MY DIARY (36)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: __
SEHEMU YA THELATHINI NA SITA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Sasa wewe fikiria mimi niliyeletewa zawadi sikujua ni zawadi gani lakini yeye tayari alishafungua na kuchungulia na kujua nini kilifungwa huko ndani.
Basi nikaendelea kumuhudumia yule mama huku na yeye akiniambia kuwa itabidi nikimmaliza hizo zawadi tusifungue hapo hapo na waniimbie wimbo wa happybirthday.
TUENDELEE...
Tuliendelea na stori mbili tatu huku kila mtu akifanya kazi inayomuhusu hapo salooni.Kulikuwa kuna wanaume wawili waliokuja kufanyiwa messaging na nilipowauliza ni halfbody au fullbody massaging waliniambia ni full body.Niliwapa appointment waje saa kumi na mbili maana niliwaambia wafanyiwe na Warida wakakataa.
Huduma hiyo ya kukandwa kandwa, kuchuliwa na kunyooshwanyooshwa viungo ilikuwa ikipendwa sana na wanaume.Pia huduma hiyo ilinipa sana umaarufu na kunipa hela nyingi kwa sababu fullbody ilikuwa ni laki moja na half body ilikuwa ni elfu hamsini tu.Na huduma zote zilikuwa hazizidi masaa mawili. Wakati wale wateja wakiondoka zao ili waje huo mda niliowambia Warida aliendelea na maswali yake. “Sasa dada kilichokufanya umwage chozi pale ni nini’? Maana Mark alipokuambia tu happybirthday machozi yalikumwagika aliendelea kuuliza Waridi.
Kiukweli mimi huwa sitaki kabisa kukumbuka siku hiyo kwa sababu tangia baba yangu afariki sikuwahi kabisa kusherekea siku hii.Pia huwa sitaki kusherehekea siku hiyo kwa sababu huwa linanikumbusha tukio la huzuni sana ambalo lilishawahi kutokea tulipokuwa wadogo.Nakumbuka siku hiyo tulikuwa na familia yangu yaani mimi,kaka yangu ,baba na mama yangu. Na nilikuwa na umri kama wa miaka 8 hivi na ilikuwa ni siku ya jumamosi tarehe na mwezi kama huu.
Nakumbuka pia siku yangu ya kuzaliwa mwaka huo iliangukia kwenye sikukuu ya Iddy al haj.Siku hiyo wazazi wangu walinifanyia bonge la sherehe na baadaye walinipeleka sehemu ya kuchezea watoto (childplay ground).Sehemu hiyo ilikuwa na vitu vingi sana kama bembea , treni, magari ya watoto na helkopta na vitu vingine vingi unavyovijua wewe.
Basi tukiwa kwenye furaha hiyo ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwangu na sikuu ya iddy kuna tatizo kubwa ambalo lilitokea.Nakumbuka kuna wazazi ambao walikuwa na watoto wao mapacha ambao walikuwa na umri mdogo ambao haukuzidi hata miaka mitano. Watoto hao mapacha wa kike walikuwa wakikimbia kimbia huku na kule. Sijui nini kilitokea ila nakumbuka ni uzembe wa wazazi wao na wasimamizi wa sehemu hiyo. Kwa sababu watoto hao walikimbia na kwenda kuingia kwenye swimming pool ya wakubwa. Sijui wasimamizi walikuwa wapi maana wale watoto walidumbukia na kupoteza maisha. Tukio hilo lilipelekea hata hoteli hiyo ambayo ni maarufu sana kufungiwa leseni yake ya biashara kwa mda.Tukio hili la wale watoto wazuri wadogo kupoteza maisha huwa nalikumbuka sana na kunitia huzuni kila ikifikaga siku hii ya kumbukumbu za kuzaliwa kwangu.
Licha ya hao watoto kufariki lakini siku hii huwa inanikumbusha familia yangu.Huwa nakumbuka sana kaka yangu ambaye naye alidata na maisha haya na kuchanganyikiwa kutokana na madawa ya kulevya. Huyu mwanaume kwa kweli alinikumbusha vitu vingi sana.Niliendelea kufanya kazi mpaka nikawamaliza wale wanawake wote.Yule mama aliyeshuhudia Mark akileta zawadi alikomaa sana eti anataka kuiona hiyo keki ipoje.Ilinibidi nifungue baadhi ya zile zawadi nilizoletewa. Jamani huyu mwanaume ni kiboko wakati Waridi na yule mama wakiangaika na keki mimi nilikuwa nikiangaika na zawadi zingine.Aliniletea nguo za ndani tena za kisasa ambazo huwa zinauzwa bei ghali sana.
Yaani kumbe yale maswali anayoniulizaga tukiwa tunachati kumbe yeye huwa anakariri majibu ninayompa.Maana kila kitu alipatia kuanzia rangi, size na muonekano. Kulikuwa na vikorombwezo vingi sana ambavyo vingine sikujua hata vilikuwa ni nini? Lakini vile vitu vidodogo vya urembo kwa mwanamke aliviweka. Pia kwa upande wa vitu vya kula kula hakubaki nyuma maana licha ya keki, kulikwa na pipi, ubuyu,chocolate na vingine sijui hata vilikuwa ni vinini. Waridi na yule mama uzalendo uliwashinda ikabidi wakate ile keki ambayo ilikuwa imeendikwa jina langu na kuanza kula utafikiri wao ndo walikuwaa wamezaliwa.
Wakati tukiendelea kula keki mara simu yangu iliita na kuangalia alikuwa ni Mark “helow babe” yes honey nilimjibu kwa kujiamini. “Upo wapi, nimekumiss alisema Mark” nikamjibu kuwa mimi bado nipo job je nikitoka nikukute wapi? Mark akacheka kidogo na kuniambia eti amesharudi Dar. ‘stop joking honey, I real miss you and I want to spend this night with you”(acha utani honey nimekumiss sana na nataka kuwa na wewe usiku wa leo) ilibidi nimwambie.Kweli tena mimi nilikata tiketi ya kuja na kurudi na mda huu ndo nimeingia Dar es salaam alisema Mark kwa kujiamini. –
Kwa hiyo huku Moshi ulikuwa na ishu gani ilibidi nimuulize kwa hamaki. “Nilikuja tu kukutakia happybirthday na kukuletea zawadi aliendelea kujibu bila hata aibu. Yaani nilitamani hata nimg’ate kwenye simu lakini nikasema labda atakuwa ananitania tu kwa sababu anajua kuwa huwa nachelewa kutoka kazini.Basi nilimuaga kwa kumwambia tutaonana baadae. Simu ilipokatwa aliingia mwanaume mmoja ambaye alitaka kufanyiwa messaging lakini alikataa kufanyiwa na Waridi kwa madai kuwa ananitaka mimi kwa sababu ndo mzoefu na pia huwa namuwezea. Ilinibidi tu niingie kazini maana ndo kazi iliyokuwa ikinipa hela nyingi kwa mda mfupi.Akanambia anataka fullbody massaging hivyo akalipia hiyo laki moja. Yaani hii kazi inavishawishi na siku zote nilikuwa sitaki Mark ajue maana angenihisi vibaya. Ebu fikiria mwanaume anavua nguo zote alafu sasa unaanza kumkandakanda na kumchua mwili mzima.
Ujue wanaume wengi wanapenda sana huduma hii kwa sababu huwafanya wajisikie vizuri sana hasa kama atafanyiwa na bint mwenye mvuto kama mimi na mwenye uzoefu na kazi hiyo.Ujue ni sisi tu watanzania ndo tupo nyuma lakini wenzetu wazungu huduma hii huwa inapatikana nyumbani na mara nyingi mke anamfanyia mumewe kama ishara ya kumjali na kumpenda. Huduma hii huondoa uchovu na kuuweka mwili katika hali nzuri ya furaha. Kwa hiyo wanawake jamani jitahidini kuwafanyia waume zenu huko nyumbani la sivyo ndo kama hivi watakuwa wanakuja kwetu na kutuletea hela nyingi wakati nyumbani mmekula dagaaa. Pia akikutana na makurubembe na makomba mwiko basi tena ndo umeibiwa mme hivyo.Sasa kama mtu anavua nguo zote na tupo wawili tu chumbani unafikiri nini kinaweza kutokea.
Unajua kwa nini huduma hiii inapendwa sana na wanaume ngoja leo nikupe siri kidogo za kazi hii ili na wewe ujifunze kitu. Unajua kitaalamu katika zile organ tano za fahamu touch is most meaningfull( ngozi ndo ima msisimko zaidi). Huduma hii inaleta hisia za ajabu na kuondoa uchovu wote. Basi niliingia kwenye chumba kile cha kufanyia message.Chumba hicho kilikuwa kikubwa ambacho kilikuwa na hewa ya kutosha na sehemu ya kuzunguka zunguka. Nikaanza kukiandaa kwa kuweka blanketi laini kwenye kitanda pia niliweka na ile mito laini.Pembeni ya kitanda kulikuwa na kiti maalaumu lakini hichi ni kwa ajili ya halfbody massage.
Nikawasha mishumaa na taa zenye mwanga hafifu kisha nikafungulia mziki laini tena ile ya classic.Nikamwambia Yule mteja aingie chumbani hapo huku mimi nikipasha mafuta ya kufanyia message.Kulikuwa na mafuta mengi sana kama olive oil, coconut oil,ovacado oil na sweat olmond oil.Yaani hapa leo itabidi mnisamehe tu mimi sijui Kiswahili cha haya mafuta. Kwa kuwa mafuta haya huwa yanataka joto lingi niliamua kuyapasha kwa kutumia chombo maalumu nilichokiweka juu ya stovu.Nikahakikisha yanapata joto linalohitajika maana yakiwa na moto sana ni tatizo maana anaweza hisi maumivu.
Basi yule mteja akapanda kitandani na nilimwambia alale na tumbo hili tuanze na mgongo.Na hiyo jamani ni mara baada ya yeye kuvua nguo zote na kubaki uchi wa mnyama. Kumbuka nilikwambia hii ni fullbody massage.Nikamwekea mto chini ya kichwa na mto mwingine niliuweka miguuni. Nilimfunika mwili wake kwa mataulo mawili makubwa yaliyokuwa yamekauka vizuri. Hapo kwa wale wanaume wanaojiheshimu basi wao huogopa kuvua nguo zote na kubaki na nguo ya ndani tu. Ila huyu wa leo hakuwa na aibu yeyote maana mmmmh alivua nguo zote.
Na mimi sikumuogopa maana nilikuwa kazini. Nilipanda kitandani nikapitisha miguu juu yake huku mmoja ukiwa juu na mwingine chini yaani kama mtu anayesubiri kipenga ili aanze mashindano ya riaza. Nikamwekea mikono yangu mgongoni mwake na kuanza kumkandamiza taratiibu. Nikachukua yale mafuta nikayapaka mikononi mwangu kisha nikaisugua vizuri kutengeneza joto la ulaini. Nikapitisha mikono yangu laini kwenye mbavu zeke huku nikimtekenya tekenya na kucha zangu huku nikimwambia avute pumzi kama mara tatu hivi. Kwa hiyo alikuwa akivuta pumzi na mimi navuta mpaka nikahakikisha anajisikia vizuri.
Hapo nikaanza kumsugua sugua taratibu kuanzia mabegani mpaka mgongoni.Nilianza na spidi ndogo na baadaye niliongeza spidi. Kwa hiyo jinsi alivyoendelea kupumua ndivyo na mimi nilijua ni sehemu ipi iliyo na maumivu ya kuchua taratibu na ipi ya kuchua kwa nguvu. Nikawa nashuka taratibu mpaka sehemu zake zile za makalio. Nilinilivyofika hapo nikatoa lilie taulo nililokuwa nimetumia kuyafunika makalio hayo. Sasa hapo kuna wanaume ambao huwa wanapenda kushikwa makalio na kuna wengine huwa hawapendi. Hivyo nilijaribu kwanza kuyapapsa na nilivyoona ameshituka kwa nguvu nikaogopa nikarudisha mikono yangu kwa spidi ndogo juu ya kiuno chake.
Baadaye niliamia miguuni na kuendelea kutumia utaalamu wangu ambao ndio unawafanya wakatae kufanyiwa na kina Waridi. Unajua wengine wengi huwa wanashindwa kutumia dole gumba na kuminyaminya mbavu na sehemu zingine amabazo huwa nauchovu zaidi.Hapa nikaenndelea kutengeneza viduara vidogo vidogo mgongoni mwake.Nikaongeza mafuta na kurudia sehemu za hips na miguu.Wakati nipo sehemu za mapajani niligundua pia sehemu zake za makalio zilikuwa hazina furaha na zenye uchovu kwani zilikuwa zimekunjamana na kusinyaaa.
Unajua kitaalamu sehemu hizo japo wanaume wengi huwa hawapendi zishikwe lakini ndo sehemu ambazo huwa zimechoka sana hasa kwa wale watu wanaofanya kazi za kukaa mda mrefu kama maboss na wengine. Kwa hiyo ilinibidi niuongeze mafuta na kupachua vizuri kabisa kwa madaa kama vile nesi anatafuta mshipa wa kuchoma sindano. Hapo alitulia tulii kama mtu aliyeaamia dunia ingine. Kimoyo moyo nikawa najisemeha kama amehamia dunia ingine na kuanza kuwaza ujinga sahuri yake mimi nipo kazini bwana acha nitafute hela. Ndio ni lazima nifanye kazi kwa utaalamu na utundu wa hali ya juu ili waendelee kusimuliana huko mjini ili niendelee kupata hela.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni