Mtunzi: Leicester Petron
SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Nilimjibu kwa furaha, “Ndio Shangazi yangu kipenzi”…
Shangazi aliniangalia vizuri sana kiasi ambacho madonda yote ya mwilini yalianza kupotea huku hali yangu ya kukohoa damu ikitoweka kabisaaa!!
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
Majirani wenye roho mbaya na chuki rohoni mwao hawakusita kuja nyumbani na misalaba huku wengine wakiwa na sanda bila kusahau rafiki zangu waliokuja na jeneza kwajili ya kunizika, Hali ile iliendelea kila siku lakini Shangazi yangu hakuchoka kuwafukuza na kunipa moyo kuwa yote hii ni mitihani ya maisha na ili kuyashinda ilibidi niwe jasiri. Baada ya Muda wa wiki 3 kupita nilitoka nje na kujiangalia kivuli changu sikuamini kwani afya yangu nzuri ilirudi huku madonda na mabaka baka ya kijani yakitoweka kabisaa! Nilirudi ndani na kumwambia Shangazi ," Shangazi yangu nakushukuru sana haya yote unayonifanyia ipo siku Mungu atakulipa, nakupenda sana shangazi"
Shangazi alinijibu huku akitabasamu, "Joshua mimi ndio mzazi wako niliyebaki hivyo ni jukumu langu kuhakikisha upati tatizo lolote lile, Sawa baba?" Nilimuitikia Shangazi kisha nilitoka nje kuelekea ziwani kuangalia hali halisi ya uvivu inavyoendelea. Nilifika ziwani nikiwa nimevaa nguo za kujizuia na baridi ambazo zilinifanya kutojulikana na mtu yeyote yule kwani nilivaa mzula (boshori) uliofunika kichwa changu. Niliona fujo na maneno makali ambayo wananchi walikua wakilalamika Uongozi mpya wa ziwa lile ulijawa na ufisadi, niliposogea karibu na umati ule wa wavuvi na wauza samaki nilisikia kundi la vijana likisema, "Daah..! Yani bora ya Joshua naamini angeendelea kuwa kiongozi leo hii tusingekua na malalimiko ya kijinga jinga"
Mara baada ya kijana mmoja wao wa kundi lile kumaliza kuongea maneno yale kundi lile kwa pamoja lilianza kuimba kwa sauti za hasira, " Tunamtaka Joshua, Tunamtaka Joshua, Tunamtaka Joshua, Tumechoshwa na ufisadi" Wimbo ule ulipokelewa na kila mtu aliyekuepo eneo lile. Nilitamani sana nionyeshe uso wangu ila roho yangu ilisita kwani usalama wangu ungekua hatarini, Hivyo niliondoka eneo lile na kuanza safari ya kurudi nyumbani. Nilipokua nakaribia nyumbani nilikutana na yule bibi aliyekua akiishi na Bahati ambaye aliniomba tuketi na alinelezea historia ya Bahati, Mungu wangu!!! Sikuamini nilichoambiwa kumbe Bahati ni mdogo wangu Neema…
Simulizi ya bibi kuhusu historia ya Bahati ilikua hivi, “Joshua wewe ni kijana shupavu na mwarevu sana pia ninaelewa ni jinsi gani umetokea kumpenda Bahati lakini Bahati si mjukuu wangu wa damu moja, Siku moja miaka 15 iliyopita nikiwa kando ya ziwa nilimuona mtoto mmoja wa kiume akiwa na mdogo wake wa kike aliyekua amembeba begani na walihaha huku na kule kutafuta mahali pa kulala na ndipo mtoto yule wa kiume aliona kiota alichoshindwa kutambua ni cha mnyama gani na kujilaza yeye pamoja na mdogo wake, Mimi nilipoona amelala kwenye kile kiota ambacho wanakijiji wa hapa walikua wakimuwinda nyoka aliyetokea kuwa tishio sana kwa miaka ile na makazi yake yalikua kwenye kile kiota nilijificha pembeni ya mti mkubwa na kuwalinda watoto wale.
Baada ya masaa kadhaa kusogea mbele nilimuona mtoto yule wa kiume akitoka na kuelekea barabarani niliposhindwa kutambua alikua akifata nini, Alimuacha mdogo wake kwenye kile kiota kwa mbali nilisikia sauti za wanakijiji zikiwa zinakaribia eneo lile na kutokana nilikua na sungura wangu ilinibidi nimfunge mdomo, miguu na mikono ili asijetoroka wala kupiga kelele kwani kuna mwanakijiji mmoja alikua ameshafika eneo lile la kile kiota na kuona kitu kikiwa kimejifunika kwenye manyasi huku kikijigusa gusa na ndipo aliondoka kuwaita wenzake waje kumteketeza nyoka yule bila kutambua alikua ni mtoto.
Hivyo nilielekea kwenye kile kiota na kumtoa mtoto yule na kisha kumfunika Sungura wangu kwenye zile nyasi na wanakijiji walipofika na kukuta bado kuna kitu kinajigusa gusa waliwasha moto na kujua kuwa wamefanikiwa kumuua nyoka yule, kumbe walimchoma Sungura wangu. Hivyo Joshua Bahati si mjukuu wangu wa damu ila yeye hatambui ilo kabisaa!!” Nilivuta pumzi kwa nguvu huku macho yakinitoka kwani historia ile ilionyesha kuwa Bahati ni mdogo wangu Neema, Nilijikaza nisilie wala nisiongee chochote cha kumfanya bibi yule kujua ukweli kwamba mimi ndio kaka wa Bahati (Neema).
Nilinyanyuka na kumwambia bibi, “Dah.. pole sana bibi, ila pia Mungu akubariki kwa kuweza kuokoa maisha ya Bahati” Tuliagana na niliendelea na safari yangu ya kuelekea nyumbani. Nilipofika nyumbani nilimkuta Shangazi akiwa ameketi chini kwenye jamvi na nilianza kumsimulia kila nilichoambiwa na yule bibi, Shangazi aliniambia, “Joshua unasemaaa..!!?”.
Muda wa wiki tatu ulipita na nilimuaga Shangazi kuwa naelekea mjini kumtafuta mdogo wangu, Nilitupilia mbali nafasi ya kurudi kwenye uongozi wa ziwani huku vijana wenzangu wakiandamana kuniomba nirudi kuongoza umoja wa wavuvi wa kisiwa kile ila yote yale hayakua na nguvu yeyote ya kunizuia nisiende mjini kumtafuta mdogo wangu (Neema).
Nilianza safari ya kuelekea mjini Mazimbwe ambapo nilibahatika kufika majira ya usiku Sanaa, kutokana nilikua na kiasi cha fedha kilichoweza kunifanya nilipie chumba kwenye nyumba ya kulala wageni sikuwa na shida ya kutafuta pa kulala. Nyumba ile ya kulala wageni ilikua ni ya kizamani zamani hivyo huduma ya kujisaidia na kuoga ilikua ikipatikana kwenye vyoo vilivyokua nje ya vyumba, Nilishtuka saa 8 usiku baada ya jasho kali kunimiminika na hivyo niliamua niende bafuni japo nijimwagie maji nitoe jasho lile.
Kwa bahati mbaya niliingia bafuni bila kubisha hodi na hivyo nilimkuta binti mmoja akiwa mtupu na kwa kuwa aliniona alishtuka na kuniambia, “Usiondoke na wala usiogope” Mhhh!!!!? Niliguna moyoni mwangu kwani binti yule alikua na rangi nzuri ya kuvutia huku sehemu ya nyuma ya mwili wake alionekana kama kafungasha virushi vya maembe La hasha!!! Mtoto alikua ameumbika walaaahi!! Dooh!!!.
Aliniambia, “Sogea karibu basi mbona unaniogopa?? Kifua chako kimenisisimua sanaaa” niliogopa sana na nilimuuliza, “Samahani dada wewe ni nani? Na kwanini upo kwenye hii nyumba?” Yule binti alinijibu, “Mimi naitwa Nasra na hapa nipo na bwana wangu ila nimechoka kukaa nae ndani kwani hawezi kitu kabisa yani huwezi amini tuna masaa matatu chumbani mtarimbo wake umegoma kusimama na nina hamu ya kufanya mapenzi, naomba unisaidie japo mshindo mmoja tu nikalale vizuri maana kwa hali hii sitoweza kulala”
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA