MY DIARY (6)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: __
SEHEMU YA SITA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Akanambia kuwa wamemwambia wapo East Africa Pub na tayari wamaeshaagiza mkuu wa mbuzi. Mmmmhhhh kusikia mguu wa mbuzi mate yalinijaa mdomoni. Basi kwa harakaharaka nikamwambia naomba niende niende nyumbani nikachukue viwalo vya club kisha nitawakuta hapo.
TUENDELEE...
Alinambia mbona hizo nguo ulizofaa zipo poa tu wewe twende hivyo bhana si upo na mimi.Nikamwambia ujue hizi nguo ni za heshima sana na kwa club watu wataniona kama ni mshamba, Je, wewe unapenda rafiki zako wanione mimi mshamba?Hakuwa na jinsi akanipa elfu kumi na kuniambia chukau tax hapo nje uende nayo fasta na ikibidi urudi nayo na pia uchukue nguo za kubadilisha kesho maana yeye yupo mpaka jumatatu ndo ataondoka.
Nikatooka nje na kwa ubahiri wangu badala ya kuchukua tax nilipanda boda boda siunajua tena mjini mipango. Nikafika gheto na nikamkuta yule kaka mwenye nyumba amekaa kwa nje.Nikamsalimia na kumwambia na haraka kidogo kuna mahali nimealikwa kuna send off. Basi atafanyanye wakati uwongo ndo unatawala dunia. Nikaingia ndaani nikamwaga nguo zangu zote kitandani, nikaanza kujaribisha mara hii mara hii, siunajua tena mtoto wa kike ikija swala la outing. Basi katika kupekua pekua nikakita kiwalo kimoja, hicho ni kiboko nilikinunuaga siku nyingi lakini sikupata sehemu ya kukuivaa.
Ni vile vya kina Beyonce, kigauni kifupi kina meremetameta na kwa nyuma kinaacha mgongo wazi. Nikajiaangalia kwenye kiooo nikasema potelea mbali leo wacha wanikome. Nikaenda kwenye kioo kikubwa na kujigeuza kwa kweli kilikuwa kimenibana saana na kufanya wowoo langu lionekane vizuri.
Nikachukua nguo zingine nikaweka kwenye pochi kama nilivyoambiwa, nikatoka nje kwa kasi tayari kuelekea eneo la tukio.Masikini yule mtoto wa baba mwenye nyumba kuniona ilibidi agune, ndio alishindwa kuvumilia akanambia take care baby.
Nikacheka yaani nishakuwa baby..Sikupoteza mda nikapanda bodaboda na kuelekea mjini lakini nikiwa njiani nikapigiwa simu na John na kuniambia “wanasema hawapo tena East Afrika hivyo mwambie akulete mpaka makumba bay.Nikamuuliza wewe ushafika akanijibu ndio. Nikamwambia boda boda anyooshe mapaka hiyo sehemu ambayo na yenyewe ilikuwa ni maarufu sana hasa kwa huduma nzuri na bei kubwa.
Nilivyofika ikabidi nimwongeze yule bodaboda mia tani kitu ambacho kilimfanya acheke na kuniona mimi mbahiri. Akanambia fanya buku dada yangu, yaani na kupendeza kote hivyo. Nikaona aibu na kupekua pekua pochi yangu lakini sikuona hela nyingine zaidi ya hile buku kumi niliyopewa nakamwambaia sina heala ndogo kwanza hapa si ni hatua mbili tu hivyo kama vipi baadaye.
Nikapiga hatua mbili za madaha kuvuka upande wa pili wa barabara.
Nikachukua simu na kumpigia Ticha wangu.Akapokea na kuniambia ingia kwa ndani sisi tupo hapa kwene masofa. Kwa uwoga wangu nilimkatalia na
kumwambia aje kunichukua na nilizidi kuyasoma mazingira wakati nikiendelea kumsubiria.Nilijaribu kuvuta taswira kama pale nje palikuwa pazuri zile huku ndugu zetu wazungu wakiwa wamejiachia kwenye vitu virefu vilivyotengenezwa kitalili talii.
John alitoka kwa mbwembwe alinikumbatia na kuniambia “umependeza sana babee” Nikamjibu kimahaba asant sana my hubby(mume wangu). Akanipa mkono kama vile bibi harusi wanaingia ukumbini. Wanaume waliokuwa wamekaa hapo nje hawakusita kugeuka na nilibahatiaka kumsikia mmoja akisema “e bwana eeh daah cheki hicho kifaa kilichoingai” Mwenzake akamjibu kweli kipo vizuri alafu inaonekana bado mdogo sana huyu. Tuliingia zetu ndani lakini huku nyuma tuliacha gumzo.
Tukafika kwenye masofa na kabla sijakaa marafiki zake wote walisimama et kwa heshima. Walikuwa wanaume wawili na msichana mmoja hivyo kufanya idadi yetu kuwa watano. Nilimwonea huruma yule kaka mmoja ambaye hakuwa na msichana kwani mda mwingi alikuwa bize na simu. Wakanambia wenyewe wameshakula hivyo hivyo mimi niagize kitu ninachotaka. Niliagiza mchemsho wa samaki nikaendelea kufurahia maisha na kusahau shida kwa mda. Nilipoulizwa kinywaji nilisema niletewe maji kitu ambacho kiliwashangaza wengi.
Yule kaka aliyekuwa na simu akaniuliza kwani shemeji hutumii kinywaji? Nikamjibu nakunywa kwanza maji ili chakula kiende vizuri.Nilikuwa najiuliza ninywe nini maana yule msichana mwenzangu alikuwa anakunywa pombe ila ni hizi laini laini.
Wale wanaume wote walikuwa wakishea ile juisi ya miwa(konyagi).Basi nikamtumia meseji rafiki yangu Joyce na kumwambia “shoga nipo na company hapa na wote wanakunywa vinywaji na wanachonga sana ebu nambie ninywe kinywaji gani ambacho akitanisumbua?” Akacheka sana kwenye meseji na kuniambia kunywa savana dry au siminof ice ila kuwa makini usizidishe zxaid ya 3 kwa kuwa ndo unaanza. Basi niliendelea kunywa maji yangu taratibu huku nikichati na rafiki yangu huyo ambaye naweza kusema yeye alikuwa ni mjanja zaidi yangu.
Na alishaanza harakati za starehe miaka mingi iliyopita. Basi kama kawaida ya walevi wengi waliendelea kunisihi ninywe pombe kwa madai kwamba eti nitawalete inzi mezani. Mwalimu John kuona hivyo alinisaidia kuniagizia alimwambia muhudumu aniletee glass ya wine na kwa jinsi alivyokuwa mzooefu alimtajia na jina kabisa lakini wakati muhudumu akienda kaunta alimwita na kumuuliza bei ya chupa nzima ya Saint Anne. Alipoambiwa alitoea hela akaletewa.
Nilipomimina tu na kuanza kunywa tu nilikumbuka ile ladha ya siku ile nilipokuwa na madam wa michezo ambayo pia ilikuwa siku niliyofungua ukurasa wa mapenzi na mwalimu John.Hapa sasa kila mtu alichangamka na stori kunoga.Mara ikatokea kasheshe ambayo ilisababishwa na yule kaka ambaye alikuwa hana mwanamke. Kumbe pale alipokuwa amekaa kulikuwa na wavulana ambao walikuwa ni wengi kuliko wavulana Kuna ishara ambazo walikuwa wakipeana na na mmoja wa wasichana na alikuwa akimwonyesha simu ishara kama alikuwa akitaka namba. Kumbe yule pedeshee aliokuwa nao alishashtukia mchezo hivyo akamshtua dada yake. Kumbe kale kabinti kalikuwa ni cha kusoma na dada yake ndo alikuwa ni kila kitu.
Basi kuna mda yule binti alienda chooni na jamaa nae akaaamka na kwenda kuchukua namba hapo ndipo kasheshe ilipoanzia. Jamaa wakati anabadilishana namba na mtoto wa kike kwenye juction ya kuingilia maliwatoni ya kike na kiume.Dada yake naye akatokea papo hapo na akaaanza kuwatukana. Aliwachanganya wote kwa matusi.Kitu ambacho kilisababisha ugomvi mkubwa na yule kaka alishindwa kuvumilia akaanza kumopa kifinyo(kipigo) cha maana. Ukizingatia na konyani zilikuwwa kichwani kwa kweli alimpiga sana.
Mpaka mabausa wanakuja kumwamulia tayari mambo yalishaharibika. Watu wengi walishanyanyuka kwenye viti na mimi mwenyewe mamaaa wa umbea nilishafika kwenye eneo la tukio na kuona kuwa yule kaka tuliyekaa naye anapigwa na mabausa nilirudi harakahara na kumwambia mwalimu John kuwa rafiki yao alikuwa akifanya fujo.Vurugu ilikuwa kubwa sana kwani kila meza ilitaka ushindi japo John yeye aliamua kutumia busura zaisi na diplomasia.
Johna hakutaka kutumia nguvu kabisas bali kauli ambazo ziliweza kuwatuliza wale wa dada waliokuwa kwenye meza ya pembeni maana walikuwa wakitukana sana. Baadaye aliongea na mabaunsa na wakamwelewa ila walitoa sharti moja tu kuwa nalo ni kuondoka na mtu wetu ili tusiendelee kuwa kera wateja wengine au wamuweke selo na sisi tuendelee kukaa hapo. Hivyo ilitulazimu kuama bar.
Tulivyotoka nje kumbe walikuwa na usafiri na sijui lile gari lilikuwa hata ni la nani ila yule kaka aliyekuwa akishughulikiwa na mabaunsa ndo alikuwa dereva kitu ambacho kiliniogopesha sana na kupoteza imani naye.Alikuwa amelewa sana hivyo angeweza kusababisha ajali mda wowote.Nilicheki mda ndo kwanaza ilikuwa ni saa nne kasoro hivyo yule shem mwingine ambaye alikuwa na mpenzi wake alipendekeza tuende kwanza Malindi Club tuvute vute mda mpaka saa 5 usiku.
Kwangu mimi ilikuwa ni zaidi ya ushindi na shangwe kwani licha ya kuishi zaidi ya miezi 3 mjini Moshi sehemu hizo nilikuwa sijawahio kufika zaidi ya kuzisikia kwenye stori tu. Tulifika Malindi Club tukaingia ndani na tulivyokaa kila mtu aliendelea kunywa kinywaji chake. Na safari hii hawakunywa tena spirit walikunywa bia. Kazi ikabaki kwangu niagize nini wakati ile chupa yangu ya waini tulizuiliwa kuingia nayo.
Nikakumbuka vile vinywaji alivyonambia rafiki yangu Joyce, ndio ilinibidi nifungue simu yangu na kusoma zile sms.Basi muhudumu aliporudi nikamwambia mimi niletee Savana baridi. Basi kinywaji kililetwa mezani na mwanekano wa chupa yake tu ulinifurahisha. Tuliendelea kunywa huku kasi yangu ikiwa ndogo na hofu yangu kubwa ilikuwa nisije nikalewa na kufanya utumbo.
Vituko viliendelea na watu wengine ambao walikuwa pembeni yetu walikuwa wakicheza na kukumbatiana na wengine wakifanya vitu vya ajabu ajabu. Macho yangu yalikuwa yakizunguka huku na kule ili kuangali watu.Niligundua kuwa kulikuwa na watu waliokuwa wamevaa vibaya zaidi yangu. Na baadaye niligundua kuwa mule wa dada waliokuwa wakijiuliza walikuwa ni wengi sana. Matendo yao tu yalikuwa yakijieleza kwani tulipokuwa nje kuna manaeno wadada hao walituambia “wapelekeni ndani mrudi nje tukapige short time tunawasubir” Wakiwa na maana John na marafiki zake watupeleke sisi watoto wa kike ndani na wao warudi nje wakawanunue. Kweli biashara matangazo na hivi vitu nilikuwa nikisimuliwa tu lakini leo nilikuwaa naviona kwa macho na kuvisikia kwa masikio yangu.
Muda ulikuwa umeenda kwani ilishafika saa 5 na nusu. Tuliingia kwenye gari na kuelekea huko Club La Liga. Nikiwa njiani nilikuwa nikijiuliza mbona kama tulikuwa tunaenda nje ya mji. Basi tulifika na bila kupoteza mda walilipa kiingilio tukaingia na tulivyofika ndani tulipnda juu kwenye kighorofa hivyo kuwaona kwa urahisi watu walivyokuwa wakicheza kwa chini.
Mimi nilifanikiwa kupata kiti japo wenzangu wote walikosa basi baby wangu yaani mwalimu John yeye hakucheza mbali maana alijua tu kwa jinsi nilivyo angeweza kupokonywa mda wowote na wanaume wenye uchu na aleji na vitu vuizuri. Yule binti ambaye tulikuwa nae alikuwa na jamaa ake wakicheza kwaito hadi nikafurahi.Nilikuwa sijawahi kwenda Club maishani mwangu japo nilikuwa ni fundi mzuri wa kucheza miziki ya aina mbalimbali na kule shuleni mimi nilikuwa ndo kibok yao.
Kwaito zilivyonoga uzalendo ulinishinda nikajikuta na mimi nashuka ngazi kuelekea chini sehemu ya kuchezea.Nilizijua kwani shuleni tulikuwa tunazicheza sana hasa kwenye yale madisco yetu ya mwisho wa mwezi.John wangu alibaki juuu akiniangalia jinsi nilivyokuwa nikicheza vizuri.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni