Notifications
  • MY DIARY (42)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA MBILITULIPOISHIA...Uzalendo ulinishinda ikabidi nimuulize ni kwanini bado wanatumia njia hiyo ya kizamani kutunza kumbukumbu wakati siku hizi kuna kitu kinachoitwa Human Resource Informaion system ambapo kumbukumbu zote za wafanyakazi kama waliochishwa kazi, wagonjwa, walioenda likizo ,waliopandishwa vyeo na taarifa nyingine muhimu uhifadhiwa kwa kutumia komputa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (41)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA MOJATULIPOISHIA...Mark anashangaazwa sana na mwanamke huyo lakini kwa kuwa shida yake ilikuwa ni hela anaamua kuachana nae na kuanza maisha mapya hapo jijiini Dar es salaamMaisha yanaendela lakini Mark amekuwa tajiri na mtu mwenye mafanikio sana kiuchumi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Pamoja na mafanikio hayo ni mtu ambaye mapenzi bado yalikuwa yakimuumiza siku hadi siku.Filamu…
  • MY DIARY (40)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINITULIPOISHIA...Alikuwa akinyata kwa kweli. Kweli hata mimi nilimkubali tu siku ya kwanza ingawa bado nilikuwa sijajua ufanisi wake wa kazi.Nilikaa nae hapo kwangu kwa mda wa siki tatu huku asubuhi tukiamka na kuendelea na kazi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Ndani ya mda huo nikagundua kuwa alikuwa na uzorfu mkubwasana hivyo kazi hiyo alikuwa akiimudu kabisa.Hapo sasa nilimkubali sana…
  • MY DIARY (39)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TISATULIPOISHIA...Nilikuwa na furaha sana huku nikiamini kuwa ndoto zangu za kuja kuwa mtu maarufu zinaweza kufanikiwa hata kabla ya kuyapata yale madini. Sikutaka mbwembwe niliamua kuikopi na kuipesti hiyo stori kama ilivyo na kuifowadi kwa Mark.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baada ya kama lisaa hivi Mark alipiga na kuniuliza kama kweli ilikuwa nai mimi nimetunga hiyo…
  • MY DIARY (38)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Usiku nilishituka usingizini baada ya mbu kuning’aata na kunisumbua sana. Niliwachukia sana hao mbu kwa sababu walinikatisha ndoto yangu ambayo nilikuwa nikiota.Ndoto ilikuwa ikielezea jinsi harusi yangu na Mark itakavyokuwa. Ndoto ilikuwa tamu sana maana ilinipa taswira ya picha halisi ya maisha yangu ya mbeleni.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilishusha neti…
  • MY DIARY (37)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SABATULIPOISHIA...Hapo alitulia tulii kama mtu aliyeaamia dunia ingine. Kimoyo moyo nikawa najisemeha kama amehamia dunia ingine na kuanza kuwaza ujinga sahuri yake mimi nipo kazini bwana acha nitafute hela. Ndio ni lazima nifanye kazi kwa utaalamu na utundu wa hali ya juu ili waendelee kusimuliana huko mjini ili niendelee kupata hela.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Wewe…
  • MY DIARY (36)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SITATULIPOISHIA...Sasa wewe fikiria mimi niliyeletewa zawadi sikujua ni zawadi gani lakini yeye tayari alishafungua na kuchungulia na kujua nini kilifungwa huko ndani.Basi nikaendelea kumuhudumia yule mama huku na yeye akiniambia kuwa itabidi nikimmaliza hizo zawadi tusifungue hapo hapo na waniimbie wimbo wa happybirthday.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Tuliendelea na stori mbili…
  • MY DIARY (35)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TANOTULIPOISHIA...Tatu niliambiwa kuwa ndugu zake na wazazi wake walihusika kwenye mipango hiyo hivyo walibariki kabisa huyo binti kuniacha mimi mumewe wa ndoa na kuamua mtoto wao aolewe upya. Nne ni kwamba huyo mzungu amewaamishia wazazi wake mjini na amewajengea nyumba ya kifahari.Kwa hiyo mimi ninavyowapigiana simu na kuwajulia hali kumbe wenzangu huwa wananichora tu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (34)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Hapo nikakumbuka kuwa zile zana zangu za kazi nilikuwa nazo ni vile vifaaa vya kupimia ukimwi ambavyo huwa navitumia kabla ya kukutana na mwanaume yeyote nisiyemfahamu. Nikaamua kumkubalia huku nikiamini kuwa hiyo ndo kinga yangu pekee iliyobaki kama mwanaume huyo atataka kuzini na mimi usiku huo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi tuliondoka na kwenda sehemu…
  • MY DIARY (33)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TATUTULIPOISHIA...Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…

MY DIARY (35)

Jina: MY DIARY
Mtunzi: __

SEHEMU YA THELATHINI NA TANO
TULIPOISHIA...
Tatu niliambiwa kuwa ndugu zake na wazazi wake walihusika kwenye mipango hiyo hivyo walibariki kabisa huyo binti kuniacha mimi mumewe wa ndoa na kuamua mtoto wao aolewe upya. Nne ni kwamba huyo mzungu amewaamishia wazazi wake mjini na amewajengea nyumba ya kifahari.

Kwa hiyo mimi ninavyowapigiana simu na kuwajulia hali kumbe wenzangu huwa wananichora tu.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Nakumbuka maneno hayo ya rafiki yake yaliniumiza sana na kujikuta nayachukia mapenzi na mbaya zaidi niliwachukia wanawake. Basi kusibitisha ukweli wa huyo rafiki yake niliamua kwenda hadi kwao kumwona. Na kwa bahati nzuri au mbaya siku hiyo yeye ndo alinifungulia mlango huku akiwa na tumbo kubwa la ujauzito. Roho iliniuma sana kwa sababu mimba yangu aliitoa na kuwa tayari kuibeba ya mtu mwingine. Jamani pole ilibidi nimuhurumie mara baada ya kuona anaangusha chozi.Kweli ukiona mwanaume analia basi ujue jambo hilo ni zito.

Mark hakutoa sauti ya kilio lakini machozi yaliyomdondoka yalitosha kabisa kuelezea machungu aliyoyapata kutokana na tukio hilo la kikatili. Lakini namshukuru mungu alinifungua yote haya na kujua ukweli aliendelea kueleza Mark.Basi nguvu ziliniishia na nikadondoka chini na hiyo ni mara baada ya binti huyo kuniuliaza nikusaidie nini? Kabla sijamjibu kitu aliniuliza wewe ni nani. Kwa kifupi alinikana kunijua. Niliposhituka nilijikuta hospitali huku nikiwa nimezungukwa na baadhi ya marafiki zangu. Tuliweza kusaidiana katika hali ile na baadaye niliweza kuruhusiwa na kurudi nyumbani.

Sikua na jinsi zaidi ya kukubaliana na ukweli huo japo ulikuwa unauma.Siku zilisonga mbele nikajikuta nimezoea hali ya kuishi upweke na sikuoa haja ya kupenda tena. Niliwachukia wanawake wote huku duniani kasorao mama yangu tu.Nikawa nikizini na mwanamke mmoja siwezi kurudiana naye hata kama ilinichukua mda sana kumpata.Hali hiyo ilinifanya nitembee na wanawake wengi sana ambao kwa kweli inatisha sana.

Kuna kipindi niliumwa sana na nilikonda sana nikajua tayari ilikuwa ni ukimwi.Ilinichukua mda sana kabla ya kuamua kupima ugonjwa huo kwa lazima.

Kilichokuwa kikiniogopesha ni demu ambaye nilizini naye mara ya mwisho kupimwa na kukutwa kuwa alikuwa ni muhathirika. Kwa kweli nilikonda sana kitu ambacho mimi mwenyewe kilikuwa kikinishtua sana.Nilijikuta nikikonda na kupungua uzito sana siku hadi siku. Nazani kitu kilichokuwa kikinisumbua ni yale mawazo mara baada ya kupata taarifa kuwa yule demu niliyetembea naye alikuwa na ngoma. Baadaye madakatari walinipima kwa nguvu na kwa bahati nzuri nilikutwa sina maambukizo ya ukimwi.Nilifanya hivyo tena mara 3 yaani kila mara baada ya miezi 3.

Kwa hiyo kipindi hicho ndo kile magazeti ya udaku yalikuwa yakikuandika vibaya ilibidi nimuulizea. Maaana kaka huyo kuna kipindi magazeti ya udaku yalimuandama sana. Ndo kipindi hicho ambacho nilipitia majaribu sana siunajua tena usupa staa mzigo wa miba alijibu Mark. Basi tangia nipewe majibu kuwa nipo salama afya yangu ilizidi kuboreka na kurudi kuwa kama zamani. Tangia siku hiyo nikawa kama malaika nikawaheshimu na kuwaogopa wanawake wote huku duniani.

Sikuwahi kuthubutu kulala na mwanamke na kufanya nae mapenzi zaidi ya kuchombeza tu kama vile nilivyokufanyia wewe ulipokuwa pale jukwaani. Kufikia hapo usingizi ulikuwa umenishika sana na sikuwa na uwezo wa kuendelea kumsikiliza tena. Nazani Mark aliligundua hilo mara baada ya kuona siitikii wala kuuliza maswali tena. Mark na yeye alivuta shuka na kujifunika.Nilijua kabisa itakuwa ni mtihani mgumu sana kwa Mark kulala na mimi bila kufanya mapenzi.

Lakini nikasema labda fani yake ya kuigiza inaweza kumfanya avumilie.

Kwa sababu mda ulikuwa umeenda sana basi wote tulipitiwa na usingizi.Nilikuja kushituka asubuhi pamepambazuka.Nilimtingisha Mark nikagundua bado alikuwa kwenye usingizi mzito sana.Nilijaribu kujikagua sehemu zangu za siri ili kujua kama nilipitiwa na mwanume huyo au la.Nikagundua hakufanya kitu chochote zaidi ya kulala kama alivyolala.Nilishangaa sana kwa kweli maana mwanaume huyo alionesha kunitamani sana pale nilipokua jukwaaani kwenye shindano la mwanamke nyonga. Au ana matatizo ya maumbile huyu, usikute ni hanisi niliwaza na kunyanyuka na kwenda maliwatoni. Niliamua kuoga zangu mara baabda ya kugundua kuwa mda ulikuwa umeenda sana na ilishafika saa nne asubuhi.Nilitoka na kumkuta Mark ameshaamka na alikuwa akiongea na simu.

Niliamua kumfanyia makusudi kwa kubadilisha nguo mbele yake ili nione ni kweli rijali au hanisi.Sikuamini kabisa kama kuna mwanaume anaweza kulala na mimi usiku kucha asitamani hata kuomba denda.Nilibadilisha nguo zangu mpaka nikimaliza lakini wala mark hakushituka ndo kwanza alivuta shuka na kujifunika vizuri akimaanisha alikuwa bado anahitaji kuendelea kulala. Nilivyomaliza kuvaa nilimueleza kuna mahali nahitajika hivyo tutaonana baadaye. Mark akanambia ni sawa lakini bado sijatoa tamko la ombi lake la jana.

Nilimjibu kuwa anipe mda nitamjibu kwa sababu nahitaji kutafakari maana ndoa sio kitu cha kukurupuka.Mark alinyamza kimya kwa sekunde kadhaa kisha akavuta suruali yake na kutoa wallet na akahesabu noti tano za elfu kumi kumi kisha akanikabidhi. Akanambia kuwa yeye ataondoka na ndege ya mchana ila tutawasiliana kama kutakuwa na mabadiliko yoyote yatakayojitokeza. Sikuamini jamani kama nililipwa hela hili hali hakuna kitu chchote alichofanya na mimi usiku huo. Nilondoka na kuanza kushuka ngazi taratibu lakini nilivyofika reception nilizuiliwa

Kwa sababu tuliingia wawili kivipi nitoke mwenyewe. Huwa wanafanya hivi kwa sababu za kiusalama. Ikabidi simu ipigwe kwenye room niliyotoka na Mark alipokea na baada ya kusema kuwa yupo salama basi niliruhusiwa na kuendelea na ratiba zangu. Nilitoka mpaka nje ya hotel na nilikutana na hali ya hewa ya mvua mvua ikanibidi nipande tax na moja kwa moja nilienda mpaka salooni ambayo nilikuwa nikifanyia kazi. Nilikuwa sina jinsi kwa sababu wikiendi huwa napata watejawengi sana ambao huwa wananilipa hela nzuri sana. Mbaya zaidi nilikuwa na appointment na wamama ambao huwa naheshimiaana nao sana.

Ingawa nilikuwa nimechoka sana lakini bado niliamua kujitutumua na kuheshimu kazi yangu. Yaani nilikuta msururu wa wateja wakinisubiri kwa hamu na jamu. Ilibidi niombe radhi kwa kuchelewa kufika lakini kwa kuwa ndo nilikuwa msusi bora nilianza kazi kwa spidi ya hatari. Wanachonipendeaga mimi ni kuwa na mkono mwepesi na mtamu usioumiza. Yaani msuko ambo ungesuka kwa msusi nwingine kwa masaa matatu mimi nilikuwa na uwezo wa kusuka kwa masaa mawili tu. Nilipambana sana siku hiyo na nilikuwa bize mpaka usiku ukanikutia hapo Mida ya mchana Mark alinipigia simu na kuniambia kuwa ataondoka na ndege ya jioni na kama naweza basi nimsindikize mpaka KIA.

Nilimwambia tu ukweli kuwa nilikuwa bize sana hivyo isingewezekana. Markilibidi akubaliane na matokeo akaondoka zake na kurudi Dar.Basi tuliendelea kuwasiliana kwenye simu na siku zilivyozidi kwenda nikajikuta nazidiwa na mapenzimazito ya kwenye simu ya mkaka huyo.Nilitokea tu kumpenda ghafla kwa jinsi alivyokuwa akinijali.Yaani alijua kuhandle maana kwa siku alinipigia simu zaidi ya mara tatu. Ingawa huwa nipo bize lakini kwa kweli ikipigwa simu yake ilikuwa ni lazima niipokee.Yaani mwanaume huyu alinirudisha utoto enzi zile ndo nayaanza mapenzi. Ukiachilia mbali na mapenzi ya simu mimi naye nilipambana na kufanikiwa kufungua salooni yangu

*********
**************
*****************

Hapo Mark akanambia “ I just want to wish you happy new born year”( nilikuwa nataka tu kukutakia kheri ya siku ya kuzaliwa).Oooooh my God nilijikuta nikiropoka mara baada ya kukumbushwa kuwa siku hiyo ilikuwa ni siku yangu ya kuzaliwa
Kwa kweli jamani acheni mapenzi yaendeshe dunia kwa sababu huyu mwanaume alinisuprise sana kwa sababu mimi binafsi nilikuwa sikumbuki kabisa kuwa siku hiyo ilikuwa ni siku ya kumbukumbu zangu za kuzaliwa.Sikuwahi kusheherekea siku yangu ya kuzaliwa tangia marehemu baba yangu anitoke duniani

Hivyo nilijikutta machozi yakinidondoka maaa alinikumbusha enzi za uhai wa marehemu baba yangu.Kwa haraka haraka nikajua machozi hayo yanaweza mchnagnnya Mark hivyo niliyafuta na kumwambia “asante babe”. Ok usijali alijibu Mark na kuongeza kuwa aliamua kunifanyia surprise na kaniomba aniacche ili niendeleaa na shughuli zangu.Alipiga hatua mbili kisha akageuka na kunianglia kimhaba kisha kuniambia “LET ME LOVE TOU” Nilitoa tabasamu zio na kumwambia thaks honey. Akaingia kwenye gari na kutoweka eneo hilo.

Nilipikicha macho yangu kuona kuwa ilikuwa ni ndoto au kweli. Haikuwa ndoto bali ilikuwa ni tukio la ukweli kabisa. Wakati naendelea kuganda pale kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme Waridi dada wa salooni alinifuata na kuniambia “happy birthday”. Wewe naye mpaka umsikie shemeji yako anasema ndo umuigizie niliamua kumshushua Waridi. Wewe si ulituficha sasa shemeji kakuumbua na uchoyo wako kamwaga mchele kwenye kuku wengi alijibu Waridi.

Lakini dada unabahati sana ya kupendwa na mwanaume kama huyu handsomeboy na superstar aliendelea kuongea Waridi huku tukiingia saloon. Uzuri wa Waridi ni binti mdogo na pia huwa ni mswahili hivyo maneno yake huwa siyatilii maanani.

“Samahani mteja wangu, mama la mama ilinibidi nimuombe msamaha kwa kumpamba yule mteja ambaye mda wote wa tukio alikuwa akinisubiri. Bila samahani fundi wangu maana hayo mambo ya kihindi yaliyokuwa yakiendelea hapo nje ni kiboko alisema mteja huyo. We acha tu shoga leo ni siku yangu ya kuzaliwa na mimi nilikuwa sina habari ndo nimekuja kufanyiwa surprise hivyo. “Alafu dada wewe si ulinambia kuwa Mark yupo Dar aliadaakia Waridi”. Si ndo maana ya surprise maana hata mimi mwenyewe sijui alifikaje Moshi.

Ila nimeshangaa sana kumbe hata Tanzania kuna mapenzi ya kihindi alisema yule mteja kauli ambayo mimi niliichukulia kama ni dongo kwangu. Wewe acha tu mama yangu kupendwa raha jamani ilibidi na mimi nijdaidai na kujishebedua maana ni wanawake wachache sana wanaopata bahati ya kupendwa na wanaume kama hao wanao jua nini maana ya mapenzi.

“Kweli kabisa dada maana hiyo keki uliyoletewa ni shiidaaaaaaa alidakia Waridi.Uzuri wa Waridi mimi huwa na mpenda sana kwa sababu huwa ni muongeaji sana na ukikaa naye kamwe huwezi boreka. Sasa wewe fikiria mimi niliyeletewa zawadi sikujua ni zawadi gani lakini yeye tayari alishafungua na kuchungulia na kujua nini kilifungwa huko ndani.

Basi nikaendelea kumuhudumia yule mama huku na yeye akiniambia kuwa itabidi nikimmaliza hizo zawadi tusifungue hapo hapo na waniimbie wimbo wa happybirthday.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
68 My Diary Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni