TANGA RAHA (13)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
Tukajikuta mimi na Halda tukiingia kwenye dimbwi kubwa la kuepena raha huku kila mmoja akijitahidi kumburudisha mwenzaka kwa mitindo anayo ijua yeye mwenyewe hadi ikafika hatua sote tukawa tumechoka kiasi kwamba hakuna aliye kuwa na hamu na mwenzake na sote tukajilaza na usingizi mzito ukanipitia
SASA ENDELEA...
Gafla chumba changu kikatawaliwa na moshi mwingi wenye rangi nyeupe huku moshi mwin-gine ukitokea chini ya kitanda,moshi ukiwa unaendelea kusambaa ndani ya chumba nikawaona wasichana wawili walio valia nguo nyeupe pee na wenye nywele ndefu zinazo fika mgongoni na warefu kwenda juu huku mmoja akiwa amevalai kama malikia huku mwengine akiwa ameshika kitu kama muamvuli na kumfunika mwenzake wakisimama kwenye mlango wa kuingilia ndani kwangu.
Nikatafikischa macho yangu ili nihisi ninacho kiona ni ndoto au.
Ila kusema kweli kila ninacho kiona ni kweli na wala sipo kwenye ndoto ili kuhakikisha tena sipo kwenye ndoto nikajifinya kwenye mkono na maumivu nikayasikia vile vile
“Usituogope kwani sisi ni viumbe wazuri tuu na karibuni kwenye milki yangu”
Mwili mzima ukaanza kunitetemeka kwani katika maisha yangu sikuwahi kuota au kuona kitu cha namna hiyo japo wasichana wenyewe ni wazuri wa sura na umbo ila nikawa ninajiuliza wameingiaje ndani kwangu wakati kila mlango tumeugunga kwa funguo
“Eddy hii nyumba ni mali yangu na hichi chumba ndio ofisi yangu ya kufanyia kazi”
Nikaupitisha mkono wangu kwenye shuka na kumfinya Halda ili aamke ajionee kitu kinacho endelea ndani ya chumba tulichopo ila cha kustaajabisha Halda mwenzangu anazidi kukoroma kiasi kwamba akaamua kugeukia upande wa pili wa kitanda
“Mwenzako hawezi kusikia kitu ambacho mimi ninakizungumza.Nilitaka niwatume vijakazi wangu waje kukushughulikia ila nimeamua kuja mimi mwenyewe ila nimekuja kiustaarabu ndio maana nimevalia nguo nyeupe…..Katika mamlaka yangu huwa sipendi kitu kinacho itwa pombe kwani kina nichefua nafsi yangu kupita maelezo.Pili sipendi wasichana wachafu kama huyo uliye lala naye,tatu sipendi mwanamke yoyote kuingia ndani ya mamlaka yangu”
Mapigo ya moyo yakabadilisha mfumo wake na kujikuta yakidunda kwa kasi ya ajabu kwani vitu anavyo vizungumza sikujua kama nitaweza kuvitimiza kwa maana ni tabu tupu
“Kw….a….ani……wewe ni….na…ni?”
“Mimi ni Malkia Olivia Hitler nilikuwepo hapa tangu mwaka 1884 kabla ya vita ya kwanza ya dunia.Mimi nina asili ya kijerumani”
Kwa haraka haraka kwa maesabu yangu huyu mwanamke ana miaka kama mia na theledhini ila cha kushangaza sioni kama amezeeka na nibinadamu gani asiye kufa na kuishi miaka yote hiyo
“Mawazo yako yanajiuliza kuwa mimi ni bidadamu ila si hivyo unavyo fikikiria wewe.Na nina-miaka mingi zaidi ya unavyo fikiria…..Ila nina ombi moja kwako ambalo nahitaji ulitekeleze hadi siku utakayo ingia kaburini”
Kajasho kembamba kakaanza kinimwagika na mwili wote ukaendelea kutetemeka.
Gafla ni-kaanza kujihisi nikinyanyuliwa kitandani na nikaanza kuelea hewani huku Olivia naye akianza kunifwata sehemu niliyo simama hewani huku akinitazama kwa macho yake yaliyo anza kubadilika badilika rangi na kutawaliwa na rangi za kila aina.
Akanishika mkono wangu kwa kiganja chake cha baridi kisha akanisogeza karibu yake
“NAHITAJI SIRI HII UITUNZE NA USIMWAMBIE BINADAMU WA AINA YOYOTE NA LAITI UKID-HUBUTU KUMWAMBIA MWANADAMU KUWA UMEKUTANA NA MIMI NITAITOA ROHO YAKO UMENIELEWA……?”
“Ndi….ooo”
“Na kingine nitahitaji uwe rafiki yangu”
“Siwez….”
Kabla hata sijaimaliza sentensi yangu nikajikuta akinisukuma na kunikandamiza ukutani huku mkono wake akiwa umenikaba kwenye koo lango na nikaanza kuhisi roho yangu ikitaka kunitoka kwani ananguvu nyingi na kingine kinachozidi kuniogopesha ni maco yake kaunza kuwaka moto huku akitokwa na machozi ya damu
“Katika maisha yangu haijawahi binadamu wa aina yoyote kunikataa”
Olvia Hitler alizungumza na sauti nzinto iliyo nifanya nizidi kuogopa,kisha akaniachia na nibaki nikiwa nina elea elea angani.Sura yake ikarudi katika hali yake ya kawaida huku akiwa ananita-zama kwa tabasamu zuri
“Eddy narudia tena kuzungumza mimi sio kiumbe mbaya wa kuwadhuru wanadamu ila ninau-wezo wa kumdhuru yule tu anaye hitaji mimi nimfanyie hivyo……Nahitaji kukufanya kuwa mtu maarufu na anaye fahamika sana Tanzania na Duniani kwa ujumla”
“Ki…v…ipi?”
“Sawali zuri,kwanza unatakiwa usiniogope.Pili unatakiwa kufwata zile amri zangu nitakazo kupa na nilizo kupa……Natambua sana moyo wako unampenda Rahma japo huyo mwnamke mchafu anakufanya ummsaliti…..Kutokana hukuwa unajua ni kitu gani kinachoendelea kwa leo nitakusamehe ila kwa sharti moja tu nahitaji ummuamshe huyo mwanamke na aende zake kwake wakati huu kisha ndio nitaendelea na mazungumzo na wewe”
“Sa..sawaa”
Nilizungumza kwa kigugumizi kisha taratibu akanirudisha kitandani na gafla akapotea na hali ya chumba ikarudi kama kawaida na nikajikuta nimekaa kitandani huku shuka likiwa limenifunika kuanzia miguuni hadi kwenye kiunoni,Nikamtazama Halda mwenzangu hana hata analo lijua ndio kwanza ananazidi kukoroma kiasi kwamba nikaanza kujipa moyo labda inaweza ikawa ndoto.
Nikaanza kumtingisha Halda huku nikiliita jina lake hadi akaamka na kukaa kama nilivyo kaa mimi huku akipiga miyayo ya usingizi
“Nakuomba uvae uende kwako”
“Eddy”
“Wewe ninakuomba uvae uende kwako sasa hivi”
“Eddy umechanganyikiwa?”
“Sijachanganyikiwa nina akili zangu ni nzima kama unavyo niona ila nakuomba tuu uvae na uenda kwako kama kulala tutalala siku nyingine”
“Eddy kama unaota nakuomba uniache mimi nilale shughuli uliyo nipa ni kubwa sawa mpenzi wangu”
Halda alizungumza huku ikijilaza tena kitandani na kunifanya nimuamshe kwa nguvu hadi akaanza kukasirika
“Eddy saa tisa yote hii unataka mimi niende wapi mwanaume gai huna huruma au unataka usiku huu nikabakwe huko barabarani?”
“Kama utabakwa ukiwa ndani ya gari basi ila ninacho taka mimi vaa nguo zako uende zako kwako sitaki matatizo na mpenzi wangu”
“Eddy siondoki”
“Kumbuka upo kwangu?”
“Hata kama ila siondoki lije WINCHI,TREKTA au KATAPILA haliwezi kuning’oa hapa kitandani na wala siondoki”
“Hilda unanijua tena vizuri? Sihitaji nikubamize ndio uondoke”
“Eddy nipige,nikate kate,nivunje vunje,nisage sage ila mimi siondoki NG’OO”
Nikazidi kuchanganyikiwa kwani Halda hakutaka kabisa kusikia kitu kinacho itwa kuondoka ikanilazimu kushuka kitandani na kujifaunga taulo langu na kumbukumbu ya maji aliypo nipa bibi ikanijia kichwani nikakaumbuka nimeyaweka jikoni
“Unakwenda wapi sasa?”
“Wewe lala kama hutaki kuondoka niache”
“Sasa Eddy huko nje usiku huu unapo kwenda untaka kwenda kufanyaje?”
“Kwani nimekuambia ninakwenda nje hembu lala huko”
“Nakufwata”
Halda akanyanyuka kitandani huku akiwa ameijifunga shuka na kuanza kunifwata jikoni ninapo elekea,Nikaikuta chupa ya maji katika sehemu niliyo iweka kaisha taratibu nikayatoa kwenye kifuko cheusi nilipo kuwa nimeyaweka
“Sasa hayo maji ni ya kazi gani?’
“Hilda hembu niache wewe rudi chumbani kalale”
“Mmmm haya mwaya kama ndio uchawi wa kwenu kunywa maji ya Dasani usiku wa manae”
Halda alizungumza huku akirudi zake chumbani kwangu,nikamchungulia na kuona tayari ameingia ndani kwangu na kuufunga mlango.
Nikapiga hatua za kwenda nje nikashika kitasa cha mlango na kufungua.Moyo ukanipasuka kiasi kwamba nikajikuta natamani kuzirai kwanik eneo zima la nje ya nyumba yangu nikakuta ni bahari tena yenye maji mengi huku Olvian Hitler akiwa amekaa kwenye kiti cha dhahabu huku pembeni yake kukiwa na wasichana wawili wanao mpepea kwa mikia ya Simba iliyo tengenezwa vizuri huku wakiwa juu ya maji
“Eddy nashindwa kuamini kama mwanamke huyo umeshindwa kumtoa ndani kwako”
Nikageuka nyuma ili nifungue mlango na kustuka baada ya kuukuta mti mkubwa nyuma yangu na urefu wake hauishi katika kutazamika kuelekea juu huku mimi nikiwa nimesimama juu ya mzizi mkubwa na mpana
“Eddy wala usiogope hapo ulipo ni sehemu salama na hauwezi kuudhurika”
“Hivi lengo lako haswa wewe ni nini?”
“Lengo langu ni wewe kuweza kukubaliana na mimi kuwa miononi mwa rafiki zangu nitakao wafanya kuwa watu wenye dhamani sana duniani”
“Kwa staily hii unadhani mimi kweli nitakubali?”
Nilizungumza kwa kujiamini kwani tayari nilisha anza kumzoea Olvia Hitler ila kitu kinacho ni-ogopesha ni bahari kuwepo nje ya nyumba yangu
“Eddy natambua kuwa katika maisha yako umeweza kupitia mambo mengi ya kusikitisha na yaliyo jenga makovu makubwa makubwa katika moyo wako na maisha yako kwa ujumla.Uliweza kuwapoteza wazazi wako katika mazingira ya kutatanisha pili ukaweza kumpoteza mdogo wako mbele ya macho yako kwa kubakwa na watu usio wajua ila cha kustaajabisha watu hao hadi sasa hivi wapo na wanaishi maisha ya amani na furaha bila ya serikali kuwachulia sheria ya aina yoyote.Tatu umekuwa ni mwanaume wa kuomba omba na kusaidiwa na mwanamke amabye kwako bado hujampa dhamani kama anayo kupa yeye.”
“SASA HAYO YOTE YAMETOKA WAPI NAKUOMBA UNIACHE NA MAISHA YANGU”
Olvia Hitler akacheka kwa sauti ya juu na kufanya majani ya mti kuanza kupeperuka huku mengi yakiniangukia kichwani
“Hembu kwanza tupa hicho kijichupa chako ulicho kishika.Usidhani kuwa unaweza kunizuia kwa maji hayo ulio pewa na binadamu mwenye uwezo mdogo sna”
“Mimi mbona sikuelewi wewe?”
“Utanielewa….Wewe ni mwalimu wa masomo ya science ila ninakuomba kuanzia muda utakapo rudi kazini uende ukafundishe somo la Historia na nitakupa kitu kizuri utakacho weza kufundisha na utakuwa mwanadamu wa kwanza kufundisha kile kitu nitakacho kufundisha mimi”
Gafla Olvia Hitler akapotena na watu wake na kujikuta nimesimama nje ya mlango wa nyumba yangu na kichupa changu kikiwa mkononi huku mwili wangu ukinitetemeka kwa hofu
“Hayo maji ndio umeamua kuja kuyanywea huku nje?”
Sauti ya Hilda ikanistua na kunifanya nigeuke nyuma kwa haraka na kumkuta amesimama huku ameshika kiuno kwa mikono yeke miwili.
Nikajikuta ninataka kuzungumza nilicho kiona ila kinywa changu kikashindwa kufumbuka na kujikuta nikirudi ndani huku Halda akiiufunga mlango na kunifwata nyuma.
Nikajutupa kitandani na kuanza kufikiria yaliyo mengi huku jacho likinimwagika na kujikuta nikianza kujutia ni kwanini niliamua kuhama uswahilini kwangu
“Eddy mbona jasho linakumwagika unaumwa?”
“Hapana?”
“Mmmm wewe mwanaume una matatizo hembu niambei una tatizo gani mpenzi”
“Hapana sina tatizo”
“Basi nyanyuka uende ukaoge”
“Ahhh henbu ligeuzie hilo feni upande wangu”
Hilda akafanya kama nilivyo muagiza kisha taratibu feni likaaanza kunipepea huku naye akiwa na kazi ya kunifuta jasho linalo nitoka mithili ya mtu aliye toka kukimbia mbio ndufu.Usingizi mzito ukanipitia na kulala fofofo,Halda akaja kuniamsha asubuhi
“Eddy chai tayari”
“Ok nakuja”
“Amka basi tukanywe wote kwani itapoa”
“Sawa tangulia ninakuja”
Nikajinyanyua kiuvivu vivu kisha nikaingia bafuni nikapiga mswakii na kuoga na kurudi chum-bani na kuvaa nguo kwa ajili ya kwenda kazina kwani hata hamu ya kukaa ndani ya nyumba niliyo hamia tayari ilishaanza kunipote
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni