JINI HUSNAT (7) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatatu, 20 Februari 2023

JINI HUSNAT (7)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
Baada ya jambo ilo kushindikanika vibaraka wote watatu wakaunganisha kwa maajabu nguvu pamoja na kuanza kutupa makombora ambayo JINI HUSNAT alishindwa kuyazuia yakamlevya na kumdondosha.akapoteza fahamu hakika yalikuwa ni majonzi katika familia ya jini husnat aliye na uchungu na mwana ni mama ni kweli.mama HUSNA alilia lakini aikusaidia miili ile mitatu ikatoweka ikielelea nyumbani kwa mfalme MUKRAIYAH

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
RAHA ya MAPENZI ni pale upendo unapopatikana pande mbili

ZULUWALAD mtoto wa jini mkuu alitokea kumpenda sana JINI HUSNAT ila moyo wake hukuwa na nafasi kwa binti yule alotoka kwenye familia ya umasikini wa kutupwa.ZULUWALAD alikuwa ni kijana mzuri ambaye alijaliwa umbo mukhtari kwa kila kiumbe kimwangaliacho wajihi wa umbo lake lilimpelelea

wanawake mbalimbali(majini) kumpend

*******

Raha ya mapenzi ni pale upendo unapokuwa pande mbili,ZULUWALAD mtoto wa jini mkuu MUKRAIYAH alitokea kumpenda sana JINI HUSNAT ila mrembo yule katu akuwa na upendo kwa prinsi yule.

JINI HUSNAT alitoka katika familia yenye umasikini wa kutupwa.

zuluwalad alikuwa ni kijana mzuri! ambaye alijaliwa umbo muhtari! kwa kila kiumbe kimwangaliacho wajihi wa umbo lake matata! lilipelekea wanawake mbalimbali kumpenda ila moyo wake ulitweka na HUSNA tu! jini yule wa kiume akuruhusiwa kutoka nje ya himaya ya baba yake kuofia kudhuriwa na maadui,na hata kama pale ikitokea akitembea baadh ya maeneo ndani ya himaya ile alikuwa katika ulinzi mkali!.kitendo icho kilimkosesha amani! ila alikula nadhiri ya kumpata JINI HUSNAT kwa namna yeyote ile ndipo alipomwita jini ZAIDATU msichana wao wa kazi aliyeaminiwa kazi ya kwenda duniani na kuchunguza nyendo za jini husnat! zaidatu akawasili duniani na kuutumia mwili wa MOURINE na kuangukia kwenye penzi la binadamu yule kabla ajafumwa na jini husnat na kuambulia kuangamizwa kikatili! na msichana yule mpole mwenye hasira za karibu(JINI HUSNAT)

Ni wakati kikao kile cha watatu wale ambao ni MFALME MUKRAIYA,MALKIA SUMAIYAH,na MTOTO WAO ZULUWALAD kikiendelea ghafla vibaraka wale watatu ambao ni DENASI.OBISHI na ZINDUNA wakatokea! hapo hapo jini husnat,vergan na mourine au jini zaidatu nao wakatokea! vergan na jin husna wakiwa wamefungwa kamba madhubuti mikononi na miguuni! Zuluwalad kwa mshtuko!! na mshangao!!! machozi yakimtoka akamrukia husna na kumwagia mvua ya mabusu zulu kwa husna alikuwa ni kichaa.hama kweli mapenz ni uchizi kwa zuluwalad ili lilidhibitika wazaz wake walimwangalia kwa huruma

"Husnat amka mpz wangu...amka husna,HUSNAAAAAA!"

ZULUWALAD akaita kwa ukelele mkali ardhi yote ikatetema,nuru ikatoweka....

"nani kamuua mpz wangu?!"

zuluwalad akauliza mda huo huo akanyoosha mkono wake upanga ukatua akaushikilia vizuri na kujongea kwa vibaraka wale watatu walokuwa wakitetemeka.kwa khofu mioyo yao ikiwapeleka mpwe

******

Mioyo yao ikaanza kwenda mpwetapweta! "nauliza tena nani kamuua mpz wangu? nliwatuma mkamuue?!"

bado ZULU aliuliza hasira zikiwa zimekijaza kifua chake macho akayanatisha kwa ZINDUNA.ambaye huku akitetemeka akajitutumua na kuufungua mdomo wake "yaah mtukufu wa himaya hii tusamehe sisi vijakaz wako husna ajafa! ajafa prinsi kazimia tu!"

"la! kama ni kweli msemacho mfungueni haraka mumpeleka chumba cha matibabu! akifa mpz wangu mtaisoma namba! akuna hata mmoja ntakayemwacha mzima"

vijakazi wale wakainama ishara ya heshima na haraka wakambeba husna na kutoweka naye.wakati wote mfalme MUKRAIYAH na malkia sumaiyah awakuwa na cha kusema walimpenda sana mtoto wao.baada ya zuluwalad naye kutoweka khusni labda alielekea hospitalini au laa! katika eneo lile wakabaki mme na mke yani mfalme na malkia wake wakiangaliana.yamkini mfalme alikuwa mbali kimawazo akashtuka na kuhema kwa nguvu! malkia wake sumaiya akimwangalia ishara ya kumuuliza kiendeleacho?! macho yake yakatua katika miili ilobaki pale ndipo akaukumbuka wadhifa wake! kama kichwa cha familia! mke wake alisubiria aambiwe na mme wake kipi kifanyike kwa sauti ya upole jini MUKRAIYAH akamwambia mke wake....

"mke wangu ita vijimweni au vijakazi kama si watumwa!"

"rabeyka mme wangu!" sumaiyah akaitika mukraiyah akaendelea

"wambebe JINI ZAIDATU arudishwe kwao akazikwe ki heshima mi ntaongea sababu ya kifo chake!" akaweka kituoa tena ili maneno yake yapatwe kusikilizwa kwa makini na akusudiwaye

"swadakta mme wangu!" sumaiyah akaitika! mumewe akaendelea

"huyu binadamu afungiwe gereza la mashetani bundi vichwa vikubwa wamtese wasimuuwe mpaka mwanetu atoe idhini auwawe au arudishwe duniani yeye ndo chanzo ya hivi vyote!"

"sawa mme wangu!"

"fanya kama nilivyokwambia wacha mi nikapumzike sijisikii vizuri"

baada ya mfalme MUKRAIYAH kutoa kazi akatoweka! SUMAIYAH akapiga kofi moja wadada wazuri wakatokea

"ubebeni huo mwili upelekeni unapostaili ipeni familia pole waambie mfalme atazungumza juu ya kifo chake!..."

******

JINI SUMAIYAH akapiga tena kofi wakatokea viumbe wa kutisha sana,viumbe hao walokuwa na pembe vichwani mwao na miba miba katika miili yao,maskio makubwa na chongo! katika macho yao,kila mmoja alikuwa na jicho moja katikati ya paji la uso,jicho lililokuwa na mwanga mkali! miguu yao ilikuwa na kwato kama za mbuzi meno yao yalikuwa marefu yalochongoka na kucha ndefu zenye ncha kali! mikono ya kila mmoja ilibeba rungu lililozungukwa na miiba akika walitisha jina lao hao viumbe waliitwa guantanamo jina hili ndilo lililotumika katika gereza kubwa la mateso nchini marekani asili yake lilitokana na mateso ya watu hawa.asili ya majini wenyewe waliogopa kupelekwa guant je kwa binadamu itakuwaje?

midomoni mwao walifoka moshi! wakatoa ishara adhimu ya salamu!

"yah malkayi kuntum dainna kanna" (ewe malkia tumeitika wito) waliongea kwa lugha asrafu ya kijini!

"naimma lau binaghadamu zantaa guantanamu mulkah mlayna aswaakrau bil kanafat dau" (mchukueni binadamu mpelekeni guanatanamo mpeni mateso ya uhai)

bila kujibu kitu wakamvamia JOHN vergan uchu ukionekana katika mioyo yao wakatoweka nae.

-....-.....-....-

NJE YA WODI

JINI ZULUWALAD akuweza kukaa kukakalika,mara akae,mara asimame,mara atembee,mara achuchumae,mara aufate mlango nakutaka kuingia subra ikionekana kumpiga mkono mara arudi! ili mradi utulivu ulikosekana moyoni mwake! mara mlango ukafunguliwa daktara kwa mwendo wa haraka akachepuka.zulu akamzuia kwa kumkwida kola la koti lake la kidaktarari daktari akapigwa na butwaaa!

"naambie mpz wangu anaendeleaje?" kiubabe zaidi zulu akaoji akiusoma woga wa waziwazi kwa daktari yule

"noup prinsi mkeo anaendelea vizuri unaweza kwenda kumuona sasa"

ZULU akaachia tabasamu la matumaini,akamuachia daktar yule nadhifu aliyejiweka vizuri kula yake na kwelekea alipokuwa anaelekea

jini zulu akaingia wodini alipolazwa mpz wake katu akuweza kuyazuia machozi kumtoka:(MACHOZI YA DAMU)

MAPENZI ni mateso ni wazi zulu yalimtesa! akapiga magoti

Jini ZULUWALAD akapiga magoti! alishindwa kuyazuia machozi kumtoka,machozi yaliyokinifu udhaifu wake kwa binti yule,machozi ya damu ishara ya maumivu katika moyo wake akaifumbata mikono yake miwili katika mikono ya kipenzi cha moyo wake jini HUSNAT akatoa sauti ndogo,sauti ya upole,sauti ya unyenyekevu sauti ya kubembeleza kwenda kwa binti yule kiadhi ambao hata robo awakulingana.

"pole sana husnat wangu! malkia wa moyo wangu nisamehe mimi....!"

kabla ajaendelea akakatishwa na sauti aloisikia kwa mbali,sauti ambayo ilikuwa ni kama ala laini ya mziki wa taratibu ubembelezao katika masikio yake.sauti hii leo ilikuwa ni kaa la moto lililopigwa katikati ya moyo wake na kuacha jeraha lisilofutika ni pale husnat alipomjibu:

"naomba niache ZULUWALAD sikupendi!,niache kwa nini walazimisha mapenzi? niache kwanza VERGAN wangu yuko wapi?"

mapenzi ni maumivu pindi hisia mbili zikishindwa kushabihana zulu alijihisi kachomwa na mkuki wenye ncha kali katikati ya moyo wake.yule aliyempenda akumpenda!,na wale asiyewapenda walijipendekeza kwake mapenzi ndivyo yalivyo: akuweza kuizuia mvua ya machozi kumwagika.kwa majini lilikuwa ni kosa kwa mtoto wa mfalme kutoa chozi mbele ya mwanamke mapenzi yana nguvu aya angalii wasifu,nyadhifa wala umaridadi wa mtu taratibu kijana yule kwa unyonge akajinyanyua na kuondoka eneo lile moyo ukimuuma.....ila hasira kwa binadamu kizuizi kwa husnat kikaongezeka akaweka nadhiri ya kumwangamiza vergan ili husnat akaki kuwa wake....wake peke yake.

-....-....-....-

GUANTANAMO

Vergan akiwa kafungwa ndani ya chumba hiki fahamu zikamrejea! alishtushwa na sehemu aliyokuwepo macho yaka ambaa kutazama mandhari ya kuogofya alokutana nayo.giza katika chumba kile kikayazoea macho yake.akaitaji angalau mwanga afifu.pua zilichoka harufu ya mwozo wa asichokijua,masikio yalisikia mwitiko wa viumbe kama nyuki au nzi akuweza kugundua ni viumbe gani!

"BINADAMU KARIBU KATIKA UTAWALA MPYA"

Ghafala akashtushwa na sauti kali kama radi iloambatana na tetemek

********

sauti ile ikasababisha tetemeko la ardhi! ardhi ikamegeka na kuacha kaupenyo kalichombana VERGAN maumivu makali yakatambaa katika mwili wake! vicheko mbalimbali vikiyasumbua masikio yake! wakati akaendelea kubanwa na vicheko vya dhihaka vikimcheka katika masikio yake akahisi maumivu makali ya kichwa mtu akipiga ngoma katika kichwa chake.hakika jumla ya maumivu aliyoyapata akuwah kufikiri kama yapo katika dunia hii.mdomo ulikuwa kama umebanwa na supaglu katu akuweza kuufumbua kuwasilisha kilio chake kwa maombi! mawazo yalitekwa na kile afanyiwacho.baada ya dakika kadhaa za mateso yale.vyote vikakoma.ghafla mwanga mwekundu ukatawala! mh! salale kutawala kwa mwanga ule lilikuwa ni jambo lingine la mateso kwake kwani wadudu wale alowafananisha na nzi au nyuki wakamvamia walikuwa mfano wa nge wapeperukao walimngata kila mahali usoni,tumboni...vergan akaanza kuembea kwa kutivuta kupepesuka huku akiwa bado kajikinga usoni na wadudu wale wa ajabu! juu ya paa damu zilidondoka na kumwagikia,akujua zinatokana na nini aliendelea kujisogeza mbele ndani ya chumba kile bila mwelekeo maalumu akuona mbele kwa kuziba macho yake ghafla akapamia kitu.wadudu wale wakatoteka!

"mbona tunagongana kaka?"

akashtushwa na sauti! akapata shauku la kutaka kumjua mmiliki wa sauti ile akatoa mikono usoni MUNGU WANGU alichokutana nacho kilimfosi kuzimia lakini akuzimia kichwa chenye chongo katika kisogo,pembe mbili katika kichwa kile jicho moja lililoleta nuru ile nyekundu katika chumba kile meno marefu ulimi kama wa kinyonga haloutoa toa nje kucha ndefu katika mkono mmoja alokuwa nao mkono huo ulozungukwa na miiba na kushkilia kitu mfano wa mnyororo wa baiskeli ulowakawaka alikuwa na mguu mmoja wenye kucha ndefu! pamoja na vyote mwili wake ulikuwa umeoza ukitembelewa na mafinyofinyo! mdomoni kila ulimi ulipotoka nje alifoka moshi! wakati VERGAN akiendelea kumtadhmini kiumbe yule ambaye akujua kama ni jini,shetani,au pepo kiumbe yule akaanza kumsogelea kwa kurukaruka

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni