SALAMU KUTOKA KUZIMU (14)

0
Mtunzi: ___

SEHEMU YA KUMI NA NNE
TULIPOISHIA...
Pamoja na kukuonya uondoe ndoto za kipuuzi kama hizo, tunakutaka uichukulie barua hii kama taarifa ya kukupokonya madaraka yote uliyokuwa nayo. Kuanzaia sasa. Uko huru…”

Proper alipofikia hapo, aliruka kando ghafla akageuka nyuma yake akitazama kila upande, bastola yake ikiwa mkononi tayari kwa lolote. Hakuona chochote alikuwa peke yake chumbani hakuamini.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Akaanza msako wa kuchunguza hapa na pale, bastola ikimtangulia. Ingawa hakuona mtu wala kitu lakini hofu ilimpanda. Ajuavyo yeye, barua hiyo ya kumnyanganya wadhifa ilikuwa pia ikiashiria hukumu ya kifo. Akiwa mtu ajuaye mengi ya hatari asingeweza kuruhusiwa kuwa ‘huru’ kwa urahisi kiasi hicho. Alichoamini yeye ni kuwa yeyote aliyeleta barua hiyo pia alikuwa na jukumu la kumuua. Wala asingemruhusu kuishi kwa muda wa dakika nyingi baada ya kupokea taarifa hiyo. Lakini mboba yuko peke yake? Nani ambaye angemuua na lini? alijiliulza huku akiendelea na uchunguzi wake kwa hadhari kubwa!

Haikuwepo dalili yoyote ya uovu.
Hakuona dalili yoyote ya hatari.

Mara alijiona akiwa mzito zaidi kuliko kawaida. Kichwa chake pia kilimuelemea ghafla na macho yake yakashindwa kuendelea kutimiza wajibu. Aliyaskikia maungo yake yote yakianza kulainika. Aliona kana kwamba angeanguka sakafuni. Ndipo alipoelewa mwisho wake ulivyopangwa. Ile harufu tamu aliyoinusa katika bahasha aliyokuwa nayo mkononi haikukusudiwa kumburudisha. Ilikuwa sumu kali yenye jukumu la kumuua. Sumu ambayo ilikuwa ikitimiza wajibu wake. Akasonya kwa kutowaza hilo toka awali. Proper angekubali kufa kwa mkono wa mwanaume mwenzake. Hilo, hakulitazamia na asingeruhusu litendeke Proper Mbezi na mwenye kiburi kikubwa. Alijikongoja kuitafuta bastola yake. Akakielekeza kifuani tayari kuifyatua. Kisha alikumbuka kuwa sumu iliyokuwa ikikaribia kumuua haikuwa ngeni kwake. Alikuwa ameisoma katika vitabu vya kemia vya kijasusi na kuifahamu kuwa ilikuwa imegunduliwa siku chache zilizopita. Sumu hii iliitwa Crycine, na ingeweza kumua mwanadamu kwa dakika chache sana. Hata hivyo, alikumbua pia kuwa, Dawa pekee ya sumu hiyo ni maji. Aliirejesha bastola yake kibindoni akajikongoja haraka kuelekea bafuni. Ambako alijaza maji kwenye beseni na kujitumbukiza ndani yake. Akahakikisha pia maji mengi yanaingia tumboni mwake. Baada ya muda, alijisikia akirudiwa na uwezo wake kimmwili na kifikra. Akajipoa kutoka majini na kuvaa mavazi yake.

Hasira kali zilikuwa zimemjaa kichwani mwake. Hasira dhidhi ya yule aliyepitisha uamzi wa kumuangamiza. Na hasa dhidi ya huyu aliyepokea amri ya kumuua bila kukumbuka ni nani kakusudiwa kuangamizwa. Alikumbuka mchango wake kwa shirika hili la ujasusi ambalo lilimtuma hapa nchini. Mchango ambao kila mara huhatarisha maisha yake. Akaona kuwa alistahili kupata medali na si kifo.

Proper si mtu wa kustahamili uovu kama huo. Aliamua kulipa kisasi. Na hakuiona njia nyingine ya kulipiza zaidi ya kuendeleza mpango wake kama alivyopanga, Ili wajue kuwa hakuwa na mzaha. Na huyu aliyethubutu kumtegea sumu? Lazima afe, alijiambia. Maadamu wamekwisha mhukumu kifo sasa walikuwa ni maadui zake. Haikuwepo haja ya kuwasamehe. Kuhusu usalama wake binafsi alijua angefanya nini. Mara baada ya kufanikisha mpango wake huo angetoweka na kwenda mbali ambako angeanza maisha mapya. Kweli, mkono wa majasusi ni mrefu na umetambaa kila upande wa dunia, lakini usingemgusa yeye. Alijua vipi angeweza kujificha na kujigeuza kuwa mtu mwingine kabisa. Hii dunia ya pesa, nae alikuwa nazo za kutosha asingeshindwa kuzitumia zimgeuze kuwa mtu mwingine. Ikibidi atajigeuza kuwa mwanamke kabisa. Wazo hilo lilimfanya Proper atabasamu.

Alikuwa na uhakika kuwa huyu mtu aliyetega sumu hii lazima atarudi kutazama matokeo ya kazi yake, pamoja na kuchukua maiti ili aifiche kokote alikopanga. Akaamua kumsubiri mtu huyo kwa namna aliyotaka yeye. Alijifanya maiti aliyefia juu ya kochi, mkono mmoja na kichwa vikining’inia. Mkono wake wa pili ulikuwa umeshika bastola kwa uficho kiasi kwamba yeyote ambaye angeingia asingeweza kuiona wala kushuku.

Mtu huyo aliyekuwa akisubiriwa aliingia kimya kimya kama kivuli. Ilikuwa baada ya dakika kadha wa kadha kupita bila ya lolote kutokea. Ndipo Proper aliposhtukia mkono ukitua juu ya kifua chake kupima kama moyo ulikuwa ukifanya kazi. Hakujua mtu huyo alikuwa ametokea wapi. Wala hakuwa na haja ya kumtazama alikuwa nani. Taratibu aliinua mkono wake wenye bastola na kufyatua risasi tatu mfululizo. Mwili wa mtu huyo ulimwangukia pale kwenye kochi huku akitapatapa. Proper alipoinuka na kumtazama hakuweza kumtambua. Uso mzima ulikuwa umefumuliwa na risasi kiasi cha kuacha nyama nyama zenye damu ambazo hata mama yake aliyemzaa asingeweza kumtambua. Kiwiliwili kilikuwa salama. Kilikuwa kiwiliwili cha mzungu kilichofunikwa na mavazi ambayo kidogo yalimshitua Proper. Yalikuwa mavazi ya kipadri. Proper aliutia mkono wake katika moja ya mifuko mingi ya vazi hilo na kutoa kijimsalaba ambacho kilikuwa na maandishi yasemayo “Father Peter Jamaa” amemuua Padri! Proper alishangaa. Kumbe ni Padri huyu ambaye siku zote alikuwa siri yake na makao makuu! na asafiri salama huko peponi. 

Masaa matatu baadaye Proper alikuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam akisoma ratiba ya safari za ndege. Mkononi alishika begi lake dogo jeusi ambalo hata hivyo lilikuwa na vifaa vyake muhimu tu. Begi hili lilikuwa na mifuko kadha ya siri ambayo wakaguzi wasingeweza kuifikia. Mifuko hii ya siri ilihifadhi baadhi ya silaha zake na pesa za kutosha.

Hakujua alikotaka kwenda. Alichojua ni kwamba ilimlazimu kuondoka hapa nchi kwa muda ili kuwahadaa waajiri wake ambao bila ya shaka wangeanza kumuwinda kwa hasira kali zaidi. Vilevile kuondoka kwake kungempa ahuweni na fursa ya kusubiri siku aliyohitaji ili aachie lile pigo lake la mwisho. Kama kawaida, Ndege za Shirika la Ndege Tanzania ATC zilikuwa zimejaa, lakini baada ya dakika ishirini hivi alipata taarifa kuwa, ingewasili ndege ya AEROFLOT itokayo Nairobi, Kenya ikielekea Bujumbura, Burudi kupitia Mwanza, ambayo ingekuwa na nafasi. Proper alikata tiketi ya Mwanza na kuisubiri. Ilipowasili, alikuwa abiria wa kwanza kuingia ndani ya ndege.

kwa Inspekta Kombora alikuwa amevurugikwa kichwa kiasi cha kuchanganyikiwa kama alivyokuwa, simu hii ilikusudiwa kumtia kichaa zaidi.

Alikuwa katika ofisi yake, juu ya kiti ambacho hakikukalika, mara kwa mara akipiga hatua kuelekea dirishani ambako alisimama akichungulia kana kwamba alitegemea wakati wowote kuona uovu aliokuwa akiutarajia kutokea. Uovu ambao hakuujua, ingawa hakuwa na shaka kuwa ungekuwa wa kutisha kuliko mengi yaliyokwisha tokea.

Lolote lingeweza kutokea, aliamini Inspekta Kombora. Dunia hii iliyojaa waovu, nchini humu wakiwemo wa kutisha. Wako watu wenye mioyo ambayo husherekea kitendo chochote cha unyama. Watu ambao hutabasamu waonapo maafa na kushangilia waonapo mauaji. Watu kama hao si wachache. Si kuna yule aliyejaribu kuitia moto Benki kuu? Bila ya kujali wala kujiuliza kuwa nchi na wananchi wangetukiwa na nini baada ya pesa zote za hapa na za kigeni kuteketea! Si wako wale ambao wamepanga kuwaua viongozi ambao wamechaguliwa na wananchi? Naam, waovu wapo na si haba.

Lakini hawa wanataka nini?

Ni swali hilo ambalo lilikuwa limezidi kuneemeka katika kichwa cha Inspekta Kombora na hasa lilimtesa zaidi ya hofu yenyewe. Swali hilo ambalo lilianza kumsumbua tangu watu hawa wasiojulikana walipoanza kumfanyia njama Joram na hata kufanikiwa kumuua! Isitoshe, hawa waovu wamemuua Neema, Katibu wa Joram! Swali hili liliongezeka nguvu na kutisha zaidi mara alipopokea habari za kifo cha Neema katibu wa Joram! Ingawa kilionekana kama kifo cha kawaida machoni mwa watu wa kawaida, lakini Inspekta Kombora aliamini kuwa yalikuwa mauaji. Na hospitali ilithibitisha hivyo baada ya kugunduliwa kwa sumu kali mwilini mwake. Sumu ile ile aliyokuwa ametegewa Joram.

Watu hawa wasiojulikana, walikuwa wamekwepa mbinu zote za upelelezi. Kufikia sasa, hakukuwepo na fununu yoyote. Wala haikuwepo hakika kama alikuwa mtu mmoja au kikundi kimoja kilichokuwa kikifanya haya. Kifo cha yule malaya mzuri, Waridi, kifo cha Joram,kifo cha Neema… kifo, kifo kipi kingefuata? Na ni vifo tu au pamoja na… pamoja na nini?… Aliendelea kutaabika kimawazo. Ni mawazo hayo yaliyomzidishia hofu na mashaka mengi kichwani.

Haya, na sasa simu hii isiyoeleweka inachohitaji! Kombora alikitazama chombo cha kusikilizia kwa hasira. Kisha alinguruma tena kwa nguvu zaidi.

“Unasemaje wewe?”

“Mbona mkali hivyo Inspekta. Hutaki kupata salamu zako?”

Kombora alikumbuka sauti hiyo. Haikuwa ngeni masikioni mwake. Hata hivyo, alishindwa kukumbuka mwenye sauti hiyo moja kwa moja. Sauti hiyo ilionyesha dalili na dhamira maalumu. Kombora alishindwa kuikata simu hiyo kama alivyokusudia awali. Badala yake aliuliza.

“Salamu salamu kutoka wapi?”

“Kuzimu”

“Nini?”
Kicheko kikasikika kutoka upande wa pili: “Mbona unashtuka Inspekta? Si kuna rafiki yako aliyekwenda huko hivi karibuni? Anaitwa Joram Kiango. Au umemsahau mara hii?”

Sekunde chache zilizofuata Kombora alikuwa akisikiliza kwa makini zaidi. Dakika chache baadae tayari alikuwa ndani ya gari yake, bastola kibindoni, akimweleza dereva wapi apelekwe, kama alivyokuwa akielezwa katika simu.

Mara alitokea mmoja ya wasaidizi wake ambaye baada ya kupiga saluti alisema, “Mzee, kuna tatizo jipya limetokea.” Kombora alimjibu kwa kumkazia macho askari huyo. Hivyo akaongeza haraka haraka, “Father mmoja ametoweka tangu jana.”

“Ametoweka!” Kombora alifoka. “Mmekwisha mtafuta katika makanisa yote?”

“Kila mahali…”

“Katazameni hata makaburini. nasikia huwa anaenda juko kuombea watu.”

“Tumetazama huko pia lakini…”

Kombora akataka kwa ukali: “Aongeze nenda kata  katika nyumba ya wanawake malaya. Nasikia wengine wana mahawara zao.” Lakini hilo hakulitamka kwa kuchelea kuonekana mhuni mbele ya “vijana” wake. Badala yake alisema, “Sikia ninaharaka sana, nitarejea baadaye. Kwani kitu gani hasa kinawatia wasiwasi kwa mtu kutoweka usiku mmoja tu? Watu si hupotea hata kwa wiki na wakarudi salama?”

“Damu.”

“Damu?” Kombora alihoji kwa mshangao.

“Nguo alizokuwa kavaa zimeokotwa mtaani. na zilikuwa na damu .”
“My God!” Kombora alinong’ona akiingia katika gari na kumwashilia dereva atie gari moto.

#################

Wajumbe wote walikuwa wamehudhuria mkutano huu, ingawa baadhi hawakuuona kama ulikuwa mkutano wa kawaida. Kwanza, hawakutegemea kama ungeweza kufanyika mapema kiasi hicho na kisha njia zilizotumika kuitisha mkutano huu hazikuzingatia usalama wa hali ya juu kama walivyozoea.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)