SALAMU KUTOKA KUZIMU (17)

0
Mtunzi: ___

SEHEMU YA KUMI NA SABA
TULIPOISHIA...
Usiku mzima alikuwa amepingana na wazo hilo. Hakuwa mtu mwenye tabia ya kuyatupa matatizo yake kwa wakubwa. Lakini hili aliliona kuwa la hatari zaidi.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Maana lingeweza kuleta madhala ya kimataifa. Hivyo, haikuwepo njia nyingine ila kuiarifu serikali mapema kabla maji hayajamwagika.

Simu ilipokelewa na Katibu Mkuu mwenyewe. Maelezo ya simu hayakumridhisha Katibu Mkuu. Akamwamru Inspekta Kombora kufika ofisini kwake saa mbili kamili ili amuarifu taarifa hiyo barabara. Ndipo Kombora aliporejea nyumbani kwake ambako alioga, akabadili sare zake za kazi kisha akarejea ofisini kimya kimya kumweleza mama watoto wake wapi walilala. Haikuwa tabia ngeni katika kazi yake.

“Unadhani ni kweli mtu huyu ameamua kuitekeleza ndoto yake”, Katibu Mkuu alimwuliza Kombora baada ya kumsikiliza kwa makini.

“Ndiyo mzee”, Inspekta Kombora alimjibu baada ya kusita kwa muda.

“Tazama mtu huyu alivyofauru kumuua jasusi mwenzake aliyekuwa akijificha kwa kuvaa mavazi ya kipadri. Kwa kila hali anakusudia kuendelea na ndoto yake”, Inspekta Kombora alieleza kwa msisitizo.

“Na unasema huyu kijana Joram Kiango ambaye iliaminika kuwa amekufa, aliyesaidia kufichua yote haya hajulikani aliko?”, Katibu Mkuu wa Wizara aliendelea kuuliza.

Kombora alikohoa kabla ya kujibu. Hajulikani mzee. Ni ajabu kuwa yeye pia alitoweka. Naamini yuko katika msako wa kumtafuta huyu ambaye amemuua pia msichana wake mpenzi Neema. Hata hivyo juhudi zake hizo za kibinafsi akiongozwa na hasira zaweza kuleta madhara.

“Ingefaa tushirikiane…” Mara Kombora akasita baada ya kukumbuka kuwa mengine kati ya maelezo yake hayakumhusu Katibu Mkuu. Yalikuwa maelezo yake binafsi.

“Ndiyo, ndiyo Inspekta”, Katibu Mkuu alimjibu, “Sasa sijui sababu za kuniona mimi. Sidhani kama hutapenda kuniambia kuwa kikosi chako kimeshindwa kabisa hivyo unaomba msaada wa wizara nzima ifanye kazi ya kumsaka na kumtia mbaroni mwendawazimu mmoja tu”.

“Sivyo mzee”, Kombora alijibu akimtazama kijana huyu kwa aibu baada ya kumwita kijana huyu ‘mzee’ ilihali alimzidi kijana huyu kwa umri. “Naamini tutampata… Isipokuwa niliona ni vyema kukujulisha ili ikiwezekana uishauri serikali iahirishe kikao cha wakuu wa nchi zilizo mstari wa mbele”.

“Hilo haliwezekani kabisa”, Katibu Mkuu aidakia. “Kikao hiki mhimu mno. Ni kikao pekee ambacho kinaelekea kufanikisha dhamira yetu ya kuipatia Namibia Uhuru. Na kadharika tumekusudia kuratibu mbinu mpya za kuharakisha kutokomeza ubaguzi wa rangi Afrika Kusini. Aidha kikao kimeadhimia kujadili vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Sudan na Ethiopia. Tumekusudia kukuza misingi ya muungano wa Afrika. Haya ninayokusimulia ni siri kubwa. Naratajia utayahifadhi. Nimelazimika kukueleza haya ubaini kuwa kikao hicho ni muhimu. Haiwezekani kuahirisha mkutano huu. Ni wajibu wako kumnasa mtu huyo mnayemwita Proper.

“Fanya kila uwezavyo”, Katibu Mkuu aliendelea. “Kadharika, siri ya kunusurika kwa Joram Kiango ingepaswa ilindwe vilivyo. Kijana huyu ana busara sana. Anaweza kukusaidia kumpata mtu huyo. Lakini itabidi isifahamike kabisa kuwa kijana huyu yuko hai”, Katibu Mkuu akasita na kumtazama Kombora. Kisha akauliza ghafla.

“Kwa nini kijana huyu hujamweka katika kikosi chako”. Kombora akatabasamu. “Joram! Tumemwomba mara nyingi. Hataki. Ni mtu apendaye uhuru wake”.

“Na pengine mkiwa naye pamoja huenda akashindwa kufanya kazi yake”, Katibu Mkuu akaongeza. “Naona njia zake za upelelezi zimo katika tapo la kipekee. Nimezisoma harakati zake magazetini na katika vitabu mbalimbali”.

“Nadhani ni kweli”. Kikafuata kimya kifupi. Kombora alifahamu kuwa Katibu Mkuu alikwisha msahau na kuzama katika mawazo ya shughuli nyingine. Hivyo, aliinuka na kuaga. “Asante mzee”.

“Naamini utafanya juu chini kumpata mtu huyu Inspekta”, Katibu Mkuu alimtupia neno Inspekta Kombora alipoukaribia mlango.

“Bila shaka mzee”, Inspekta Kombara alijibu, huku kichwani mwake akijiuliza angeweza kufanya nini zaidi.

Proper alikuwa juu ya kitanda katika chumba cha mojawapo ya Hoteli nyingi za Mji wa Mwanza. Mkono wake wa kulia ulikuwa ukichezea matiti ya mischana mrembo aliyelala kando yake, mkono wa kushoto ulikuwa ukipepesa kiuno cha msicha huyu. Wote walikuwa uchi na miili yao ikitokwa jasho. Jasho liliendelea kuwatoka asubuhi hii yenye baridi kali. Jasho lililotokana na juhudi za miili yao katika kuthibitisha utaalamu na uwezo wao kimahaba.

Huyo alikuwa msichana wa tano tangu Proper aingie mjini Mwanza na kufikia katika hoteli hii… Wawili waliotangulia, alikuwa amewaona wa kawaida tu. Zaidi ya uzuri wao wa sura na maumbile ya kuvutia, kitandani hawakuwa na la ziada. Hivyo aliwapa ujira wao na kuwaaga. Lakini huyu wa tatu, hakuonekana kama alikuwa mtu wa kuagwa kwa urahisi. Sura haikuwa nzuri sana. Wala umbile lake halikuwa kama yale ambayo huwafanya madereva wa magari waroho wasababishe ajali barabarani kwa kuwatazama. Msichana huyu alikifahamu kile alichopaswa kuwatendea wanaume. Alielewa alichokusudia Muumba wake kwa kumwezesha kuwa na viungo tofauti. Kila kitendo chake kitandani alikitenda kwa ari na nia, bila uchoyo wa aina yoyote. Kila kiungo chake mwilini alikitumia kikamilifu bila hiana. Na hakuonekana mwanafunzi katika vitendo vyake vyote.

Ni hayo yaliyomfanya Proper ajisahau kwa kiasi fulani.

Ni kweli kuwa aliyoyaona Mwanza hayakuwa ya kawaida. Katika Jiji la Dar es Salaam ambako aliishi sana, kupata msichana au mwanamke wa kujiburudisha haikuwa tatizo. Ziko saa za jioni, au usiku, ambazo utajitokeza mitaani na kujipitisha. Hutavuka mtaa wa tatu kabla hujapata mtu ambaye ataivunja safari yake na kuandamana nawe hadi chumbani kitandani, ambako ataondoka alfajiri na siku ya pili. Lakini si hivyo kwa muda wa Mwanza. Hapa unachotakiwa kufanya ni kujipatia chumba chako kwanza katika moja ya hoteli nyingi zilizogaa. Kaa chumbani kwako kwa utulivu. Haitapita muda mrefu kabla hujapigiwa hodi na watoto wa kike ambao watajitia kuuliza hili na lile hadi maswali yao yatakapokufanya utoe jibu litakalowafanya waangukie kitendani.

Proper pia alitulia chumbani kwake kimya akingoja hodi yake. Haja yake haikuwa kujiburudisha tu, bali alitaka kujificha, ili aonekane kama wapangaji wengine. Kama vijana ambao waliamua kuonyesha ujana wao au wazee ambao waliifurahia fursa ya kuwaasi wake zao. Ndipo alipoanza kuwakaribisha wasichana mmoja baada ya mwingine hadi alipotokea huyu, ambaye hakuonekana kama alistahili kuondoka.

“Jina lako”, Proper alimwuliza huku akihamisha mkono mmoja kutoka kiunoni na kuupeleka kichwani kwa ajili ya kuchezea nywele ndefu zilizotimuliwa kutokana na zoezi lililokuwa likiendelea kitandani hapo.

“Sofia” msichana huyu alijibu kwa sauti ya mahaba. “Na wewe?” akaendelea kuuliza.

“Bakari, ingawa rafiki zangu hupenda kuniita Beka”, Proper alimlaghai.

“Kwa maana hiyo nikuite Beka siyo”.

“Hapana. Niite mpenzi”.

Sofia akacheka. Na kicheko chake kilikuwa cha kupendeza.

Baada ya muda, msichana huyu alipitiwa na usingizi. Kichwa akakiegemeza katika kifua cha Proper, mkono wake akauweka mahala fulani katika mwili wake, akawa amelala kwa utulivu mkubwa. Uso wa msichana huyu ulikuwa kama anacheka, kwa jinsi alivyokuwa amelala.

Proper alimtazama kwa muda. Kisha alijitoa kitandani hapo kwa uangalifu bila ya kumwamsha Sofia. Akaliendea begi lake ambalo alilifungua na kulichunguza. Sehemu za kawaida zilikuwa na mavazi yake, vitambulisho vyake bandia na vikorokocho vingine. Mifuko ya siri, ambayo kama alivyotegemea, wakaguzi wa uwanja hawakuweza kuifikia, ilikuwa na silaha zake, nyaraka zake muhimu, dawa zake maalumu, na pesa nyingi. Kila kitu kilikuwa kama kawaida. Proper akakirudia kitanda ambako alikiinua kichwa cha msichana huyo taratibu na kukirejesha kifuani kwake na mkono kuuweka kama ilivyokuwa awali. Kisha akayafumba macho yake kwa namna ya utulivu.

Lakini akilini hakuwa na utulivu wowote. Kichwa chake kilikuwa kazini kikitafakari matukio yote yaliyopita na ajali. Aliukumbuka kwa hasira mpangi wake madhubuti ambao aliuandaa kwa gharama kubwa na muda mrefu, na ulivyokaribia kumpotezea maisha. Ilimchukiza kuona kuwa waliokusudia kumwangamiza walikuwa watu wa upande wake. “Kwa ajili ya uoga”, aliwaz. Uwoga usio na msingi. Uoga ule ule ambao umewafanya kwa muda mrefu watumie pesa nyingi kukamilisha mabomu ya nyuklia, lakini hadi leo hawajadhubutu kufanya majaribio walao katika nchi moja. Wapi basi haja ya kusumbua vichwa? Yeye Proper angewaonyesha. Liwalo na liwe lakini mpango wake aliouanzisha lazima atautekeleza. Peke yake na kwa mkono wake Dunia ione Ulimwengu usikie.

Proper aliyarejesha mawazo yake kwa Inspekta Kombora na jeshi lake. Walikuwa wanafanya nini alijua kwamba, kifo cha yule Padri kiliwafungulia polisi mwanya fulani. Hata hivyo alielekeza fikra zake zote kwa kazi hii ya mwisho. Hakuna ambaye angeweza kulizuia pigo la mwisho, Pigo la kihistoria.

Proper alimtazama Sofia usoni. Akamuona alivyolala kwa utulivu. Angetokwa na kicheko kwa kumhurumia msichana huyu alivyolala kwa utulivu bila kufahamu amelala na mtu wa aina gani. Hajui kama amelala na kifo! Alinongona kimoyomoyo. Kisha alimwamsha na kumtaka wafanye tena mapenzi. Kama kawaida, msichana alikuwa tayari. Kama kawaida yalikuwa mapenzi ambayo yaliacha kumbukumbu akilini mwao.

“Wapi unaishi Sofia?” Proper aliuliza baada ya kukusanya pumzi kwa dakika kadhaa.

“Kirumba, nyuma kidogo ya Uwanja wa mpira”.

“Unaishi na nani Sofia?”.

“Peke yangu”, Kimya kifupi kikapita. “Kwa nini unapenda kujua?”.

Proper alipeleka ulimi wake kuchezea chuchu za Sofia kabla hajatoa jibu.

“Kwa sababu nyingi. Kubwa ni kwamba ni kwamba sijapata kukutana na aliyeniburudisha kama wewe. Nisingependa kutengana nawe tena, kwani nikikukosa huenda nisipate mtu wa aina yako. Hivyo, nimependa nihame hapa hotelini na kuishi kwako hadi shughuli zangu zitakapokwisha hapa Mwanza, halafu twende zetu pamoja Bujumbura. Unasemaje?”

Habari hii ilimfurahisha sana Sofia. Msichana huyu alikuwa ametoroka kwao Sengerema baada ya kupata mimba isiyokuwa na mwenyewe. Mimba hiyo iliishia chooni. Tangu siku hiyo, amekuwa mtu asiyekuwa na tumaini la kupata bwana wa kudumu. Sura yake pia, ilikuwa pingamizi kubwa. Daima mabwana aliowapata, walikuwa hawa wa ‘kuokota’ Mabwana waliosukumwa na uchu tu wa kuwa na mwanamke. Hali hii ilimfanya msichana huyu ajikabidhi kwa kila mwanaume bila kujali lolote, akiwatimizia kila haja bila aibu wala kinyongo.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)