AISEE KUMBE RAHA (16)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI NA SITA
"Weeee suzaniiiiii.!!!??" ile tunatoka tu nje ya gesti ile nikasikia sauti kali ikimuita suzan na kujikuta wote mimi na suzan tegeuke kwa uoga lakini bila ya kutegemea kabisa macho yangu yakamshuhudia Chiku akiwa Na mama yake akiongoza na Mama catherini na catherini mwenyewe"Tobaaaaa!!!".............
SASA ENDELEA...
Maneno ya uoga yakatamka katika kinywa cha suzan ambaye hakuamini kabisa hali ile ambayo ilikuwa imetokea na kujikuta mpaka akijiziba uso wake kwa kutumia mikono yake na kuganda pale na kuanza kutetemeka kwa uoga.Hata mimi hofu kubwa ikatanda na kujikuta nikiungana na suzan pale kuganda na kujikuta nikiinamia chini baada ya kuona Mama chiku na chiku wakiwa wananiangalia kwa hasira sana."Suzan shoga yangu yani hata wewe.??" Chiku akasema kwa hasira na kumuangalia kwa jicho baya suzan ambaye alikuwa kainamia chini huku kaziba macho yake kwa uoga mkubwa kutokana na hali ile ambayo hakuitegemea kabisa.
"Me si nilikuambia shosti yani hao hawajaanza leo."catherini kwa sauti ya chini akaongea huku akikwepesha macho yake yasiangaliane na yangu kutokana na kunionea mimi aibu.Hali ile ilishangazwa na Mama catherini ambaye akuongeza hata neno moja na hata mama chiku naye alikuwa akiniangalia mimi kwa hasira kwa sababu ya maneno yake aliyoniambia kuwa alikuwa hataki mimi kujihusisha na wanawake wengine.katika hali isiyotegemeka ghafla chiku ambaye alikuwa na hasira sana akamvamia kwa kasi suzan hadi akadondoka naye chini na kuanza kumshambulia Mangumi.hali ile hakika sikuivumilia na mimi haraia nikaingilia na kumtoa chiku asiendelee kumpiga suzan.
"niache pablo niachee mpumbavu weee niache."Chiku akaanza kutaka kupambana na mimi kwa kutaka kunishindilia mangumi lakini kwa kutumia nguvu za kiume nikawa na mzuia asiendelee kunipiga.
"Tulia Malaya wewe."Sauti ya hasira ikanitoka na kumuambia chiku huku nikiambatanisha na kibao kikali kibao ambacho moja kwa moja kikampata chiku katika uso wake huku nikimtukana na Hapo ndipo nilipouchokoza moto ambao wala sikuutegemea kama ungetokea katika hali ile.Mama chiku na Mama catherini hakika hawakuvumilia kabisa jambo lile la mimi kumtandika kibao chiku wote wawili isipokuwa catherini wakanivamia na kuanza kunishindilia Mangumi yasiyokuwa na idadi na hata nilipokuwa nataka kujaribu kujizuia lakini nguvu ya wanawake wawili shupavu ikachukua nafasi yake.
"Weee nani aliyekuambia umpige mwanangu wakati mimi mwenyewe sijawai kumpiga."
"Yani unampiga mtoto wa shoga yangu nikuache sasa subiri nikuonyeshe lazima tukuumize na wewe."
"Wewe chiku na wewe mtandike."Yalikuwa ni maneno ya mama chiku akisaidiwa na Mama catherini ambao walikuwa wakinishindilia makofi mazito ambayo mengine yalitua katika uso wangu huku mengine yakitua muda mwingine mgongoni,tumboni na kifuani.Maneno ya mama catherini yalimteka na chiku ambaye naye akaungana na wamama hao kunishambulia.Suzan wala hakubaki pale na wala hakuingilia yeye akaondoka haraka na kumuacha catherini ambaye ngoma iliponoga naye akawa anaongezea vimaneno.
"Oyooo Mpigeni mpigeni Mpigeni huyo apigwe."hayo yalikuwa maneno ya catherini aliyeonekana kabisa kushangilia kwa nguvu mchezo ule ambao baada ya kuona na Mimi nikilegea sana basi watanifanya wanavyotaka na mimi makofi mengine nikawa nayavuia na nilipokuwa napata nafasi ya kurusha Ngumi basi nilikuwa narusha.Kwa ujuavyo Waswahili bana Hali ile ambayo ilikuwa mida ya jioni jioni kama ya saa kumi kuendea saa kumi na moja hivi Mamia ya wananchi ambao walijikusanya kwa wingi kuangalia hali ile na cha kushangaza sasa si wanaume wala wanawake kwanza wakaanza nao kushangilia huku baadhi ya wanawake nao wakawa wanaongeza nipigwe nipigwe na makelele yale yalioleta kama ushabiki flani hivi yalitosha kabisa kuwapandisha mori Mama chiku,chiku na Mama catherini kuendelea kuniyumbisha Na ujinga sasa catherini naye ambaye alikuwa naye anashangilia naye akajisogeza kuja kushambulia baada ya kuona sasa Mwanaume naanza kujitetea baada ya kumkamata kisawa sawa mama catherini na kuamua kufa naye kwa kumshindilia Mangumi mazito huku nikiyavumilia mateke mabao na Mangumi yaliokuwa yanarushwa na kunipa ya Mama chiku,chiku mwenyewe na catherini.Lakini kama ujuavyo kuwa kati ya watu kumi na tano basi lazima watakuwepo hata wanne wenye akili za kutosha.majamaa wanne ambao walikuwa wakiangalia nao mtanange wakaingilia ule ugomvi ambao kabisa haukuwa hauwahusu na kuanza kunitetea Mimi kwa kawata wale wakina Mama na wasichana ambao hakika walinishambulia kidogo.Mama catherini naye damu zilikuwa zinamtoka usoni kutokana na mimi kumkamta na kuanza kumshambulia kwa Mangumi.Mimi sikutoka damu ila uso wangu ulivimba haswa kutokana na makofi yale.
"Wee kaka nakuheshimu niachie niachie nikamfundishe mtoto mdogo yule asiyejua hata kunyoa chini nimuonyeshe niachie."Mama catherini alikuwa akikoroma kwa hasira na kunipandisha na Mimi hasira nakujikuta nikitaka kujitoa katika mikono ya jamaa mmoja ambaye alikuwa amenishika mimi.
"Nyie wote naaenda kuwachukulia rb mkaozee jela nyie." Na Mimi nikamjibu Mama catherini ambaye aliendelea kugombana na wale majamaa waliomshika huku akiwa bado na hasira na mimi.
"Oyaa broo sisi tumekusevu kama vipi jikatae."jamaa aliyenishika akaniambia vile na mimi baada ya kuona nimeponyeka kweli nikaanza kuondoka huku nikichekwa na watu na kwa mbali nikasikia nikizomewa na akina Mama catherini.hakika Nilionekana rafurafu hata shati niliyovaa ilichafuka hata jeans yangu ilijaa mavumbi kila niliyekuwa naonana naye alinishangaa lakini nikajuka kauvu Mpaka nikaenda kupanda Gari ambapo nikakaa kwenye siti kisha nikajisachi na mfukoni nikakuta simu yangu ipo na pesa zangu zipo salama.Nikachukua simu yangu nakuiwasha na kukutana na Messeji katika uwanja wa mtandao wa whatsapp.Taratibu nikaingia nakukuta messeji imetumwa na suzan.
"Samahani Pablo nimegombana na Marafiki zangu kisha wewe tu na najuuta kwanini nilikuomba penzi.Sasa kurudisha Mapenzi kwa rafiki zangu sina budi kukufanyia kitu ambacho umemfanyia catherini." Hakika messeji ile ya suzan haikuingia kabisa kichwani na kujikuta nikiirudia irudia kuisoma na kujikuta tena nikiisoma kwa sauti ya nguvu kama nimechanganyikiwa nakusababisha watu niliokuwa nimepanda nao gari kuniangalia kwa kunishangaaa..............
Hakika majasho nayo yalianza kunitiririka kama nilikuwa nakimbia vile.Na bila ya kupoteza Muda nikajikuta nikimjibu suzan ambaye alionekana yupo online kama Mtandao wa whatsapp unavyooneshaga.
"Umemaanisha nini suzan mbona sikuelewi."Nikamjibu suzan ile messeji yake na kusubiri jibu ambapo baada ya kumtumia mimi messeji ile whatsapp ikaonyesha kuwa naye alikuwa sasa anarudisha jibu baada ya kuandika pale juu katika namba yake typing ikamaanisha uliyemtumia messeji naye anakujibu na Hapo anaandika.
"Pablo samahani sana unajua Hata mimi imeniuma Ulivyombaka rafiki yangu catherini nakuona haitoshi ukampiga Picha na kumsambaza katika Mtandao mzima wa facebook umedhalilisha sana Mpaka nimeumia."Suzan akanijibu na kuzidi kunichanganya na kujikuta nikianza kutetemeka sasa kwa hofu kubwa na kugundua kuwa suzan kuna kitu atakuwa amenifanyia kwa Muda huo ndio Maana alikuwa akiongea Vile.
"Sasa suzan una uhakika gani kama Ndio mimi Niliyepost picha zake huyo Catherini wewe una ushahidi wako uko wapi suzan Halafu hizo inshu hazikuhusu ujue suzan."Nikamjibu suzan Huku nikiendelea bado kuwa na hofu kubwa hakika hata kwenye gari walikuwa wananishangaa jinsi nilivyokuwa.Nilionekana Kama mtu aliyechanganyikiwa flani vile lakini Mimi sikujali wale watu waliokuwa wananiangalia nikiwa bado Mule kwenye gari.
"Hayanihusu??,yule ni mwanamke Mwenzangu na lazima nimtete mwanamke mwenzangu kwa swala hili ambalo ni la udhalilishaji Pablo na dawa yako wewe imeshapatikana."
"Mmmh dawa gani suzan wewe mimi si Mpenzi wako Mume wako."
"Wewe sio Mume wangu wala mpenzi wewe kwangu ni Hawara na hii Ndio mwanzo mwisho kuwa mimi na wewe kwa sababu Ya kuwatetea Marafiki zangu."Hakika suzan alikaza na kushikilia msimamo wake ambao ulitosha kabisa kuniogopesha Mwanaume na kujikuta nikimshangaa.
"Huyu kapatwa na Nini sasa au zile Ngumi alizopigwa kidogo na Chiku."Nikajikuta nikiwaza na kujisemea kimoyomoyo kwa sababu suzan ilikuwa sio kawaida yake kuongea kama vile na Muda wote yeye alikuwa ni Mwanamke ambaye mara nyingi Nilipokuwa naongea naye alikuwa akiniambia kwamba alikuwa akinipenda Mimi kuliko mwanaume yoyote yule.Nikiwa nawaza nimjibu nini suzan baada ya kunitumia Messeji yake ile ghafla messeji mbili za picha zikaingia katika simu yangu picha ambazo mara ya kwanza zilipotumwa sikuzitambua fresh kwa sababu ziliweka ukungu kama ujuavyo watu wanaotumia whatsapp kuwa ukitumia picha ambalo mpaka uidownload ndio ionyeshe huwa kwanza unaweka ukungu flani ambao unakufanya usione vizuri picha uliyotumiwa.kwa hofu kubwa huku nikianza kutetemeka nikazifungua zile picha ambazo baada ya kuzibonyeza ile nizifungue zikachora duara ambayo ilikuwa na mwaga wa kijana ambao baada ya kujaa katika duara lile picha zikafunguka.Nilipoifungua Picha ya kwanza hofu ikaanza kutanda na kujikuta nikihema kwa Nguvu sana hakika sikuamini lakini nikajikuta nikiangalia vizuri ile picha ilikuwa ni picha iliyopigwa kuanzia kiunoni mpaka katika Miguuni huku kukiwa uchi na karoti iliyosimama kwa nguvu ilikuwa ikionekana vizuri kupita maelezo na Nilipoangalia sana Hofu ya kuwa mimi ilianza kutanda baada ya kuangalia vizuri ile picha na kuliona shuka ambalo lilikuwa limetandikwa katika ile gesti tuliyotoka kufanya Mapenzi Mimi na suzan.nikajikuta nikipagawa huku nikiwa nimetoa Macho kama vile nilikuwa nimebanwa na Mlango haraka nikaangalia na kwenda kuifungua picha nyingine moja kati ya picha zile mbili ambazo moja nilikuwa nishaifungua.kwa Macho yangu nikashuhudia picha nyingine na safari ile ilikuwa ni picha ambayo ilikuwa ni yote nzima Nikiwa nimelala huku nikiwa mtupu kabisa.Hakika niliishiwa nguvu pale katika daladala ile niliyopanda baada ya kuangalia zile picha.Mwanaume nikajikuta nikianza kudondosha chozi ambalo liliwashangaza abiria wengi ambao walikuwa wakiniangalia kwa sababu ya mimi kuongea na peke yangu kwa sauti.Nikiwa bado na mawazo huku machozi yakinibubujika ghafla simu yangu ya mkononi ikaita na nilipoangalia mpigani nilikutana Na namba ngeni ambayo sikuijua taratibu nikaipokea na kuanza kuisikiliza.
"Haloow"
"Halooow mambo mpenzi hahaha mimi chiku bwana."Moyo wangu ukaanza kudunda baada ya kusikia sauti ya chiku ambaye alikuwa akicheka kwa nguvu na kuzidi kunitia hofu na kujikuta nikiwa kimya na kushindwa kabisa kumjibu.
"Enhe mbona kimya haloo na sasa ujanja wako umeshafikia mwisho mwisho kabisa leo mtandao utaeleza
Na kupendezaaa kwa picha zako ukiwa mtupu na kutangaza biashara kuwa una hitaji mwanamke mwenye ikulu kubwa kuweza kuhimili mikiki mikiki ya karoti lako hahahahahahahahahah umekwisha."yalikuwa maneno ya chiku ambayo hakuna hata neno moja nililomjibu na Baada ya kumaliza kuongea akakata simu.Nikabaki kimya mwanaume huku machozi yakiendelea kunibubujika na daladala ile ilipofika kituoni ambacho Mimi nashuka likasimama na Mimi haraka nikashuka na kuelekea nyumbani.Lakini kabla hata sijafika mbali baada ya kushuka katika daladala na kuelekea nyumbani kizunguzungu cha ghafla kikanikumbaa na kunijikuta nikijishika kichwa baada ya kuanza kuhisi maumivu lakini kabla hata sijaendelea ghafla ukungu mzito ukatanda katika mboni zangu nakujikuta nikishindwa kujizuia na Haikuchukua hata dakika nikadondoka mzima mzima mpaka chini na kuzimia Hapohapo...............
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO


USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA SABA
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni