JINI HUSNAT (11) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumanne, 21 Februari 2023

JINI HUSNAT (11)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
walipoangalia kuzimu apakuusika,sasa tatizo? mganga mkuu wa himaya ile akaitwa akapanda kilingeni kwa mbwembwe alikuwa ni jitu nene jeupe lenye kichwa cha ngurue tumbo kubwa manyoya ya kutosha kucha ndefu na meno yalochongoka nje! baada ya kufanya vimbwanga akatoka na jibu lililo waacha hoi majini wote

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
"WAPO DUNIANI! BINADAMU WABAYA WAMENUNUA VITA!"

"tutapambana nao kufa na kupona hawana nguvu kutushinda sisi"

"hidumu himaya hii"

"hidumu! hidumu! hidumuuu!"

vijakazi walinzi watatu wakatumwa duniani.mchezo ndo ulikuwa unaanza.....

-....-....-....-

NDANI YA ULIMWENGU WA DUNIA
Ilikuwa ni nyumba moja ya kifahari sebuleni mwa nyumba hiyo waliketi watu watatu! mzee wa makamo ambaye kichwa chake kilitawaliwa na mvi zilizo meremeta,usoni alivaa miwani na mwilini alivaa nguo za gharama,huyu aliitwa MZEE VERGAN CHILO maarafu kama mzee CHILO baba yake VERGAN,pembeni yake aliketi mwanamama wa makamo alovaa gauni la kitenge lililonakshiwa na mapambo ya kuvutia alikuwa ni mama alojaliwa macho mazuri na unene ulopitiliza huyu alikuwa ni MAMA VERGAN,na watatu alikuwa ni msichana mrembo mwenye umbo namba nane macho malegevu,dimpoz katika mashavu yake huyu alikuwa ni JASMINI mfanyakazi wa ndani nyumbani kwa JOHN VERGAN.Wazazi hao walikuwa wakimsikiliza kwa makini binti yule mzee CHILO akauliza swali kwa mshtuko

"umesema wiki nzima VERGAN ajaja nyumbani?"

JASMIN huku akiwa anatetemeka akatingishwa kichwa ishara ya kukubali...

********

Mzee CHILO na mke wake wakatazamana kwa mshangao!!

"mke wangu ulishaongea na huyo mtoto siku za karibuni?"

mama VERGAN akatingisha kichwa ishara ya kutokubaliana na jambo ilo,chilo akachukua simu yake na kuitafuta namba ya VERGAN akaipiga lakini namba ile aikuwa ikipatikana!

"rudi nyumbani mamaa ntalifatilia hilo!" mzee yule akamweleza mfanyakazi aliyejinyanyua kwa uchovu na kuaga! akiacha hali ya sintofahamu katika familia ile yenye uwezo kiuchumi

"au atakuwa kasafiri?"

Mzee CHILO alitoa sauti ndogo kama anaongea mwenyewe lakini ukweli alikuwa anaongea na mke wake

"sidhani mme wangu! asafiri bila taarifa?"

"itabidi niende kazini kwake ntajua pa kuanzia kumtafuta huyu mtoto kabla atujatoa taharifa polisi"

mzee CHILO akaitimisha kwa kujinyanyua katika sofa lile alilokuwa kakalia mke wake akaachia muayo mkubwa ambao aukujulikana kama ni wa uchovu,usingizi,ama mashaka....

.......................

kwa jina alitambulika kama ALEX ila wengi walimtambua kama MWANDISHI,kutokana na tabia yake ya umbea,unoko,unafki na uchunguzi akiwa ni mmoja wapo wa wafanyakazi walotegemewa katika kampuni alomiliki VERGAN,akipendwa na viongozi wa juu kutokana na kuwasilisha umbeya alougundua chini kwa wafanyakazi wenzake!,na pia alipendwa na wafanyakazi wenzake kwa kuwaletea umbea utokao juu.huyu ndo alikuwa mwandishi kijana mrefu kiasi,maji ya kunde mwenye tabasamu la ucheshi muda wote!

mwandishi Alikuwa ndo wakwanza kuwa na wasiwasi juu ya upoteaji wa VERGAN lakini ilibaki siri ya moyo wake! ALISHUGHUDIA kila kitu akiwa katika uchunguzi wake! jicho lake likiwa katika tundu la funguo mlangoni aliuona ugomvi wa JINI HUSNAT,VERGAN,na MOURINE mpaka MOURINE aliposhambuliwa shoti na WAKATOWEKA.hakika kitendo cha kuona kilimchanganya sana.maajabu ni kwamba akuweza kufungua mdomo wake kusema.japo hamu ya kutoa habari ile ambayo ingempa uma harufu alikuwa nayo lakini alishindwa kusema.alikuwa kama kagandishiwa gundi mdomoni KWA NINI? sababu aikujulikana mwandishi akakosa amani..

Ilikuwa ni kampuni kubwa katikati ya jiji ilomilikiwa na kijana mdogo JOHN VERGAN,jengo ilo lilikuwa ni kivutio kwa wapita njia,jengo ilo la kisasa lilibeba ghorofa nne za vioo kwenda juu lilikuwa ni moja wapo ya majengo maarufu jijini pale

mzee wa makamo alishuka ndani ya gari yake ya kisasa aina ya TOYOTA VEROSA,alikuwa ni mzee chilo,baba yake vergan akachepuka kwa mchepuko wa hatua zake fupi fupi ila za haraka haraka kuelekea ndani ya jengo lile "RECEPTION" ulisomeka mlango ulokuwa mbele ya macho yake ambao palikuwa na uwazi pasina mlango wa kuingilia akazama ndani alipopokelewa na wafanyakazi nadhifu ambao kila mmoja wao alikuwa bize katika kompyuta yake na ma faili katika meza zao

"shikamoo mzee!"

mwandishi akatoa salamu huku akiamisha macho yake toka katika kompyuta kujua kulikoni? alihisi kitu

"si kawaida huyu mzee aje kututembelea! kuna kitu lazima niwe makini nisipitwe!" aliji tahadharifa

"marhaba! JANETH naweza nikamuona meneja?" baba yake VERGAN akajibu salamu wakati huo huo akimfata msichana ambaye alionekana ndo secretari.msichana yule akatabasamu akaukwapua mkonga wa simu na kuuweka masikioni akabonyeza tarakimu kadhaa MWANDISHI alikuwa makini asipitwe.kwake lilikuwa ni kosa kubwa

"haloow bosi! mzee anaitaji kukuona!....sawa mzee ingia!"

mzee CHILO akaiparamia ngazi kuelekea juu! mwandishi naye akajinyanyua na kumfata kinyume nyume wafanyakazi wala hawakumshangaa walishamzoea walisubiri habari mpya mzee chilo akafika katika mlango uloandikwa maneno "mkurugenzi" akabisha hodi mara moja kabla ajakitekenyua kitasa cha mlango ule kikamtii akazama ndani.mwandishi akaishia mlangoni akapiga chabo kujua kinachoendelea ndani! ndani mzee CHILO alimkuta mzee wa makamo kidogo JENGUA wakakumbatiana kwa furaha! huyu alikuwa ndo msaidizi wa VERGAN baada ya makaribishano CHILO akaeleza shida,dhumuni la kwenda pale ni juu ya kupotea kwa mwanaye mmiliki wa kampuni ile JOHN VERGAN

mwandishi akashtuka pale mlangoni na kuweka mkono..

********

mwandishi akashtuka!,akaweka mkono mdomoni kwa mshtuko aloupata kumbukumbu zikarejea wakati JINI HUSNAT na MOURINE(JINI ZAYDATU) wakirushiana shoti na wote watatu wakatoweka sasa ni wiki mbili zimekatika bila kuonekana kwa bosi wao VERGAN! kwa unyonge mikono kaiweka nyuma akarudi eneo alipotokea "mapokezi!" akapokewa kwa bashasha na wafanyakazi wenzake!

"mwandishi baba kaja na shida gani?" mfanyakaz mmoja alimchokonoa akikaa kiumbea

"sijui sijawa kivuli chake" mwandishi alijibu kwa mkato na kuendelea na kazi! umbea ulimwisha.ilimlazimu afunge domo lake akujua kwa nin

kule ndani mzee jengua alishangaa kupotea kwa mkurugenz wake VERGAN katika mazingira ya kutatanisha! akukuwa na habari ambayo ingewafumbua macho.ikabidi mzee CHILO aage kwa minajili ya kwenda kituoni.akaruhusiwa bila kipingamizi.akatoka,akawaaga mapokezi! muda wote mwandishi alitaka kufumbua mdomo wake lakini alijikuta akishindwa mpaka mzee CHILO akaondoka katika eneo lile.

............

alishangaa siku iyo mawazo kumtawala na kuyakosea majibu! ili kuyapoteza mawazo hayo ni lazima akapate bia mbili tatu! mwandishi SIRI ilimtesa aliitaji kuwa huru mwingi wa furaha kwa kuitoa siri hiyo! ila kwa nini kila nikitaka kusema nashindwa? akawaza akigubia bia ile kwa fujo! ghafla pombe zikamkaa kichwani wazo ambalo alikuwa mwanzo likajijenga! akatabasamu ni wazo ambalo lingemwingizia hela! wazo hilo lililomtesa kwa muda mrefu tangu alipolishughudia kwa macho yake mawili likageuka dili.dili ambalo kama angelicheza vizuri angekula ela nyingi,..akili ya pombe sasa zilimletea faida.akashika simu yake na kupiga namba kadhaa

"naongea na mama VERGAN?"

"ndiyo mimi ni mwandishi ALEX....ndiyo baba alikuja kazini nkashindwa kumwambia kutokana na itikadi zake za kidini ila naitaji tuonane uwe peke yako nikueleze mahali mwanao alipo! kweli mama sikutanii ila uniandalie ela kidogo! nyumbani? amna mtu? poa naja saivi mama"

baada ya kumaliza kuongea na simu akaikata na kujinyanyua kiuchov huku akiwa anapepesuk

******

Akiwa anapepesuka MWANDISHI alianza kujongea kutoka eneo lile la club muda mwingi akikosa muhimili na kudondokea meza na viti maeneo yale! akujali alinyanyuka na kuliendea gari lake.akaingia ndani na kuliondoa.....

maajabu!! usingeweza kuamini yule mlevi ambaye dakika chache alikuwa akipamiana na viti ndo aliyomo ndani ya gari ilo.mwandishi alikuwa makini barabarani japo aliwaza kilevi!

"ili ni dili la fedha! kwa kuwa ni swala nyeti...ni dili ambalo ntashrikiana na familia hii mpaka nijue mwisho alafu habar hii sitomuadithia mtu ntaipeleka kwenye magazeti ambapo ntalpwa kiwango kikubwa cha ela! aya macho yanaenda kuntajirisha." aliwaza huku akiingia mtaa walokuwa wakiishi wazazi wa bosi wao.akaelekea mpaka kwenye nyumba ya kifahari mlinzi akafungua geti mwandishi akaingiza gari lake mpaka ndani.akashuka huku akipepesuka akaelekea sehemu alimostaili kuelekea.....

...........

alipigwa na butwaa alomkuta ndani akutegemea kumkuta.moyo ukaanza kumwenda mbio na pombe taratibu zikaanza kuyeyuka.ni baada ya kumkuta mzee chilo baba yake VERGAN ambaye kiukweli alimuogopa

"karibu sana mwandishi sijui uletewe kinywaji gani?"

"maji tu yanatosha" alijibu ki khofu huku mwili wote ukimloa jasho kwa anguko la tetemeko.mwandish Alex alitetemeka hadi meno mama VERGAN akaliona ilo ili kumtoa khofu akamwambia

"mwandishi usijali kama ni pesa utapata na usimwogope mzee naye yupo pamoja nami tueleze mwanetu yupo wapi au katekwa na nani na wanaitaji nini?" moyo wa Mwandishi kidogo ukaridhika baada ya kutolewa khofu akaanza kuongea kwa kujiamini

"wazee wangu hii ni siri nyeti siri ambayo baada ya kuitoa yaweza chukua uhai wangu je ntaiachaje familia yangu? bila milioni 50 kuingizwa kwenye akaunti yangu sifumbui mdomo"

"unasema?" mzee CHILO akauliza kwa hasira

"milioni 50 nieleze ninachojua juu ya bosi hata nikifa familia yangu isipate tabu"

"milioni 50 eeh subiria nkakuletee....." mzee chilo akaingia ndani na kuchukua simu na kupiga kituo cha polisi

aliyepokea simu kituoni akaidi robo saa kuwa maeneo yale.

............

afande au waweza kumwita SAJENTI KIKOTI akiwa kituoni,alikuwa kavaa nguo za kiraia,wakati akiwa kituoni hapo mara simu yake ya mkononi ikaita akaangalia mpigaji akaachia tabasamu dogo na kuaidi kufika eneo la tukio robo saa.akainuka na kuchukua maafande wawili na kuingia katika difenda!

........

wakati mwandishi akiwa anasubiria milioni 50 zake aliamua kukunja nne kabisa,mawazo yake yalikuwa mbali sana kifikra! maendeleo aliyoyawaza yalikuwa ni zaidi ya fedha alizoitaji! aliwaza kutengeneza bonge la nyumba maeneo ya wanaoishi matajiri ufukweni mwa bahari!,magari ya kisasa,ajenge maoteli ya nyota kah! kwa milioni 50? na vimilioni 5 vyake benki! akaachia tabasamu afifu alilolizima ghafla baada ya kuingia maaskari  moyo wake ukapasuka paaaaa! tayari hatari ilishawaka katika fikra zake.

"afande huyu kijana anajua kila kitu anaitaji milioni 50 eti ndo atueleze"

"what?"

kikoti alistaajabu akaendelea

"afande marwa piga pingu ilo likaeleze kila kitu kituoni sijapata kuona jambaz jinga namna hii"

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni