MUUZA CHIPS (88)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: MoonBoy
SEHEMU YA THEMANINI NA NANE
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
"aahhhhh sasa njoo nikuoe pesa tu ukanunue gunia moja kwanza kisha tutaagiza gari ilete gunia kumi"
"sawa boss"
Chidi aliacha ile kazi na kumfuata boss ili akapewe pesa ya kwenda kununua viazi kwa ajili ya usiku,… Lakini mama miriam ana sababu ya kumtuma sio bure tu kirahisi rahisi..
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
Chidi alichukiwa tax na kwenda sokoni kununua viazi, wakati huo mama yupo juu kabisa ya ghorofa akimwangalia chidi anavyo ondoka kwenda sokoni kununua viazi gunia moja…..
Sasa tukija huki kwa mama sarah akiwa yupo hotelini kwake, wakati huo sarah mwenyewe yupo ofisini kwake na wakati huo ana hamu ya kukutana na chidi ila sema bize inamzidia…
Lakini wakati huo mama sarah yeye alikuwa na mawazo mengi sana juu ya kijana wake chidi,
"yaani chidi ananifanyia hivi kweli,.. Anatembea na mtoto wa rafiki yangu kipenzi, hapana lazima waachane"
Aliongea hivyo mama sarah huku akishika simu yake na kutaka kupiga,..
Alifikiria mengi sana lakini ghafla anaahirisha kufanya hivyo, mana kuna jambo kaliwaza kubwa sana kiwa.. Endapo atanwambia mama miriam kuwa anajua mwanae alipo, chidi atakamatwa afu mama sarah anatamani kumtoa, hapo lazima watu wajue chidi na mama sarah wana mahusiano ya kimapenzi, hivyo ndio mana kasita kufanya hivyo,…
Wakati huo sarah anapiga simu kwa chidi
"haloo chidi mambo"
"poa baby nambie"
"safi tu.. Nimekumisi baby"
"mimi ni zaidi mamy"
"leo lazima nije kulala kwako"
Aliongea sarah huku akitia ulazima wa kwenda,..
"Sarah usije.. Dada yangu kaja"
"waaooooo… Safi sana nataka nije nimjue wifi yangu"
"amnaaa, sema nae yupo bize…"
"kwani huyo dada yako analala hapo hapo"
"kwani si yule mdogo wangu.. Yupo bize na shule hivyo mchana hutomuona na usiku atakua kalala"
Chidi alizidi kujitetea kwa njia hio lakini anajua fika kule nyumbani kwake hakuingiliki mana kuna miriam, na pia chidi hajui kama sarah na miriam ni marafiki tena zaidi ya marafiki, na siku wanajua hii ishu sijui itakuwaje…
"na gesti je, pia itakuwa ngumu kuja"
"labda huko, lakini nikipata nafasi ndio nitakwambia uje hoteli flani tuinjoi au sio baby"
"sawa baby"
Simu ilikata kisha sarah akaendelea na kazi zake huku moyo wake ukiwa mweupeee
Sasa tukija huku kwa chidi, alikuwa anarudi kazini kutoka sokoni alipotumwa kununua viazi,.. Aliisimamia ile kazi vizuri sana kisha akaingia jikoni kuendelea na kazi,…
Lakini haikupita hata nusu saa simu yake iliita, kucheki jina alikuwa ni kaka yake Ibrahim,…
"haloo kaka shkamoo"
"samahani kijana wewe ni ndugu yake na Ibrahim"
"ndio kwani we nani"
"mimi ni dokta tunahitaji uje hospitalini mara moja"
"hospitali gani dokta"
"maunt meru hospital"
"ok nakuja dokta"
Simu ilikata, kisha chidi akaenda katika ofisi ya bosa wake
"boss, kuna shida kidogo naomba ruksa"
"shida gani tena omari, hizo CHIPSI zitaandaliwa na nani"
"biss, kaka yangu anaumwa sana na yupo hospitalini"
"Ufyuuuuuu…. Lakini umeshatengeneza kidogo mpaka jioni"
"zipo mpaka jioni, na pia sio kuwa sintorudi, naenda kumuona kisha narudi boss"
"ok hebu nenda.. Afu una pesa ya hospitali"
Heeeeeeeeeee chidi alishangaa sana leo anaulizwa mambo ya pesa,.. Na pia inashangaza kwanini mama miriam keshabadirika ghafla, yaani kawa mpole kama maji ya mtungi na hata sijui ni kitu gani kimemfanya awe katika hali kama hio
"ndio boss ninayo"
"sawa ila saa 10 uje, uandae chipsi za usiku sawa"
"sawa boss"
Chidi aliingia jikoni na kuchukuwa begi lake, kisha akamuaga rafiki yake saidi
"oyaa saidi, mi nawahi hospitali aisee"
"hospitali??… Kuna nini"
"braza Ibrahim anaumwa aisee"
"aaaahhh chidi acha utani"
"kweli na ndio naenda sasa hivi"
"daaa mpe pole aisee, unajua wewe ndio unaepewa nafasi ya kutoka, lakini sisi hatupewi nafasi hio"
Chidi hakutaka kupoteza muda aliondoka lakini huku nyuma mama miriam alikuwa akioiga simu, yaani huyu mama anakula na kupuliza hataki akukwaze,..
