RANIA (35)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
JINA: RANIA
SEHEMU YA THELATHINI NA TANO
ILIPOISHIA...
Haraka alimwita mlinzi wake mkuu na baadhi ya watu wanaowaamini.Haraka alituma mjumbe apeleke taarifa kwa Mfalme wa Tharia kuhusu uasi unaoendelea ili nao waungane.
SASA ENDELEA..
Mjumbe yule bila kuchelewa alikwenda hadi Tharia safari ambayo ilichukua kama siku mbili njiani.Alifika ikulu na kuonesha kitambulisho chake kisha akaruhusiwa kuingia ndani na kuonana na mfalme.mjumbe yule alimkabidhi mfalme ujumbe ule na kukaa kusubiri majibu.
Mfalme aliwaita watu wake wa karibu ili kujadili nao jambo la kushirikiana na mfalme wa Lazi.
Mfalme alikua ashajua tayari mipango yote ya suya na kuhusu kushirikiana ba Faritha.kwahiyo aliita watu wake ili tu kuona kama kushirikiana na Lazi inafaa au la.
Alimwita omandi, Fasha na Rai na kuwaeleza kilichojiri.
Fasha na omandi waliifika ila Rai alikua bado hajafika.
Baada ya kumsubiri kwa muda mrefu kidogo Rai aliingia.
Oooh..tumekusubiri sana...alisema mfalme baada ya Rai kufika.
Ingia..mbona unabakia nje?...alisema Rai huku akimwangalia Mtu aliekua mlangoni.
Ni nani huyo?.. Aliuliza Mfalme.
Mara aliingia mtu ambae alikua hajakaribishwa na mfalme.. Mfalme alishituka kidogo kumwona.
Mtu huyo alitoa heshima kwa Mfalme na mwanamfalme kisha rai akamwambia akae.
Kwanini umemleta huyu?.. Aliuliza Mfalme.
Huyu ndio kila kitu...huyu ndio jeshi lenyewe...alisema Suya.
Mfalme na omandi walibakia wameshangaa..Fasha alishtuka na kupata wasiwasi huku akimwangalia mama yake ila alijitahidi kukaa kimya.
Mfalme unaweza kuendelea tu na maongezi wala usihofu..alisema Rai.
Haya...kuna barua imekuja kutoka Lazi..alisema Mfalme kisha alimkabidhi Fasha aisome mbele yao.
Ni jambo sana...tufanye kama wanavyoomba..alisema omandi.
Wote waliunga mkono ila Rai alikua kimya.. Mfalme aliamua kumuuliza yeye anasemaje.
Mfalme sijui kuhusu huyu mlinzi wako kama ni vyema akisikiliza maongezi haya ninayotaka kuyaanzisha..alisema Rai.
Aaah...ni salama tu wala usiwe na wasiwasi kuhusu yeye..alisema mfalme.
Hapana..simwamini mtu katika hili maana mimi Simfahamu huyu.. Alisema Rai.
Mfalme alitabasam tu kisha akamwomba omandi aondoke... Omandi alitii na kuondoka.
Fasha....wewe nakuamini katika hili ila hata wewe naomba utupishe kidogo...Alisema Rai
Fasha alishtuka kidogo ila ilibidi aondoke.
Baada ya Fasha na omandi kuondoka mlango ulifungwa.
Kwanini Fasha umemwondoa?...aliuliza Mfalme.
Nitakueleza tu..alisema Rai
Sawa... Ni nani huyu??... Aliuliza Mfalme.
Ni NADISH.. Alisema Rai.
Mfalme alishituka nusu akimbie baada ya kujua yuko na NADISH mbele yake.
Mfalme wala usiogope.. NADISH haiko kwa ajili yako.. Kuna mtu mmoja tu ambae NADISH ilizaliwa kwa ajili yake...alisema Rai.
Ni nani huyo mtu?.. Aliuliza Mfalme.
Rai alimweleza yote kuhusu uwezo na nguvu alizonazo suya na kua amefanya jambo hili kua siri hata kwa watu anaowaamini sana.
Mfalme.. Wewe wala mfalme wa Lazi hamuwezi kumshinda Suya kama akisema atumie uwezo wake wote.. Ananguvu nyingi sana..alisema Rai
Mfalme alizidi kutetemeka kusikia habari hizo.
Nguvu hizo alitoa wapi?.. Aliuliza Mfalme kwa wasiwasi.
Historia ya suya ni ndefu na ya kutisha sana.
Suya alipokua mdogo sana alikua akiishi na wazazi wake..alipozaliwa tu siku hiyo kulitokea moto usiojulikana chanzo chake na ukasababisha vifo na uharibifu wa mali nyingi sana.
Kwahiyo ilisemekana kua Suya ni mtoto mwenye mkosi na amezaliwa na hilo balaa la moto kwakua kw siku hiyo alizaliwa yeye peke yake nchi nzima.
Lakini kiukweli sio kwamba ule moto haukua na chanzo maalumu..bali kuna watu walikua wakifanya ushirikina halafu dawa zao zikashindwa kufanya kazi na kusababisha moto.
Kwahyo suya alitambulika kama laana na hata alipokua mkubwa kidogo watu wa kijiji chake na nchi kwa ujumla walijaribu kumuua ndipo wazazi wake wakamtorosha na kwenda nae mbali.. Wakiwa huko walivamiwa wakauawa ila suya pekee ndie aliepona.
Baada ya hapo alikwenda nchi za mbali ndipo akapewa nguvu za miujiza alizonazo sasa..hapo alipo nguvu zake ni nyingi sana ila kuna kitu anakosa..kitu hicho ni kiti cha ufalme na akikipata hicho basi nguvu zake zitaongezeka mara dufu..alisema Rai kisha akaweka kituo.
Sasa hizo nguvu ni alizitafuta za nin?...aliuliza Mfalme
Kwa ajili ya kuwasambaratisha waliowaua wazazi wake na wale waliosababisha moto hadi yeye akahesabiwa mwenye laana....alisema suya.
Ni akina nani hao?..aliulza Mfalme.
Ni watawala wa nchi ya Baseki (ile nchi iliyopigana vita na Tharia kipindi cha nyuma hadi Rania akaenda lazi) pamoja na baadhi ya watu wao.Suya anawajua wote...alisema Rania.
Kwahiyo maadui Zake hao wote wako hai?..aliuliza Mfalme.
Wote wako hai na hakuna aliekufa...na mmoja wapo ni mjomba wake...alisema Rai.
Mmmhh...haya mapya.. Alisema Mfalme.
Suya anahangaishwa na tatizo la kisaikolojia...tangu akiwa mtoto alikua akiandamwa sana na kutaka kuuawa...hakuwahi kua na furaha maishani..na baada ya kupoteza wazazi wake hivi ndivyo alivyoamua kua..ni katili sana asie na huruma wala hamwamini mtu tofauti na kujiamini yeye.
Ikitokea akapata kiti cha ufalme basi hao maadui Zake atawamaliza vizuri sana..kwa sasa hawezi maana wana nguvu kumshinda yeye kidogo..ila kadri siku zinavyoendelea anaongezeka nguvu na atakuja kuwaua..alisema Rai
Na mpango wake baada ya kuuchukua ufalme huu kazi ya kwanza ni kuua wazawa wote wa kelkuni maana ndio damu pekee inayoweza kumletea upinngamizi kwenye kazi zake na kumpunguzia uwezekano wa kua mwenye nguvu anazozitaka alisema Rai.
Aisee Mfalme alihisi kuchanganyikiwa... Suya hakua mtu wa kawaida wala hakua kiwango chake.
Kwahiyo sasa tunafanya nini?..aliuliza Mfalme..
Huyu ndie NADISH... Ndie anauwezo wa kupambana na Suya ingawa kumuua haiwezekani..alisema Rai.
Rania... Hata kwa uhai wangu nitahakikisha unaweza kupambana na Suya.. Sio rahisi hata kidogo.. Ni hatari sana..ila naamini utaweza... Alisema Rai.
Mimi niko tayari kwa lolote lile..nitapambana..alisema Rania.
Unajua kua inaweza kugharimu maisha yako?..aliuliza Rai.
Haijalishi..sina jinsi.. Nitapambana....Alisema Rania.
Mfalme huu Ndio ukweli.. Sikutaka hata Fasha mwenyewe asikie haya maana asingekubali Rania kuhatarisha maisha yake kwa ajali ya kupambana na Suya.
Rania tukiondoka hapa hutaruhusiwa kuonana na Dom wala Fasha na wala hawatakiwi kujua kinachoendelea..alisema Rai.
Baada ya maongezi hayo Rai a Rania walitoka na kwenda kwenye chumba cha siri cha Mfalme ambacho Mfalme aliwapa kwa ajali ya maandalizi yao wao wawili tu.
Walipofika huko Rai alimkabidhi Rania siraha maalumu ya kupambana na Suya.
Kilikua kisu kidogo cha miujiza cha kuweza kukata ile pete ya suya.
Hakikisha unakitunza kisu hiki na ukae huku wala usitoke nje..alisema Rai kisha yeye akaondoka na kurudi nje.
Alipofika kwenye makazi yake alikutana na Dom.
Mama..Rania yuko wapi?.. Aliuliza Dom.
Rai alikaa kimya wala hakujibu kisha akaondoka. Dom alishangaa sana na alijisikia vibaya sana.
Alihisi yeye tu ametengwa wakati wengine wameshirikishwa kila kitu.
Alikaa kiunyonge sana kwa muda kama masaa mawili akiwaza.
Akiwa amekaa mara Fasha alikuja...
Hivi umeshajua aliko Rania?..aliuliza Fasha.
Au mimi ndo nikuulize wewe... Alisema Dom.
Mimi sijui..niliambiwa nipishe kidogo wana maongezi ya watatu..mama,Rania na mfalme.. Alisema Fasha.
mmmh....kwani mara ya kwanza si uliitwa..alisema Dom
Ndio..ilikua ni kuhusu barua iliyotoka Lazi inayoomba muungano wa kijeshi.. Baada ya maongezi kuhusu barua hiyo mimi na omandi tumeambiwa kupisha wakabaki watatu.. Wanaongea muda mrefu tu..nimekutana na mama nikamuuliza akanipita tu kimya..alisema Fasha.
Mmh..na mimi amenipita kimya..alisema Dom...
Basi kutakua na jambo la siri.. Labda tukimwomba Rania atujulishe atatujulisha....alisema Dom..
Haya ngoja tusubiri...alisema Fasha.
Tharia na lazi waliungana kupambana na Faritha na Suya.
Kwa muda wa mwezi mzima maandalizi ya vita yalikua yakiendelea..Rania aliomba muda huo yeye akawaone Namadi na Hanna huenda kwa mara ya mwisho maana hana hakika ya kua hai baada ya vita.
Rai na mfalme walimruhusu akaenda
Alipofika Hanna ndo alikua nje na akampokea.
Rania aliingia ndani na kumkuta Namadi amekaa.. Hakuamini macho yake alipoangalia pembeni kumwona baba yake pamoja na bibi yake... Machozi ya furaha yalimtoka..
Rania... Mwanangu... Alisema kaasha kwa mshangao mkubwa.
Rania alifurahi kuwaona..alikumbatiana nao kwa muda mrefu huku machozi yakimtoka.
Baba,bibi nisameheni jamani... Sijawatafuta Siku zote hizi..alisema Rania.
Usingetupata mwenyewe Rania... Tushukuru Mungu tumekuona sasa... Sitakubali uishi ikulu tena mwanangu..ni wakati wa kuishi wote tena baada ya miaka mingi ya kutengana alisema kaasha.
Rania alimkubalia tu kumpa moyo ila akilini mwake alijua yeye.
Baada ya kuongea mengi na baba na bibi yake alongea ba hanna na Dom na kuwashukuru kwa kuwatunza wazazi wake.
Rania..mbona unaongea kama unakata roho??. Aliuliza Hanna kwa utani..
Haha..wewe nae...alisema Rania huku akiumia moyoni.
Alikaa huko kwa wazazi wake hadi zikabaki siku mbili kabla ya vita kuanza..
Usiku ulipowadia Rania aliamka taratibu na kutoroka huku akiwa ameacha ujumbe mfupi kuwaeleza wazazi wake kua wasihofu atarudi maana ameenda kuwatafutia usalama.
Kaasha na mwanae pame walihisi kuchanganyikiwa..kaasha alilia sana baada ya kujua Rania akaenda vitani.. Alilia hadi akapoteza fahamu.
Rania alifika ikulu na kumkuta Rai amemsuburi kwa wasiwasi kua hatarudi.
Oooh.. Rania.. Umekuja..alisema Rai
Mama..nahitaji kuwaona Dom na Fasha hata Mara moja kabla sijaenda huko..hata nisipoongea nao..alisema Rania.
Hapana mwanangu moyo wako utapata hofu na utaogopa kupigana..alisema Rai.
Mama naomba hata kidogo.. Sijui kama nitarudi nikiwa hai au nitakufa huko...alisema Rania
Dom Muda wote hakua na amani..alikua akimfuatilia mama yake kwa siri angalau ajue kitu
Wakati huo wanaongea Dom alikua amejificha anawasikiliza yote wanayoyaongea..
Dom alishtuka sana kusikia Rania akisema "sijui kama nitarudi nikiwa hai au nitakufa huko""
Alishituka sana mapigo ya moyo yakaenda kwa kasi sana..NINI KINAFUATA?
USIKOSE SEHEMU YA THELATHINI NA SITA
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni