kwa muda tu"
"aahhhhh Ebwana eee we mkali kinoma asee"
Lakini kumbe Salma nae alisikia kila kitu, mana Jackson na jems walikuwa wakiongea nyuma ya nyumba hio hio, bila kujua kuwa Salma alikuwa akiwasikiliza maneno yao… Kwahio salma akajiona kumbe yeye sio kitu katika nyumba ya watu,..
Salma alilia sana na kuanza kumkumbuka mume wake ambae ni kijana chidi,.. Salma alilia sana tena sana, na haamini kuwa kumbe hata ile harusi haikuwa yakwake bali ilikuwa ni ya mtu mwingine.. Alilia sana tena sana.. Ila hatujui atachukuwa uwamuzi gani hapo..
Wakati huo akina Jackson wapo ndani ya gari lake… Yaani Jackson alichukuwa gari yake na kutoka nayo yeye na rafiki yake baada ya kukubaliana wanaenda kula bata sehemu fulani ya kuinjoi mana kama nipe wanazo za kutosha…
Sasa tukija huku jijini Arusha tunamkuta chidi kaingia katika duka la nguo za kike, tena duka la gharama kubwa haswa,.. Chidi alinza kuchagua nguo, magauni, sketi, kanga na kila kitu, sasa kafikia kwenye kuchagua chupi kasahau saizi ya mpenzi wake… Alikumbuka pale alipotoka nyumbani alimuuliza miriam kuwa
"sasa hizo chupi mi nitajuaje saizi yako"
Alimuuliza huku akiiangalia ile chupi nyingine ambayo aliishika miriam na kushindwa kuivaa mana imechafuka kwa vile vitu vya jana…
"heeeeeeeeee ina maana na kunishika shika kote huko jana usiku bado hujakijua kiuno changu ni namba ngapi… Hebu nenda ukoo,.. Kama vipi jipime wewe"
"izo dharau sasa mamuu"
Chidi alitaka kumpiga ile kiutani huku miriam akikimbilia kitandani….
Chidi alimaliza kumbukumbu zake akiwa yupo hapo dukani
"we kaka, nguo hizi hapa unataka saizi gani"
Aliuliza yule dada muhudumu kisha chidi akaziangalia zile chupi, kisha akanyoosha tu mokono…
"nipe size hio hapo"
Alichagua size ile anayopenda kuiona,
"ok… Ngapi"
"mmmhhh nipe kumi,.. Kwani moja ni shilingi ngapi"
"moja ni elfu kumi"
"khaaaaaaaaa…. Hio ni chupi au Dera"
"kaka… Duka letu ni Spesho, sio kama hizo za mtaani"
"mmmhhh haya nipe basi"
"ok.. Sasa kama ni kumi inabidi uchukie kumi na mbili dazeni nzima"
"duuuuuuuuuuuu…. Sawa nipe tu sasa"
Chidi alifungiwa kila kitu na kununua begi papo hapo hapo…
"aahhhhhhhh yaani laki tano imeisha hapa hapa, kwa begi moja tuuuu"
Aliongea chidi huku akitoa pesa mfukoni mana alinza kwenda benki kwanza…
Sasa chidi wakati wa kurudi, akajiuliza maswali
"ivi nikizidi kujificha nitaonekana kweli ninae,.. Sasa dawa ni kwenda huko huko"
Chidi aliamua kwenda kazini huku akiwa kashika begi lake….
"kama kweli mama miriam anahisi mimi ndio ninae mwanae sasa ajue kuwa siko nae"
Chidi alijipa moyo,.. Huku akielekea hotelini na alishaambiwa kuwa huko ni hatari asiende…
Wakati huo huku kwa mama miriam alikuwa akipiga simu kituo cha polisi
"eeeehh haloo afande… Yule kijana nimeshamuita ila sijui kama atakuja"
"hakikisha kama anakuja ili sisi tuje tuizingire hio hoteli yote"
Aliongea afande huyo huku mama akiangaza macho nje kama atamuona, lakini ukweli ni kwamba chidi anakuja na yupo njiani
"ngoja basi nimpigie"
Mama miriam alikata simu kisha akampigia chidi…
Chidi kuona simu ya boss kaipokea chap chap,
"haloo boss"
"eeeew omari.. Upo wapi huku jikoni unasubiriwa utengeneze chipsi"
"nipo njiani nipe dakika tano boss"
"ok sawa"
Mama alikata simu na kuwapigia polisi
"eee haloo afande…. Anakuja, sasa mimi nitawapigia mje hapa hotelini"
"sawa sisi tukiona simu yako tu tunakuja"
Dakika 5 mbele chidi kafika hotelini hapo na yupo tayari kwa kufanya kazi,… Ebwana chidi kawa jasiri wa ujinga, mana kajiingiza jela peke yake,.. Hata wafanyakazi walikuwa wakimuangalia chidi vile alivyokuwa akiingia,..
Wakati huo boss alikuwa yupo ofisini kwake na hajajua kama chedi keshafika.. Ila ghafla simu yake inaita..
"haloo"
"boss, yule omari huyo anakuja yupo ndani, anaelekea jikoni"
Haikujulikana ni nani aliotoa hio taarifa
Ila boss kuskia hivyo tu katoka ofisini kwake na kuja huku jikoni ili kumzuia asiingie kwanza… Sasa ile chidi anataka kuingia tu,.. Aliskia sauti
"we kijana unakwenda wapi uko"
Chidi kuinua macho kakutana na boss uso kwa uso….
PATAMU APO
Baada ya chidi kumaliza kuchagua nguo za mpenzi wake, akiwa anafikiria ni jinsi gani ataweza kujiaminisha kwa mama yake miriam kuwa yeye hako nae bali huenda ni fikra zake tu,.. Chidi aliamua kwenda kazini ili mama miriam aamini kweli chidi haishi na miriam na hako nae, mana kama chidi angelikuwa nae na kama ishu anaijua, asingelikuja kazini, sasa hio ndio sababu maalumu ya chidi kwenda kazini ili ajulikane haishi na miriam na hajui alipo na pia hajui kinachoendelea baina ya familia hio
"haloo"
"boss, yule omari huyo anakuja yupo ndani, anaelekea jikoni"
Haikujulikana ni nani aliotoa hio taarifa
Ila boss kuskia hivyo tu katoka ofisini kwake na kuja huku jikoni ili kumzuia asiingie kwanza… Sasa ile chidi anataka kuingia tu,.. Aliskia sauti
"we kijana unakwenda wapi uko"
Chidi kuinua macho kakutana na boss uso kwa uso….
Chidi hakutaka kuonyesha kama kashtuka baada ya kuitwa na mama miriam au boss wake,.. Lakini aliogopa kimoyomoyo ila hakujionyesha na kujifanya hajui kitu chochote kile baina ya mama huyo na kijana huyo
"shkamoo boss"
Chidi alimsalimia mama miriam huku akiwa kainamisha kichwa chake chini
"marahaba.. Wewe jana ulikuwa wapi"
Mama alijikuta anauliza maswali badala ya kuita polisi,…
"mke wa kaka yangu jana alikuwa hospitalini hivyo tulimpeleka sisi, na hata hivyo nilimuaga boss miriam, hata umuulize nilimuaga kweli boss"
Sasa mama miriam akafikiria mambo mengi, kama kweli miriam yupo kwa chidi, sasa mbona hata yeye hajui… Lakini mama lile begi lilimtia mashaka pia na kuzania kuwa labda chidi alikuwa akitoroka kwa kuhama mji..
"nenda kaendelee na kazi"
Mama miriam alimruhusu chidi aingie ndani lakini nia yake ni kumkamata akiwa ndani huko anaendelea na kazi, ili hata polisi wakija wasipate shida ya kukimbizana nae huku na kule,.. Basi chidi aliona bora akaandae chipsi kisha aondoke zake,….
Chidi akiwa yupo jikoni anaendelea na mapishi ya CHIPSI… Lakini kwake ilikuwa ni mtego wa yeye kukamatwa kiulaini bila tabu..
Lakini wakati chidi anaendelea na kazi, mara ghafla mama miriam kafika jikoni hapo, tena alifika kwa makusudi flani hivi
"we omari kuna kitu gani kimepungua hapo"
Aliulizwa kijana chidi mana yeye ndio mkuu wa wapishi katika kitengo cha chipsi tu… Huko kwingine hahusiki..
"nadhani hata viazi sio vingi kwa ajili ya balansi ya usiku… Ila hebu muulize boss miriam atajua tinafanya nini"
Yaani chidi alikuwa akijifanya hajui kitu, na mama nae pia anazidi kupata mashaka mtoto wake yuko wapi kama huyu hajui,…
"aahhhhh sasa njoo nikuoe pesa tu ukanunue gunia moja kwanza kisha tutaagiza gari ilete gunia kumi"
"sawa boss"
Chidi aliacha ile kazi na kumfuata boss ili akapewe pesa ya kwenda kununua viazi kwa ajili ya usiku,… Lakini mama miriam ana sababu ya kumtuma sio bure tu kirahisi rahisi..
INAENDELEA...
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni