TANGA RAHA (21)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
“Jamani wewe mwanaume una wivu....Haya naondoka”
“Sawa jamani naondoka natafuta pa kukaa”
Dada akakata simu na kunitazama huku akishusha pumzi nyingi
SASA ENDELEA...
“Mume wako anaoenekana na wivu sana ehee?”
“Wee acha hapa nimemuambia nimekaa na mwanaume basi anataka nihame.....Acha nifanye hivyo kaka yangu kwa maana akinikuta hapa anaweza akanipiga vibao mbele za watu”
“Sawa mwaya”
“Asante kwa gazeti na ukarimu wako”
“ Na wewe pia asante kwa kampan yako”
“Ila kaka nakushauri wewe jiunge na Facebook usome story za huyu jamaa alafu bado ni bwana mdogo sana”
“Ahaaa kumbe yeye mwenyewe bado ni mdogo na nyinyi munazisoma story zake?”
“Udogo sio ishu ila anashangaza kwa jinsi ya story zake zilivyo tamu”
“Haya mwaya”
Tukapeana mikono na dada niliye kaa naye kisha akaenda kukaa kwenye meza nyingine na ndani ya dakika mbili kuna jamaa akakaa kwenye kiti kilichopo kwenye meza aliyopo yeye huku akionekana akiwa na hasira na akaanza kufoka foka na kila kitu anacho kizungumza kinahusiana na yeye kukaa na mimi
“Sasa jamani kukaa tu na mwanaume ndio unanifokea fokea kiasi hicho mbele za watu?”
“Kwanini ukae naye hukuona meza zote hizi?”
“Zilikuwa zimejaa watu”
“Wewe mwanamke Malaya sana na yule bwege pale ndio anakutia jeuri na kujifanya unanipan-dishia sauti?”
Jamaa alizungumza huku akininyooshea kidole mimi ikanibidi niliweke vizuri gazeti na kuwatazama jinsi wanavyo jibizana
“Hembu muache kaka wa watu wala yeye hausiani na mimi kukujibu wewe....Ila ukweli ni kwamba mwanaume wewe una gubu.Unadhani nilivyo kaa naye ndio amenivua chupi?”
“Wewe mwanamke nitakuwasha makofi sasa hivi mbele za watu”
“Mimi si nimeshakuwa ngoma yako hata ukinipiga unadhani nitashangaa.Wewe nipige tuu”
Watu wa meza nyingine waliacha kufanya wanayo yafanya na tukaendelea kuutazama ugomvi ila kwangu nikajikuta moyo wangu ikiniuma kwa jinsi jamaa anavyo mgombesha mpenzi wake pasipo kuwa na sababu ya msingi.Jamaa akamzaba mpenzi wake kofi ambalo lilisikika vizuri kwa watu tulio karibu na meza yao.Nikashindwa kuvumilia nikaliweka gazeti mezani na kwenda hadi kwenye meza walipo wao
“Na wewe Chok* umefwata nini hapa?”
Jamaa alaizungumza huku akiwa anahema kwa hasira na mbaya zaidi mimi ni mrefu na jamaa ni mfupi kiasi kwamba nikawa ninamtazama kama mtoto mdogo
“Acha kuwanyanyasa wanawake hujui hawa ndio wazazi wetu”
“Wewe fala nini...Nani awe na mama Malaya kama huyu mwanamke hapa?”
“Rama mimi leo unaniita Malaya........”
“Wewe Malaya na wazazi wako wotee Malaya munakazi ya kukalia umasikini wa kuomba omba”
“Nashukuru mimi ni masikini bora na wewe kwenu mulio matajari ila ninaona hapo ulipo fikia kunatosha ni bara tuachane”
Dada wa watu alizungumza huku akimwagikwa na machozi kiasi kwamba nikazidi kumuonea huruma
“Oya kaka hembu kuwa mstaarabu,usimtukane mwenzoko ni maswala ya kukaa chini na kuya-maliza kumbukeni nyinyi ni wapenzi”
“Wee niaje kwanza juu wewe ndio muhusika wa hili swala alafu unaniletea michongo yako ya kiseng* seng*”
“Powa ila tazama jinsi munavyo jizalilisha mbele za watu”
“Hayakuhusu.......Wewe Malaya si umesema tuachane sasa lete hiyo simu niliyo kununu-lia,cheni,herein na saa vyote nivulie”
Dada wa watu akaanza kuvua kitu kimoaja baada ya kingine huku akilia ikanibidi nimzuie asiendelee kuvivua
“Kwani vitu vyote hivi vina gharimu shilingi ngapi?”
“Wewe vipi......Huna pesa ya kunilipa”
“Sema ni shilingi ngapi nikulipe?”
“Laki nne na nusu”
“Subiri”
Nikafungua waleti yangu iliyo jaa pesa alizo niachia Rahma kisha nikaanza kumuhesabia kiasi anacho kihitaji kisha nikamuwekea juu ya meza na jamaa akabaki ameshangaa
“Unashangaa nini chukua pesa zako uondoke”
Jamaa akazichukua na kuzihesabu na kukuta zipo kamili kisha akamtazama mpenzi wake anaye lia
“Wewe ingekuwa si huyu jamaa ningekuvua hadi chupi”
Dada akataka kuzungumza ila nikamziba mdomo na kujua kitakacho endelea hapo kitakuwa nai fujo.Jamaa akaondoka na kuwaacha watu wengine wakimshangaa huku akionekana mshamba.Nikamshika mkono dada na kurudi naye kwenye meza tuliyo kuwa tumekaa naye na nikapata kazi ya kuanza kumbembeleza hadi akanyamaza
“Hivi yule jamaa yako ana akili vizuri?”
“Hana hata kidogo”
“Sasa na wewe imekuwaje ukawa naye mwanume kama yule?”
“Kaka yangu wee acha tuu ni mambo ya dunia ndio yananifanya nikajikuta nipo naye”
“Kwanza umekula?”
“Sijala kaka yangu....hapa ninapo zungumza nina mia tatu ya dala dala tu kwani tulipanga na ja-maa tuje tukatane hapa ili anipe pesa za kuitunza familia yangu”
“Pole kwa hilo”
Nikamuita muhudumu na dada akaangiza chakula anacho ana kihitaji na baada ya muda kikale-tewa chakula anacho kihitaji nikamuacha ale kwanza ndio tuzungumze.Akamaliza na akanishu-kuru kwa msaada nilio mpatia
“Kwa hiyo wewe unaishi na wazazi?”
“Ndio ila wazazi wangu ni wazee sana ambao hawajimudu kimaisha na mimi ndio mtoto wao wa pekee niliye bakia nikiwashuhulikia wengine wawili wa kiume ambao ni kaka zangu wamekuwa mateja na wala hawana muda wa kujishulisha”
“Mmm pole sana kwani unaishi wapi?”
“Ninaishi Magomeni”
“Mmmmm na wewe una mpango gani wa kimaisha kwa maana jamaa ndio hivyo amesha kua-cha?”
“Yaani hata mimi sijielewi.....Ila kidogo ninafanya fanya kazi za kutengeneza dawa za miti sham-ba,Kazi ambayo alinifundisha baba ila kwa hapa mjini hailipi kutokana watu wengi wanakimbi-lia kwa wamasai na sisi watu wa kawaida hutuacha tukiwa na ujuzi mwingi kupita hata hao wamasai”
“Ahaaa sasa wewe unatengezeza dawa gani na dawa gani?”
“Dawa ya chango kwa wanaweke,dawa ya kuongeza nguvu za kimume,dawa za kufukuza majini na vimizuka daw...........”
“Ehee hapo hapo kwenye hiyo dawa ya kufukuza majini unaweza ukanisaidia?”
Ndio ukihitaji ninaweza kwenda kukuchukulia?”
“Wapi?”
“Nyumbani”
“Powa basi kama huto jali nikupe pesa ukodi boda boda ukanichukulie hiyo dawa”
“Sawa”
“Unaitwa nani?”
“Mwajuma”
“Sawa mimi ninaitwa Eddy”
Nikatoa noti ya elfu kumi na kumkabidhi akaaondoka huku nikibaki na pochi yake kubwa ambayo sikutaka niufungue ndani.Ndani ya dakika 45 akarudi akiwa na kifuko cheusi na ku-niomba twende nyumbani kwangu.
Sikuwa na kipingamizi tukakodi bajaji hadi nyumbani kwangu nikafungua geti tukaingia na dereva bajaji akaondoka baada ya kumlipa.Tukafika sebleni na kushangaa kumuona mwenzangu akianza kuvua baibui lake na kubakiwa na skintait iliyo mchora umbo lake lililo jazia huku kifuani maziwa yeke makubwa kiasi yakiwa yamezibwa na sidiria na kuyafanya yajichore vizuri.
Gafla akaanza kuzichangua nywele zake huku akipiga chafya za mfululizo kiasi kwamba nikaanza kumuogopa.Akasimama kwa muda akitazama mlango wa kuingilia chumabi kwangu na akaanza kunguruma kama Simba huku mwili wake akiutunisha misuli
“HAPA NDIPO KWENYE MLANGO WA KUINGILIA KUZIMU”
Alizungumza kwa sauti nzito ya kiume na sikujua ameitolea wapi,akanigeukia huku sura yake ikiwa imejikunja na kuufanya uzuri wake wote kama mwanamke kupotea
“TUNAHITAJI DAMU YAKO”
“Ehhhh......!!”
“DAMU YAKO”
Akaanza kupiga hatua zenye vishindo vya hali ya juu huku akinifwata taratibu,nikaona sio se-hemu nzuri ya mimi kukaa nikachomoka kwa kasi na kuufungua mlango wa kutokea njee na kwapupa nilizo nazo zilizo chaganyikana na woga nikajikuta nikipiga mwereka mmoja mkali na kuanguka kifudi fudi kama mtoto anayeanza kutembea.
Nikastuka zaidi baada ya kuona miguu ya watu wawili wakiwa wamesimama mbele yangu.
Nikainyanyua sura yangu na kukutana na Hilda akiwa na msichana mwengine ambaye siku-wahi kumuona hata siku moja.Wakabaki wakinishangaa kwani hawakujua ni kitu gani kinacho-nikimbiza.Nikananyayuka na kuanza kujifuta futa vumbi lililo jaa kwenye mwili wangu
“Eddy unatatizo gani wewe?”
Nikatazama nyuma na sikumuona Mwajuma na kuukuta mlango ukiwa umefungwa,
“Eddy mbo haueleweki?”
“Wee niache tuu sijajua ni kwanini ulinileta kwenye hii nyumba?”
Nilizungumza huku nikipiga hatua za kwenda nje na kuwafanya Halda na mwanzake kunifwata kwa nyuma huku wakiniongelesha na wala sikuwaelewa ni nini wanacho kizungumza.
Nikakaa kwenye msingi wa bustani ya maua iliyopo nje ya ukuta wa nyumba yangu na Hilda akasimama mbele yangu huku akiwa amejishika kiuno
“Eddy hembu niambie una tatizo gani?”
“Tatizo ni hii nyumba hembu tazama nina siku kadhaa nimesha anza kuchakaa kiasi hichi je ni-kikaa wiki hapa si nitakuwa tambara la deki”
“Jamani Eddy kwani humo ndani kuna tabu gani.....?”
“Hembu nitolee unafki wako hapa inamaana hujui kinacho endelea humo ndani?”
“Sawa japo na tambua ila sio wewe kukimbia kimbia utakuja uumie kwa vitu vya kitoto”
“Wewe unaumwa nini kwanza ninaomba umpigie simu baba mwenye nyumba aje hapa ili mka-taba kama ni vipiti tuuvunje na mimi anipe nusu ya malipo na hiyo pesa nyingine mimi ninasa-mehe”
“Eddy.....”
“Hakuna cha Eddy wewe unaona Raha hivi mimi ninavyo teseka Si ndio?”
“Shem kwani tatizo ni nini?”
Rafiki wa Hilda akaniuliza na kunifanya nibaki nikimtazama pasipo kumjibu kitu cha aina yoyote hadi akajistukia
“Muulize huyo rafiki yako”
“Shosti wala hakuna kitu huyu mwanaume ni uwoga wake tuu”
Sote tukastuka baada ya geti kupigwa kikumbo hadi likafunguka na hapakuwa na mtu aliyetoka na tukajikuta tukikimbia huku kila mtu akishika njia yake.Baada ya kukimbia kwa muda nikaji-kuta nikiporomosha katika kilima cha bichi ya Raskazone.
Nikatafuta sehemu na kukaa ili kiji-upepo kinipige vizuri na nikapata wazo la kuingia ndani ya bichi hiyo,Nikalipa kiingilio na kuta-futa sehemu iliyo tulia na kukaa huku nikijishauri jinsi ya kurudi nyumbani kwangu.Nikajikuta nikiyafwatilia mazungumzo ya wanaume wawili walio kaa pembeni yangu
“Katika ulimwengu huu hakuna kitu kinacho shindikana mbele ya Jina la Yesu kristo”
“Kweli mchungaji kwa maana nilipo toka ni mbali sana hadi leo ninatazamika kama mtu kweli Mungu ni mwema”
“Unajua shetani anamambo mabaya sana katika ulimwngu huu,Huwa hapendi kuona watu wa Mungu wakifanikiwa kiasi kwamba anawafunga kwa mambo ya ajabu ajabu kama wewe jinsi alivyo kupeleka kuzimu”
“Yaani kipindi kile sikujua ilikuwa vipi kwa maana nilikuwa ni muumini mzuri wa dini.Ila kuna siku nilikutana na dada mmoja katika mtandao wa Facebook....Basi tulikuwa marafiki wa kuchati chati hadi ikafikia hatau tukawa ni wapenzi kabisa...”
“Hambe ngoja kwanza......Inavyoonekana tatizo lilianzi hapo?”
“Ninavyo hisi kwa maana yule dada aliniambia kuwa yeye anatokea Zanzibar na tukapanga siku tukutane Dar kipindi nilipokuwa ninafanya kazi kwenye bandari ya Dar es Salaam.......Haikuwa ngumu kwa sisi kukutana na kutokana nilikuwa ninajuana na watuw engi ambao ni manahoza wa boti zinazo kwenda Zanzibar niliwatumia wao kufanya upelelezi juu ya binti huyo na wakanihakikishia kwamba yupo na anajiheshimu”
“Ehee ikawaje”
Nikakohoa kidogo na kuwafanya mchungaji na mtu wake kunitazama kisha wakaendelea na mazungumzo yao
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni