Simulizi Mpya
Tidak ada notifikasi baru.

MZIMU WA WAUFU (15)


SEHEMU YA KUMI NA TANO
TULIPOISHIA...
Makaburini hapakua mbali sana na nyumbani hivyo safari ya mwendo wa miguu tu ilitosha kuwafikisha katika viwanja hivyo vya makaburi ndani ya muda wa kama nusu saa hivi, na taratibu zote za mazishi zikafanyika na hatimae Kishindo akazikwa, ilikua ni huzuni na vilio kila kona, vijana kwa wazee walishindwa kuzificha huzuni zao na kuangua vilio hukohuko makaburini

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
Hapakua na Jinsi tena maana neon la Mungu limetimia, Wafiwa na ahali zao wakarejea nyumbani baada ya kumalizia dua ya mwisho katika kaburi la Marehemu Kishindo

MKOANI SHINYANGA, Kama ilivyo ada nje ya nyumba ya Mzee Kagomba hukusanyika watu wa rika tofauti kwa ajili si tu ya kununua kahawa bali pia kupashana habari zinazojiri ndani na nje ya mkoa wao, na kwa siku hiyo habari iliyochukua ‘Ukurasa wa mbele’ katika kijiwe hicho cha kahawa maarufu kama BBC ni taarifa za matukio yanayoendelea huko jijini Dar katika familia ya swahiba wao Mzee Kikoko, walikua wakizipata habari za matukio yote kupitia kwa wenzao kadhaa walioko huko, na kwakua Kikoko mwenyewe alishapata kuwaeleza kila kilichokua kikimsibu mwanae kupitia Ndoto ya ajabu,

“Unajua tangu mwanzo sisi tulimuhadhari Bw Kikoko kua hiyo Ndoto ya mwanae si kitu chepesi kiasi hicho na tukamnasihi kua aende kwa Mzee Maguno huenda akasaidiwa ushauri na tafsiri ya Ndoto hiyo ya mwanae lakini Mjuaji Yule akatupuuza..” Mzee Kagomba alikua akizungumza na hadhira ile iliyojikusanya kuizunguka meza yake ndogo ya kahawa, Bahati nzuri siku hiyo mzee Maguno nae alikuwepo kijiweni hapo, akamuwahi kumdakia neno Mzee Kagomba

“Kwangu asingeweza kuja kwakua mimi naijua vema kesi yao hiyo ya Mizimu ya Waufi”

“Ni mizimu ya waufi au Dini ya waufi? Maana sisi tulisikia kua ni dini”

“Hakuna dini ya hivyo hiyo ni mizimu ya huyo mkewe mkubwa, ila katu hawatomuweza Masu japo ni kijana wao wenyewe, mwenzao anasaidiwa na Mizimu kutoka Kigoma kwa babu yake mzaa baba na pia anasaidiwa na mizimu ya umamani kwake Tabora” Maneno haya yalionesha kuwaingia sana watu wote pale, ikawa kimya kimetanda mpaka Mzee Kagoma alipovugumiza swali kwa Mzee Maguno

“Sasa mnatuchanganya, huko Tabora kwa mama yake gani wakati mama yake ni huyuhuyu Mama Masu wa hapo kwa hayati bwana Masanja, na inakuaje unasema kua hiyo mizimu ya Waufi ni ya mke mkubwa wa Kikoko wakati huyo mke mkubwa ndie mama yake mzazi na huyo Masu?” Mzee Kishindo akacheka kidogo, kisha akajiweka sawa katika kiti chake kirefu cha uvivu kilichofungwa kwa kitambaa cha rangi ya maziwa ili aanze kuwapa somo wadau wa BBC KAHAWA. Lakini kabla hajasema chochote aliwasili motto mkubwa wa Mzee Kangomba anaefanya kazi ofisi za Tanesco, anaitwa Abuu, alipofika akawasilimu

“Wakubwa Shikamooni”

“Marahaba..”

“Jamani mna habari za mjini huko au mmekaa tu?” Swali hili liliwashtua wanywa kahawa wote na kufanya Mzee Kagoma amjibu manae huyo

“Habari gani tena mwenzetu?”

“Mzee Kasimba amefariki huko”

“We motto!! Kasimba Amefariki?.. Innalillah..”

“Kasimba ndo nani huyo?” aliuliza Mzee Maguno aliekua ameunika kidogo kwa mshituko kutoka pale katika kiti cha uvivu alichokua amejiegesha

“Aaah yaani we humjui Kasimba? Sema tu mtu kidole unamjua ukimuona ni shemeji yake na Bwana Kikoko”

“Aaah nimeshamjua si ni Yule bwana mrefu anapenda kunyoa kipara muda wote pia hua kama mgangamganga hivi?”

“Naam huyo huyo, na huo uganga ni wa urithi kutoka kwa marehemu babu yao” Watu wote walisikitishwa na taarifa zile, ndipo sasa Mzee Maguno alipomgeukia tena aliezileta habari hizo ambae ni Abuu

“Enhee, alikua anaumwa? Na amefariki saa ngapi?”

“Sasa ninyi ndo mnajifanya eti BBC halafu hamna habari nyeti kama hizo, hamna u BBC wowote” Abuu alijibu kwa mzaha huku akimuangalia usoni mzee Maguno ambae alikua kama hamuoni vizuri kutoka na mwanga hafifu wa chemli ndogo iliyopo juu ya meza ya kuuzia kahawa

“Embu acha upuuzi wako bana, hii ni BBC ndo maana hata wewe umetoka na habari zako huko na kuja kuripoti hapa kitu kikuu cha habari Shinyanga mjini” Watu wote wakacheka kwa pamoja kabla ya Abuu kuanza kuwapa habari zilizozidi kuwaacha vinywa wazi

“Yule bwana amekufa ghafla, amekutwa katika vile vijumba vyake vya kufanyia mambo yao ya uganga mnaviita ‘Nzu’ Akiwa na jeraha dogo kifuani upande wa kushoto lililotengeneza tobo, Baadae imegundulika kua alinyofolewa moyo kwenye jeraha hilo, na pia amekutwa na alama za vidole na michubuko kama vile alikabwa sana kooni na kukwaruriwa kwa kucha maeneo ya Shingoni” watu walizidi kupigwa na mshangao huku wakimkodolea macho Abuu ili aendelee kuwapa habari,

“Ebwana eeh, mbaona mauji ya kinyama sana!! Sasa kama hizo alama za kucha na vidole ni za muuaji basi lazima atapatikana kama hakuzitifuta kwa kitambaa, siku hizi teknolojia imekua sana” alisema kijana mmoja aliekua ameketi tu bila ya kinyaji maridhawa cha kahawa

“Agundulike mara ngapi?” alijibu Abuu na kuwafanya watu wote wamgeukie kumsikiliza nae kwa maringo akajifanya kama hana hamu ya kuwapa habari hizo akaanza kuondoka kuelekea ndani kwao

“We mtoto kuja hapa, na ukiondoka nitakutolea radhi” Aliongea Mzee Maguno kwa sauti kali lakini ya Mzaha ili kumfanya Abuu arudi, nae karejea

“Mie siwezi kusimama hapa naongea tu hata kiti hamnipi, wala kahawa hamninunulii wakati nawapa habari nyeti ambazo pamoja na uBBC hamjazipata licha ya kua zimetokea tangu saa sita mchana”

“Hee tangu saa sita? Kweli dunia sio kijiji tena, hebu kaa kiti hicho hapo kipo wazi”

“Mninunulie na kahawa kwanza”

“Hilo tu? Sema jingine, kama kahawa inalewesha basi leo utaema kushoto kasha utafukia kulia, utakunya TANI yako” Alijibu tena Mzee Magunokwa mshawasha wa hali ya juu, hakika zilikua ni habari tamu na za majonzi kwa upande wa pili,

“Hizi habari bado ni siri, mie ninawadokeza tu kwakua nilizipata kutokea kwa chanzo changu cha habari ndani ya kitengo muhimu na nyeti sana, hivyo muwe makini kuzisemasema kwa sasa, mkikamatwa mie simo”

“Tupe ufyetere huo kaka mkubwa” alijibu kijana mwininge aliekua ametulia akisikiliza kwa usongo

“Baada ya maiti kufikishwa hapo katika Hospitali ya ‘Gavumenti’ vipimo vikafanyika ambapo walizichunguzo hizo alama za vidole mnaziita sijui fingaprint” Watu wote walikua kimya wakimsikiliza, akachukua kikombe kidogo cha kahawa alichokua tayari ameshamiminiwa na baba yake Mzee Kagomba ambae muda wote alikua kimya akisikiliza kisa hicho kipya

“Alama za vidole zilizopo katika mwili wa marehemu zimegundulika kua na za mtu mmoja anaitwa Kishindo Rehani”

“NINI?? Kishindo rehani huyu wa Dar?” aliliza kwa mshangao Mzee Kagomba

“Huyo huyo aliekufa majuzi kwa kupigwa na Radi na kuzikwa juzi”

“Mtoto acha maskhara tafadhali”

“Sio wewe tu, hata uongozi wa usalama na jopo la madaktari wote hawaamini kilichoonekana kwenye vipimo vyao wenyewe na ndomaana wameamua kuifanya siri kwanza”

“Sasa nimepata majibu kamili, vita ya mizimu imeanza” alidakia tena mzee Maguno ambae ni gwiji wa Nujumi(Masuala ya Nyota) na Tafsiri za Ndoto, Kauli hiyo sasa ikawafanya watu wote pale wapate kiu ya kusikiliza hiyo vita, nae Mzee Maguno hakusubiri kuambiwa aendelee ‘kumwaga mchele’

“Iko hivi siku yoyote ukikuta mtu ameuawa kisha ametobolewa sehemu ya kifuani wakaunyofoa Moyo wake ujue huyo mtu ni Mchawi au anahusishwa na Uchawi…” Akavuta kikombe chake cha kahawa kisha akaendelea “..Iko hivi wachawi wote duniani hua wana kitu mfano wa Fitra kinakua ndani ya moyo wa kila mmoja wao na hicho ndo uchawi wenyewe hasa, na kinamtambulisha kwa wachawi wenzie popote atakapokwenda hata kama ni nje ya nchi, pia kazi ya kijidubwasha hicho ni kumuamsha huyo mchawi kila ifikapo usiku wa manane kwa ajili ya kujumuika na wenzake katika shughuli zao za kichawi, ndomaana mchawi yoyote hata kama awe amechoka vipi ikifika muda wa kwenda kuwanga usiku lazima atashituka tu, sasa huyo Bw Kasimba anahusika kikamilifu katika hii kadhia ya huo mzmu wa Waufi akisaidiana na dada yake ambae ni mke wa Kikoko, sasa itakua nguvu ya Mizimu ya WASWEZI ya huko Tabora umamani kwa Masu na nguvu nyingine ya mzimu ya WALUWA kutoka Kigoma na Kongo kwenye asili ya

ubabani kwa Masu imeanza kumsaidia mtumishi wan a kijana wao ndomaana katolewa moyo ila ngoja tuvute subra tutayasikia mengi tu..” Maneno hayo ya Mzee Maguno yaliwaogopesha wengi pale kijiweni na pia yalizidi kuacha maswali mengi hata kwa mtu mzima Kagomba pia ambae alishindwa kujizuia na kuendelea na maswali yake ya kidadisi na kichokonozi

“Sasa kwani mama yake na Masu sio huyu tumjuaye sisi? Na ni yeye anaemroga Masu? Na kwanini sasa vipimo vioneshe kua muuaji alikua ni marehem Kishindo ambae sio Masu anaeteswa kama ni kweli” Baada ya swali hilo kila mmoja alimgeukia Mzee Maguno kusikia jibu ambalo bila shaka lilikua likimkwaza kila mmoja pale

“.. Jibu ni jepesi sana, Ni hivi Ya Ngoswe mwachie Ngoswe, nay a Kaisari..??” alijibu kimkatao tu Mzee Maguno

*****

NDANI ya Nbs, Basi lifanyalo safari zake toka Dar es Salaam kwenda Shinyanga, seat za katikati walikua wameketi Sheikh Jabu na Mama Masu, na safari yao hii ilikua ni kuelekea Shinyanga msibani, tayari taarifa za kushtua za msiba huo ziliwafikia tangu jana yake hivyo ikabidi tu sasa wapange safari ya kurudi Shinyanga ili wajaribu kuwahi mazishi, ndani ya gari sura zao zilikua zimesawajika kwa matatizo makubwa yanayoendelea kujitokeza, Matatizo ambayo hakika ni mitihani mikubwa kwa familia yoyote ikikubwa, Raha na amani ilianza kufifia tangu ilipoanza ile Ndoto ya ajabu aliyokua akiiota Masu, Ndoto hiyo ikapelekea Mzee Kikoko akapigana na marehem Kishindo akimtuhumu kumfitinisha na mwanae, Ndipo Mzee Kikoko akacharazwa na mkia wa taa, Mara Kikoko akazidi kugombana na Mkwe wake kwa Masu akimtuhumu kumroga mwanae na kumtorosha pale nyumbani, Kesi ya Kikoko ikiwa tayari chini ya mikono ya Polisi mara Kishindo akafa kwa kupigwa na radi akiwa safarini,

ikagundulika kwamba katika Safari hiyo iliyomtunukia kifo Mzee Kishindo kumbe alikua na Masu, Cha ajabu baada ya tukio hilo la ajali ya Radi ane akapotea ghafla huko msituni, mara msibani mke wa marehemu kapandisha majini akidai kua mumewe katekwa na Waufi, mara mtoto wa Masu anasema Yule Ng’ombe aliebebwa na Kimbunga ndie alikua baba yake, Basi ni songombingo kila kukicha, na sasa Bw Kasimba kaka yake na Mama Masu nae ameuawa kinyama sana kwa kunyofolewa moyo, mawazo yalionekana kumzidia mama Masu aliekua akitiririsha machozi mashavuni mwake kila nukta..

Maziko yalikua yamepangwa kufanyika siku hiyohiyo kutokana na hali ya mwili wa marehemu lakini ikabidi muda waupeleke mbele kidogo mpaka saa kumi alasiri ili kujaribu kuwavutia muda Mama Masu na Sheikh jabu ambao walikua wameshatoa taarifa kua wapo njiani wanakwenda

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
64 Mzimu wa Waufu Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni