Mtunzi: Omary John Mndambi
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Waliamka baadae sana wakiwa na njaa kali ambapo waliagiza chakula ambacho kila mmoja alikitamani lakini ajabu walishirikiana kwa kila mmoja kula chakula alichoagiza mwenzake kwa pamoja.
Walikaa wiki nzima wakiwa honeymoon ambapo kila siku mchana na usiku walikuwa wanafanya ngono kwa raha zao.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Sam alishamsahau Nisha na Verity na sasa alikuwa amejaa kwenye penzi zito na mkewe, alikuwa ammpenda na kumuona ni mwenzake, ni ubavu wake, ni mkewe lakini pia rafiki yake ambaye akikaa nae mbali kidogo anamkumbuka na kummisi.
……………………..
Hatimaye walirudi nyumbani na maisha yaliendelea kwa raha mustarehe yakiwa yamegubikwa na mapenzi mubashara.
Miezi ilisogea na hatimaye Verity alijifungua mtoto wa kike, mtoto Yule alikuwa mzuri kweli kwani alikuwa na afya njema.
Taarifa za kujifungua kwa Verity ziliifikia familia ya Sam na Rafiki kwa namna tofauti, Sam alifurahi akijua kuwa huenda mtoto aliyezaliwa ni wake japo hana mamlaka nae.
Rafiki alitaka amuangalie mtoto ili kama anafanana na sam basi atajua kuwa mtoto ni wa Sam, na ukweli huu ungemuumiza sana.
“nasikia Verity amejifungua”
“Eeeh kumbe” sam alijifanya hana taarifa wakati alishatumiwa ujumbe na Verity.
“Kwani hujui?”
“sijui wewe ndio wa kwanza kuniambia”
“Itabidi twende tukawaone ”
“Lini sasa”
“Hata kesho”
“Mhhh twende keshokutwa ndio siku nzuri kwanza ni wikiendi”
“Sawa”
“Basi ukawanunulie zawadi tuwabebee”
………………………………….
Sam na Rafiki walikuwa nyumbani kwa Verity na mumewe Gwakisa wakiwa wameenda kuwatembelea, walipokelewa vizuri wakakaribishwa chakula kisha wakaambiwa wasubiri sebuleni mama na mtoto wanajiandaa watakuja kujumuika nao.
Baada ya muda waliitwa sehemu ambayo ilikuwa imeandaliwa kwa ajili ya wageni wanaokuja kumtizama mzazi.
“Karibuni jamani”
“Ahsanteni….dah hongera mdogo wangu kwa kupata baby girl”
“Asanteni jamani sasa ni zamu yenu”
“Mhhhh sisi bado kidogo”
Walikaa kisha wakapewa mtoto wampakate akiwa amefunikwa nguo na kuacha uso kidogo.
Wakwanza kumshika Yule mtoto ni Rafiki ambaye alimfunua uso wote ukawa wazi kwa lengo la kumchunguza,
Alijikuta akishtuka kiasi kwamba hadi mikono ilimtetemeka, mtoto alifanana mno na Sam, kuanzia maumbile ya kichwa na jinsi nywele zilivyojichora kwenye paji la uso , aina ya uchekaji na tabasamu, pua na midomo mpaka masikio ilikuwa ni kama copy iliyotolewa kwenye photocopy machine mpya kabisa.
Sam nae alipopiga jicho kwa mbali alikuwa kama anajiangalia kwenye kioo kitendo kilichomfanya mapigo ya moyo yadunde kwa kasi ya umeme.
Sam alimtazama Verity kwa jicho la kuiba na kukutana uso kwa uso kwani Verity nae alishatamani kujua jinsi Sam atakavyopokea muonekano wa Yule mtoto.
Walivyokutana macho Verity alimminyia jicho Sam kisha SAM akakwepesha jicho haraka sana ili kitendo kile kisijeonekana na Rafiki ambaye hata hivyo aliziona action zote kisha akaamka na kumkabidhi sam mtoto.
“Shika mtoto wako Sam umtazame”
“Mtoto wa nani?” sam aliuliza.
Rafiki alitaka kujibu lakini alisitisha alichotaka kusema baada ya kumuona Gwakisa akiingia, kisha akanyamaza.
Walipiga stori nyingi lakini katika moyo wa Sam na Rafiki walikuwa wanawaza mambo mengine kabisa isipokuwa kwa Verity ambaye alikuwa anajua kila kitu kinachoendelea.
………………………………………….
Katika siku ambazo Gwakisa alifurahia ni baada ya kusikia mkewe amejifungua, alifurahi sana kwani katika umri wa miaka 34 aliokuwa nao alikuwa hajapata mtoto na aliona ni nafasi nzuri kwa yeye kuitwa baba kwani hata marafiki zake walikuwa wameshapata watoto na wengine walikuwa na watoto zaidi ya mmoja.
Alipopata nafasi na yeye kuitwa baba aliona ni nafasi adimu na nyeti sana, alimnunulia mtoto nguo na mahitaji mengine vinavyofikia thamani ya milioni moja.
Chumba kizuri cha mtoto kilikuwa kimeandaliwa kwani kwa nafasi ya meja aliyokuwa nayo jeshini ilimpa nafasi ya kumiliki kipato cha kutosha.
…………………………………..
Katika mambo ambayo wanawake hawajui ni kwamba Mungu amewapa nafasi adhimu sana ya kujua siri ambazo wanaume inabidi watafute kwa tochi.
Siri hii ni ile ya kumtambua Baba halisi wa mtoto, siku zote mwenye uhakika wa asilimia zote ni mwanamke.
Na ndio maana mtoto anapozaliwa mwanamke shauku yake ni kujua kuwa ni wa jinsia gani na ama anafanana nayeye ama amefanana na Baba yake wakati mwanaume anataka aangalie zaidi ya hapo, anaangalia jinsi gani amefanana nae ili ajithibitishie kuwa ni wake hata kama anamuamini mkewe kiasi gani, ndio maana wanaume wengi hujisikia fahari sana wakiwa wamefanana na watoto wao sana.
Hali kadhalika kitu cha kwanza kwa Gwakisa japokuwa alikuwa na hamu sana ya kuitwa Baba lakini haikutosha, alipomchukua mtoto kitu cha kwanza ni kumkagua amefanana nae ama vipi.
Alimkagua kuanzia kichwani mpaka miguuni lakini hakuona alichofanana nae, alikagua macho pua, viganja, kucha lakini wapi.
Wazo lililomjia ni kwamba huenda amefanana na mama yake lakini pia hata alipojitahidi kumfananisha na mama yake hakuona kuwa wamefanana sana.
Aliamua kuachana na fikra mbaya na kuamua kusubiri mtoto akue huenda akaonyesha sura halisi.
Kila siku zilivyosogea na mtoto kukua alionekana kufanana na mtu ambaye Gwakisa anamjua kabisa lakini anashindwa kuelewa ni nani.
Siku moja aligundua kuwa mtu anayefanana na mwanae kwa kiwango kikubwa ni Sam….ghafla alijikuta akikosa raha na kuanza kuoanisha mambo ambayo alishakuwa na wasiwasi nayo, alikaa akapata wazo kisha akaiendea simu ya mkewe aliyekuwa anaoga bafuni na kuanza kutafuta alivyojua yeye mwenyewe!
Miezi ilikuwa imekatika na hatimaye mwaka ukawa umeisha, Rafiki alikuwa akijisikia vibaya kichefuchefu kingi kiasi ambacho aliamua kwenda hospitali.
Alienda hospitali akiwa na mme wake (SAM) hadi hospitali ambayo ilikuwa na daktari bingwa, kwakuwa mda ulikuwa umesogea sana na hawakuwa wamepata matokeo chanya ya ndoa wakahisi huenda ana Mimba.
Walipofika vipimo vilichukuliwa vizuri na alionekana kuwa hakuwa na tatizo lolote na wala hakuwa na Mimba.
Wasiwasi ulikuwa mwingi kwani kwa muda wa zaidi ya mwaka ambao walikuwa wamekaa ndani ya ndoa lakini hakuna mimba ilikuwa sio ishara nzuri hata kidogo, aliyekuwa na wasiwasi sana ni Rafiki ambaye alijiona ana tatizo kwani kwa imani yake aliamini kabisa mtoto wa Verity kazaa na Sam, ushahidi aliokuwa nao ni ule mfanano na simu aliyopigiwa sam kutoka kwa Verity.
Hofu yake ilikuwa kubwa na alihisi huenda ana tatizo.
“Vipi mwanangu naona Shem siku hizi ananawiri kweli, ndoa imejibu nini?”
Sam alikuwa na marafiki zake wanapiga story kisha mwenzie akaingizia ishu hiyo
“Acha zako wewe, unapenda kufwatilia sana mambo ya wenzako, unadhani kila mtu anapenda kuzaa zaa kama wewe”
“Ohoo kuzaa ni nafasi adimu, kuna watu wanazeeka hawajawahi kuitwa baba”
“Sasa nani mzee hapa?”
“Hahahahaaaaaa umepanik brazaaaa, fanya mambo mtie Mimba mtoto Yule bado mbichi, shauri yako utasaidiwa”
“Dullah tuheshimiane mwana, mambo ya ndani kwangu hayakuhusu”
“Poa sam natania tu mwana ila …. Majibu broo ndoa inataka majibu wanawake wanasuburi nderemo na vigelegele”
“Unazingua sasa mimi naondoka zangu”
“Hahahahaaaaa nenda Baba ukatie mimba brooo, huku usikae sisi wenzio tayari tunaitwa Dadiiiii”
Maneno aliyokuwa anaongea Dullah alidhani ni utani lakini yalikuwa yamemuumiza sana Sam kiasi kwamba njia nzima alitembea akiwa na mawazo lukuki.
Ndani ya akili yake aliamini fika kuwa mkewe ndie mwenye shida kwani yeye alikuwa na uwezo mzuri tu wa kuingilia mwanamke na alikuwa ana sifa zote za kiume kwani hadi kutia mbegu shinani alikuwa anatia hivyo alihisi ardhi anayoweka mbegu ndio ilikuwa haina rutuba.
Alitembea njia nzima mpaka nyumbani akamkuta mkewe akiwa kajiinamia kwa mawazo, kila mtu alikuwa na mawazo yake na hakuna aliyemsemesha mwenzake.
Sam alikuwa na njaa lakini ham ya chakula hakuwa nayo, aliwasha TV aangalie mikanda lakini alikuwa hata haelewi anachokiangalia.
“Sam mme wangu”
“Unasemaje”
“Jamani mbona unaniitikia hivyo”
“Ulitaka nikae kimya?”
“Kwani vipi baba mbona kama una hasira”
“Nikiwa nazo utazishusha”
“Mhhh kama kuna tatizo tuambiane”
“kwani wewe umeniitia nini”
“Chakula mme wangu”
“Nakuja wewe endelea tu”
Rafiki aliondoka huku akiwa na mawazo lukuki akiwaza ninini kimemfanya mmewe awe kwenye hali ile, alidhani amekerwa lakini mbona hajamkera yeye mpaka amnunie na kumjibu vibaya?
Kwa mlolongo wa mawazo aliokuwa nao alijikuta akidondosha chozi.
Sam alitoka akamkuta mkewe akiwa kwenye hali ile kitendo kilichomfanya aingiwe na moyo wa huruma huku akijiona huenda amemkosea sana mkewe.
“Mbona uko hivyo?” sam aliuliza
Rafiki alijifuta machozi haraka kwani hakujua kuwa Sam alikuwa anamuona, “No niko sawa tu Sam”
“ oky chakula basi mke wangu”
“Sam aliwekewa chakula akaanza kula huku mkewe nae akiwa anakula taratibu”
“Samahani Rafiki kama nimekujibu vibaya mke wangu”
“Usijali ila kama kuna tatizo tuwe tunashirikishana”
“sawa haitajirudia”
“Ila mme wangu wewe majibu ya daktari kwamba sina Mimba wewe umeyachukuliaje?”
“Sasa mimi ningeyachukuliaje labda? Ndio hivyo hivyo”
“Hivyo hivyo kivipi?”
“Kwamba huna Mimba”
“Mhhhh unajua lakini mwaka na zaidi vimekatika? Watu watakuwa wanatutazama tu na huenda wanajiuliza”
“Hata mimi kwakweli najiuliza kwanini hushiki mimba”
“Labda nina tatizo mme wangu”
“Inabidi uende hospitali”
“Nitaenda kesho”
“Itakuwa vizuri”
………………………………………….
Pamoja na rafiki kuhudhuria hospitali nyingi na kufanyiwa vipimo vya kutosha majibu ni kwamba alionnekana kila kitu kwake kilikuwa sawa na hakuwa na tatizo lolote. Hapo ndio aliwaza kuwa ana shida gani mpaka asishike mimba.
“Usiwaze sana dada yangu, wewe si umeolewa?”
“Ndio”
“Basi mje na mme wako”
“MMMH mme wangu hana shida yeye tayari ana mtoto”
“Sio sababu dada, wewe njoo nae tu, sio matatizo yote yanakuwa ni ya kuzaliwa, mengine humtokea mtu wakati wowote na haijalishi mwanamke ama mwanaume”
“Sawa dokta nimekuelewa”
Rafiki alirudi nyumbani baada ya kupitia kazini kwake na kuweka mambo yake sawa, njiani alikuwa anatafakari jinsi gani atamueleza Sam ishu ya kwenda Hospitali kupima.
Alibuni njia mbalimbali hatimaye akapata wazo ni jinsi gani atawasilisha ujumbe wake,
Alipofika nyumbani alimkuta Sam amekaa nje anapunga upepo.
“Karibu mke wangu, habari za kazi?”
“Nzuri je za wewe?”
“Njema tu, hebu shika hii”
Sam alimkabidhi mkewe bahasha iliyokuwa na barua ndani, mkewe aliifungua na kuanza kuisoma.
Aliposoma na kumaliza aliona mme wake amechaguliwa kwenda Kenya kwa ajili ya Kozi za kipolisi ambapo atakaa miezi sita na hatimaye atapata likizo ya miezi miwili na kwenda tena kumalizia miezi mingine sita, kozi hiyo anatakiwa asafiri siku ya kesho yake.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)