RANIA (1)
Zephiline F Ezekiel
4 min read
JINA: RANIA
SEHEMU YA KWANZA
Maskini wa mungu Rania,huna bahati mjukuu wangu...alisikika akisema bibi kaasha akiwa amembeba Rania ambae ndo alikua amemaliza kuzaliwa mda huo..Kaasha alikua akitokwa machozi yasiyo pimika baada ya mka mwana wake hikkan kupoteza maisha baada ya kujifungua mtoto Rania..
Sijui mwanangu atalichukiliaje hili swala...anampenda sana mke wake halafu ndo kamwacha mapema kiasi hiki..jamani mwanangu mimi eeee....alilia kaasha.
Vijakazi wake walijaribu kumbembeleza lakini haikusaidia kitu...alilia sana.
Muda mfupi baadae pame alifika akiwa na zawadi mbalimbali alizo mletea mkewe ambae alitarajia kumkuta amejifungua.
Aliingia ndani kwa shamrashamra maana alikua alishadokezwa na rafiki yake kua mkewe alishajifungua tayari..mtoto wa kike.
Cha ajabu alipoingia ndani alimkuta mama yake akilia..alipoangalia pembeni aliona mwili wa mtu aliepoteza maisha...bila kuuliza alikwenda na kuufunua.
Pame hakuamini macho yake baada ya kumwona aliefariki,..alikua mkewe kipenzi hikkan..alirudi nyumanyuma akiwa ametumbua macho na kujikut akiishiwa nguvu kabisa.
Alilia kama mtoto mdogo, lilikua pigo kubwa kwa pame kumpoteza mkewe ambae alikua akimpenda sana.
Hikkan,mbona umeniacha mke wangu?... Kwanini hujasubiri kumwona mwanao anakua?...nifanyeje mimi mke wangu? Nitaishije kwa furaha bila wewe mke wangu.... Alisema pame akilia.
Mwanangu, kazi ya mungu haina makosa, alisema mama yake pame bi kaasha...
Hikkan alizikwa na mwanae akalelewa na kaasha bibi yake..
MIAKA KUMI BAADAE.
Rania alikua na umri wa miaka kumi..akiwa njiani na bibi yake wakati wakifanya manunuzi ya vitu mbalimbali, mara Rania alipompotea bibi yake..
Kaasha alipogeuka hakumwona Rania.. Rania alikua haonekani..kaasha alichanganyikiwa sana.
Mungu wangu!!!!.. Amekwenda wapi huyu mtoti jamani?..alijiuliza kaasha.
Raniaaaaaaaaa....Raniaaaa...aliita kaasha bika mafanikio.
Wakati huo Rania alikua upande wa pili akilia baada ya kuvamiwa na kundi la vijana wadogowadogo kama yeye mwenyewe..
Haka kanajidai sana kakiwa na bibi yake...alisema mmoja wa wale watoto.
Kweli yaaan...sasa leo utajuta..kwanza tupatie hiyo pete ya dhahabu tukauze sie...alisema kijana wa pili.
Sitaki,,mimi bibi yangu aliniambia nisimpe hii pete mtu.. Siwapiiii...alisema Rania huku akilia.
Anhaaa...unajidai wewe mjanja eee..sasa ngoja uone..walisema wale vijana na kumvamia Rania na kuanza kumshambulia
Rania alipiga kelele za kuomba msaada.
Dom alikua akipita zake akienda kwao baada ya kutoka mawindoni..
Mara alisikia sauti ya mtu akiomba msaada..Dom aliahirisha safari ya kwenda kwao na kuelekea zilikokua kelele zile.
Dom alifika na kuwakuta vijana wale wadogo tu kama yeye wakijaribu kumpora Rania pete ile..
Nyie mnafanya nini hapo?..aliuliza Dom huku akiwaangalia watoto wale kwa kujiamini..
Haha...ona huyu nae...au unataka na wewe tukuunganishe hapa muwe wawili?... Aliulza mmoja wa watoto wale..
Dom hakuwa na maneno mengi, alotoka nduki na kuwavamia watoto wale.aliwatembezea kichapo kitamu sana.
Baada ya muda mfupi, wale watoto walikua walishatimua wote..
Muda wote huo Rania alikua anashangaa tu uwezo aliokua nao Dom kwenye kupigana na jinsi alivyowatembezea kichapo watu wale.
Baada ya kuwafukuza wote Dom aligeuka na kumtazama Rania ambae alikua amekodoa macho kwa uoga
Baada ya muda walikaa chini na kuanza kuonge
Hivi unaitwa nani vile??...aliuliza Dom.
Rania....
Jina lako zuri...alisema Dom.
Na wewe je unaitwa nani?...aliuliza Rania.
Dom...
Asante kwa msaada wako Dom... Alisema Rania.
Aaah...usijali.. Hiyo kazi ndogo sana...alisema dom.
Unaonekana uko vizuri sana kwenye kupigana...alisema Rania.
Aah..mimi?..mimi ni mpiganaji mzuri sana..yaan kule kwetu napiga wote,wakubwa kwa wadogo..mimi akija hata simba napigaa,chui napigaa,kila kitu napiga..nina nguvu sana mimi...hata aje nani napiga... Alijisifu Dom kweli kweli
Rania aliinama chini na kucheka maana alijua Dom ameongeza chumvi ya kutosha..et hata simba,chui anapigaaaa😂
Haa...unanicheka?...aliuliza Dom baada ya kumwona Rania anacheka.
Hihihihi...alicheka Rania akiwa ameinama.
Unanizarau ee...hujaona nilivyowapiga?.mimi baunsa yaani manguvu yangu hayapimiki...alijisifu Dom.
Sawa.. Asante kwa kunisaidia...ngoja mimi niondoke alisema Rania akainuka na kwenda zake.
Haa...yaani nimejisifu kiasi hiki halafu hata hanioni wa maana.....jinga sana huyu.. Alijisemea Dom huku amevuta mdomo na baada ya Rania kutokomea nae aliondokaa zake huku akilaani Rania kumdharau licha ya kujipamba.
Rania alikwenda moja kwa moja hadi nyumbani ambapo alimkuta bibi yake analia kwa kumpoteza Rania.
Bila hodi aliingia hadi ndani... Bibi yake alishtuka kumwona..alimka na kwenda kumkumbatia mjukuu wake aliempenda sana.
Ulikua wapi mda huo wote? ..aliulza bibi.
Nilikua nimekamatwa na wezi wanataka kunipora hii pete yangu..ila kuna mtu kanisaidia..alisema Rania.
Pole mjukuu wangu..usirudie kutembea mwenyewe.. Alisema bibi.
Dom alitembea umbali mkubwa sana na mwisho alifika nyumbani akiwa amechoka sana.
Akiwa amekaa nyumbani kwao alikua akiwaza jinsi alivyowapiga wale watoto na kujiona bingwa..
Mwanangu, leo unafuraha sana..kuna nin?...aliuliza mama yake bi samari.
Eeh..mimi?...hamna kitu mama...alijikanyagakanyaga Dom.
Mara alipita binti wa jirani yao jina lake warid wa rika kama la Dom karibu yao na kuwasalimia..alipofika mbali samari akasema:
Binti mrembo sana huyu sijawahi ona
Wee...sio kweli.. Sio mzuri kama Rania... Alilopoka Dom bila kutarajia.
Nani?...Rania?.. Wawapi huyo?... Aliuliza samari kwa kimshituko kidogo.
Aaah...hamna kitu mama.....alisema Dom.
Wewe Dom wewe..una miaka 15 tu ushajua wazuri!!!...umemwona wapi huyo Rania...?
Aah..mama nimepitiwa tu.. Hata huyo Rania sijawahi kumwona... Alijitetea Dom.
Jinga kweli wewe...et humjui..kama humjui na jina lake umetoa wapi?..aliuliza samari.
Mama na wewe....si ufanye kama hujaskia...alisema Dom baada ya kugandwa na mama.
Tse..tse...tse...huyu mtoto jaman..alisema samari huku akiinuka na kuondoka zake..
Eee....Rania ni mzuri..sio haka ka warid...hata sio kazuri...alijisemea Dom kisha akacheka...
Katika jumba la kifalme mwanamfalme wa pekee (fasha) alikua akijitahidi kuruka ukuta wa jumba la kifalme ili akatembee huko mtaani maana kwa kawaida haruhusiwi kwenda huko bila ridhaa ya mfalme.
Lakini mwanamfalme,mimi ni jukumu langu kukulinda...sasa mfalme akijua umetoroka na mimi nipo si ataniua..alisema mlinzi wa fasha..
We kazi yako ni kunilinda ila unatakiwa kufuata amri zangu si ndio?..aliuliza fasha.
Ndio mwanamfalme,lakin... Alisema mlizi kisha akakatizwa na fasha..
Kimyaaa....nani kakuruhusu kunibishia?..ruka ukuta haraka unifuate..alisema fasha.
Mlinzi (jao) hakua na jinsi ilibidi atii amri ya mwanamfalme yule jeuri..
Akiwa njiani watu walimsujudia kumpa heshima maana alikua anafahanika kwa watu..kwakua alipenda sifa na ukubwa..alikwenda sokoni iki akasujudiwe na wengi.
Alikua na tabia hizo licha ya kua na umri mdogo wa miaka 15 tu!!!
Fasha akiwa anatembea huku na huko mara alimparamia binti mmoja (Rania)..
Kwakua fasha alikua jeuri,hata hakuthubutu kuomba msamaha.. Aliondoka tu...
We mjinga wewe, umemwaga vitu vyangu halafu hata huombi msamaha!!!..alisema Rania.
Fasha aligeuka ili amwone hiyo ambae hamwogopi hadi kamwita mjinga..
Mjinga!???... Unajua mimi ni nani hapa kwenye hii nchi hadi unanitukana mjinga!???....aliulza fasha kwa majigambo.
Najua kua wewe ni fasha mwanamfalme wa nchi hii ya Tharia ...kwahyo, kama wewe ni mwanamfalme nitetemeke?..mwanamfalme ni Mungu?..aliulza Rania kwa kujiamini..
Kwa mara ya kwanza fasha alimshuhudia mtu mwenye tabia kama hizi..alishangaa sana kwanini huyu binti hajamwogopa kama wengine walivyo..
Ha..haaa.haa...wewe jeuri kumbe!!!!...alisema mwanamfalme kisha akamwamuru jao:
Jao,kamata huyu twende nae akapate adhabu yake ikulu....Alisema fasha kwa hasira.
Ndio mkuu..alisema jao na kumkamta Rania..
USIKOSE SEHEMU YA PILI
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni