JINI HUSNAT (9) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatatu, 20 Februari 2023

JINI HUSNAT (9)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
JOHN VERGAN bado alikuwa katika bumbuwazi la wazi wazi wajenzi huru yeye alisadiki kuwasikia tu! tena katika midomo ya watu! akupata kuisi siku moja angeitajika naye awe mfuasi huru.ALITAITIKA! akataitika! baada ya lusifa kumuona yupo kimya akaendelea....

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
"tunakupa mda masaa 48 utafakari ili! ndani ya masaa hayo tutakutembeza katika maeneo mbalimbali humu kuzimu uone sawa?"

vergan akajikuta anatingishwa kichwa kuafiki!

"huyu anaitwa fidodido nadhani mara nyinyi sana mnamtumia kama katuni huko duniani kwenu kiumbe hiki kipo na leo ndo kitakutembeza maeneo mbalimbali katika ulimwengu wangu huu...."

fidodido akaibuka alikuwa ni kiumbe mwenye nywele saba! usoni alivaa miwani ya shaba! akaachia tabasamu pana!

"nifate!"

akamwambia VERGAN ambaye naye alimtwii bila shurti akuwa na kipingamizi chochote

lilikuwa eneo lililokuwa na joto la kupindukia! joto ilo lilitokana na mioto mikali ya rangi tofauti tofauti.

moto wa kwanza kuutembelea ulikuwa ni ule alonusurika kutupwa.ghafla akawa na shauku! shauku kuu la kujua baadhi ya mambo akashindwa kuuzuia mdomo wake kutokuuliza.akauliza swali.swali lililotegemewa na fido kuulizwa!

"hawa binadamu wamekosa nini mpaka wanateswa hivi?"

fido! akatabasamu,kinywa kilikuwa wazi akukuwa na jino hata moja! si jino tu hata ulimi akuumbiwa nao huyu kiumbe! maajabu! sijui aliwezaje kuongea.....

"viumbe hawa ni watakatifu! walokataa kujiunga na dini takatifu ya frimason baada ya kuonekana wana vigezo! wengi wao ni mapadri! masheghe na baadh ya binadamu wamuogopaye MUUMBA..."

mwili wa vergan ukatetemeka woga ukamtawala yamkini naye baada ya siku mbili kama angekaza msimamo wake naye angekuwa miongoni mwao.

"kwanini MUNGU amewaacha viumbe wake wateseke namna hii kwa nin? ajawapa nusra? ya wokovu!" swali hili likakivamia kichwa chake kama wazo kuu.wazo ili likanyakwa na fido naye akalijibu swadakta!

"wengi waliomo humu wananguvu za MUUMBA sasa walipokuwa duniani walikuwa wakiwasema vibaya friimason lusifar aliwatumia watu"

*******

@ "wengi wa walioko huku duniani walikuwa waki ikashifu dini ya freemason!,wakiandaa mikanda ya video na kutupinga vikali japo tuliwatuma wajumbe kuwaonya awakusikia! walitegemea nguv za MUUMBA! na MUUMBA ni mwingi wa mitihani hii ni moja wapo ya mtihani wake kwao! kuingia peponi (paradiso) si mchezo sheghe wangu lazima ukutani na vikwazo vikali kule uwezi ingia hivi hivi...."

VERGAN akataharuki maneno ya fido yakamuingia vyema naye alimtambua MUNGU? kah! wakatoka eneo lile ambalo alipata kuwaona watu alowafahamu walokuwa wakiitangaza vibaya dini hiyo duniani katika membari za misikiti na mahekalu ya makanisa.ilosemekana wamekufa wengine kwa magonjwa wengine ajali n.k

moto mwingine waloutembelea ulikuwa ni wa rangi nyekundu huu aliushangaa sana.alipata kuwaona wasanii maarufu wa filamu na muziki waloiwakilisha vyema nchi yake kimataifa!

"hawa nao?"

"hawa nao walikula agano mfano yule msanii wa muvi alivuma sanaa akajulikana lakini alipoambiwa amtoe mama yake sadaka akakataa ndipo tukamchukua na kumleta humu kwa jeuri yake! yule mwingine aliitaji miaka ishirini ya mafanikio na kula bata kama muitavyo duniani baada ya miaka yake ya awali 20 kuisha inayobakia anakuja malizia huku ivyo ndo ilivyo"

MAKUBWA! tafakuru la mawazo ya mshangao yakajijenga katika pande la uso wake! wasanii wakubwa karibia wote alowajua walikwemo kule kumbe awakufa kwa mapenzi ya MUNGU? ALLAH! okoa kizazi chako.

wakapiga hatua watu walikuwa uchi wazee vikongwe kwa vijana

"kah na hawa? fido"

tayari vergan alishamzoea kiumbe yule fidodido

"hawa ni wanga wamezoea kula nyama za wenzao wachawi wenzao zamu yao imefika awana cha kutoa wengine asahasa vile vibibi vimetoa watoto wao wote muda wao nao ukafika! wengine ndo walotolewa kafara ndo kana ivyo dogo"

sasa VERGAN alikuwa kachoka mwili na roho aliitaji kupumzika.fidodido akalitambua hilo.tutazunguka tena badaye saivi ukaoge upate mlo upumzike..umechoka sasa

"naam swadakta"

akajibu vergan kwa tabasamu pana.Itaendelea usiku.....

******

wakajongea kwa mwendo wa taratibu kuondoka katika eneo lile,eneo la mateso kwa viumbe jamii yake viumbe vilivyosadikika vimekufa kwa mapenz ya MUNGU!

Wakaelekea katika lango kuu la chuma lililonakshiwa kwa dhahabu tupu walipolifikia lango lile likajifungua lenyewe wakapita likajifunga ndani walikutana na mazingira tofauti na walipotokea! kwanzia khali ya hewa,mandhari,

"bado tupo kuzimu kweli?"

swali likamponyoka kuuliza,swali ambalo akuliandaa kabisa katika serikali ya kichwa chake! fido akatabasamu akujibu swali ilo wakaelekea katika nyumba moja ya ghorofa isiyo na mwisho kuelekea juu wakaingia katika lifti fido akabonyeza namba kadhaa za kirumi lifti ikaanza kupanda juu dakika chache ikafika ilipoitajika mlango ukafunguka! MAAJABU! wakatokea katika ukumbi mkubwa ulotawala watu wa asili tofauti tofauti waarabu,wazungu,wataliano wakicheza miziki ipigwao duniani,miziki ya watu maharufu ambao baadh yao walikuwa wakichomeka! kitendo cha kuingia tu msichana mrembo alovaa kimini,matiti yote yalikuwa nje akamfata vergan!

"nipo kwa ajili yako je unani itaji?"

vergan akamtupia jicho fido! fido yeye alitabasamu tu!

"chukua mzigo huo"

nafsi ilimsihi.macho yake yakadondokea kidoleni! PETE,

JINI HUSNAT,kwa mara ya kwanza toka amezwe na OBISHI na kusafirishwa kuletwa katika ulimwengu wa maaswi KUZIMU akamkumbuka jini yule! faraja ikatoweka moyoni mwake,mshangao ukageuka na kuwa simanzi! dada yule akamlalia kifuani mkono wake akiuingiza katika sehemu nyeti zilizokwisha simama.mazingira ya ndani mule ayakuvutia kabisa ilikuwa baadh wanacheza mziki,wengine wanafanya mapenz adharani akuna alokuwa na habari na mwenzake!

"samahani dada naomba niache!"

dada yule akapigwa na butwaa akamuacha,

"tuondoke maeneo haya fido."

fido akatii wakaifata ngazi na kupanda kuelekea juu katika ukumbi ambao watu walikuwa wamepumzika.wakatafuta sehemu wakakaa

"najua kinachokuumiza best! ni juu ya jini wako siyo?"

VERGAN akapigwa na butwaa.

"pEndo la moyo wako! ila pole vergan HUSNAT sasa ni mke wa mtu?"

"what? hapana fidodido unataka kunambia nin? siyo husnat wangu! aiwezekani! haiwezekani aiwezekan fido husnat akubali kuolewa! vip kiapo tulichokula wakati tukiwa dunian kabla ajanipa hii pete? eti leo aolewe kama uwez kaa na mim katika ukanda huu wa kuzimu ruksa kuondoka na kuniacha mwenyew..."

"common vergan listen my frandy sit down kwanza punguza munkari nipe maskio yako upasw kuamaki mpak watu wanatwangalia? unageuka burudani kwa wapumzikao!"

"aijalishi fido! ila ukwel uwez nambia husnat...yah kipenz changu jini husnat kaolewa"

"VERGAN!..." fido akaita! vergan akamtumbulia macho ishara ya kumsikiliza!

"uwezi pindisha ukweli kuwa uwongo nevar happen! pokea ukwel japo mchungu! husnat ajakusaliti kaolewa kwa sababu maalumu!"

"sababu maalumu? ipi hiyo?"

"ni juu ya kisas kwa OBISHI! yule nyoka alokumeza!" kwa mara ya kwanza kumbukumbu za vergan zikaanza kutiririka kama maji yatiririkayo kutoka bombani.akakumbuka akiwa kakamatwa kisawasawa na nyoka yule mpaka akapoteza fahamu! baada ya hapo ikawaje? akukumbuka! naam fido akayasoma mawazo yale akamjibu!

"akakumeza na kukusafirisha mpaka huku kuzimu akakutema nje ya lango la ujinini ukapokelewa na toxic walojua tayar u maiti ulokufa duniani wakawa tayar kukuwaisha katika moto ndipo father mkuu alipokuokoa"

vergan akawa kashaelewa kila kitu! ila fido akazidi kumwelewesha! "ujinini kule majini wanajua ukimezwa na nyoka yule ni lazima uwe umekufa! hivyo hata husnat wako anajua obishi kausika na mauaji yako na obishi aonekani kwa nguv za kawaida! lengo la husnat kuolewa ni aongezewe nguvu kama malkia wa zuluwalad nguv zitakazo mwezesha kukutana na obishi ana kwa ana na kumwangamiza papo hapo"

"ooohpsss!!!"

vergan akaachia mwayo mkubwa! alichoka!

"naitaji kuongea na husna kumtaarifu kuwa bado nipo hai!"

"wazo zuri JOHN but utamchanganya hali ya ujinini bado si shwari yupo katika uangalizi wa babu yake muu ajuaye kila awazacho take time".....

******

MAUMIVU ya kusalitiwa tena mshtuko wa kushtukiziwa unauma inakuwa ni sawa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali katikati ya moyo! moyo wa VERGAN uliraruliwa na fido! akutaka kusikia la muwadhin wala la mnadi swala! yeye alichoitaji ni kuwasiliana na HUSNAT tu! alishindwa kabisa kuyazuia maji mepesi yalotoka katika kingo za macho yake na kulowanisha mashavu yake.vergan alilia.alililia penzi la jini! akaukumbuka utamu aloupata! wakati wakiwa pamoja,utani walofanyiana! kilio kile kikabadilika na kuzaa kwikwi! ghafla akanyanyuka fido akajaribu kumzuia lakini alishachelewa akauendea mlango ulokuwa mbele ya macho yake mlango ukafunguka JOHN akapita mlango ukajifunga.ndani akapokelewa na chumba kipana chenye kila aina ya uzuri ndan yake! akaenda kujibwaga katika kitanda.akaiangalia ile pete kwa hasira akaivua! pete ikagoma "HUSNA, HUSNA!,HUSNAT nakuita ewe kiumbe msaliti amka kwa nin umenfanyia hivyo nimekukosea nini? umeolewa etieee! na jini mwenzako si ndiyo? nakuitaji mbele ya macho yangu husna njoooo njoooo njoooo nakusubir HUSNA"

GHAFLA mtetemeko ukaanza,ulianza taratibu ukamtupa huku na kule ukampigiza katika ukuta

"HUSNAAAAAAAA"

Akapiga ukelele,akijaribu kuzuia kupandishwa juu akujua anapopelekwa! mikono akainyanyua juu,sauti ya vicheko vikimkejeli katika masikio yake.akujua tayari MUU alishafanya yake.yeye ndo alikuwa kikwazo.aliitaji amuondoe haraka kuzimu kuiokoa ndoa ya mjukuu wake HUSNAT na sasa alikuwa angani akisafiri kwa spidi kali kuelekea katika sayari ya marz.

HIMAYA YA JINI ZULUWALAD
Ulikuwa ndo usiku wa kwanza, kwa wachumba hawa kuwa pamoja,husnat alikuwa mwingi wa furaha alimwangalia mume wake kwa jicho lililolegea ashki za kufanya tendo la ndoa likampanda ZULU akamvamia husna,naye bibie akampa ushirikiano wakawa wamekumbatiana kabla awajandondoshana katika kitanda kipana."HUSNA kwa nini umensaliti!? kosa gani hasa nlokufanyia vipi ahadi tuloahidiana HUSNA HUSNA HUSNAAAAA"

Ghafla sauti ya vergan ikayavamia masikio yake.

*********

Sauti ile ya malalamiko iliingia mpaka katikat ya moyo wake!,kwa kasi ya ajabu akajirusha kutoka kitandani mpaka katikati ya pembe,alishaiona hatari ilokuwa mbele ya mpz wake! jini zulu akiwa na mshangao akajiandaa kumfata HUSNAT,kumzuia,jini yule akamwona mumewe kama kikwazo kwake! akamwangalia kwa macho ya hasira na kumnyooshea mkono wake! shoti kali za umeme zikamtoka na kumvamia ZULU akadondoka na kutulia tuli

"HUSNAT umeua?"

aliisikia sauti ya babu yake muu! akaipuuza! muu kosa alilofanya nikuelekezea nguvu zake zote kwa VERGAN bila kukumbuka hatari ilokuwepo pale HUSNAT atakaposikia sauti ya kipenz chake na hata pale alipokumbuka alikuwa tayari kashachelewa.zuu aligeuka maiti! KIZAAZAA,....

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni