MY EVA (20)
Zephiline F Ezekiel
2 min read
JINA: MY EVA
SEHEMU YA ISHIRINI
ILIPOISHIA...
Danny aliamua kwenda moja kwa moja baada ya kuona sim haipokelewi...Mda huohuo victor nae alikua akianza safar pamoja na watu wake...
Kazmoto nae alikua anaanza safar na watu wake...
SASA ENDELEA..
We danny mbona unahema kama unafukuzwa?...aliulza eva baada ya kumfungulia mlango Danny...Eva unatakiwa utoke hapa sasahiv...alisema danny huku anahema...
Kwan una nini danny ...
We twende utajua mbele ya safar....alisema danny huku alimvuta eva mkono waondoke...
Mara ghafla taa ilizimwa kukawa giza...
Nani wewe???.... Alijihami eva kwa uoga.
Danny alimvuta eva kweny kona....victor akajua eva anakwepa...akapiga risas lakin ilimkosa eva..
Ile wanajarib kukimbia ilipigwa risas nyingne...
Mara ghafla danny alishindwa kutembea.....risas ilikua imempata yy badala ya eva.
Danny!!!!!!!!.... Danny.... Daniiiiiiiiiiii!!!...alilia eva kwa saut kubwa..
Victor alishtuka kusikia vile....
Danny???!!!... Danny mwanangu au...alijiuliza victor kama haamin vile.
Victor aliamua kuwasha toch lake kubwa...
Aliishiwa nguv kuona ni mwanae danny... Alibak ameduwaa yeye na majambaz wake..
Victor alilia kama mtoto mdogo...
Danny mwanangu.... Danny tafazal....alilia victor..
Baba...aliita Danny kwa shida....
Mwanangu...mbona umekuja huku...ona sasa yaliyokukuta danny jaman....ntamwambia nn mama yako.???.....danny mwanagu jaman...
Baba mbona unamfanyia hiv eva???.... Aliulza danny
Victor alikosa la kusema akabaki analia tu.
Jambaz wake mmoja kwa hasira alitaka kummaliza eva...ile anainua tu bastola yake....mkononwake ulidakwa na kazmoto... Na akampora bastola na kumuwekea jambaz kichwan..tulia hivyohivyo...alisema kazmoto..
Aliangaza kumtafta eva..
Alishangaa kuona eva analia huku Danny ameanguaka akivuja dam nyingi sana....
Victor imekuaje??....nini hiki tena..
Victor hakua na la kujibu zaid ya kulia..
Ona sasa victor ulichofanya...sasa si umpeleke hospitali?..
Ntampelekaje hospital?....na police ntasema nn??..
Sasa utafanya nn?
Nitamuita daktari wangu...
Sasa ataweza peke yake?...mwite huyo daktar wako halaf aje huku kambin asaidizane na daktar wangu...alisema kazmoto baada ya kuona hali ya danny ni mbaya.
Nashukuru kazmoto na unisamehe sana...
Usijal..fanya haraka mtoto apone...alisisitiza kazmoto.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Eva alikua akilia tu mda wote akiwa pemben ya danny... Alijua yy ndo kamsababishia yote haya..
Alimpigia sm miriam na kumweleza...miriam nae alihuzunika sana
Mda wote huo maria alikua hajui kinachoendelea...hakua kambin maana alikua ameshapona...alipelekwa sehem nyingne nzur..
Kazmoto hakutaka kumshtua kwa habar zile...alimuacha atulie
Huku mama danny alikua akijiuliza kwann victor hapokei sim...Danny ndo hapatikani kabisaa..
Wako wapi hawa?...alijiuliza rachel
Victor alishindwa hata kupokea sim ya mke wake...alijiuliza angemwambia nn?..badala yake alituma watu wakamlete kambini ili aje amweleze ana kwa ana na amuone danny..
Mda haukupita mara rachel aliletwa akiwa haelew kinachoendelea..
Rachel alifika kambin akakutana na victor... Baada ya salam victor alimchukua rachel na kumpeleka alikokua Danny..
Rachel kuona hali ya mwanae...alishtuka..
Victor ndo nini hiki????...amekuaje mwanangu... Mwanangu kawaje tena..
Rachel heb tulia ntakwambia kila kitu
Nitatuliaje victor!!!.... Rachel aliishiwa nguv na kuanguka chin huku akilia...
Danny wangu jaman!!!
Victor alimtoa nje akimtuliza
==============
Eva akiwa pemben ya danny.... Alikua akilia huku ameushikilia mkono wa danny aliekua hajazinduka bado..
Danny tafazal amka.....danny usiniache peke yangu....ntabaki nan danny... Alisema eva hukua akiwa ameinamisha kichwa chake akilia..
Mara ghafla mkono wa danny ulicheza....
Eva alishtuka... Danny umeamka...eva alitokwa machoz ya furaha....
Eva....aliita danny
Abeee......
Usilie eva...nimeshaamka sasa..
Danny unajisikiaje...aliuliza eva kwa shauku....
Eva umekonda mara hii...Baba yuko wapi....
Anakuja mda sio mref...
Victor alifika akiwa na mkewe...
Danny umeaka mwanangu.... Aliulza rachel
Ulikuaje jaman mwanangu....ulitaka kuniacha mama yako jaman Danny.
Walifrah kuona danny amezinduka..
===========*
Nini??????!!!!....unasemaje wewe...aliuliza rachel kwa mstuko baada ya kuambiwa yote na victor...
Kwahyo unamaanisha niamin ulichosema???..
Kila kitu nlichokuambia ni kwel...alisema victor
Na kwann hukusema mapema??
Nisamehe mke wangu
Ntakusameheje victor..... Kwann lakn ulifanya ukatili ule...had maria ulimuua!!!!...mwanang nusu afe kisa wewe!!!!
Hivi victor una roho ya mwanadam wewe au nyang'au...??
Yaan umefanya nimchukie eva kama mtoto wa zimwi...mtot wa watu hakua na kosa..
Yaan had najihisi kama jambaz fulan mbele ya eva.....kwann lakin.
Nisamehe tu rachel...alisema victor
===================
Rachel alikua peke yake analia.....anajilaum sana..mara eva akafika..
Mama..aliita eva
Eva mwanangu.....nisamehe..nisamehe eva...sikujua mwanangu..
Usilie mama...huna kosa...hukujua ukwel...
Hata kama...bado nlikua nakufanyia ubaya....nisamehe mwanangu...
Usijali mama...alisema eva..
Mara ghafla....maaskari walifika pale na kumkama victor..
USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni