MY DIARY (18)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: __
SEHEMU YA KUMI NA NANE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Halafu eti akawasha simu na kuonesha zile picha alizotupiga kweli huyu rafiki yangu alikuwa hamnazo sio picha tu alituchukua video kabisa na sauti. Akanambia ngoja ampigie paparazi mmoja hivi aje ili atengeneze habari tupate hela. Kauli hiyo ilinikosesha amani na kunikera sana akanmabia eti kuna namna ya kufanya ili sura yangu isitokee.
TUENDELEE...
Kwa hasira nilimpokonya ile simu na kuzifuta zile video. Basi mda huo tuliokuwa tumekaa hapo nilikuwa nikiendelea kuchati na yule kaka tuliyekutana naye kwenye basi mombo na akaniomba namba. Na alisisitiza kuwa nisirudi moshi bila kuonana nae.
Nilimpuuza ingawa alikuwa tayari ameshanitupia misitari. Nilipomwambia ziara yangu imeisha na kesho narudi moshi alichanganyikiwa na kuniambia yupo tayari tuonane usiku huo. Basi mimi nilimtajia sehemu tulipo na alinambia tumsubiri anakuja na tuendelee kuhudumiwa atakuja kulipa bill. Mda huo kila mtu alikuwa bize na simu yake na mimi nilikuwa nikichati na watu watano na wote walikuwa ni wanaume. Kwanza nilikuwa nikichati na marafiki zake mwalimu John yule ambaye tulitoka naye out siku mwalimu John aliponifuata Moshi.
Kuacha huyo pia nilikuwa nachati na yule shombe shombe niliyekutana nae stend nilipokwenda kumpokea mwalimu John. Na pia nilikuwa nikichati na wale wazungu tuliokutana nao kule waterfalls tukiwa na mwalimu John. Yaani tukio lile la mchana kumwona mwalimu John akiwa na kidemu kingine ilinifanya nikumbuke vitu vyote tulivyowahi kufanya nikiwa na mwalimu John. Niliwakumbuka pia marafiki zake mmoja baada ya mwingine
Mwalimu John ni mwaanaume ambaye nilimpenda sana na pamoja na madudu niliyofanya kwa kipindi hiki kifupi ambacho sikuwa naye bado nilitamani kama siku moja angekuja kunioa. Nilichati na marafiki zao ili kufikisha kilio changu kwao kwa mambo yote yaliyotokea maana mimi naamini kama mwanaume huyu hasingenikimbia basi nisingeingia kwenye mitego ya Joyce. Nawengine nilichati nao ili kutengeneza mianya ya kupata hela maana piga ua wiki hiyo nilitakiwa niripoti chuoni.
Wengine niliwadanganya kuwa baada ya tukio lile baina yangu na Mwalimu John nilipoteza pochi yangu hivyo nilikuwa sina hata nauli ya kurudi Moshi. Na niliwambia kuwa ilikuwa ni lazima kesho nifike moshi ili niende chuo. Yaani huwezi amini mda huo nilishatumiwa elfu 50 na marafiki zake mwalimu John.
Sijui kwa nini walinikubali kirahisi hivyo na wote walisisitiza kuwa nikifika Moshi niwatafute. Pia niliwatumia sms baba mwenye nyumba na mwanaye na kuwaambia kuwa nimepatwa na majanga hivyo wanitumie hela.
Baba mtu alituma elfu 50 na mwanaye alituma elfu 20. Na kwa mahesabu ya haraka haraka nilibakiza laki tu kukamilisha hela ya kujisajili na kuingia chuo.
Tatizo siku ile tulitumia hela nyingi sana kufanya shoping lakini ilikuwa haina jinsi kwa saababu mtoto wa kike lazima ung’are mjini lasivyo utakosa hata wa kukutamani na kukupa hela. Mara akaingia Yule kijana ambaye nilikuwa namsubiria kwa jina Bryan na alivyofika kwa ustaarabu alituomba radhi kwa kuchelewa.
Basi tuliendelea kula vyuku na maji ya mende. Baadaye aliniomba ampigie rafiki yake ili tuwe pea pea, nikamkubalia hivyo Joyce naye akapata kampani.
Mimi na Joyce tuliendelea kuchati hapo hapo huku tukiwasoma hao vijana tuone kama watahitaji huduma ili tupate hela maana tulikuwa hatuna hata pa kulala na tulikuwa hatupo tayari kutoa hela yetu eti tutoe hela ya kukodi chumba la hasha hakuingia akilini. Walionekana wana hela na tamaa ya wanawake wazuri hasa huyo rafiki yake aliyekuja na kutukuta. Wamesahau kuwa ukiona vyaelea ujue vimeumbwa. Joyce tayari alishamuweka kwenye himaya yake lakini mimi sikutaka kuonesha kuwa ni mrahisi kihivyo. Bryan pombe zilipoanza kumkolea hakusita kuanza kunichezea chezea kwa kunipapasa papasa sehemu zaa nyuma mgongoni na kwenye makalio. Baadaye kila mtua aliongozana na mtu wake na kuchukua vyumba hapo hapo maana kwa mbele ilikuwa ni bra lakini kwa nyuma ilikuwa ni vyumba vya kulala wageni.
Mambo yakanoga na tulivyofika chumbani niligoma kutoa penzi na nikamwambia kama anataka alipie kwanza. Kauli hizo zilimchanganya sana Bryan akahisi labda ni zile pombe nilizokunywa zilikuwa zikinizuzua. Yeye kilimshangaza lakini ndivyo tulivyopanga mimi na Joyce. “Kwa hiyo ndo unaniuzia au ndo kazi yako alihoji Bryan kwa hasira” Na mimi nilimjibu kwa dharau kuwa kizuri ni gharama na kama anataka cha bure basi asubiri mpaka tujuane vizuri. Maneno hayo ya shombo yalimfanya kaka wa watu afungue pochi yake na kumwaga hela zote zilizobaki kitandani. Mungu wangu alikuwa amebakisha shilingi elfu 20 tu.
Japo nilimuonea huruma lakini sikuwa tayari anichezee siku nzima kwa shilingi elfu 20 tu. Nilimwambia tatizo mimi simfahamu vizuri ndo maana sipo tayari kwa kufanya mapenzi ila kama hatojali aongezee 30 ili ifike hamsini ndo nimpe. Sa hiyo namfanyia hivyo tushafanya romance ya hatari na kila mtu yupo hoi akisubiri mechi ianze. Niliamua kjitoa ufahamu na kuvaa sura ya kazi kabisa ikabidi anitumie hiyo hela kwa m-pesa. Baada ya kutuma ndo nikamruhusu ajilie vyake ingawa siku hiyo sikuwa na mzuka kabisa kwani nilikuwa nimechoka sana na miongaiko ya siku nzima.
Nililala kama gogo na kumwacha yeye ajibakulie mwenyewe ingawa nilikuwa na mpagawisha kwa kutoa milio ya ajabu ajabu na kumsifia…Yeah yeah hapo hapo hapo nikue nikune baby wangu hayo ni baadhi ya maneno ambayo yalinitoka kwa sauti ya mahaba. Alimaliza tukalala na nilikuwa makini sana usiku maanaangeweza kunifanyia ukatili kwa jinsi nilivyomfanyia.Nilipanga asubuhi ikifika ile ya alfajiri nimpe kitu roho inapenda ili asinisahu na pia asiwaze tene ile hela yake bali huduma niliyompatia.
Na asubuhi ilivyofika nimlifanyia kitu ambacho kilimfanya aimbe nyimbo za kizaramo. Muyego muyego mtoto huko vizuri utaniua jamanai alilalamika kaka wa watu mara baada ya kumkalia na kuzungusha nyonga zangu.
“Muyego muyego mwanaetu upo vizuri utaniua wewe mtoto kwa mahaba” alisema Bryan mara baada ya kumfikisha kileleni. Kwa kweli nitafunga safari nije moshi hata kama huduma ni ya kulipia. Kumbe ndo unajua mpenzi hivyo aliendelea kunisifia. Sikutaka porojo nyingi nilijiandaa na kuondoka kwa sababu tulitakiwa kuondoka na gari la kwanza. Kwa kuwa room yetu ilikuwa ikifuatana na ya kina Joyce nilimgongea best yangu huyo kisha tukaondoka zetu na kuelekea ubungo terminal. Tulianza safari na tulifika Moshi mida ya jioni lakini Joyce yeye aliunganisha safari mpaka Arusha.
Kwa kuwa mimi nilikuwa nimechoka sana sikutaka kwenda Arusha niliamua kushukia Moshi ili nipumzike na kesho yake nianze michakato ya kuingia chuo.
Ingawa siku hiyo yule mtoto wa mwenyee nyumba alikuja kunipokea lakini tulivyofika nyumbani nilimwambia naomba aniache tu chumbani kwangu nipumzike kwa maana nilichoka sana. Sikuweza kufanya lolote kwani mwili wangu ulikuwa umechoka sana. Alikubali japo kwa shingo upande na nilimwahidi kesho nitatimiza ahadi yake ya kutoka nae out kwani alishavumilia sana.
Usiku huo nililala kama mfu na hii ni kutokana na uchovu wa wiki nzima niliokuwa nao. Kesho yake niliamka mapema sana na kwenda benki kulipa ada. Ingawa kulikuwa na foleni kubwa sana lakini nilipata bahati ya kuonana na mfanyakazi mmoja ambaye kwa kweli mimi sikumfahamu lakini yeye alinichangamkia sana na alinisaidia kunilipia ada kupitia mlango wa nyuma. Baadaye alinishangaza kwa kuniomba namba za simu nikajua kuwa alitumia mbinu hizo ili aweze kupata mawasiliano yangu. Niliondoka na kwenda benki ingine na kukamilisha zoezi hilo.
Nikaenda mpaka chuo lakini sikuweza kufanya usaili siku hiyo kwa sababu bank statement zilikuwa bado hazijafika.Sikutaka kubishana nao nikarudi zangu nyumbani na kuendelea na dozi yangu ya kulala. Nililala sana siku hiyo mpaka saa moja jioni ndipo nikashtuliwa na mtu ambaye alikuwa akigonga mlango wangu. Ilinibidi Kuamka na kwenda kufungua kumbe ni Ramadhani yule mtoto wa mwenye nyumba. Aliamua kunigongea kwa sababu mimi nilizima simu kuepuka usumbufu. Siku taka aingie ndani kwangu hivyo nikiwa wima wima nilimwambia samahani nilizima simu lakini ngoja nijiandae tutoke.Hakuwa na jinsi zaidi ya kutabasamu na kurudi chumbani kwake.
Niliingia bafuni nikaoga kisha nikajipara tayari kwa mtoko ingawa sikuwa na hamu kabisa ya kutoka siku hiyo lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kulipa fadhila alizonitendea kaka huyu. Basi tuliingia kwenye gari lake na tukaenda sehenu moja inayoitwa Big 5GB ambayo ipi Rau kwa wale wakazi wa Moshi watakuwa wanapajua.Tuka kaa zetu hapo na aliagiza nyama choma huku tukiendelea kunywa vinywaji. Mimi siku hiyo nilikuwa nakunywa maji tu. Kabla mboga haijafika mezani kuna mtu aliingia ghafla na kuchafua hali ya hewa. Alikuwa ni baba yake Ramadhani yule mzee mwenye nyumba na hakuwa peke yake bali alikuwa na kabinti kadogo ambacho kwa kweli kalikuwa ni kazuri cha sura
Ramadhani akachanganyikiwa kumwona baba yake yupo na binti huyo. Sikujua kwa nini alichanganyikiwa ila nilihisi labda alikuwa ni demu wake. Akaenda jikoni kuchukua ile nyama na aliifunga na akanambia tuondoke huku machozi yakiwa yana mtoka.
Tukaingia kwenye gari na nilishangaa kuona tuanarudi njia ya nyumbani akafungua geti na tukaingia ndani. Tukiwa njiani yule baba mwenye nyumba alinitumia meseji na kuniuliza mbona mmeondoka? Nikamjibu wewe unaona unavyofanya ni vizuri. Nae akajibu usimjaji mtu bila kujua kinachoendelea mbona mimi nilivyowaona sijahisi kitu kibaya. Kabla sijamjibu akatuma sms ingine “ila chondechonde nakuomba usije ukatembea na mwanangu itakuwa ni aibu sana kutuchanganya. Nilimjibu kwa kifupi noted. Yaani kwa jinsi Ramadhani alivyokuwa amechanganyikiwa niliogopa kumwacha mwenyewe aingie chumabni kwake.
Hivyo tuliingia wote ndani kwake na yeye akaingia chumabani na kuniacha mimi pale sebuleni.Alikaa mda mrefu bila kutoka kitu ambacho kiliniogopesha.
Ikabidi nimwite akatoka na moja kwa moja akafungua friji na kutoa pombe kali na hakutaka kuniuliza kuwa natumia au la bali alinimiminia kwenye glass.
Akachukua sahani akamimina ile nyama na kunikaribisha. Hakuonesha tena kuwa na mawazo na tukio lililotokea kwani aliwasha Tv akaweka nyimbo za bongo flever tukaendelea kuangalia. Tuliendelea kula ile nyama ya kuchoma huku akilalamika eti chachandu haikuwa kali. Nilishangaa kwa sababu mimi kwangu ilikuwa kali sana na ilikuwa ikiniwasha kupita maelezo.
Baada ya hapo niliendelea kumdadisi juu ya tukio lile lakini hakuwa tayari kufunguka zaidi ya kusema aliumia sana. Hapo nikaamua kuutafuta ukweli kwa kutumia mbinu za kike.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni