PETE YA MVUVI (6)

0

SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
“Mimi naitwa Nasra na hapa nipo na bwana wangu ila nimechoka kukaa nae ndani kwani hawezi kitu kabisa yani huwezi amini tuna masaa matatu chumbani mtarimbo wake umegoma kusimama na nina hamu ya kufanya mapenzi, naomba unisaidie japo mshindo mmoja tu nikalale vizuri maana kwa hali hii sitoweza kulala”

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Nilitazama mwili wake ule wenye umbo nambari 8 nilishindwa kukataa kwani mimi pia nilikua nina hamu sana, Hivyo tulisogeleana na nilifanikiwa kula tunda lake kwa ufundi zaidi kiasi kilichomfanya akalale na mimi chumbani kwangu na kumuacha bwana wake chumbani peke yake akiwa amelala akikoroma kama chura wa mtoni. Yote yali yalinifanya nisahau kilichonileta mjini na hivyo asubuhi ilifika Nasra aliniamsha na kuniomba nimpatie huduma ya asubuhi kwani hatopata tena akirudi kwa bwana wake na kwa vile mtoto yule alitaka name sikua na jinsi nilimpatia, Ila sasa wakati tunafanya mapenzi mlango wa chumbani kwangu nilisahau kuufunga na hivyo ulifungulia na tulikurupuka kuangalia ni nani anaingia.

Tulibaki tukitoa macho kwani tulishindwa kuelewa kundi lile la polisi lililoingia chumbani bila hata kubisha hodi wala kusalimia, Polisi wale walianza kukagua mizigo yangu na kisha walikagua mkoba wa Nasra na kukuta akiwa na dawa za kulevya zikiwemo Bangi pamoja na Mirungi kwenye ule mkoba. Polisi hawakutaka maongezi na mtu yeyote walituchukua na kutupeleka kituo kikubwa cha polisi ambacho kilikua karibu na nyumba ile ya kulala wageni, Nilipokua kwenye gari ya polisi nikiwa natafakari mikosi yote hii niliyojitafutia kwa mbali kidogo nilimuona Bahati (Neema) akiwa anapakia mizigo kwenye gari ndogo ambayo ilionekana kuwa ya kwake huku tumbo lake likiwa limenona na bila fikra zangu kukosea Neema alikua mjamzito wa miezi 5.

Nilimuita kwa nguvu zote, “Bahati Bahati Bahatiiii” kwa kuwa alikua anaongea na simu hakuweza kunisikia kabisa, Niliumia sana kwani nilikuja mjini kumtafuta yeye ila tamaa na roho za shetani zilinifanya nijiingize kwenye matatizo yote haya. Tulifikishwa kituoni na kila mtu alihojia maswali kwa muda tofauti, nilijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuwaelezea polisi ukweli bila kuwaficha chochote, Kamanda mkuu wa kituo kile alinielewa na aliniruhusu niondoke kwani mizigo yangu haikuwa na tatizo lolote.

Niliondoka kituoni pale na kuanza kutanga tanga huku na kule nikiwauliza watu kama wanamfahamu Bahati japo kwa kuwaelezea jinsi alivyo, Siku tatu zilipita sikufanikiwa fedha zikiwa zimeniishia sikuwa na pa kula wala kulala, Siku iliyofata niliamua niende kituo cha polisi na kuwaomba wanitangaze kuwa nimepotea na nilikuja mjini kwa rafiki yangu Bahati, Polisi wale waliniomba pesa kidogo na kwa kuwa sikua nayo walishindwa kunisaidia, hivyo niliendelea kuzunguka bila kuwa na matumaini yoyote yale. Kadri siku zilivyozidi kusogea nilijikuta nikipoteza nguvu huku mwili wangu ukidhoofika kwa kukosa chakula lakini yote yale nilijisemea moyoni, “Sirudi Luvile bila mdogo wangu acha nife na njaa”.

Kwa bahati nzuri siku moja nikiwa maeneo ya sokoni nilibahatika kumuona Bahati (Neema) akiwa ananunua bidhaa za nyumbani nilimkimbilia kwa furaha na kwa kuwa alikua amebeba mizigo mizito nilimpokonya mizigo ile bila hata kunijua vizuri, Bahati alikasirika sana kwani hakuweza kunitambua kwa urahisi kama nilivyodhani na hivyo alipiga kelele za mwizi, “Mwiiiziiii jamani mwiziiiiiii” kwakuwa nilikua mgeni maeneo yale watu walishindwa kunitambua na hivyo walinishambulia kwa mawe huku wengine walinipiga na mbao zilizokua na misumari mikubwa,

Maskini!!! Nilijeruhiwa vibaya mno lakini kwani sehemu yangu ya kichwa ilipigwa sana na mawe na kutokana nilipoteza damu nyingi huku ubongo wangu ukichanganyika na damu sikuweza kuendelea kupumua, JOSHUA ALIFARIKI DUNIA. Bahati alipofika nyumbani alimsimulia mchumba wake kilichomtokea sokoni na alipokua akitoa mizigo yake kwenye mifuko aliiona PETE iliyokua na kidani cha rangi ya bluu iliyomkumbusha JOSHUA kwani pete ile alikua nayo Joshua na alipenda sana kuishika pale alipokua akionana na Joshua,

Bahati alishtuka sana kwani alianza kurudisha fikra zake nyuma na kukumbuka tukio lile la yule kijana aliyemuitia mwizi na kwa msaada wa ile pete iliyodondokea kwenye moja ya mifuko ile wakati JOSHUA alipokua akimpokonya mizigo yake kwa nia ya kumsaidia. Bahati alimuomba Raheem (Mchumba wake) ampeleke sokoni kumuangalia yule mwizi kwani alihisi amefanya makosa kumuita mwizi, Walipofika walikuta mabaki ya majivu kwani JOSHUA alichomwa moto, Bahati alilia sanaaaa!! Kwani alisabibisha kifo cha Joshua bila yeye kutambua.

Taarifa za kifo cha Joshua zilifika kijijini Luvile na kufanya kijiji kile kuwa na upweke wa hali ya juu huku vilio na maombolezo yaliochukua muda wa mwezi mzima kumuhenzi kwa sala na nyimbo za huruma na majonzi kwani hawakubahitika kuuona mwili wa Joshua kumbuka alichomwa moto. Shangazi wa Joshua alibahatika kuonana na Bahati na alimuuleza ukweli wote juu ya yeye kuokotwa na maisha yake yote mpaka pale alipofikia, Ukweli ule ulimfanya Bahati azidi kuumia na kumfanya mwenye majonzi kila kukicha.

Bahati ndiye Neema mtoto aliyetupwa njiani mara tu alipozaliwa na Joshua alimuokota na kumlea mpaka pale walipokuja kutengana, Juhudi za Joshua kwenda kumtafuta mdogo wake aliyekua amepotezana nae kwa muda mrefu zinamfanya apoteze maisha. Bahati (Neema) alijifungua mtoto wa kiume salama na alimpatia jina la JOSHUA. Wavuvi wa ziwa la Luvile walitumia gharama nyingi sana kuchonga sanamu ya Joshua huku wakibadili jina la ziwa lile ambalo hapo awali lilikua likijulikana kwa jina la FAHARI YA LUVILE na Kuliita SHUJAA WA LUVILE jina hilo liliambatana na ile sanamu kubwa ya Joshua.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
MWISHO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)