DOKTA SIUMWI HUKO (15)

0
Mtunzi: ___

SEHEMU YA KUMI NA TANO
ILIPOISHIA...
Janeth alikuwa mdada mzuri
sana aliumbika sana mwili wake
ulio jinyonga kama umbo la namba nane kiukweli tuliendana
kiumbo mpaka tabia zake zilikuwa nzuri sana kwa Muda mchache nilio kaa nae nili mjuwa kama ni mtu mwema.
“kweli sina muda wakumsingizia kabisa”

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
“sawa ila nashukuru kwa kuniambia mapema maana
Hawa Maboss hawakawiagi kutongoza wafanyakazi”
“yah na ilo ndilo kusudi langu kukujulisha ili uwe makini nae sawa”
“asante sana Janeth maana ilibakia kidogo sana niingie”
“nilijuwa vizuri tyuu sasa kaa chonjo”
_________________­__­____________________

“Monica usi jiraumu sana
kila kazi ina ulinzi wake ona umbo
lako zuri sana jiulize kwa nini wanaume hawakutamani eeh ujuwe kuna kitu hapo
jicgunguze mara mbili sawa usikae ukilaumu sana”
hayo ni maneno ya changudowa
mmoja aliye kuwaakimwambia Monica baada ya kuingia katika
kazi za kujiuza alifanya kazi hiyo bira mafanikio hata siku moja hakupata mwanaume wa kulala nae siku moja alikuwa kasimama sehemu yao yakujiuza
alikuta gari ikisimama alipo kimbilia akasubili kioo kishushwe chini ndipo akakutana na sura ya mwanamke.
“binti haujambo”
“sijambo”
“vp upo hapa sahizi”
“maisha tyuu”
“maisha kivipi”
“story ndefu sana kifupi kama wataka mpaka uwe na muda ndomaana nipo hapa”
“ok ingia ndani basi nielezee”
“ok kwa ufupi,
_________________­__­________________

ndiyo hivyo mama angu maisha yangu yalivyo
najuta sana kuipoteza ndoa yangu
nilitamani sana mtoto”
“mtoto yuko wapi sasa”
“Nime mfungia katika chumba nilicho panga”
“je tunaweza kwenda”
“ndiyo”
Walipo fika Monica na yule mama
katika chumba chake walimkuta mtoto kalia mpaka kachoka sana
walimchukua na kumnyonyesha.
“sasa mbona wamnyonyesha wakati umeingia katika kazi mbaya”

“yani mama angu tokea niingie katika kazi hiyo
sija fanya mapenzi na mwanaume yeyote”
“mh kwajinsi ulivyo hivyo monica”
“niamini mama angu niliongea na
mmoja katika marafiki nilio kua nao aliniambia kuwa wao
wana tumia dawa za mvuto mimi nilikuwa sina nilionekana kama vichekesho kwa wateja”
“mmh sawa una muda gani tokea
uingie”
“miezi mi3 sasa”
“poa takusaidia leo
chukua hii pesa kama elf50
kesho takuletea godolo na kitanda sawa mambo mengine yatakuja sawa mama”
“asante sana mama angu Mungu akubariki sana”
“Amina”
_________________­__­____________________­__

“hallow janeth unasemaje sahizi usiku upo wapi”
“nipo nyumbani”
“kuna tatizo”
“Hapana Adams, Najuwa wewe ni Boss wangu kila Mara nakuelezea
hisia zangu kwako kwanini hutaki kunielewa Boss nakupenda nakuhitaji uwe Mume wangu nasiyo Boss tena”
“Janeth janeth mara ngapi nakukatalia kuhusu suara hilo
eeeh siko tayari kuwa na mke kwa sasa sawa”
“sawa boss ila tambua hata mimi
nahisia kama mtu mwingine sina cha kuhitaji zaidi yako nakupenda
nanitazidi kukupenda daima
Adams hata ukiniona sikufai tambuakuwa kunamtu anaye kupenda sawa”
“Asante Janeth kwakuonyesha upendo wako kwangu ila tambua unaweza kumpenda mtu asiye kupenda hapo mbeleni unaweza kuteseka sana katika penzi lako”
“niko tayali kuteseka nasiyo kukukosa wewe Adams naumia sana kila siku kwa penzi lako ninalo lihisi unapo nipa katika ndoto zangu nipe nafasi”
“haita wezekana kabisa”
“sawa napenda kukutakia usiku mwema”
“asante nawe pia, Sulee”

Asante sana”
Baada ya mwezi mmoja Mahusiano kati yangu na Adams
hayakuwa mazuri sana kiujirani kati simu tofauti na mwanzo ilivyo kuwa kila akinipigia simu nilikuwa nikikata au kuto pokea
katika simu yangu ya mkononi
Adams aliamuwa kupiga ya ofisini kwangu nilipokea kwa Haraka sana kwakujuwa huko hawezi kusema kuhusu mapenzi lakini ikawa siyo.
“sulee haujambo”
“sijamo vipi wewe”
“yah niko poa sana”
“mbona haujachangamka
leo”
“nipo kawaida mbona jamani”
“hapana sulee sijakuzoea hivyo
umeanza lini au una umwa, yes utakuwa unaumwa wewe ebu mwambie Janeth akupeleke
hospitali sawa”
“hapana Adams niko sawa”
“mmh haya basi ngoja nikuache”
_________________­__­____________________

baada ya masaa ma5
“kaka kisarawe nina tatizo”
“Tatizo gani tena kama biashara
zinaenda poa mbona”
“aaah najuwa kaka ila zangu
binafsi kaka”
“ehe”
“kaka yule dada niliye mtoa dar niliye mpeleka Iringa ana nichanganya sana naomba ushauri wako”
“kaka wanawake hawafai
kabisa mtu anaweza akawa mke wa Mtu lakini aka toa penzi inje tena kidhembe kabisa achana nae Adams kama unataka
kaoe bush pia mpatie ubize ili asiweze kutoka mara kwa mara
ila sijuwi kama itawezekana kuto saritiwa maana hata mimi kipindi
cha nyuma nilikuwa nikiwakomesha ndani ya nusu saa tena wake za watu katika ofisini”
“uliwezaje kufanya hivyo”
“Adams utakuta mke wa Mtu anakuja mrembo sana
kama ilivyo kuwa Mimi ni Dokta wa akina Mama nilikuwa nikiwatamani sana nilipenda
kila umbo la mwanamke nipate
ili nifanye nae mapenzi ili Roho yangu irizike kweli nilikuwa nikifanikiwa tena wale wasio shika mimba ndiyo walikuwa wengi sana”

“ehee ikawaje”
“mfano mzuri kuna madada wawili nilio wapa mimba kwa nyakati tofauti
kuna mmoja alikuja akilalamika
hajawahi kushika mimba miaka 8
nilimpima pima kinafiki huku nikimtomasa tomasa mpaka nikampandisha nye… Kweli nikala mzigo ikawa kawaida mara kwa mara ananiletea nagonga mpaka
mimba juu aka mmoja nae Maonica hivyo hivyo nikala mzigo
mpaka mimba hapo ikawa kasheshe baada ya mumewe kupima nakujulikana hana uwezo wa kuzalisha kutokana na kupata ajari sasa mkewe akamwambia kuwa anamimba weee palichimbika kumbe yeye na yule wa mwanzo ni zaidi ya marafiki.

Nako moto ukawake
baada ya kujuwa walikuwa wakija
wote kwangu kutibiwa Monica akasema kweli mimba ya kwangu mbele ya muewe”
“yule wa mwanzo ana itwa nani
vile”
“sikumbuki sana maana kitambo sana, eeh nimekumbuka
anaitwa sulee”
“Nani”
“sulee”
“ok poa tuishie hapa kwaleo sawa
ndugu utanisimulia kesho siku njema.

Adams kwa nini nisikumalizie
kisa hiki chote leo leo tafadhari
sana nipe muda maana
usipo juwa leo hii sizani kama utapata Muda wakunisikiliza”
“Unajuwa nina mambo mengi sana yakufanya leo”
“ika juwa kuwa sita kwambia sawa napia kwa nini Nimelitaja jina la sulle alafu ushtuke”
“Hapana hakuna kitu”
“Niambie nitakusaidia”
“ok kisarawe ni hivi, SULEE ni huyo
hoyo mdada niliye mleta yupo iringa”
“Aaah kweli”
“ndiyo ni kweli kabisa”
“Ehee una mpango gani nae sasa”
“Yah nampenda sana ila yeye ndiye kanitamkia kunipenda
yani tatizo lipo kwangu kuku bali”

“oh sasa nihivi sina mpango nae mimi sulee kama vipi nipeleke Iringa yeye aje hapa nakama itashindikana niache kazi”
“kakaaaa noo haiwezekani
kabisa wewe ni kila kitu kwangu
siyo mwanamke pia kutoka hapa moro nikitu ambacho hakitawezekana kabisa”
“sasa tutafanyaje”
“ok tamleta hapa moro ila tutafanya usionane nae kabisaa
siku zote sawa”
“hakuna haita wezekana
kabisa”
“sasa tutafanyaje”
“mlete sitaonana nae kipindi chote hicho sawa ila akisha zoeya mji huu sasa tuta onana sawa”
“ok”
“ila sasa siana mtoto wangu”
“hapana mimba ilitoka kwa sababu ………….. Nishangazi yake aliye sababisha”
“aaah Mungu wangu sijuwi na monica itakuwaje”
“uyo ana mtoto wa kike anaitwa happy”
“aah nasijuwi kama ana ishi na Mumewe”
“aliachana na Mumewe”
“daah Najuta sana yani Najuta
kuwaalibia maisha yao”
“kaka usiwaze sana ngoja nifanye mpango wakumleta”
“sawa”
_________________­__­­___________________­_

Baada ya myezi mi2
Adams alikuwa akimbembeleza sana Sulee aje Moro pia alikuwa akijaribu kumshawishi kimapenzi lakini sulee alikuwa mbali sana.
“sulee sikuhizi umebadilika sana
yani ulikuwa ukinibembeleza sana
nikupe penzi langu lakini leo
mimi ndiyo nimekuwa ni msumbufu kwako
nilikuwa nakuchunguza
mwenendo wako nimeshajuwa
wewe ni bora kuwa mke wangu
naomba nikubalie tafadhari”
“Adams nimebadili maamuzi
sitaki tena naomba tuwe kaka na dada”
“je nina tatizo lolote kuwa
mume kwako”
“hapana hisia zime hama kwako tena naomba nipumzike sasa katika mapenzi”
“sulee unaniumiza sana
kwa maamuzi yako hayo”
“pole Adams”
_________________­__­­___________________

“Adams leo kutwa nzima nimekuwa nikikuwaza hata kazi kwangu ilikuwa nzito sana”
“Janeth nimekwambia siku pendi siku taki sawa nakama ukiendelea
kunipigiaga simu nakuniambia
kuhusu mapenzi ujuwe kazi huna sawa”
“Adams hapana usifanye hivyo”
“lakini umenielewa”
“ndiyo”
“ok fanya yako sasa
“sawa sawa boss”
_________________­__­­___________________­_

Monica hapa lakini siyo pazuri pakukaa sasa inatakiwa uhame
uhamie hata kawe ili upate kupumzika sawa”
“Mama tapa pesa wapi nikakae sehemu ya kifahari kule”
“kuna nyumba yangu yupo mdogo wangu ana kaa peke yake
sasa kampe kampani ya kukaa wote”
“sawa haina shida”
“ok”
Monica alikaa kawe yeye mwanae na husna mdogo wake na Huyo mama msamaliya kwake
maisha yali songa mbele
mtoto alikuwa ana pata maziwa ya kopo na vilutubisho mbali mbali alikuwa na afya njema kabisa.
______­___________________­_

sulee nimeamuwa nije Iringa ili nijuwe nini tatizo sawa”.
“Boss chai tayali”
” Asante Janeth nakuja na maongezi na sulee dk chache”
“sawa boss”
.
.
“sulee je umepata Mchumba
mapema hivyo”
“hapana Adams nilitokea kukupenda sana lakini nimeamuwa kuku chukia/kukutenga na mimi”
“kivipi”
“Nimetokea kusingiziwa kuwa nina ukimwi iweje leo hii unataka kuniambukiza ukimwi wako”
“Nini sulee paa paaa(makofi)
nani ana ukimwi eeh nina miaka 15 sasa nipo bize na kazi/biashara
simjuwi mwanamke wala nini
mke wangu ni mari zangu mimi
iweje niwe na ukimwi mimi
sulee ndomana ulikuwa huni taki
nakama ningekuwa nataka kukuambukiza ukimwi ningeshakuambukiza dar
unakumbuka ulikuwa ukining’ang’aniza kufanya nini”
“Najuwa sana(Nilijibu huku nalia)
ndomana nilikuwa sijuwi Na Mungu akaniepusha”

“sulee Nakupenda sana tofauti ujuwavyo sawa nipo tayali
tuka pime wote wawili tulipo kuwepo dar uliponisimulia
story yako yoote ya maisha nilichukulia kama somo kwako
najuwa hauta Rudia tena pia ulitaka sana tusex ili unipate
lakini niliogopa baada yakuniambia kuwa walikusingizia kuwa una ukimwi sikuamini kama kweli huna sasa naomba tuka pime wote sawa ili tuwe na uhakika nakama ukigundulika unao takutunza mpaka mwisho wako wa maisha sawa sulee”
“sawa nipo tayali hata leo hii”
“ok twende sahizi”
“sawa Adams”
TULI ONDOKA MPAKA HOSPITAL
TUKA CHUKULIWA DAMU WOTE WAWILI nakupimwa baada ya saa moja na nusu majibu yalikuwa tayali
mezani.

“hongereni sana wote mko safi ila tunawashauri mkapime tena baada ya mwezi mmoja sawa”
“asante dokta”
Nilimkumbatia Adams huku
niki mkiss kiss kwa fujo sana.
_________________­__­­_

Hakika ningekupoteza Adams kijinga sana ivi kina endelea nini
kati yako na Janeth, Adams?”

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)