JINI HUSNAT (10) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumanne, 21 Februari 2023

JINI HUSNAT (10)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
"HUSNAT umeua?"
aliisikia sauti ya babu yake muu! akaipuuza! muu kosa alilofanya nikuelekezea nguvu zake zote kwa VERGAN bila kukumbuka hatari ilokuwepo pale HUSNAT atakaposikia sauti ya kipenz chake na hata pale alipokumbuka alikuwa tayari kashachelewa.zuu aligeuka maiti! KIZAAZAA,....

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...


JINI HUSNAT akiwa juu ya farasi wake aendaye kwa kasi! aelea hewani mkononi kashika upanga unaomeremeta bado ghadhabu zilimuandama,hasira hizo zilimkosesha umakini na kujikuta akiwa katikati ya walinzi wa himaya yao.vita vikali vikatokea! jini husnat mbele ya majemedari makamanda watano akashindwa kujitetea nguvu zikamwisha.atimaye akasamli amri! akaweka katika nyavu tayari alikuwa ni muuaji akuthaminika tena katika himaya ya ujinini tena

vivyo hivyo hata kwa JOHN VERGAN babu muu baada ya kuona mjukuu wake tayar kakamatwa akuwa na sababu tena ya kumshikilia binadamu yule! majemedari wale wakamtia mkonon vergan na kumuambatanisha na jini husnat kuwarudisha ujinini kwa HUKUMU

Hakika taharifa aloipata jini mkuu MUKRAIYAH juu ya kuuwawa kwa mwanaye kikatili na JINI HUSNAT kilimfadhaisha sana

"naitaji wawe mbele yangu hapa sasa ivi?"

MUKRAIYAH akatoa amri,makamanda wale wakatoweka! malkia sumaiya kila mara alipoteza fahamu kwa mfadhaiko aloupata,wanajamii wa himaya ya ZULUWALADI na MUKRAHIYA wote walisikitika,zulu alikuwa ni jini mpole,msheshi mwenye kusaidia wenye matatizo mbalimbali,kila mtu alikuwa na hasira na JINI HUSNAT na VERGAN.ni wazi wangetafunwa wazimawazima.amani katika himaya ya zulu ilitoweka.majini waso na subira waliwavamia wazazi wa HUSNA

*****

Majini wale wenye wahka uvumilivu uliwashinda! wakawateka wazazi wa HUSNAT na kuwaweka pamoja wakawafunga na minyororo! katikati ya tanuri la moto! awakuwa na kosa nani alilitambua ilo? walizomewa wakapigwa mawe! majini walikuwa ni wengi katika uwanja mkubwa wakishuhudia kusambaratishwa kwa familia ya jini HUSNAT.

dakika chache badae jini HUSNAT na VERGAN waliwasilishwa wakiwa katika nyavu zenye matundu madogo madogo,kelele,na hasira zikazuka! uwanja ule mkubwa ulozungukwa na viumbe vilivyotisha,vikatili,vilianza kwa kuwanyanganya nguvu zote za asili! kwa wausika wote isipokuwa vergan yeye akuwa na nguvu za kijini.sasa awakuwa na uwezo wowote wa kujikinga na dhahama ilokuwa ikiwanyemelea kwa kasi ya ajabu WALIKUWA HATARINI.

Alikuwa ni jini mwenye sura mbaya pengine kuliko kiumbe chochote katika asili ile ya ujinini pembe mbili zenye ncha kali,mweusi tii zaidi ya mkaa macho yake yalowaka zaidi ya tochi,maskio kama ya ngurue kitovu kilichochongoka meno marefu kucha zake ndefu na miguuni alikuwa na kwato alikuwa na manyoya mengi katika mwili wake mkononi alishika upanga mkali ulowakawaka,alikuwa ni JINI MAUTI jini mwenye idhini ya kutoa uhai wa kiumbe chenye asili kama yake,jini asiye na huruma mkorofi na mwenye uchu katika kuuondoa uhai wa kiumbe hai chenye asili kama yake.yeye ndo alokabidhiwa rungu la kuwatoa uhai familia hiyo na kuifuta katika ramani ya ujinini akasimama na kuusogelea mwili wa baba yake HUSNAT na kunyanyua panga lake majini wote wakapiga kelele kushangilia.husnat na wenzake wakafunga macho walipofumbua waliachia kilio kikali cha uchungu!

mwili wa baba yake ulikuwa chini huku mkononi jini mtoa roho yule akiwa kashikilia kichwa cha baba yake akikitafuna kwa uchu! moyo ulimuuma akashindwa kuyazuia machozi kumdondoka.hata vergan huruma ilimjaa katikati ya kifua chake.wote walilia.ilikuwa ni furaha kwa majini wote walojaa katika kiwanja kile.baada ya kumaliza kuutafuna mwili ule jini maiti akausogelea mwili wa mama yake kipenzi....

Jini mauti yule akiwa kaushikilia upanga wake akaendelea kujongea taratibu mahali alipofumbwa mama yake HUSNA,uchu wa kula nyama za mama yule ukiwa umemvaa akaunyanyua upanga juu tayari kuushusha katikati ya shingo ya mama yule.

wakati jini maiti akijongea viumbe vyote vilikuwa makini kushughudia kinachoenda kutokea! ghafla jemedari wa ulinzi akaenda kumnongoneza kitu mfalme MUKRAHIYA,mfalme akashtuka akanyoosha mkono juu kuzuia kuuwawa kwa mama yule "kuna jambo la dharura limetokea ulinz uimarishwe tunavamia walinzi kaeni tayari kwa chochote!" mfalme alitoa taharifa ulinzi ukaimarishwa eneo lile ghafla mvua ya moto ikaanza kunyesha! watu wakatupwa huku na huko ardhi ikamomonyoka na kuwabeba baadh ya viumbe waloathiriwa na tetemeko lile! mvua ile ya moto yenye damu ndani yake ikazidi maradufu!...ghafla ikagoma,hali ya utulivu ikarejea.mvua ile waloweza kuizuia baada ya kuacha iliacha maafa makubwa ya raia.chanzo chake akikujulikana.wakati utafiti wa maafa yake ukiendelea ghafla kikazuka kimbuka kikali! kimbunga kilicho kuwa na nguvu ambayo si ya kawaida,jini mukraiyah akakinyooshea kimbunga kile fimbo yake huku akizungumza lugha asiyoielewa kimbunga kile kikajiunda umbo la kiumbe! mbabu mwenye ndevu nyeupe.babu muu.mwokozi alobakia katika familia ya jini HUSNAT!

"Amuwezi teketeza kizazi changu nami nkakaa kmya MUKRAHIYA!"

"ha! ha! ha! we shetwan mwenye nguvu za kuiba ulokimbia kujificha marz! leo umerudi nakwangamiza kwa mikono yangu!"

"uwezi ibilisi! nakwangamiza kwa mateso makali!"

alijitapa muu! na hapo hapo akaachia kombora la ghafla,Mukrahiya aliyoliona vyema akalikwepa na kuachia lake ambalo lilimpata vyema MUU! akapepesuka,kitendo kilichopelekea mukrahiya kutabasamu kwa dharau.muu akatema moto ulomezwa na mukrahiya mukrahiya akaivuta fimbo yake na kumchapa nayo muu.muu akaachia yowe la uchungu,nguvu zake zilikuwa ni ndogo sana kulinganishwa na MUKRAHIYA. akamchapa alivyotaka.muu akalegea mukrahiya akamsogelea tayari kwa kummaliza.............

*********

Akiwa kashika fimbo yake ya kifalme ambayo sasa iligeuka na kuwa upanga kwa mwendo wa taratibu bila haraka akajongea kusogea eneo alilokuwepo MUU.Mdomoni akiachia tabasamu la dharau.MUU alimwangalia kwa macho ya huruma yamkini akiwasilisha ujumbe aurumiwe! ila MUKRAHIYA alipuuza! watu walipiga kelele ishara ya kushangilia! jini mukrahiya alimfikia muu na kunyanyua upanga wake juu alipoushusha uliondoka na uhai wa jini yule alobaki tumaini! katika kizazi kile kidogo! akainyonya damu yake kwa kuifyonza! huku akiungamua utamu kwa kukitingisha kichwa chake taratibu!

"hudumu utawala wa mukrahiya"

"hudumu,udumu,udumu milele na milele!"

"sasa wakati naendelea kula nyama tamu ya huyu swaiba wangu MUU sasa ni mrudishie uwanja jini maiti aendelee kunyofoa uwah wa viumbe hawa! jini HUSNAT awe wa mwisho akishuhudia vifo vya vipenz vyake."

JINI mukrahiya alitoa maelezo yakinifu yalopokewa kwa vifijo.jini maiti akajongea eneo la tukio na kuondoka na uhai wa mama yake HUSNAT mwili wake akaukata kata mapanga na kuupiga shoti kwa nia ya kuugeuza mlo mara eneo lile likatawaliwa na harufu ya nyama ya kuchoma akawa anakata mapande ya minofu na kuwatupia walokuwa wanashughudia tukio lile nao wakawa wakiigombania nyama ile! huku kinywaji ikiwa ni damu mbichi ya maiti zile.Sasa HUSNAT akulia tena,machozi yalikata,uchungu uliushambulia moyo wake mdogo! babu yake MUU,baba yake,mama yake wote walikuwa maiti kwa ajili yake! kwa ajili ya penzi la binadamu ambaye naye anaelekea kufa! akamwangalia VERGAN ambaye aliona mtetemeko wa wazi.alikuwa akitetemeka huku akiwa kaachia haja zote kubwa na ndogo.kilio cha kwikwi kikisikika kwake.

"chanzo cha matatizo yote ni huyo binadamu atauwawa kwa kukatwa kiungo kimoja kimoja! yeye ndo kaja kuuchafua mji huu.kama si yeye HUSNAT asingemuua mwanangu nawachukia binadamu jini maiti anza kukata kidole kimoja kimoja ukimaliza vyote kata mguu paja kiuno na kichwa."

JINI MUKRAHIYA akiwa anamwangalia VERGAN kwa jicho kali akatoa maelekezo.....

*********

Majini wale wenye hasira! bado waliendelea kupaza sauti! kuarakishwa kwa hukumu ya kifo kwa wapenzi wale wawili! JINI HUSNAT na JOHN VERGAN!,wahka!,jazba vilimpanda jini maiti yule alihisi kitendo cha kumkata kiungo kimoja kimoja binadamu yule angechelewa kuitafuna nyama yake ilokuwa ikipendwa sana na viumbe wale.akaunyanyua upanga wake na kumsogelea VERGA,muda wote husna alikuwa akilia huku akiomba msamaha akijutia kwa alichokitenda.alijiesabia tayari yeye ni mfu mwenye mda mchache wa maumivu! alifumba macho pindi jini maiti aliponyanyua upanga juu ili asishughudie kichwa cha mpenzi wake kikitenganishwa na kiwiliwili.

JINI MAITI kwa nguvu zake zote akaushusha upanga kuelekea shingoni kwa vergan....ghafla akalakiwa na sura yake mwenyewe! yani sura ya vergan ilitoweka na sura ya jini maiti ikaonekana.yani akawa anajiona.HATARI! akaisi kitendo cha kujikata angejiua mwenyewe AKASITISHA ZOEZI LILE huku akiwa kahamaki kwa mshangao wa alichokiona,bumbuwazi likauvaa uso wake macho yake akayapeleka kwa jini HUSNAT alokuwa kaiweka mikono yake miwili usoni kutokushughudia tendo lile.liumizalo moyo.shingo yake akairudisha kwa VERGAN alikuwa ni vergan naye akishangaa kutokujua kulikoni! jini maiti akazidi kupigwa na butwaa! jini HUSNAT alifumbua macho akitegemea kuiona maiti ya mpz wake naye akapigwa na butwaa baada ya kumuona jini maiti akiwa kamtumbulia vergan macho ya mshangao! si jini husnat pekee alokumbwa na mfadhaiko ule hata umati ule ulibaki ukimshangaa jini yule mwenye roho mbaya kwa kitendo cha kusitisha zoezi lile,minongono ya chini kwa chini ikaanza! jini maiti kwa mara nyingine akaunyanyua upanga wake alipotaka kuushusha hali ikawa ni ileile....VERGAN alibadilika na kuivaa sura yake

"ni ni ni kinachoendelea hapa?" jini maiti akajiuliza akakata shauri liwalo na liwe kama ni kujiuwa na iwe.akafumba macho yake makali kama taa na kuushusha kwa nguvu upanga ule kuelekea kichwani kwa VERGAN...,.kwa nia dhabiti ya kuuondoa uhai wake bila kujali maajab

*******

JINI maiti akakata shauri liwalo na liwe! akayafumba macho yake makali na kuushusha kwa nguvu upanga ule...akakata hewani.wakati kabla ajafumba macho alilenga sawia shingo ya kijana yule akafumbua macho yake! asalaleee! watuhumiwa wake awakwepo! mashuhuda wote midomo wazi,tayari jini HUSNAT na VERGAN walishatoweka katika mazingira ya kutatanisha!!!

NGUVU gani zinazotumika hapa? zilizojuu ya nguvu zao? akuna alojua! kimuyemuye kikazuka! tafakuru makelele yakazuka! yamkini akuna aliyetambua nani yupo nyuma ya mchezo ule! walipoangalia kuzimu apakuusika,sasa tatizo? mganga mkuu wa himaya ile akaitwa akapanda kilingeni kwa mbwembwe alikuwa ni jitu nene jeupe lenye kichwa cha ngurue tumbo kubwa manyoya ya kutosha kucha ndefu na meno yalochongoka nje! baada ya kufanya vimbwanga akatoka na jibu lililo waacha hoi majini wote

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni