MZIMU WA WAUFU (12)
Zephiline F Ezekiel
---
Jina: MZIMU WA WAUFU
Mtunzi: Maundu Mwingizi
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Mvua alikua kubwa mithili ya enzi zile za Elnino, takribani nusu saa ilinyesha mvua kubwa ya mawe iliyofanya hali ya pale porini kuwa ya kutisha na kuogofya sana
Baada ya nusu saa ya kunyesha mvua ya kishindo sasa hali ikaanza kua shwari, mvua ilianza kupungua na hatimae kukatika kabisa
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Ilipokatika sasa Masu akiwa almelowana chepechepe akaanza kuangaza huku na kule kama atamuona mzee Kishindo lakini hakumuona ila kilichomshangaza zaidi hakuliona Basi walilokua wamepanda haikuchukua muda mrefu akasikia sauti ikimuita kwa kasi
“Masuuuuuu, njoooo” Masu akageuka haraka aliifahamu vema ile sauti, ilikua ni ya Mzee Kishindo, sauti ile ilikua ikitokea kwenye kichaka kikubwa tu upande wa mashariki mwa pori lile, Masu akakimbia mpaka maeneo yale na punde akamuona Mzee Kishindo akiwa amekaa chini, cha ajabu licha ya Mvua kubwa iliyonyesha lakini mzee Kishindo hakua amelowana hata kidogo
“Mzee vipi? Ulikua wapi?”
“Lete haraka ule USINGE wangu, tumeshavamiwa na Waufi “
“heee, Mzee usinge umo kwenye Basi na Basi lenyewe hata silioni itakua limeshaondoka”
“Kwanini sasa ulishuka jamani? Tumekwisha sasa”
“Sasa ningefanyaje maana uliposhuka wewe kwenye Basi ukachelewa kurudi ndo maana ikabidi nishuke kukuangalia”
“Halafu mbona umelowana hivyo?”
“Mzee inamaana wewe hukuiona mvua hii yote? Mvua kubwa yam awe mpaka mie nikawa sioni mbele”
“Mvua gani? Mbona mie sijalowana?” Masu alipigwa na butwaa, akaendelea kumuhoji Mzee Kishindo
“Kwani imekuaje mpaka ukasema kua Waufi wameshatuvamia?”
“Wakati nikiwa najisaidia hapo kichakani ametokea kijana mmoja mweupe kiasi ana Jicho bovu…” Kabla Mzee Kishindo hajamaliziakuongoa wakasikia mlio mkali sana kama wa Simba aliyejeruhiwa na ghafla akatokezea mnyama mmoja mweusi, mnyama wa ajabu haelewekua ni aina gani ya mnyama, akaanza kuja kwa kasi ya ajabu usawa ule waliokua wamesimama Masu na Mzee Kishindo
“TOBAA.. Masu kimbiaa” Mzee Kishindo alipayuko kwa hofu, wakatimua mbio za hatari, wao mbele yule mnyama nyuma, walikimbia kwa muda mrefu na kwa umbali mrefu mpaka wakabaki hio bin taaban bila ya kujua hatima yao ni nini na ghafla walipogeuka nyuma hawakumuona tena yule myama,
*****
“Khaa!! amepotelea wapi?” aliuliza Masu
“Mungu wangu hii sasa ni hatari kabisa”
“Sasa tutafanyaje hapa Mzee?”
“Tusubiri kufa tu, maana Usinge nao umeutelekeza kwenye Basi” wakiwa wamesimama wako hoi kwa zile mbio za bila kutarajia ndipo tena mvua ikaanza kunyesha ikabidi sasa wakimbile kwenye mti mkubwa uliokua pembeni ili wajisitiri, walipofika tu chini ya mti ule yaani kitendo bila kuchelewa Ikapiga RADI kubwa na yanguvu ikamrarua hapo hapo mzee Kishindo, akakauka na kua mweusi kama mkaaPia Radiu hiyo ikaunguza na ule mtiwaliokua wamesimama ukawa sasa unawaka moto tu! ilikua ni Radi ya hatari kisha mvua ikazidi kuchukua kasi yake, hakika Masu alikua amechanganyikiwa kisawasawa , akaanza kulia huku akiukimbia mwili wa Mzee Kishindo uliokauka kama vile ulio chomwa kwenye tanuri la mkaa, wakati masu akiwa ametaharuki ndipo tena alipomuona Yule mnyama mkali asieleweka akija tena kwa kasi inaonekana kama aliekua amewapoteza machoni pake akina Masu na Mzee Kishindo ambae tayari bila shaka ameaga dunia kwa Radi ya ajabu iliyomtandika vilivyo, Yule Mnyama
alionekana ana ghadhabu ya hali ya juu..
Masu akaanza kukimbia kwa kasi ya nguvu, sasa yule mnyama alikua amedhamiria kabisa kummaliza Masu, na sasa alikua akizidi kumkaribia, Masu alikua ameulenga mti mmoja mkubwa ili akifika ajaribu kukwea japo hakua na uwezo mkubwa wa kukwea miti, ila alijipa moyo kua angeweza tu bila ya kujali hata kama Mnyama huyo nae anaweza kukwea mti pia. Mnyama Yule alikua anakimbia kwa kasi kubwa kiasi sasa cha kumkaribia Masu, sasa Masu akajua kua mwisho wake umefika akaanza kulia kwa sauti kubwa sana lakini haikusaidia kitu, ilipobakia hatua kadhaa mnyama Yule amkamate Masu Masu akaongeza Speed kwa nguvu zake zote, Laa Haula!! Kumbe mbele kulikua na Shimo kubwa sana Masu hakulitambua hilo masikini! akatumbukia, lilikua ni Shimo refu kupita kiasi, Masu aliendelea kwenda chini bila kufika mwisho huku akijipigiza hovyo pembeni mwa shimo hilo bila ya kufika mwisho, hakujua kama lilikua ni Korongo au ni shimo la aina gani maana aliendelea kwenda chni bila ya kujua
atafikia wapi na muda gani.. hatimae alianza kusikia kizunguzungu kutoka na na kasi kubwa iliyokua ikimpeleka chini na hapo ndipo sasa akaanza kujua kua halikua shimo la kawaida bali itakua ni nguvu tu ya Waufi maana sasa ilichukua takribani masaa matatu akiwa anaenda tu bila kufika mwisho wa shimo hilo na hajui yataongezeka masaa mangapi kabla ya kufika chini, Pumzi ikawa inamuishia kutokana na upepo mkali aliokua akikutana nao wakati anazidi kwenda chini
DAR ES SALAAM
Nyumbani kwa Mzee Kishindo kilio kilikua kimetawala, watu wengi walikua wamejumuika, wake kwa waume, ndugu na majirani wote walikua wakilia kwa uchungu mkubwa, ni baada ya kupokea taarifa kuwa Mzee Kishindo amefariki kule Porini aliposhuka kujisaidia akapigwa na Radi kali, taarifa hizo zililetwa na Polisi baada ya kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo…
“Jamani samahani, kwani ilikuaje?” aliuliza mzee Jfari jirani yake na Bw Kishindo, alimtupia swali hilo Sheikh Jabu aliekua tayari ameshawasili hapo msibani
“Kwa maelezo tuliyoyapata kutoka kwa mkwewe ni kwamba Kishindo na Masumbuko yule kijana wa Mzee Kikoko walikua safarini wakielekea Tabora lakini masaa mawili yaliopita amepokea simu kutoka Polisi kua mumewe amefariki kwa kupigwa na Radi ndipo akanipigia mimi haraka nikaenda Mochwari kuutambua mwili”
“Duh jamani mbona kama siamini vile!! Kishindo huyu huyu nilikua nae jana hapa?”
“Ndio huyo hivyo hakuna cha ajabu hapo, kwa Mungu ni madogo hayo, ila mwili umeharibika hivyo tunasubiri tu Ruhusa ya daktari tukauchukue mwili tuje tuusitiri, cha ajabu huyo Masu aliekua nae hajulikani alipo, wanadai amepotelea hukohuko Porini, yaani hizi taarifa zinachanganya sana”
“Hajulikani? Kivipi?”
“Inasemekana kua Mzee Kishindo alishuka kweny Basi kwenda kujisaidia lakini akachelewa sana kurudi ndani ya Basi hivyo sasa Masu akaenda kumuangalia lakini nae hakurudi wakati huo mvua kubwa ikawa inanyesha, na kabla ya mvua kukatika ndo ikapiga Radi kubwa, mvua ilipotulia ikabidi abiria washuke kwa ajili ya kujaribu kuwatafuta, ndipo walipomkuta Mzee Kishindo akiwa amefariki kwa KUPIGWA NA Radi hiyo mpaka kakauka, Lakini Masu hawakumpata kabisa”
“Mmh, haya sasa Maajabu’
Masu aliendelea kwenda chini na hatimae akajikuta ameanguka kama mzigo au kifurushi, Naam Maajbu na mauzauza yameanza tena kwa Masu, kajikuta ameangukia katikati ya Zizi la Ng’ombe, cha Ajabu na yeye ni Ng’ombe pia, japo ameumia kwa jinsi alivyoanguka vibaya lakini sasa anastaajabu kujiona katika hali ile, akaanza kuhata hata, inaonekana hata wale Ngo’ombe wenzie wameshangaa kumuona pale bila shaka hawamjui kabisa, kulikua na Ng’ombe wakubwa sana, wana pembe mpaka zimejikunja kwa juu ya vichwa vyao, Masu akaanza kulia kwa woga lakini haikua sauti yake ile ya mwanzo, ilikua ni sauti mujaribu ya Ng’ombe, Ghafla akaanza kupokea kichapo cha haja kutoka kwa Ngo’ombe wenzie, Masu akawa anavuja damu kichwani baada ya kuchomwa na pembe la mmoja kati ya wale Ng’ombe waliokua waimuadhibu,,
Masu akiendelea kujaribu kujinusuru na kichapo kutoka kwa Ngo’ombe wenzie ndipo akawaona watu watatu wakija mpaka pale kwenye zizi, akawa anasikiliza mazungumzo yao, anatamani kuwajibu lakini kila akitaka kuwasemesha sauti inatoka kama ya Ng’ombe wengine tu, hali hiyo ilimtia sana uchungu sasa ikabidi tu atulie asubiri hatma yake, huku mazungumzo ya wale mabwana yakiendelea
“Mzee Songoro sisi ni ndugu zako na tumepatwa na msiba hivyo tunataka Ng’ombe kwa ajili ya pale msibani hivyo tufanyie tahfuf kidogo” aliongea mmoja kati ya wale vijana wawili
“Ni kweli, hata mimi na marehem Kishindo tulikua na ujamaa pia ila hiyo be nimewatajia ni ya chini kabisa kwakua tu nawafahamu na nimeangalia uzito wa jambo lenyewe” Masu alizidi kushangaa kusikia zile taarifa kua hawa jamaa wamekuja kununua Ngo’ombe kwa ajili ya kwenda kuandaa chakula msibani kwa Mzee Kishindo, alianza kulia baada ya kuamni sasa kua Kishindo amekufa, laiki alizidi kushangaa kua yaani pamoja na kuzama kwenye lile shimo kule kumbe ametokezea tena sehemu uliko msiba, hakika alijua kua amepatikana
Baada ya makubaliano ya muda mrefu sana hatimae wakaafikiana bei, wakalipana pesa, kisha Mzee Songoro akaingia zizini na kumkamata Masu(Ambae kwa sasa kawa Ngo’ombe) halafu akaanza kumfunga kamba, na baada ya muda ikaja gari na kumbeba Ng’ombe huyo na kumchukua mpaka msibani, Walipokua njiani Masu alishangaa kuiona mitaa ya jiji la Dar es Salaam, akajua kua kumbe amerudishwa kule kule mjini na sasa anakwenda kuchinjwa, Roho ilimuuma lakini hakua na ujanja tena na Baada ya muda akawa amefikishwa nyumbani kwa Mzee Kishindo, akateremshwa kwenye gari na akafungwa kwenye mti kwa kamba ngumu ya manila, Hali ya pale nyumbani ilithibitisha kua Kishindo hayupo tena duniani watu walikua wakilia kwa uchungu sana, Masu alimuona Sheikh Jabu, pamoja na vijana kadhaa kutoka kule dukani wanakokwenda kupiga stori, nao walikua katika majonzi na simanzi ya hali ya juu, kilichomuuma zaidi aliwaona kwa pembeni wanawe wadogo wale mapacha wakiwa wamesimama pale uani japo
hakumuona mkewe yaani Masu alipatwa na uchungu wa aina yake aisee
“Sasa jamani tugawane majukumu hapa haraka haraka kwakua wenzetu wameenda kufuatilia mwili, sasa sisi tungeanza majukumu mengine ya kupanga mazingira wakati wengine mkamchinje kabisa huyo Ng’ombe na mumchune kabisa” alikua ni Sheikh Jabu akijaribu kugawa majukumu pale msibani
“Sawa ila hapa hakuna mtaalam wa kuchnja Ng’ombe, Labda mumuite Mzee Kikoko ndio hua anachinja Ng’ombe” alijibu kijana mmoja pale msibani lakini alikatishwa na Jabu
“Mzee Kikoko hayupo ameenda kule ilipotokea hii kadhia, si mnajua mwanae kapotea ghafla huko ndio ameenda Polisi kujaribu kumtafuta”
“Aaah sasa nani ataweza kuchinja?”
“Ngoja nijaribu kuuliza hapo nje kwa hao waliokaa kwenye jamvi kama kuna mtu wa kuchinja” Sheikh Jabu akatoka, Masu alikua akiyasikia mazungumzo yote yale, alikua akilia kwa uchungu lakini haikusaidia kitu, alionekana kua ni Ng’ombe tu
Baada ya Muda Sheikh Jabu alirudi akiwa na kijana mmoja amevaa kofia ya kibaraghashia, bila shaka ndie Mchinjaji mwenyewe maana tayari ailiakua na kisu kikubwa mkononi, Masu alivyoinua macho AFANALEKI!! Alikua ni Hunudu Bin Waufi, Hunudu alisogea mpaka pale kwa Ng’ombe kisha akawaita wale vijana
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni