JINI HUSNAT (6) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumapili, 19 Februari 2023

JINI HUSNAT (6)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
Kwa upande wa VERGAN kama maranda yateketeavyo katika moto moyo wake uliteketea kwa binti MOUREEN,ni binti alompenda ata kabla ajakutana na HUSNA akajipa tumaini.penzi lake lilikuwa tamu zaidi ya ata la HUSNA...ghafla moyo wake ukanyongonyea baada ya kukumbuka machungu ya usaliti alosalitiwa na jini yule./.sidhani kama atakuja tena kwangu/...

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...


Zuberi Musa Maruma's photo.

*********

UPANDE WA PILI WA SHILINGI
NJE YA TUFE LA DUNIA
Kilikuwa ni kiumbe kilichokaa juu ya mnyama mfano wa farasi,farasi yule alokuwa na mabawa pia mwenye speed zaidi ya upepo,kiumbe yule alokb juu ya mnyama mkononi alishika upanga ulowaka waka nywele zake ndefu zilipepea kukinziana na upepo wa eneo lile.awakuwa kwenye kasi ya kawaida! huyo kiumbe alikuwa ni JINI HUSNAT katika moja ya safari zake zakuelekea katika sayari ya marz walokuwepo viumbe wenye asili kama yao lakini wenye nguvu zaidi yao.lengo la kwenda kule ni kuitaji idhini ya kumpa nguvu za kijini mpz wake VERGAN ili akienda nae ujinini asipate tabu.moyo ulimuuma kuondoka bila kumuaga mpz wak yule lakini akuwa na budi ilikuwa ni safari ngumu ambayo ilimlazimu kupoteza mawasiliano na duniani na ujinini.nafas hiyo ndiyo MOURINE aloitumia kumuadaa kijana yule na kumuweka katika himaya yake.

usiku na mchana ndani ya wiki moja akiwa katika faras wake alikata mbuga mara chache akiingia katika ardhi ilotokota moto yenye shaba na joto kali ilimlazimu wapae hewani.jini husnat alikuwa ni kiumbe mwenye hasira za karibu kwa viumbe walojitokeza mbele ya macho yake kwa lengo la kuizuia safar yake aliviteketeza kwa upanga wake damu yao akiifanya ndo chakula katika safari ile alotegemea kuchukua wiki moja.atimaye ndani ya siku tatu na nusu aliifikia sayar ile na kupokelewa kwa shangwe na viumbe wale.akafikishwa mpaka kwa babu zake.

baada ya salamu za hapa na pale story na vionjo vya vyakula akaeleza shida yake.babu yake alimsikitikia sana

"mziwanda wangu nshakukataza mara ngapi kuwa na binadamu?"

"siwezi muu nampenda sana yule nsaidie babu nkamwongezee nguvu nataka nkamtambulishe nyumbani!"

"achana na binadamu olewa na jini mwenzako!"

"hapana babu muu cwezi nampenda mbona wewe ulimuoa binadamu?"

ghafla babu muu akanyongonyea ni kweli yeye kabla awaja amia huku aliwah kumuoa binadamu enzi za ujana wake miaka elfu na kitu ambaye alishakufa siku nyingi sana.ndo akamuoa jini mwenzake ambaye ndo bibi yake HUSN

*******

Babu muu alikumbuka mbali sana! ila kwa mjukuu wake huyu alimsikitikia! sana.akainua kiganja cha mkono wake

"hivi unajua kinachoendelea duniani saivi kwa mpz wako?"

jini HUSNAT akatingisha kichwa kukataa kutokujua kilichoendelea duniani akiwa na shauku la kujua kulikoni macho akiyakaza katika kiganja cha babu yule.ghafla kiganja kile kikaanza kumuonesha VERGAN akiwa na MOUREEN katika matokeo mbalimbali kama wapenzi,moyo wa HUSNA ulimpasuka.na bila kuaga aliondoka kwa speed kali aki hema kwa hasira baadh ya majini walijaribu kumzuia bila mafanikio hasira zilimzidi akuitaji tena kuongezewa nguvu alichoitaji ni kufika duniani na kumwangamiza tu Mourine.

DUNIANI
Kama mapenzi ni ukichaa wao sasa walikuwa ni machizi katika ofis ya secretary VERGAN aliketi akimchombeza mpenz wake yule.ghafla upepo mkali ulivuma na vitu vikaanza kurushwa rushwa madirisha yakajifunga na milango pia...tayari MOUREEN alishajua huo ni ujio wa HUSNAT ivyo akawa tayari kwa kukimbia alipoufikia mlango ukajifunga na kutupwa mpaka katika meza ile....akanyanyuliwa kidogo na kimbunga kilichoingia mule ndani kimaajabu na kubwagwa chini jini ZAIDATU akukubali kwa spidi kali akajinyanyua mkononi akiwa na upanga.VERGAN akashtushwa kwa ilo lakini akukuwa na muda wa kutafakari yalokuwa yakitokea jini HUSNAT Alikuwa katikati ya kimbunga kile akiunguruma kwa hasira.waka angaliana ana kwa ana na zaidatu.

"naomba niambie wewe ni jini wa wapi? na kwa nini uingie kwenye himaya yangu?"

HUSNA alimuuliza jini mwenzake uku akiwa kamgandisha na upanga wake....

"sema kabla sijakutenganisha kichwa!" HUSNA alizidi kusisitiza

"mimi natoka katika himaya yetu ya MUKRAIYA"

"Nini?" HUSNA akuamini kama jini yule anatoka nyumbani kwao.

"nawe umetumwa?" akaendelea kumuuliza huku akiwa kamkaba

"nd..i..io"

"unasema? ina maana umetumwa na mshenzi ZULUWALADI?"

"NDiyooo usiniuwe shoga..."

"utansamehe shetani mkubwa wewe!"

akampulizia moto uloanza kumteketeza kisha wote 3 WAKATOWEKA.....

HUSNAT Alikuwa katikati ya kimbunga kile akiunguruma kwa hasira.waka angaliana ana kwa ana na zaidatu.

"naomba niambie wewe ni jini wa wapi? na kwa nini uingie kwenye himaya yangu?"

HUSNA alimuuliza jini mwenzake uku akiwa kamgandisha na upanga wake....

"sema kabla sijakutenganisha kichwa!" HUSNA alizidi kusisitiza

"mimi natoka katika himaya yetu ya MUKRAIYA"

"Nini?" HUSNA akuamini kama jini yule anatoka nyumbani kwao.

"nawe umetumwa?" akaendelea kumuuliza huku akiwa kamkaba

"nd..i..io"

"unasema? ina maana umetumwa na mshenzi ZULUWALADI?"

"NDiyooo usiniuwe shoga..."

"utansamehe shetani mkubwa wewe!"

akampulizia moto uloanza kumteketeza kisha wote 3 WAKATOWEKA.....

*********

CHINI YA BAHARI
HIMAYA YA JINI MUKRAIYA
Kulikuwa na mabishano makali! kati ya mtoto kipenzi! mtoto pekee wa jini mkuu MUKRAIYAH aliyeitwa ZULUWALAD na baba yake jini mukraiyah

"baba siwezi kuishi bila yeye baba lazima nimfate duniani nampenda sana JINI HUSNAT..." aliongea ZULUWALAD kwa hisia machozi yakitoka kila kingo za macho yake baba yake ambaye ndo mfalme akaufungua mdomo wake kwa sauti ndogo ya kushawishi

"mwanangu! nishakwambia ilo swala tuachie sisi mimi kama baba yako na mama yako malkia SUMAIYAH tuta akikisha HUSNAT anakuwa wako!"

"aswaaa mme wangu! na jambo zuri zaidi kijakazi tulomtuma dunia jini ZAIDATU akamwangamize yule binadamu wake tumewasiliana naye anaendelea na kazi vizuri na ameshamteka kimapenz kijana yule.sasa akasema bora awe naye kwa kuwa HUSNA atakuwa kasalitiwa lazima arudi huku awe na mwenetu."

ZULUWALAD kusikia hivyo aka achia kicheko ishara ya furaha.

"na je ikiwa mipango yote ikagoma pengine ZAIDAT aka uwawa itakuwaje?" ZULU akaoji...

"ZAIDAT ni msichana tunayemwamini na kama ikitokea akashindwa angetoa taharifa lakin mama yako kasema amewasiliana naye na mambo yapo fresh...."

wakati MFALME MUKRAIYA akiendelea kuongea ghafla kijakazi mleta taharifa akaingia huku akiwa ana hema.akafungua mdomo kusema maneno yalovunja mioyo ya wanafamilia wote

"mfalme! habar nlotumwa nkufikishie ni kwamba JINI HUSNAT na binadamu wake pamoja na mwili uso na uhai wa jini ZAIDATU wamerudi himayani"

"nini?" watatu wale wakauliza kwa pamoja wakitegemea jibu lingebadilishwa tofauti na mategemeo yao walipewa majibu yaleyale.

"naitaji walinzi wawili muende popote mtakapo waona waletwe mbele ya macho yangu haraka!"

"sawa mfalme." kijana yule akatoweka.na kuwa acha wahusika wakiwa katika dhamira ya majonzi makuu.

-.....-......-......-

katika nyumba hii kulitawala majonzi! aikuwa ni nyumba ya kifahari ila ni nyumba ya kawaida mama mwenye nyumba ile kwa mara ya pili sasa akiongeza sauti yake kidogo akauliza swali lile lile

**********

mama HUSNAT akiwa na uso wa majonzi alimwangalia mme wake na kurudia swali lake lile kwa mara ya pili "mme wangu siku zinazidi kukatika bila mwanetu HUSNA kurudi nyumbani toka akimbilie duniani! unafanya jitihada gan tumpate mwanet....."

"shataaaaaap!" akakatishwa na sauti kali iloambatana na radi! eneo lote likazizima.mama HUSNA akazid kunyongonyea akimwacha mwanaume yule kuendelea kufoka.kibabe

"nimesha sema HUSNAT si mwanangu kakataa kuolewa na jini mwenzake? tena mtoto wa mfalme MUKRAIYA linaenda kupendana na lijibinadamu sijui! sasa kwanzia sasa simtambui na sitaki kusikia habari za HUSNA katika kizazi changu! ndo nimesem....."

kabla ajamalizia JINI HUSNAT,VERGAN,na jini ZAIDATU akiwa mweusi tii kutokana na kombora alilopigwa wakatokea maeneo yale.VERGAN alikuwa ana fahamu,JINI HUSNAT hasira zilikuwa zimempanda,akiwa kaushikilia upanga wake ulowakawaka mkononi akikoroma kama simba,urembo wote ulitoweka alikuwa akitisha,meno yalochongoka,kucha ndefu zenye ncha mwili wake ulijengeka kimazoezi.hakuwa yule binti mrembo mwenye uzuri wa kiindi alowatoa udenda wanaume wamwangaliaye! huyu alikuwa ni HUSNAT mwingine.akainama ishara ya kutoa heshima wakati huo huo akimtupia jicho la kumtaadharisha baba yake juu ya alichokuwa akifikiria.mzee yule akanywea alimjua vizur mwanae akiwa katka hali ile

"baba,mama huyu anithi,fedhuli jini ZULUWALAD anantafuta nini lakini? anatuma vibaraka zake kunchezea nao wanaingia hadi kwenye moyo wangu....."

hasira za uchungu zikamzidi akaanza kulia akiendelea kumwadhibu maiti ya MOURINE kwa kuicharanga charanga na kucha zake kama vile mwili ule una uhai.

"nipo tayari nifukuzwe IMAYANI lakini si kumpoteza VERGAN hata babu muu nimemwambia nampenda sana huyu kiumbe akuna wa kututenganisha nay....."

"NYAMAZZZAAAAA!!!"

Baba HUSNA akapayuka wote wakakaa kimya kwa dakika chache kupunguza hasira katika mioyo yao mikono ya HUSNA na mdomo wake ulikuwa ukitetema kwa hasira upanga wake ukiwa mkononi

tayari kwa chochote mdaa wowote.

********

"NYAMAZAAA!!!"

Wote wakakaa kimya kila mtu akihema kwa hasira! hasira kuu!,mdomo wa jini HUSNAT ulimtetema kwa hasira zilizokidhiri! upanga unaowaka waka ukiwa mkononi! kabla baba akaendelea kuongea vibaraka watatu walotumwa na mfalme MUKRAIYA wakatokea......

kwa uwepesi wa ajabu JINI HUSNAT akaurusha upanga wake kule kwa adui alokuwa anamfata VERGAN na wakati huo huo naye akiruka kwa yule mtu wa pili alokuwa akimwendea akampokea kwa ugoko wa sehemu za siri kibaraka yule akatoa kilio cha maumivu kilichopokewa na yule kibaraka mwingine alotembelewa na upanga ulokifyeka kichwa chake.kichwa kile kikadondoka chini na upanga ukarudi mkononi mwa JINI HUSNAT kwa maajabu kichwa kile kilichokuwa pale chini mara kikapata uhai na kupaa kumfata yule alokatwa alokuwa chini akigugumia kwa maumivu.

Kichwa kile kikarudi katika muunganiko wake pale shingoni.na ghafla kijana yule akawa kama awali.haya yote yalitendeka kwa wepesi wa ajabu ndani ya sekunde za kibinadamu.yule kibaraka aliyepigwa sehemu za siri huku akiwa na tabasamu la dharau usoni akamnyooshea HUSNA mkono short za umeme zilizoambatana na makombora vikaanza kutoka! na kumwendea HUSNAT aliyekuwa na kazi ya kuzikinga kwa mikono yake.baada ya jambo ilo kushindikanika vibaraka wote watatu wakaunganisha kwa maajabu nguvu pamoja na kuanza kutupa makombora ambayo JINI HUSNAT alishindwa kuyazuia yakamlevya na kumdondosha.akapoteza fahamu hakika yalikuwa ni majonzi katika familia ya jini husnat aliye na uchungu na mwana ni mama ni kweli.mama HUSNA alilia lakini aikusaidia miili ile mitatu ikatoweka ikielelea nyumbani kwa mfalme MUKRAIYAH

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni