MAMA MWENYE NYUMBA (35)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA THELATHINI NA TANO
Hapo milinga akamsimulia kilicho tokea kama yeye alivyo simuliwana mzee Ngonyani, lakini yalikuwa ni marudio kwa mke wa bwana Kazole, “sasa meambiwa mimi mganga?, akachukue ela alizonywea mipombe zimpeke hospital”SASA ENDELEA...
Kiukweli siyo mala moja kwa bwana Milinga kusikia shemeji zake wakikataa kusaidia ndugu zao, lakini leo mzee Haule alikuwa anaitaji msaada, simu ilikuwa imesha katwa, lakini wakti huo huo aliliona gali moja dogo aina ya Toyota lav 4, likisimama kwenye uwanja wa nyumba ya mzee Haule, akashika mwana dada mrembo Selin, ambae alikuwa ame kuja na habari njema sana kwao, juu ya kuanza ukarabati wa nyumba yao na kufungua mlado utakao wawezesha kujiingizia fedha kwa matumizi ya pale nyumbani, lakini alishangaa kukuta watu wengine watatu tena wote wakiwa na sura za uzuni, alipata jibu baada ya kumwona mzee Haule ambae sasa alibebwa na kuwekwa sebuleni juu ya kochi chakavu, Selina alisimuliwa kilichotokea, na vitu vyote alivyo polwa, hapo hapo Selina aka shauri kuwa mzee Hule apakizwe kwenye gari kisha safari ya hospitari ianze, wakati mzee Haule akipakizwa kwenye gari yeye Selina alipigaa simu kwa Suzan ambae alitoka kuongea nae muda mfupi uliopita akimsisitiza kwenda kwa wazee wa Edgar ili ampe jibu wajuwe la kufanya
Selina alimpa taali fay a kilicho tokea kwa mzee Haule hapo hapo Suzan alituma fedha kwenye a/c ya Selina kiasi kama million moja, kisha akasisitiza kuwa awe anajulishwa kila kitakacho endelea, nusu saa baadae mgonjwa alikuwa kwenye hospital binafsi ya Baraka hospital yenye ma doctor bingwa ila ghalama yake uwa nikubwa sana sema cha msingi huduma zake za uakika, mzee Haule alikuwa amwsha patiwa chumba chakupumzika ambacho ni VIP, na sasa alikuwa anapatiwa matibabu ndani ya chumba kile, ambacho kilikuwa na kila kitu, ndani utazani analazwa raisi, kitendo hicho kili washangaza sana Faraja na mume wake ambao waliamua kuacha shuguli zao pasipo kujali watapatawapi fedha za kuendeshea maisha yao kwa siku yaleo, wakati wanajiuliza pesa ya kulipia ghala za hospital zitatoka wapi, mala wakashangaa yule mwana dada akiwa kabidhi lisiti ya laki sita iliyo fanyiwa malipo ya pale hospital, nakwamba mzee huyu ata pumzishwa pale kwa siku tano, akipata matibabu, na huduma nyingine kama chakula N.K. hapo ndipo waanza kunong’o nezana wakiulizana, huyu mdada ni nani?, ndipo walipo shangaa akimpatia mama yao fedha kiasi cha laki tano, “mama, hii fedha ametuma mkweo, kwenye a/c yangu nimeitoa ya watu nitaifidia nikisha itoa yakule benk nitakuja kuwaona nikitoka kazini, alisema Selina akiwaaga na kuelekea kazini, huku akipiga simu kwa Suzan kumjulisha alipo fikia, akiwa acha wakina Faraja wakishangaa, mkwe tena?
Ok Suzan alikuwa amemaliza kumsimulia Edgar akilicho mtokea baba yake jana usiku, akaelezwa pia atua aliyo ichukuwa Selina ya kumpeleka hospital akaelezwa pia kuwa ameshanza kupata matibabu na yupo pale dada yake faraja na shemeji yake Milanzi, hapo Edgar alipiga simu kwa shemeji yake huyo maana namba yke ya simu alikuwa nayo, licha ya kuongea na Shemeji yake kijana milinga, pia alifanikiwa kuongea na mama yake baba yake na dada yake, wote walimsifu sana kwa kusababisha baba yake kupata huduma wakisifia Selina kwa moyo wa kujitolea, pia walimsifa huyo mkwe ambae hwakuwa wana mjuwa, huku Faraja akiomba kuongea na wifi yake, ambapo Suzan akaongea na Faraja kisha mama na kumalizia na baba, akiwa ahidi kwa tumia fedha kwaajili ya kununua simu nyingine, pia akiwa sisitiza kuw makini sana kwa matembezi ya usiu na wasionyeshe fedha zao kwa watu, wakikubaliana baba akipona aende kufungua a/c kwaajili ya kuifadhia fedha
Naam siku tatu baadae mzee Haule akiwa bado hospital, hakuna ata mmoja kati ya watoto wake watatu wakubwa au wakwe zake, alie kuja kumtazama mzee Haule pale hospital, na hakuna alie wapigia simu tena, zaidi ni Milinga na mke wake Faraja wakisaidiwa na jilani mzee Ngonyani waliendelea kumuuguza baba yao ambae alikuwa ameshaanza kupata nafuu, akisubiri sikumbili mbele apewe luksa ya kurudi nyumbani, ambako kijana Milinga alikuwa ame pata kazi ya kusimamia ukalabati wa Nyumba ya wakwe zake na ujenzi wa chumba kimoja cha nje cha flame, kwaajili ya duka, akilipatiwa fedha kwaajili ya kuwa lipa mafundi na pia akapewa laki tatu kwaajili ya kuendeshea maisha yake, akiambiwa kuwa endapo atakuwa na tatizo amweleze Selina nayeye atawajulisha wakina Edgar
Mambo yaliendelea kwa Edgar akiishi na Suzan kama mume na mke uku akiendelea kupanga ratba yake vyema akiwa shughulikia mama na mwana, pia Joyce kwa wakati wake, siku moja akiwaanatoka chuoni usiku akiwa ame toka kuachan ana Joyce alishangaa kuona vijana watatu wakitokea mbele yake “hoyaaaa kidume simama hapo” wote walikuwa wame shikili vipande vya vigongo mokononi mwao, Edgar akasimama na kuwa tazama usoni akawa gunduwa kuwa ni wanachuo wenzake, na mmoja wao ni yule anae msumbua sana Joyce Masoud, “vipi wakubwa kuna tatizo,?” aliuliza Edgar huku akijiweka tayari kwa lolote, mana alijuwa kuwa hapa kuwa na amani maali pale, “tatizo wewe ulioni, siunajifanya bingwa wakupola mademu wawatu”
Aliongea Masoud akimsogelea Edgar huku akiwa ameinua gongo hewani akitaka kulishusha kichwani kwa Edgar, lakini zaidi ya umakini, Edgar aliwai na kulidaka, akampiga ngumi ya usoni na kumnyang’anya lile gongo, kisha kilicho fwata ni zaidi ya balaha, maana ndani ya dakika moja wote walikuwa wana kimbia huku wana chechemea, hapo Edgar aka timua mbio kurudi nyumbani kwao ambako alikuwa anaishi na Suzan kama mke na mume
Kule nyumbani Suzan ambae alikuwa anamsubili Edgar ambae kwa sasa alikuwa kama mume wake, alikuwa jikoni ana anapanga vyombo kwenye kabati, ni aada ya uviosha baada ya kuvitumia usiku hule kwa chakula cha jioni masa mawili kabla Edgar ajaenda chuo kwa masomo ya jioni, wakati anapanga vyombo hivyo sijuwi kitu gani kili mkumbusha atazame kwenye droo ya chini ya kabati, akakuta chupa mbili za mvinyo mwekundu, akajaribu kukumbuka aliziweka lini hakupata jibu akazitoa na kwenda nazo sebuleni moja ilikuwa ime tumika na nyingine ilikuwa nzima kabisa, akaziweka mezani akipangakesho yake kwa kuwa ni juma mosi aklirudi kazini azitumie, pamoja na mpenzi wake, ata alipo ingia Edgar akamwuliza kuhusu zile chupa mbili za mvinyo mwekundu maana yeye hakuwa na kumbukumbu ya chupa zile nyumbani kwake. “itakuwa ni zile alizo kuja nazo rafiki yako Sophia,” nikweli maneno hayo ya Edgar yli mkumbusha jambo Suzan, kwamba siku ile alilewa sana baada ya kunywa pombe aliyo letewa na Sophia, pasipo kumweleza jambo Edgar Suzan akaziifadhi zile chupa pale pale alipo zikuta, kabla awaja ingia kuoga na kujibwaga kitandani, na kama destuli yao, walikuwa kama wapenzi wapya, kila siku lazima waliamshe dudu
Zilikuwa zimepia wiki mbili tokea mzee Haule atoke Haspital siku hiyo akiwa anatumia gongo maalum kwa watu wenye matatizo ya mguu, alikuwa amesimama nje sambamba na mke wake wakitazama jinsi nyumba yao ilivyo pendeza, huku chumba cha biashala kikimaliziwa kupakwa rangi inayo fanana na ile ya nyumba yao, na hapo ni jana tu Tanesco walikuwa wame unganisha umeme, mzee huyu ambae mguu wake ulikuwa ume viligiwa POP alifarijika sana, tena alijivunia kuwa na mtoto kama Edgar, yaani licha ya yote haya lakini leo, pia walikuwa wana subiri gari ambalo lilikuwa linaleta vifaa vipya vya ndani, kuanzia makochi mpaka makabati na meza za vioo, huku chini wakiwa wame wekewa tyles na kuta zime pigwa plasta na kusikimiwa nje na ndani na kupakwa rangi, mzee Haule na mkewake sasa walikuwa wanawasiliana moja kwamoja na mkwe wao Suzan, bila wasi wasi wowote, na sasa kila mmoja alikuwa na simu yake
Edgar aliendelea kutumia ratiba yake vizuri kuwa panga Sopia na mama yake, huku mama Sophia akizidi kuna wili wa furaha maana hakuitaji kumsumbua tena mume wake na hakuwa na mawazo yoyote juu ya kuchelewa kwa mume wake wala kufikilia ata kata wapi kiu yake, alicho akikisha ni kwamba anampatia Edgar mkwanja wa maana ili azidi kumpatia dudu bila kumbania, nisawa na Sophia yeye alisha wasahau wapenzi wake wote sasa alikuwa ni nyumba ndogo ya kijana mdogo Edgar, huku akiakikisha ana fanya kila linalo wezekana kumfulahisha kijana huyu ili aendelee kupata utamu, siku zika songa mbele, Edgar na Suzan waka shamili katika mapenzi yao huku akijitaidi kusoma kwa juhudi akifidia siku za mwanzo alizo zipoteza wakati alipo kuwa akianza mausiano na Suzan, Suzan licha ya kuendelea kutoa huduma kwa wazee wa Edgar pia hakuwa sahau wazazi wake na ndugu zake huko Iringa
Ilisha pita mwezi mmoja tangu, mzee Haule atoke hospital sasa aliweza kutembea, japo siyo vizuri lakini angalau alikuwa anauwezo wa kwenda ata dukani kwake, ambako alikuwa anauza binti yake Faraja, huku mkwe wake mume wa Faraja akikusanya mazao kwa kuyanunua toka vijijini na kuya leta pale nyumbani kwa mkwe zake, maisha yalikuwa mazuri sana, tena sasa mzee haule alipoitaji kinywaji alikunywa bia na rafikiyake mzee Ngonyani wakiagizia pale pale nyumbani, Selina akuacha kuwa tembelea mala kwa mala kuwa Julia hali
Ni mda mrefu sasa tokea alipo sikia baba yake ame vamiwa na vibaka, dada mkubwa wa Edgar au mke wa bwana kazole alishangaa kuto kupata simu yoyote zaidi ya ile iliyo toka kwa shemeji yake na kwa mzee ngonyani, “au walikuwa wana danganya ili niwatumie fedha, wame noa kwanza mimi mwenyewe na kiu ya fedha, tena safari hii sijuwi vikoba itakuwaje, maana wiki sasa sija peleka malejesho” aliwaza dada yake Edgar akizidi kutembea kuelekea dukani, alifika dukani na kununua maitaji yake kisha akaanza kurudi, kabla haja fika mbali toka dukani akasikia mama mmoja ana msimamisha “niambie binti Haule” walisalimiana kisha maongezi yakaanza, “kwanza ongeleni mwaya” alisema yule mama “ongela ya nini tena?” alisha ngaa dada yake Edgar, yule mama alimweleza kuwa, siku mbili zilizo pita alikuwa ametembelea luhuwila seko, akakatiza kwa mzee Haule amekuta mabadirio makubwa sana, alipo uliza mabadirko yale yame fanywa na nani, akaambiwa na watoto wake, na alisibitisha hilo kwa kumuta Faraja pale dukani, kiukweli dada yake Edgar mkubwa hakujuwa aseme nini, zaidi alipoagana na yule mama aka elekea nyumbani kwake nakuingia ndani, akaitoa simu yake na kuanza mawasiliano, kwanza alipiga simu kwa mdogo wake anaye mfwata, “we! mama semeni, hivi una taalifa yoyote ya kule nyumbani,”
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA THELATHINI NA SITA
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni