Notifications
  • MY DIARY (45)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TANOTULIPOISHIA...Ndio niliona hipo haja ya kuokoka na kuishi maisha ya utakatifu kwa maana nishaishi maisha yote ya kuwa mbali na mungu. Nakumbuka nilipokuwa mdogo kipindi hicho naujua mlango wa kanisani tuisahawahi kufundishwa kuwa mtetezi wa kweli wa maisha ya mwanadamu ni Mungu.Na siku zote alaaniwe mtu yule amtegemeaye mwanadamu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Sio kazi ya…
  • MY DIARY (44)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA NNETULIPOISHIA...Yani alianza kutaka uhusiano na mimi tena uhusinao wa mapenzi.Mda wote alikuwa akiniganda kama luba.Na mimi nilikuwa mjanja sana maana nilijifanya sinywi pombe wala kuvuta sigara.Pia baada ya kugundua kuwa wahusika wengine walikuwa wanajiachia niliamua kujifanya mshauri wa mapenzi na mahusiano.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilikuwa nawasshauri sana mshiriki wa…
  • MY DIARY (43)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TATUTULIPOISHIA...Wakati nabadilisha staili kwa kukichua kile kifaa na kukiweka vizuri huku nikibinya ile switch hili iongeze spidi Mark aliingia. Ni kweli nilimuona ila sasa sikuwa na jinsi ilibidi nimalizie furaha hiyo ya uwongo uwongo. Yaani wazungu jamani sijui walifikiria nini maana kile kifaa ukikiminya kwa juu kinakuwa kinajizungusha chenyewe.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (42)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA MBILITULIPOISHIA...Uzalendo ulinishinda ikabidi nimuulize ni kwanini bado wanatumia njia hiyo ya kizamani kutunza kumbukumbu wakati siku hizi kuna kitu kinachoitwa Human Resource Informaion system ambapo kumbukumbu zote za wafanyakazi kama waliochishwa kazi, wagonjwa, walioenda likizo ,waliopandishwa vyeo na taarifa nyingine muhimu uhifadhiwa kwa kutumia komputa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (41)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA MOJATULIPOISHIA...Mark anashangaazwa sana na mwanamke huyo lakini kwa kuwa shida yake ilikuwa ni hela anaamua kuachana nae na kuanza maisha mapya hapo jijiini Dar es salaamMaisha yanaendela lakini Mark amekuwa tajiri na mtu mwenye mafanikio sana kiuchumi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Pamoja na mafanikio hayo ni mtu ambaye mapenzi bado yalikuwa yakimuumiza siku hadi siku.Filamu…
  • MY DIARY (40)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINITULIPOISHIA...Alikuwa akinyata kwa kweli. Kweli hata mimi nilimkubali tu siku ya kwanza ingawa bado nilikuwa sijajua ufanisi wake wa kazi.Nilikaa nae hapo kwangu kwa mda wa siki tatu huku asubuhi tukiamka na kuendelea na kazi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Ndani ya mda huo nikagundua kuwa alikuwa na uzorfu mkubwasana hivyo kazi hiyo alikuwa akiimudu kabisa.Hapo sasa nilimkubali sana…
  • MY DIARY (39)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TISATULIPOISHIA...Nilikuwa na furaha sana huku nikiamini kuwa ndoto zangu za kuja kuwa mtu maarufu zinaweza kufanikiwa hata kabla ya kuyapata yale madini. Sikutaka mbwembwe niliamua kuikopi na kuipesti hiyo stori kama ilivyo na kuifowadi kwa Mark.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baada ya kama lisaa hivi Mark alipiga na kuniuliza kama kweli ilikuwa nai mimi nimetunga hiyo…
  • MY DIARY (38)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Usiku nilishituka usingizini baada ya mbu kuning’aata na kunisumbua sana. Niliwachukia sana hao mbu kwa sababu walinikatisha ndoto yangu ambayo nilikuwa nikiota.Ndoto ilikuwa ikielezea jinsi harusi yangu na Mark itakavyokuwa. Ndoto ilikuwa tamu sana maana ilinipa taswira ya picha halisi ya maisha yangu ya mbeleni.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilishusha neti…
  • MY DIARY (37)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SABATULIPOISHIA...Hapo alitulia tulii kama mtu aliyeaamia dunia ingine. Kimoyo moyo nikawa najisemeha kama amehamia dunia ingine na kuanza kuwaza ujinga sahuri yake mimi nipo kazini bwana acha nitafute hela. Ndio ni lazima nifanye kazi kwa utaalamu na utundu wa hali ya juu ili waendelee kusimuliana huko mjini ili niendelee kupata hela.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Wewe…
  • MY DIARY (36)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SITATULIPOISHIA...Sasa wewe fikiria mimi niliyeletewa zawadi sikujua ni zawadi gani lakini yeye tayari alishafungua na kuchungulia na kujua nini kilifungwa huko ndani.Basi nikaendelea kumuhudumia yule mama huku na yeye akiniambia kuwa itabidi nikimmaliza hizo zawadi tusifungue hapo hapo na waniimbie wimbo wa happybirthday.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Tuliendelea na stori mbili…

TANGA RAHA (35)

SEHEMU YA THELATHINI NA TANO
ILIPOISHIA...
Akiiunyanyua mkono wake mmoja wa kushoto huku akiyafumbua fumbua macho yake na nikazisikia sauti za watu wakija karibia na mlango na kunifanya nikimbilie bafuni na nikajifuta maji usoni na kukitoa kichupa cha dawa na kujipaka usoni na kusubiri kwa muda
SASA ENDELEA...
Nikamuona Hilda akiingia bafuni na kwa haraka akaanza kuzishusha nguo zake na kujisaidia haja ndogo na akageuka sehemu niliyo mimi na akaupitisha mkono wake katikati ya miguu yangu na kuchana kipande kaidogo cha toilet paper na kujifuta sehemu zake za siri kisha akajiweka sawa na kutoka na nikaamini hajaniona.

Nikapiga hatua hadi chumbani na kumkuta Rahma akifumbua fumba mdomo wake huku akiliita jina langu na kumfanya Hilda na msichana mwengine niluye muona wakibaki wakishangaa huku sura zao zikiwa zimejaa tabasamu.

Hilda akanyanyuka kwa haraka akaungua mlango na kusikia sauti akimuita baba Rahma na baada ya muda wakaingia wazazi wa Rahma wakiwa na polisi na Rahma alipo muona baba yake akaanza kuatokwa na machozi
Watu wote ndani ya chumba hawakuweza kuniona kiasi kwamba nikazidi kujiamini uendelea kukaa ndani ya hichi chumba
“Baba”
Rahma aliita kwa sauti ya upole na yaunyenyekevu
“Naam wamwanangu”
“Yupo wapi Eddy wangu?”

Swali la Rahma likawafanya watu wote kutazamana na kukaa kimya pasipo kujibu kitu cha aina yoyote
“Huyo Eddy ni nani?”

Askari mmoja aliiuliza huku akionekana ni mkubwa kwa cheo hii ni kutokana na mavazi yake aliyo yavaa kutawaliwa na vyeo vingi vya kijeshi na kuwafanya ndugu wa Rahma pamoja na wazazi wake kutazamana tazama pasipo kuwa jibu.

Gafla nikastukia shangazi wa Rahma akinishika mkono huku akinikonyeza akiashiria nijikaushe kama nilivyo na akatoa simu yake mfukoni na kuandika baadhi ya maneno na kuiweka mbele yangu na nikayasoma
{NIMEKUONA MIMI PEKE YANGU JIKAUSHE HILI SWALA LIPITE NDIO TUTAJUA MIMI NA WEWE}

Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbioa kiasi kwamba nikahisi nimeingia tena mikononi mwa familia hii makatili
“Wee mama hembu hiyo simu yako”
Askari mmoja akaichukua simu ya shangazi wa Rahma na kuusoma ujumbe kwa sauti ya kichini chini.
“Huyo uliye muona ni nina?”

Watu wote wakamgeukia shangazi wa Rahama na akaniachia mkono kwa haraka na kutingisha kichwa akimaanisha kuwa hukuna kitu
“ILA BABA KWANINI UMUUE EDDY WANGU?”

Swali la Rahma likawafanya watu wote kumtazama na nikaanza kuziona sura za askari zikianza kubadilika na kuweka mikunjo askari wawili wakaziweka bunduki zao sawa kuzielekeza kwa baba Rahma huku mkuu wao akipiga hatua hadi kitandani na kumuuliza Rahma swali
“Unasema kuwa Eddy ameuliwa na baba yako?”
‘NDIO”

Chumba kizima kikatawaliwa kwa ukimya kiasi kwamba kila mmoja macho yake yakamgeukia baba Rahma
“Huyo Eddy kwako alikuwa ni nani?”
“Ni mpenzi wangu ninaye mpenda sana”

Nikanyata taratibu huku shangazi Rahma akiwa anaendelea kuwaomba askari waweze kuzun-gumza juu ya swala alilo lizungumza.

Nikashuka kwenye ngazi za gorofa lao na nikatoka nje na moa kwa moja nikeelekea nje na safari ya nyumbani kwangu ikaanza.

Moyoni mwangu nikaanza kuhisi hizto na wa ushindi mkubwa kwani swala la kuingia nyumbani kwa kina Rahma pasipo wazazi wake kufahamu na nimtu mmoja ndio amelitamvua hilo kidogo likanipa faraja ya kuweza kumtorosha,nikanawa sura yangu na nikarudi katikahali yangu ya kawaida

Siku nzima nikajifungia ndani na sikutoka nje huku nikiwa ninapanga mipango ya kumtorosha Rahma katika hali ya kawadi,Picha nyingi nilizo zichora kwenye karatasi nyeupe zikiwa kama ramani ya nyumba ya baa 

Rahma zinakanitosha zaidi kujua kuwa ninaanzia wapi katika kufanikisha swala la kumtorosha Rahma hadi nikajikuta ninapitiwa na usingizi katika kocho nililo kalia.Asubuhi na mapema nikaelekea nyumba ya pili kwa mzee 

Mmoja ambaye na mstaafu wa jeshi na kipindi cha nyuma aliniomba niweze kumfundisha mwanaye wa kiume masomo ya kumbo yake ya PCM na kwa bahati mbaya sikuweza kupata muda huo kutokana na matatizo

Nikagonga geti lake nalikafunguliwa na mlinzi na akaniruhusu kuingia ndani na kwabahati nzuri nikakutana na mzee 

Ngoda akifanya mazoezi kwenye moja ya bustani yake na nikamfwata hadi sehemu alipo na kumsalimia
“Vipi Eddy kuna siku nilisikia sikia kelele huko kwako ila kutokana nilikuwa ninawageni muhi-mu sana nikashindwa kutoka”
“Mzee wee acha tuu kuna mambo mengi yalinikumba hivi vijiwiki kadhaa vya nyuma nikajikuta hata ninashindwa kutimiza ile ahadi ya kumfundisha mwano”
“Mambo gani kwa maana nilipo kuja kuchungulia sikukuta mmtu zaidi ya ukimya mwingi?”

Nikaanza kumsimulia mzee Ngoda kuanzia mwanzo hadi mwishio kuhusiana na mkasa wa Rahma hadi ninamaliza akabaki akisikitika huku akishusha pumzi nyingi mara kwa mara
“Duuu sasa wewe unataka nikusaidie nini juu ya hilo swal lako?”
“Mimi ninataka unisaidie juu ya mipango na mbinu za kijeshi ili niweze kwenda kumtorosha yule binti”
“Hjui hilo ni kosa la jinai na kama ukikamatwa hapo unachukuliwa kuwa kama gaidi na kifungo chake nina imani unakijua”
“Ndio ninakutambua mzee wangu ila naomba tuu unisaidie”
“Wee koma wenyewe wanasema uzee mwisho msata kila mtu mjini ni baby”

Nikajikuta nikangua kicheko kwani sikutegemea kama mzee ataweza kuniropokea maneno ya namna hii ukilinganisha na umri wake.
“Eddy mimi kama mimi kwenye hilo sinto weza kukusaidia labda kuna jengine useme nitakusaidia kwa maana nitakuwa nimevunja sheria na kanuni za jamuhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na sheria za jeshi.”

Mzee Ngoda akanikatalia kata kata na sikuwa na kingine cha kuzungumza zaidi ya kuondoka zangu na kurudi nyumbani kwangu.

Nikajipikia kifungua kinywa na baada ya kumaliza kupata chai nikaelekea kwenye maduka ya wachaga yaliyopo barabara za namba na kazi yangu ikawa ni kutafuta ni nguo gani ninaweza kuzinunua na kuzivaa na zikabadilisha muonekano wangu kabisa.

Hadi mwisho wa mizunguko yangu nikajikuta nikinunua overol jeusi pamoja na kofia kubwa na kurudi nyumani kwangu mida ya saa kumi na moja jioni.Nikapanda kitandani na kulala huku saa yangu ya mkononi niiitega muito wa kunistua saa nne usiku.

Kama nilivyo itega saa yangu ndivyo ilivyo niamsha nikanyanyuka kitandani na kuingia bafuni na kunawa uso ili kutoa uchovu kisha nikarudi ndani na kuvaa overoli langu na pamoja na ko-fia,Nikatafuta mabuti yangu ya mvua kisha nikavaa,nikazichukua karatasi nilizo chora ramani ya nyumba ya kina Rahma na kuanza kuipitia moja baada ya nyingine.

Nikachukua beki langu dogo na lenye vijimikanda vyembaba na kulivaa mgongoni huku likiwa ni vifaa kama koleo,bisibisi na nyundo

Kabla sijafungua geti langu nikasikia likigongwa taratibu na kunifanya nistuke,likarudiwa ku-gongwa na taratibu nikapiga hatua za taratibu huku nikiwa na tahadhari kubwa na nikacjungulia nikaona gari aina ya ‘geap’ lililo kibanda wazi na ni kama magari ya jeshi likiwa limesimama nje ya geti langu.

Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio ila nikapata ujasiri wa kufungua geti na kumkuta mzee ngoda akiwa amevalia nguo za jeshi huku mkononi mwake akiwa ameshika begi la wastani
“Eddy ndio umevaa nini hivyo?”
“Ehee ndio mavazi ninayokwenda kumuokoa mpenzi wangu”
“Kijana hembu acha uzembe tuingie ndani”

Tukarudi ndani na geti tukalifunga kisha tukaingia sebleni na akalifungua begi lake na akatoa nguo za jeshi na kunirushia
“Kamata hizo uangalie kama zinaweza kukutosha”

Nikaanza kuzitazama moja baada ya nyingine na nikalivua overoli langu na kuva nguo alizo nipa mzee ngoda na kwabahati nzuri zikawa zinanitosha vizuri kuanzi suruali hadi shati la juu.

Pia akanikabidhi viata vya jeshi japo vinanibada kidogo ila vimekaa vizuri mguuni mwan-gu,akanikabidhi begi nilibebe na nikaona kamba pamoja vifaa vingine ambavyo sikujua matumizi yeke ni nini
“Unaweza kutumia bunduki ya aina yoyote au ulisha zoea manati za uwindaji wa ndege huko kwenu Morogoro?”
“Ahaaaa sijawahi mzee wangu”
“Eddy hilo jina lako la mzee silipendi”
“Hhaaaa haya baba”
“Hapo kidogo sawa na mtu unapokuwa umevaa hizo nguo niite kamanda”
“Ndio kamanda”
“Ahaa hapa kuna hiizi bastola tatu nimekuja nazo moja inatumia risasi baridi na hizi mbili zina-tumia risasi moto….Hii ya risasi baridi itakulazimu ukae nayo wewe na hizi nyingine nitakaa na-zo mimi sawa”
“Sawa kamanda..je nikitaka kufyayua risasi ninafaje?”
“Unashika hapa na unaparudisha nyuma na unakuwa risasi umeipandisha kwenye chemba na ukiminya hapa unairuhusu kuchomoka kuelekea kule ulipo iagiza kwenda”
“Sawa nimekuelewa kamanda”
“Vaa kofia yako na ninaomba hizo karatasi unazosema umechora ramani ya hiyo nyumba”

Nikamkabidhi karatasi zote na akaanza kuzipitia moja baada ya nyingine hadi akazimaliza zote
“Kumbe wewe ni mtaalamu mzuri wa kuchora ramani?”
“Ehee kidogo kidogo ninajaribu”
“Ina bidi nikupeleke kambini wakakuajiri kwa kazi hii kwa maana wa taalamu kama nyinyi ni wachache sana”
“Ukiachilia kuchora ramani hata kuchora watu au vitu Mungu amenibariki sana kwenye hilo”
“Ahaa wewe utalifaa jeshi ngoja kwanza twende nikakuone ufanisi wako wa leo”

Tukatoka nje na kuingia ndani ya gari na nikawa na kazi ya kumuelekeza ni wapi tunapaswa kufika na ndani ya dakika kadhaa tukawa tumefika nje ya jumba kuwa la kina Rahma.

Mzee Ngoda akashuka na kuniacha mimi ndani ya gari na akaanza kulichunguza vizuri na akaingia ndani ya gari tukaondoka na gari tukaenda kuisimamisha kwa mbali kidogo na tukarudi hadi ilipo nyumba ya kina Rahma kisha akiitoa bastola yeke na kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti kisha akaniomba nikae nyuma yeke nimfwate kila anapo pita.

Cha kushangaza sikujua hata uogoa nimeutoa wapi kwani nikajikuta mwili mzima ukinitetemeka kiasi kwamba hata kutembea kwenyewe nikawa ninayumba nyumba.

Tukafika kwenye ukuta mrefu kidogo na nikamshangaa mzee Ngoda akijirusha juu na kuishika sehemu ya juu japo ni mfupi ila mwenzangu ameweza kufanya hivyo

Kazi ikaanza kuwa kwangu kila nilipo karibu kujirusha kupafikia nikawa ninashindwa na kui-shia kuburuzika ukurani
“Sikia wewe ukitaka kuruka hakikisha mguu wako wa kulia unakanyaga ukuta na kujirusha juu sawa”
“Sawa”

Nilijibu kama nimeelewa vile wakati sikujua hata nifanye nini,Nikajaribu kujirusha mara kadhaa hadi nikafanikiwa ila mikono yangu ikijaa michubuko mingi.

Mzee Ngoda akawa wa kwanza kuingia ndani na mimi nikafwatia na sehemu tuliyo shuka ina maua mengi na taratibu tukajificha kwenye maua
“Mkango wa kuingilia upo wapi?”
“Kwa mbele”
“Kuwa makini na kuna walinzi wangapi?”
“Mmmm wala sifahamu”

Tukaanza kwenda kwa mwendo wa tahadhari huku mimi mara kwa mara nikitazama nyuma na tukafanikiwa kuingia hadi sebleni na kuwakuta watoto wadogo wakitazama filamu za kumi kwenye Tv kubwa humu sebleni.

Tukapiga hatua za kimya kimya hadi sehemu waliyo kaa na walipo tuona mmoja akajaribu kupiga kelele ila Mzee Ngoda akamzaba kofi zito hadi mtoto wa watu akazimia na wengine walio ona hivyo hakuna aliye dhubutu kufungua kinywa chake

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

18 Simulizi Tanga Raha
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni