DOKTA SIUMWI HUKO (1)

0
Mtunzi: ___

SEHEMU YA KWANZA
“Ulikwenda hospitali mke wangu?” Masofa alimuuliza mke wake Sulee.
“Nilikwenda, lakini daktari kasema mimba nitapata tu ndani ya mwezi mmoja.”
“Ndani ya mwezi mmoja utapata mimba? Inawezekana kweli? Hujamwambia kwamba tumehangaika kutafuta mtoto kwa miaka nane, sasa ndani ya mwezi mmoja mimba itapatikana vipi?”
“Mimi sijui Masofa.”

“Mh! Haya, kwa sababu tumeambiwa na mtu tunayemwamini tuangalie, labda kweli daktari yule atatusaidia. Hakusema uende na mimi?”
“Hakusema Masofa, ila alisema kama naweza kesho na keshokutwa niende usiku saa moja ili anipime vizuri.”
“Alikupa dawa?”
“Dawa atanipa kesho.”

Masofa alichukua simu akampigia rafiki yake Miraji…
“Ee bwana Miraji, yule dokta uliyemsema kasema ‘waifu’ aende kesho saa moja usiku, wewe si unamwamini?”
“Yule hana neno, aende tu. Bwana Masofa we hukumbuki jinsi mimi na shemeji yako tulivyohangaika kutafita mtoto?”
“Nakumbuka.”
“Sasa kama si huyo daktari wa wanawake unadhani tungepata mtoto?”
“Oke, nimekuelewa bwana Miraji.”
“Sawa Masofa.”

Masofa alikata simu, akaendelea kukaa chumbani. Akili yake ilikuwa nzito sana kumruhusu mkewe arudi hospitali kesho yake, tena usiku wa saa moja…
“Sasa huyo daktari wa watoto ni kwa nini anataka mke wangu arudi usiku? Ni tiba gani hiyo ya usiku wa saa moja?”

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Siku ya pili iliingia, saa moja jioni Sulee alikuwa kwa daktari wa wanawake anaitwa Dokta Kisarawe.
Dokta Kisarawe alikuwa amekaa ndani ya chumba cha utabibu kwenye zahanati yake huku akimwangalia Sulee kwa macho yenye huruma…
“Kwa hiyo tatizo kubwa ni mtoto tu anti yangu?”
“Ni mtoto tu.”
“Miraji unamjua?”
“Ndiyo, ni rafiki wa mume wangu Masofa kwani vipi dokta, mbona umemtaja huyo?”

“Ah! Nimeangalia kwenye maelezo yako, nikagundua kuwa mnatoka eneo moja kwa maana ya ubalozi…,” Dokta Kisarawe alijibu huku akimuangalia Sulee kwa macho ya kumkagua f’lani hivi.
“Ooh…!, maana nilishangaa ni kwa nini umuulize huyo na umejuaje kama ninafahamiana naye…,” Sulee alihoji huku akiyakimbiza macho yake pembeni baada ya kukutanisha na ya Dokta Kisarawe.
“Hata mkewe alikuwa na tatizo kama la kwako, lakini aliponea kupitia mikono hiihii…”
“Kweli dokta…?”

“Kweli nakuambia, niamini mimi.”
“Mm!, sawa lakini nimesumbuka sana kwani naumia kukosa mtoto jamani…,” alisema Sulee safari hii akionesha sura ya upole zaidi, hali iliyomfanya Dokta Kisarawe amkazie macho zaidi.
“Kwani mmehangaika kwa muda mrefu sana anti…?”
“Yaani wee acha tu dokta, ikishindikana na hapa itabidi niridhike tu kuwa sikupangiwa kuzaa kabisa…”
“Ndoa yenu ina muda gani sasa…?,” Dokta Kisarawe alizidi kumdadisi Sulee huku muda nao ukizidi kuyoyoma na tayari saa iliyokuwa ukutani ilisomeka saa mbili na dakika nne.

“Miaka mitatu sasa dokta…”
“Mm..!”
“Mbona unaguna dokta jamani, au huamini?”
“Hapana anti, naguna kwa kushangaa mwanamke mzuri kama wewe hujapata mtoto…!,” alijibu Dokta Kisarawe huku akimkazia macho Sulee hasa maeneo ya kifuani na mapajani kutokana na sketi aliyokuwa amevaa kupanda hadi kuvuka juu ya magoti.
“Kwani mimi mzuri ja..ma..ni…?,” aliuliza Sulee lakini safari hii kwa sauti iliyokatakata.
“Dah! Wewe ni mzuri sana anti, nashangaa hadi sasa hujapata mwanaume wa kukupa mimba…!”
Hapo Sulee hakusema neno zaidi ya kuendelea kumtumbulia macho Dokta Kisarawe aliyekuwa bize na kumungalia.
Alipoona Sulee yuko kimya, Dokta Kisarawe akazidi kumsifia huku akimhakikishia ni lazima atapata mimba.

“Yaani mwanamke umeumbika haswa, ona maeneo kama haya ya kifuani jamani…,” Dokta Kisarawe aliendelea kumchombeza Sulee huku sasa akionesha kwa vitendo na kuyagusa maeneo ya kifuani ya mwanamke huyo mrembo wa sura na umbo achilia mbali rangi yake ya chokoleti.
“Kwe…kwe…lii dokta jamani…?,” Sulee aliuliza kama kweli anaweza kuzaa lakini kwa sauti ya mkwamo kutokana na mkono wa dokta kugusa maeneo nyeti ya kifuani.
“Duh! yaani anti na nido nzuri kama hizi halafu huzai…!”
“Mm!,” Sulee aliishia kuguna huku akijikunja kiaina kwani safari hii vidole vya dokta viligusa kisawasawa nido zake kutokana na blauzi nyepesi aliyoivaa mwanamke huyo.
“Hujapata tu mwanaume rijali…”

“Kwa nini unasema hivyo dokta jamani…,” Sulee aliuliza katika hali ya kutojiweza, huku macho yake yakianza kubadilika rangi na kuwa mekundu kiasi.
“Mimi ni daktari si kwa matokeo ya mtihani bali kwa kukidhi vigezo, ina maana nina uwezo wa kujua tatizo la mgonjwa hata kwa saikolojia tu, yaani wewe unahitaji mwanaume rijali tu, kweli tena nakuambia,” Dokta Kisarawe alizidi kutoa maelekezo kwa vitendo zaidi na safari hii mikono yake ikiparaza juu ya mapaja ya Sulee.

“Aah! Sasa huyo mwanaume rijali nitampata wapi jamani mbona haya ni majaribu sana dokta…?”
“Kha! Mbona wapo wengi sana, huko mitaani au hata mimi…”
“Mimi wa mitaani naogopa, mume wangu ni mkorofi sana…”
“Basi mimi…,” Dokta Kisarawe alipasua ukweli wake huku mikono yake ikiwa na kazi ya kumpapasa na kumbinya kimtindo Sulee, kuanzia maeneo ya kifuani, mapajani hadi mgongoni na kumalizia kwenye kiuno kipana na cha mviringo cha mwanamke huyo.
Kutokana na joto la mikono ya dokta, Sulee alikuwa akipeleka upinzani hafifu na kuruhusu mikono hiyo izidi kutalii kadri iwezavyo na kumuacha akilalamika kimahaba huku akitamka maneno ya kukolea penzi.
“Aaah, jamani dokta lakini mimi siumwi huukooo…,” Sulee alilalama huku akitoa ushirikiano kwa dokta.

Baada ya kuona amekolea, Dokta Kisarawe hakuwa na ajizi zaidi ya kumuandaa na kumsogeza hadi kwenye kitanda kilichotumika kwa wagonjwa kulazwa wakiwemo wale wa kujifungua.
Dakika chache kila mtu akawa ameiva na kuhitaji kukabiliwa na mwenzake, vilio na miguno ya kimahaba vikatawala ndani ya chumba hicho cha Dokta Kisarawe.
Haikuchukua muda mrefu, Sulee akatangaza kufika mwisho wa safari na dokta akimkaribisha kwa bashasha zote.

Baada ya shughuli pevu, dokta alimtaka Sulee arudi siku ya kesho kwa ajili ya vipimo zaidi kwa wakati huo, muda ulikuwa umekwenda.
“Ahsante sana dokta jamani, wewe ni tofauti sana…,” alisema Sulee baada ya kuagana na dokta na kisha kuondoka huku akiangalia nyuma.
***

Masofa ambaye ni mume wa Sulee alikuwa sebuleni akimsubiri mkewe ambaye alichelewa sana kurudi kutoka kwa dokta.
“Ina maana huyu hadi sasa ni tiba gani hiyo…,” alijiuliza Masofa akiwa na hasira.
Wakati akiwaza hayo, alisikia hodi na kwenda kufungua akakuta ni mkewe.
“Jamani mke wangu Sulee, hadi saa hizi ulikuwa kwa dokta tu…?”
“Sasa kumbe nilikuwa wapi tena jamani mume wangu…?,” alijibu Sulee huku akitupia mkoba wake kwenye kochi.

“Dokta alikuwa na watu wengi, ndiyo maana nimechelewa kwani sasa hivi saa ngapi?”
“Angalia saa mwenyewe…”
“Mm! yaani saa tano kasoro mara hii…!”
“Haya, niambie huyo dokta amesema nini…?”
“Kwa leo amenipa ushauri tu wa kisaikolojia, amesema nirudi tena kesho muda kama wa leo…,” alijibu Sulee.
“Mm!, ina maana leo amekupa ushauri tu…?”
“Ee mume wangu…”
“Inabidi kesho twende wote…,” alisema Masofa na kumuacha Sulee ametumbua macho.

“Sasa mbona umekaa kimya, umenielewa…?” aliuliza tena Masofa akiwa amemkazia macho Sulee aliyekuwa bado amemtumbulia macho ya mshangao.
“Mm…!,” aliguna Sulee kabla ya kukubaliana na uamuzi wa mumewe, hapo moyoni alibaki na maswali mengi juu ya hali itakavyokuwa baada ya kufika kwa dokta siku inayofuata.
“Sawa,” aliitikia huku akitingisha miguu mahali alipokuwa amekaa.
“Sawa, ndiyo nini…?”
“Kha!, si nimekubaliana na ulichosema…!,” alisema Sulee huku akimwangalia mumewa kwa jicho la ‘usinichoshe bwana’.
Masofa alibaki kimya kidogo, akaanza kuondoka kuingia chumbani huku akigeuka na kumwangalia Sulee.

Muda mfupi badaye, Sulee aliungana na mumewe chumbani ambapo bila hata kuvua nguo alijitupa kitandani.
“Aah, nianche bwana…,” alikuwa ni Sulee akimjibu mumewe aliyekuwa bize kwa kumshika sehemu mbalimbali za mwili hasa maeneo ya nyuma akiomba kutafuna tunda.
“Sasa nikuacheje jamani mke wangu…?”
“Mimi nimechoka bwana…”
“Umechoka na nini…”
“Kha! si kazi jamani, au watu huchoka na nini…?”

Masofa hakujibu kitu zaidi ya kusitisha alichokuwa anakiomba.
Walipitiwa na usingizi hadi asubuhi ambapo Masofa alikuwa wa kwanza kuamka kabla ya Sulee aliyekuwa bado akiufaidi usingizi wa asubuhi uliokuwa ukisindikizwa na kibaridi cha alfajiri.
Masofa alijiandaa na kuelekea kazini, hakutaka kumsumbua Sulee akihofia mzozo usiokuwa na maana kwani aliyakumbuka vyema majibu yake ya jana.
***

Sulee aliendelea kulala hadi saa tatu na nusu aliposhituka ghafla. Akakurupuka na kukimbilia bafuni ambako alioga kabla ya kuanza kuandaa kinywaji.
Akiwa anakunywa chai, ghafla mazungumzo na majibizano yake ya jana na mumewe Masofa yakaanza kujirudia kichwani mwake.
“Haya, niambie huyo dokta
amesema nini…?”
“Kwa leo amenipa ushauri
tu wa kisaikolojia, amesema
nirudi kesho muda
kama wa leo…,” .
“Mm!, ina maana leo
amekupa usahauri tu…?”
“Ee mume wangu…”
“Inabidi kesho twende…”
Kufika hapo, Sulee akaishiwa nguvu kimtindo.
“Sasa huyu naye anataka twende wote kwa dokta ili iweje?, wengine wanasumbuliwa na wivu, sasa kama yeye kazi hawezi si awaachie wenzake…”, aliwaza Sulee.

Akaendelea na majukumu mengine kama mama wa nyumbani, huku moyoni akiombea mumewe apatwe na dharura yoyote ili asiende naye kwa Dokta Kisarawe!
Mawazo yakampeleka hadi kwa Dokta Kisarawe ambaye tayari hisia za mapenzi zilishaanza kuchipuka baada ya kupatiwa raha ya ajabu jana yake.
“Nakupenda, nakutaka, nakuhitajiiii….moyo wangu wakuwazaaa… mpenzi uko mbali namii….,” Sulee alijikjuta akiimba wimbo huo wa Lady Jay Dee uitywao Distance baada ya hisia juu ya Dokta Kisarawe kuzidi kumuwaka vibaya…!”

Hatimaye muda wa mumewe kutoka kazini uliwadia, ambapo maandaliazi ya kwenda kwa dokta yakaanza.
Ilipotimu saa moja na nusu, Masofa akiwa na mkewe walikuwa njiani kuelekea kwa Dokta Kisarawe.
Wakamkuta dokta akiwa peke yake kwenye chumba chake akiwa bize na ukaguzi wa mafaili mbalimbali ya wagonjwa.

Dokta Kisarawe alipomuona Sulee, mapigo ya moyo wake yakaongezeka, ikabaki kidogo tu aropoke jambo ambalo lingeharibu kila kitu.
“Jamani hon…,” alijikuta akikomea njiani japokuwa lile neon hon alitaka kutamka haoney, lakini akajikuta akibadili haraka baada ya machale kumcheza haraka.
“Hata haujachelewa, aisee unazingatia sana muda…”

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)