"haloo afande"
"yes bosa sema tuje sasa"
"hapana msije kwa leo"
"sawa boss"
Je? Ni kwanini mama miriam kaahirisha kumkamata chidi, hatujui ni kwanini lakini ndio imekuwa hivyo…
Chidi alichukuwa tax, ili awahi nyumbani kwanza kumpa miriam nguo zake, kisha aondoke kwenda hospitali,…
Robo saa mbele kijana chidi anafika nyumbani, na kumpa miriam begi lake lililojaa nguo mpya zote
"chukuwa hebu jaribu hizo za ndani… Afu halima yupo wapi"
"atakuwa nje anacheza, ila keshakula tayari"
Sasa begi lilipofunguliwa lilionekana kuchanguliwa sana,… Lakini chidi alipotezea na kuona labda ni mtikisiko wa gari…
"sasa mbona na hii ATM CARD umeiweka huku kwenye begi"
"aahhhhh ni pale dukani, nilikuwa na haraka sana, sasa nikaona uvivu kuiweka kwenye waleti, ndio nikaitupia tu humo kwenye begi"
"iiiiiii una hatari babuu"
"sorry mamuu wangu"
Basi miriam alianza kujaribu zile nguo, na zilimuenea vizuri sana, yaani chidi kama alipima kiuno cha mtoto wa kike,.. Na nguo zote alizipenda…
"sasa mamuu… Nilikuwa nina ombi moja"
"nini tena babuu"
"kaka yangu anaumwa sana na nahitajika kule hospitalini"
"sasa wataka nini"
"nilikuwa naomba nitembee na hii kadi yako ya ATM ili iniseidie kwa mambo madogo madogo, si unajua wenyewe mnavyochelewesha mishahara"
"Khaaaaaa sasa kitu kidogo hicho unaniuliza mimi.. Kwani huyo kaka yako hanihusu mimi??… Ebu twende uko"
"hapana miriam, hutakiwi kwenda.. Afu leo nilikuwa kazini"
"Whaat??… Ulienda kazini.. Na umefanya kazi"
"ndio"
"waaooooo Amaizing thing, so i wish mama kakukubali"
"ila nimewnda kwa kujifanya sijui, hivyo hajui kama nipo na weww, mana hata mimi nimejifanya sijui kama haupo pale kila saaa nakuulizia"
"ahahahahahaha,…"
Saa ngapi miriam asimrukie chidi na kuanza kupeana madenda ya hali ya juu,..
"omari… Leo usiku nakupa haki yako, sintoogopa tena"
"aahhh tena umenikumbusha, wewe hufai kabisa wewe"
Aliongea kijana chidi huku akiondoka
"babuu jamani, leo usiku ntoe bikra bwana nipo tayari"
"wapi uongo tu"
"kweli babuu, yaani leo nakupanulia pyuuuu"
"kwendaaaaa huna lolote wewe"
"sasa utaona leo, labda ushindwe mwenyewe"
Basi chidi hakutaka kuchelewa kwenda hospitalini…
Ile ile tax iliomleta nyumbani ndio hio iliompeleka hospitali,.. Kijana huyo alifika hospitali na kuanza kuulizia wodi aliolazwa kaka yake,… Chidi bila kuchelewa alikwenda ofisini na kuuliza wodi aliolazwa mr Ibrahim
"shkamoo dokta"
"mara haba ujambo kijana"
"sijambo… Aahhh mzee mimi ndio mdogo wake na Ibrahim"
"aaahhhh ndio wewe eee"
"ndio dokta"
"hebu nikuulize, kaka yako alikuwa anaishi ishi vipi"
"kivipi dokta…. Lakini hebu tuulizane baadae nataka nimuone broo yupo wodi gani"
"kijanaaa, punguza hasira,… Ila nitakachokwambia usishtuke"
"una maana gani dokta… Hebu niambie, nisishtuke kwa sababu gani"
Chidi alianza kupata wasiwasi juu ya maneno ya dokta…
"sikiliza kijana, nisitake kukuzungusha sana mana wewe ni mtoto wa kiume,… Ukweli wa hali ya kaka yako ni kwamba…
kaka yako kapatwa na mshtuko wa ghafla uliopelekea kufumua magonjwa mengine yaliojificha"
Aliongea dokta huku chidi akiwa na wasiwasi juu ya kaka yake,..
"kwahio sasa nini kifanyike ili kaka yangu apone"
"aahhhh hospitali yetu ni kubwa lakini kwa bahati mbaya haina madaktari bingwa, hivyo ombi letu sisi ni ninyi ndugu mtie saini, kisha mgonjwa ahamishwe hospitali"
"sasa dokta, kama hospitali hii imeshindwa, je? Ni hospitali gani tena itakayoweza matibabu ya kaka yangu"
Aliongea kijana chidi huku akiwa na jazba juu ya dokta huyo
"hapana kijana… Hatumaanishi apelekwe hospitali ya hapa jijini, bali anatakiwa apelekwe Dar es Salaam"
"duuuuuuuuuuu…. Dar es Salaam… Huko Dar es Salaam anakwenda na nini"
"kwakuwa ni mgonjwa na hahitaji mtikisiko wowote ule itabidi pande ndege"
"UuuuuuuuuuuuWiiiiiiiii haya mambo ya ndege tena ya nini jamani dokta.. Au gharama zinakuwa kwa nani"
"kwa familia yake"
Chidi alichoka na kuchoka kabisaa baada ya kusikia mambo ya usafiri wa ndege unamuhusu.. Chidi alijikuna kichwa kisha akatoka nje na kumpigia simu Miriam
"aahhhhh nimesahau kumbe simu yake kaizima duuuu"
Aliongea chidi baada ya kusikia simu haikuwa ikipatikana kwa wakati huo
Kijana aliita tax kisha akarudi nyumbani, alipofika kitu cha kwanza alimkimbilia Miriam na kumuomba kiasi cha pesa,.. Unajua chidi sio kuwa hana pesa ila kuna vipimo anavipima kwa miriam, lakini kwa pesa anazo tena za kutosha tu, japo hakuti pesa za mpenzi wake huyo,..
"Enheee Babuu vipi shem anaendeleaje"
Aliuliza miriam huku akionekana kuwa na wasiwasi sana juu ya shemeji yake…
"aahhh hali yake ni mbaya sana, ila kuna kitu kinaniumiza kichwa"
"nini tena babuu, nawewe unaumwa tena au"
"hapana siumwi, ila nina shida kidogo"
Aliongea chidi huku akiwa anataka kuomba kiasi cha pesa mana karuhusiwa kuitumia pesa ila sio kwa nauli za ndege,
"nini kwani jamani babuu"
"kaka yangu, anahitaji kuhamishwa hospitali apelekwe Dar es Salaam, ila hatakiwi kutumia gari, lakini sas…"
Kabla chidi hajamaliza kuongea kanyamazishwa na Miriam
"shiiiiiiiiiii…. Tulia hapo hapo,.. Ivi we mwanaume umeshaona tuna pesa za kuchezea eee"
Miriam kageuka, hata chidi haamini kama miriam angelikuwa mkali kiasi hiki,
"lakini sijatumia mamuu kama ni kadi yako hio hapo"
Lakini ghafla miriam alianza kucheka tena kicheko cha kutoa mpaka machozi kabisa
"ivi mi naweza kuigiza eeee…. Sema nimecheka mapema, nilitaka nione ujanja wako"
Miriam aliongea hivyo huku akikaa kitandani mana alinyanyuka wakati ule anamsuta chidi wake
"una maana gani"
"No, nimekutania tu babuu,.. Sasa huyo shem keshapanda hio ndege au"
"bado, si ndio nimekuja kuomba kwanza"
"ivi kwanini unajali pesa kuliko utu, ina maana mimi huyo kaka yako hanihusu mimi"
Chidi kuskia hivyo wala hakuchelewa kushangaa shangaa, alitoka na kuita tax mpaka hotelini, lakini kabla ya kwenda ofisini kwa boss, alimpitia saidi na kwenda nae mpaka kwa boss sasa haijulikani kuna nini hapo
"nimerudi boss"
Aliongea chidi baada ya kufika ofisini kwa boss ambaye ni mama yake na miriam,.. Na wakati huo saidi yupo kwa nyuma
"sawa endelea na kazi"
"hapana boss"
Mama miriam alishtuka kuskia chidi kakataa kuendelea na kazi,
"kwanini"
Aliuliza mama miriam huku akiwa na wasiwasi
"kaka yangu anaumwa sana, na anahamishwa kwenda Dar es Salaam, hivyo kule Dar es Salaam hakuna mtu wa kuwa nae,.. Hivyo naomba ruksa kati ya mimi au saidi aende kuwa nae kule Dar es Salaam"
Mama kuskia hivyo akapumua kidogo mana alijua chidi ndio anatoroka na mtoto wake nini japo hana uhakika sana kama chidi yupo na miriam, mana kama angelikuwa nae angeliogopa kuja kazini…
"kwani huyu kijana mnafahamiana"
Aliuliza mama miriam huku akishangaa,
"ndio.. Huyu ni mtu wa kijijini kwetu"
"Alaaaaa, mbona taarifa za kujuana kwenu sizijui mimi"
INAENDELEA...
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni