JINI HUSNAT (8) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatatu, 20 Februari 2023

JINI HUSNAT (8)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
Mkono huo ulozungukwa na miiba na kushkilia kitu mfano wa mnyororo wa baiskeli ulowakawaka alikuwa na mguu mmoja wenye kucha ndefu! pamoja na vyote mwili wake ulikuwa umeoza ukitembelewa na mafinyofinyo! mdomoni kila ulimi ulipotoka nje alifoka moshi! wakati VERGAN akiendelea kumtadhmini kiumbe yule ambaye akujua kama ni jini,shetani,au pepo kiumbe yule akaanza kumsogelea kwa kurukaruka

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...


"nadhani! (nadhani! nadhani!) ujanijua! etie (nijua! nijua etiee)" kiumbe kile kiliongea kwa sauti ya mwangwi huku kikiushikilia mnyororo wake vizuri

"obishi ndo jina langu! kiumbe katili ewe binadamu unajua kupendwa etie?"

vergan akujibu kitu alitetemeka! akuweza kusogea eneo lile alilokwepo.alikuwa kama kagandishwa na gundi.ghafla obishi akageuka na kuwa nyoka mkubwa aina ya chatu akimfata kwa spidi vergan alijaribu kupiga kelele sauti aikutoka,akuwezaa hata kujitingisha nyoka yule akamfikia na kujiviringisha kwake akaanza kumbana maumivu makali yakasambaa katika mwili wake ghafla akamdunga sumu kali ikaanza kutambaa katika mwili wa kijana yule mguu taratibu ukaanza kuwa mweusi! nuru usoni ikaanza kutoweka! giza kutawala na atimaye akapoteza fahamu! obishi nyoka! akamwelekeza mdomoni vergan na hatimaye akamdumbukiza katika mdomo wake mkubwa na kummeza!.

JINI HUSNAT alikonda kwa mawazo! hakupata taharifa yoyote juu ya aliyopo mpz wake! aliwekewa ulinzi maalumu

shamra shamra na maandalizi ya harusi ya mtoto wa mfalme ZULUWALAD yalipamba moto! na hatimaye kwa kasi ya ajabu HUSNAT akawa gumzo kwa kila kiumbe.mama yake akuacha kumtembelea na kumweleza juu ya mateso ayapatayo VERGAN

"sijui kama atapona mpz wangu mamaa chanzo ni mimi!"

"usiseme hivyo mwanangu utazoea tu! ishu ni tumuombee MUNGU asiteswe na OBISHI CHATU maana akimmeza ndo atutomwona tena."

neno ilo likazidi kumuumiza HUSNA machozi yakatawala katika kingo za macho yake akapanua mkono wake akanuia maneno kadhaa taswira ya guantanamo ikajijenga katika kiganja cha mkono wake.akashtuka baada ya kumuona vergan akiwa kabanwa na chatu obishi na atimaye kummeza.husnat akaangua kilio alijua uo ndo mwisho wa vergan! alilia alimlilia mpz wake! mtu au kiumbe kilichomezwa na chatu yule uwa akikurudi! ilo lilitambulika na wanajini wote.ivyo husnat alikuwa kampoteza rasmi vergan wake! aliomboleza akaweka nadhiri ya kulipiza kisasi! kwa kuanza na obishi...kiumbe kisicho onekana kilichommeza mpz wake..

******

Hakika uchungu wa mapenz umpata apendaye! uchungu huo ulimuathiri sana HUSNAT! kitendo cha kugundua kuwa kamezwa na obishi asiyeonekana kilimfadhaisha sana! alilia! lakin kilio icho akikufuta majonzi yalomuathiri! ZULUWALAD alijitaidi kuwa naye karibu nakumfariji! kiafya hali yake ilitengemaa.

"sasa ni wakati muafaka wa kufanya nnachotakiwa kufanya ntakuwa mnyonge mpaka lini!?"

aliwaza jini husnat.tayar alishapata jibu! akatabasamu na tumaini jipya likajengeka usoni mwake!

"lazima nikuangamize obishi!"

akaweka kiapo kwa mara nyingine tena.....

-....-....-....-....-

kesho yake aliamka mwingi wa furaha ata ZULU alipokuja kumtembelea.alimpokea kwa bashasha kumbatio na mabusu mfululizo mwili wa kijana yule wa kijini ukasisimka AKUAMINI

"Maandalizi ya harusi yetu yanaendeleaje mpz?"

lilikuwa ni swali lililomwacha njia panda zulu.alitetemeka kwa kutokuamini kabla ajajibu akapeleka kidole chake jichoni ilhali akihisi pengine alikuwa ndotoni.ulikuwa ni ukweli mtupu akuweza kukizuia kicheko.kicheko cha furaha.hatimaye zulu anaenda kuwa mke wake kamili lilibaki kuwa bumbuwazi lililobumbukia katika fikra zake

"nop wa moyo wangu maandaliz yanaendelea vzr!"

"waoooh nataman siku zikimbie nami niwe mke wa mtu malkia mtarajiwa wa himaya ya zuluwalad nakupenda mume wang mtaraji...."

aliongea husnat kichwa chake akiwa kakilaza katika miguu ya zulu

upande wa pili jini OBISHI alipomaliza kummeza VERGAN akarudi katika umbo lake la kijini! ni wazi alikuwa kashamuamisha vergan toka GUANTANAMO mpaka kuzimu! kambi kuu ya mashetani makao makuu ya mateso kwa viumbe viovu.

KUZIMU

Alishtuka! toka katika usingizi wa mauti akuweza kujitambua kama yu mzima au maiti! akaangaza macho yake eneo alilokuwepo asalalee akatahamaki! kumbe alikuwa amezingirwa na viumbe wa ajabu viumbe walokuwa na mafuvu tu na mapembe vimiguu njiti! mifupa! vipingili ya mifupa vilionekana midomoni mwao walikuwa na damu wakambeba juu juu huku wakipiga kelele akujua wanampeleka wapi!

viumbe wale toxic wasio na nyama! wakiwa wamembeba vergan juu juu.kijana yule alilia kilio kilichoonekana kuwa kero kwa toxic wale! nao wakawa wakipiga kelele zilizomeza kelele za kwake! kwakuwa alibebwa juu juu akujua anapopitishwa ila kule alipokuwa anapelekwa alihisi joto likiwa linaongezeka kila walipopiga hatua kusogea mbele ilifikia khali akahisi kama anachomwa kwa joto lile yan ni kama jua kali lakini akukuwa na jua! maajabu! ghafla akabagwa chini puuu! MUNGU wangu! moto mkali ndio ulokuwa mbele yake.moto wa njano...viumbe wale waliruka ruka kufurahia wakionacho ndani ya moto ule kulikuwa na mijitu yenye mguu mmoja jicho moja mkono mmoja ikiwa imevaa minguo mirefu myekundu.mkononi imeshika mijeledi ya moto ikiwa bize na kuwachapa viumbe.yah! viumbe kama yeye watu! walokuwa wakilia...naye alikuwa anaelekea huko.naye vergan alikuwa anaelekea motoni!...ina mahana...no i cant beleve it..machozi yakamtoka akamkumbuka baba yake mzee chilo akamkumbuka mama yake bi mwenda.walikuwa wanamtegemea sana! mawazo hayo yakakatishwa baada ya kubebwa juu juu na toxic tayari kutupiwa katika moto wa jahanamu.huku viumbe watesao wakimsubiria kwa hamu......

-....-.....-......-

Shamra shamra vifijo nderemo zilitawala! bwana alikuwa amepata bibi! bibi alikuwa amepata bwana! wanawake wazuri! ninaposema wazuri nama anisha wazuri walikwepo kuudhuria ndoa hii.wao waliyoihita takatifu.jini husnat alikuwa kapendeza! mrembo alorembeka,...ilikuwa ni ndoa ya historia ujinini wageni walikuwa wengi wakishughudia tukio ilo adhimu! ghafla tabasamu la jini husnat likatoweka! bila shaka alikumbuka kitu! bila tafkhiri alimkumbuka kivutio cha moyo wake JOHN VERGAN!

"ina mahana! kwele leo...! no hapana siwezi..." aliwaza akipingana na akili yake

"siwezi! siwezi! siwezi kumsaliti VERGAN wangu! liwalo na liwe." mawazo yalibadilika aliamua na akiamua ameamua! utofauti wake haraka sana uligunduliwa na mumewe mtarajia zuluwalad

"una nini mke wangu mbona umekosa raha?"

Akutaka kumjibu kitu mwanaume yule kila alipozidi kumwangalia hasira zilizidi mara mbili!

"kama ngwai acha iwe ngwai mi naondoka!" akajiwazia na muda huo huo akanyanyua mguu wake kabla ajapiga hatua akasikia sauti ikimnongoneza tena kwa ukali! nsauti aliyeieshimu!

"unataka kufanya nin HUSNAT? hakuna kiumbe kilichowah kuleta aibu katika koo yetu iweje wewe binti izayya usiye na adabu wala heshima mpumbavu wewe!"

sauti ile ilimnyongonyesha! akapigwa na butwaa.ilikuwa ni sauti ya babu yake MUU,mzee aliyoko katika sayari ya marz.ikabidi afute ujeuri wake! kwani bado aliitaji msaada mkubwa sana kwa MUU hususani cha kuongezewa nguvu kitendo cha kutomtii ni wazi angejivika majivu ya moto katika uso wake.kuiparamia vita asiyo na uwezo nayo.akanongona

"nsamehe babu mapenz! yanauchakaza moyo wangu!"

"najua uwazacho mjukuu wangu izzadan fil kudain fanya kila kitu kwa mpango."

"sawa babu nakupenda babu yangu"

"thawa babu nakupenda bab yangu ndo utake kutuaibisha?"

"hapana muu wangu si yameisha?"

"kama yameisha basi mgeukie mume wako kwa tabasamu muktahiya mkumbatie kimahaba binadamu wanasema mpeti peti...."

"mh babu!"

"fanya hivyo..."

wakati jini husnat akiwa anawasiliana ki digitali na babu yake muu akuna alojua kinachoendelea wengi walimwona akiwa kimya ilhali pengine walichukulia anasikiliza mawaidha au wosia wa afungishaye ndoa kipindi babu yake akimwambia amkumbatie mwanaume wake naye mfungisha ndoa ndiyo alosema maneno yale yakapokelew vema na masikio ya jini yule akamvamia mume wake na kumkumbatia kwa mahabat mazito fikra kichwani kwake akizijenga kuwa kamkumbatia mume wake VERGAN.ndoa ikapita husnat akawa mke halali wa ZULUWALAD kilichofatia ni kula kunywa na kusaza.mke na mume wakaruhusiwa wakapumzike.....

TOXIC wakamnyanyua juujuu VERGAN wakaanza kuesabu ile ndo wanataka kumtupa wakapokelewa na sauti ya walomwita mungu wao.pengine ni mungu wa nafsi zao na mungu wa nafsi zote chafu! aliyeuaribu ulimwengu kwa kumuadaa eva/hawa kulila tunda

***

Sauti tukufu masikioni mwao,sauti ya shetani mkuu aliyelaaniwa akalaanika LUSIFAR.

"TOXIC mnataka mfanyeje? mwacheni huyo binadamu ajafa duniani."

toxic wote wakaduwaa! wakaangaliana kwa mshangao.

"kama ajafa amefikaje humu?" toxic mmoja akaoji!

"ni stori ndefu ila haya ni makosa ya obishi! akaletwe obishi ateswe kafanya kosa kubwa sana huyo binadamu mleteni kwangu kwani anakipawa naitaji tufanye naye agano sawa?" losifar alizidi kuagiza!

"sawa mungu wa miungu!" viumbe vile vilizidi kumkufuru MUNGU muumba kwa kumlinganisha.ni kosa kubwa sana walofanya ambalo binafsi wao awakulijua

dakika chache walikuwa katika jumba la kifalme jumba lililotengenezwa na madini pekee.akika vergan akuwahi kuona nyumba nzur kama hiyo.naam akafikishwa mbele ya shetani mkuu lusifar.ndugu wasomaji kuna vitu viwili tofauti ambavyo watu wengi awajavijua kuna shetani na wafuasi wake ikiwepo mapepo vinavyoishi KUZIMU na duniani pia uishi katika vyoo,katika miti,misituni n.k mashetani,na mapepo vyote ni viumbe viovu na lengo lao ni kuiadaa dunia na kuakikisha wanapata wafuasi wa kutosha watakaoingia nao katika moto wa jehannamu.moto mkali uloandaliwa na MUNGU muumba ardhi na mbingu,moto huo ni tofauti na moto ule tulouona wa kuzimu uloandaliwa na lusifar akimuiga MUNGU kwa kuwaadhibu watu wanaoenda kinyume na yeye.na MAJINI ni viumbe wengine waishao chini ya bahari! viumbe hawa ni tofauti na mashetani kabisa wao kuna wema wanaomtwii MUNGU na wako waovu wema wataiona pepo na waovu watauona moto.majini wanapenda na wanamapungufu yao.walichotuzidi sisi ni uwezo wao walojaliwa na MUNGU ingawa kuna binadamu wenye uwezo zaidi yao wachache wakiwemo waganga,masheghe,masharif,mapadri,wachungaji n.k

"Tumegundua una kipaji! cha biashara na ushawishi kwa watu ivyo una bahati kubwa sana kufika huku na kuokoka sisi tutakurudisha duniani ukiwa tajiri mkubwa ila kubali kujiunga na dini yetu ya WAJENZI HURU (FREE MASON) ukitakadili mi ndo MUNGU je upo tayari?"

lusifar akamwacha vegan ajibu..

******

JOHN VERGAN bado alikuwa katika bumbuwazi la wazi wazi wajenzi huru yeye alisadiki kuwasikia tu! tena katika midomo ya watu! akupata kuisi siku moja angeitajika naye awe mfuasi huru.ALITAITIKA! akataitika! baada ya lusifa kumuona yupo kimya akaendelea....

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni