HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (17)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA KUMI NA SABA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Amatagaimba kabla ya kuondoka akachukua maji kutoka kwa Seidon na kumpa Anna, akayanywa kwa fujo na kuyamaliza. Nguvu zikamrejea. Anna akapanda juu ya farasi na Amatagaimba akatua nyuma yake, safari ikaanza.
TUENDELEE...
Seidon akapiga mbio kwa ustadi akipita vijilima vilivyo ndani yake, “Amatagaimba, Sherhazad na Wafuasi wake wamezingira eneo lote!” akamwambia.
“Sasa tunafanyeje, inatubidi kutoka nje?” Amatagaimba akauliza.
“Hapana, hatutoki nje kwani fuvu limedondokea humu ndani na tukilipata tu mlango wa kuifikia Klakos uko hukohuko chini,” akamjibu huku akimchochea farasi yule kusonga mbele, mote walimopita mlikuwa giza tupu, mara ghafla yule farasi akapiga ukelele na kupoteza muelekeo, akajipigiza katika jiwe na wote watatu wakaanguka chini. Yule farsi alilala chini kimya, Amatagaimba akachomoa nyoka kutoka usawa wa kifua cha farasi, akamshika mkononi, yule nyoka alikuwa ametumbukia kichwa ndani ya mwili wa huyo farasi. Akamsika mkia na kichwa akamvutaq kwa nguvu yule nyoka akakamaa kama mshale, Amatagaimba akautoa uta wake na kumpachika yule nyoka kisha akauvuta na kuufyatua gizani. Kitendo kile kilimuudhi sana Sherhazad ambaye alikuwa akitazama kila tukio kupitia dirisha lake la ajabu.
§§§§§
“Ni nani huyu anayeniuzi? Ana nguvu gani za kunifanya mimi mjinga, nilishamdhibiti sasa katoka vipi? Enyi Wachawi wa Soria, wazuieni njia, nataka sasa niende mwenyewe kwani fuvu lkile liko jirani kabisa na Klakosi, sasa hivi wanaweza kulirudisha, name sintokubali walirudishe,” Sherhazad alipiga kelele, akatoka dirishani na kuliendea joho lake kubwa la kung’aa, akakwea farasi wake wa kijini mwenye uwezo wa kupita angani, “Sasa sintotuma kivuli changu tena ila nakuja mwenyewe, naona mlipofika ni pabaya,”
Sherhazad aliondoka kwa kasi kuelekea Hamunaptra, ilimchukua nukta kadhaa tu kufika katika mji huo, mji wa kale, mji ambao kwa macho ya kibinaadamu hauonekani kwa kuwa umepotea. Hasira zilimtawala Sherhazad, alikuwa akipiga mbio zisizo za kawaida na farasi wake, akitaka kuwahi kabla Seidon na Amatagaimba hawajaingia mle shimoni ambako huko ndiko kwenye njia ya kuifikia Klakos. Kwa kuwa hakuweza kuipita Ikweta, ilimbidi azunguke njia ndefu ambayo ingemtolea upande wa pili wa mji huo, huko angeweza kuingia kiurahisi zaidi.
“Angusha tufani kubwa ya mvua yam awe ndani ya shimo hilo,” akasema huku akiwa mwendo wa kasi juu ya farasi wake. Wale wachawi wake walisikia ombi lake na kuanza kufanya linalowezekana. Sherhazad alikasirishwa na jibu la wale wachawi kuwa imeshindikana kuteremsha tufani katika shimo ile.
“Nini, nini kimewashinda enyi wachawi Wapumbavu?” akawauliza kwa kuongea nao kwa hisia tu mawazoni mwao.
Akajibiwa kuwa ndani ya shimo hilo kuna nguvu kubwa ambayo ipo kinyume na wao, ndiyo inayokinga yote hayo.
“Shiit! Nikimpata huyu kijana namla nyama,” akajisemea huku akiendela na safari yake. Mbele yake alikabiriwa na bonde kubwa, kwa akili yake ya haraka akakumbuka kuwa bonde lile ni mto mkubwa wa maji ambao umekauka miaka mingi, karne na karne. Na alijua wazi kuwa mto ule ulikuwa ukiingia moja kwa moja chini ya mapiramid na kutokea kwenye kiti cha Klakos.
Nitapita hapa, nitatokea moja kwa moja kwa Klakos, alijisemea na kumwamuru farasi wake aliyekuwa angani kulipita bonde hilo abadili njia na kurudi chini.
§§§§§
Wakati wale wachawi walipokuwa wakijaribu kuumba mvua yam awe ili kuwanyima njia Seidon na Amatagaimba, ndani ya shimo lile kubwa nako kulikuwa na jambo lingine, Amatagaimba akiwa na ile pete yake ya ajabu alikuwa akiomba iwafikishe salama waendako kwani ni kitambo kidogo tu kilichobakia wao kufika chini katika lile shimo.
Kishindo kikubwa kikasikika na vumbi la wastani likatimka. Amatagaimba, Seidon na Anna Davis walidondoka katika udongo laini, chini ya shimo hilo lenye giza. Seidon aliamka haraka bila kujali maumivu aliyoyapata akaamua kuliwahi fuvu ambalo lilikuwa mahala hapo, alipoweka mkono tu kulinyanyua, akaona kitu kama upanga kinatua karibu na kiganja chake cha mkono, akawahi kuutoa, akatazama juu akamwona mwanamke mrefu mweupe mwenye nywele nyingi, nguo yake iliyofunikwa na joho kubwa ilikuiwa ikimetameta na kuyafanya macho ya Seidon yashindwe kuona sawasawa.
“Amatagaimbaaaa!!!!” Seidon akaitwa kwa nguvu huku mikono yake ikiziba macho yake. Amatagaimba akashtuka na kumtazama Seidon aliyekuwa kajiinami ilhali lile fuvu limesogea mbali kidogo.
“Seidon, Seidon!” akaitwa na kunyanyuka haraka kisha akamwendea Seidon lakini kabla hajamfiki, alihisi kama jiwe zito limempiga kifuani akatupwa upande wa pili na kujibamiza ukutani. Mara tu baada ya kujibamiza ukutani kishindo cha ajabu kikasikika, na ule ukuta ukapasuka katikati, radi kali iliyokata ule ukuta ilitisha na mwanga mkali kutoka ndani ya ule ukuta ilipenya na kung’aza lile shimo lote. Hakuna aliyeweza kutazama mwanga ule lakini Amatagaimba alihisi kua upande wa pili kulikuwa na kitu kama chumba kikubwa, kilichong’aa kwa dhahabu safi kutokana na miali ya kitu kama jua iliyokuwa ikipenya kupitia matundu Fulani. Hakuelewa sawasawa lakini aliona vitu kama viumbe Fulani vilivyojiinamia katika mtindo wa nusu duara na mbele yao akiwapo mwingine, lakini kwa jinsi miali ile ya mwanga ilivyopishanapishana mle ndani hakupata uhalisia wa kile anachokiona.
“Klakos!” akatamka Seidon, na mara ileile ukatokea mngurumo mkubwa wa kutisha uliofuatana na ardhi kutetemeka. Seidon akajirusha kulichukua lile fuvu, lakini akapambana na upanga mkali wa Sherhazad.
“Tulia Mpiga mbio, huna uwezo wa kulichukua hilo fuvu na wala huwezi kuingia pale kwenye kiti cha enzi cha Cleopas, kabla sijakuua, ulinifanya mimi mjinga ukanihadaa sio?” Sharhazad aliongea huku akimzunguka Seidon aliyekuwa bado pale chini kajiinamia.
“Ewe mwanamke jinni dhalimu, kwa nini hupendi neema za wanadamu ilhali wanadamu hao hao unawatumia katika mambo yako mengi?” Amatagaimba akauliza huku akijiweka sawa, upanga wake ukiwa mkononi.
“Kelele! Ewe kiumbe wa dunia, kwanza umeingilia vita isiyo yako na kwa hilo utaijutia nafsi yako,” Sharahazad akamwambia Amatagaimba na wakati huo akijibizana na Amatagaimba, Seudon alijinyanyua kwa haraka na kujirusha sarakasi akalikamata lile fuvu na kutaka kumpiga chenga Sherhazad, lakini lo, jinni ni jinni tu, Seidon aliona taswira nyingi za Sherhazad ndani ya lile shimo akashindwa kujua hasa yupi ni yupi.
Amatagaimba akavuta hatu na kujirusha kumkabili Sherhazad, panga zao zikakutana hewani, wote wawili wakashuka chini na kutua kwa miguu yao. Sherhazad alitumia nguvu zote kumsukuma Amatagaimba ili apate nafasi ya kufanya shambulizi, lakini Amatagaimba alitulia palepale hakusogea hata milimita moja. Nguvu mbili zilizshindana, sherhazad akaingalia pete ya Amatagaimba, pete inayompa jeuri, akautoa upanga wake ghafla na kujizungusha kwa umahiri mkubwa. Amatagaimba akaitambua hila yake, akainama na Sherhazad akapita juu yake, alaipotua tu, upanga wa Amatagaimba ukapenya mbavu za Sherhazad.
“Aaaaaaaaiiiiiggghhhhh!!!!!” kelele za Sherhazad zikapasua anga, mara kilicho kwenye kuta, paa, nje , ndani ya kaburi kikarudiwa na uhai.
“Aisatuuum, Aisatuuum,” akaongea lugha isiyoeleweka, pale ulipochoma upanga pakawa panatoka moshi wa buluu, Amatagaimba alikuwa bado kashikilia upanga wake palepale na kumfanya Sherhazad asisogee popote, kwani alipochoma ndipo hasa penye uhai wa kiumbe huyo.
Kelele za watu wa kutisha zikaanza kuzikika ndani ya shimo lile. Amatagaimba akaona hapo mambo yataharika wakati tayari wameshafika mwisho. Akauchomoa upanga wake haraka kutoka katika mwili wa Sherhazad.
“Seidoooonnnn!” akaita huku akinyoosha upanga wake kule kwenye ule mlango uliojitokeza katika ukuta, Seidon akaruka na kujitupa upande wa pili kwenye ule mlango lakini hewani alikutana na kifua cha Sherhazad, Seidon akaanguka na kukohoa.
Anna Davis, akarudiwa na fahamu akasimama haraka haraka akiwa anathema kama aliyekimbizwa na mbwa.
Seidon alitambaa huku akiwa na maumivu, na fuvu likiwa mkononi mwake, Sherhazad alijitahidi kumshambulia lakini alijikuta anaishiwa na nguvu, anashindwa, viumbe wake aliowaita kijini nao walijikuta wanakosa nguvu ya kufanya lolote. Amatagaimba akamshika mkono Seidon na Anna, Seidon akajitahidi kunyanyuka na kuvuta hatua taratibu kuuelekea ule mlango.
Sauti za watu waliokuwa kwenye ibada zikaanza kusikika kwa mbali zikitoka ndani ya kile chumba cha Klakos.
Sherhazad akajitahidi kuruka ili amkamate Seidon haikuwezekana, alijikuta anashindwa kufanya lolote. Kila walipozidi kuufikia mlango walijikuta wakipata nguvu na kuanza kukimbiua kuelekea ndani, kelele za watu waliokuwa kama wakishangilia zilisikika. Kufumba na kufumbia, tena waligundua kuwa wanapita hewani nyanyo zao hazigusi ardhi. Punde si punde wakajikuta ndani ya chumba kile tulivu, mvumo wa kitu kama upepo ulikuwa ukisikika taratibu. Jinsi walivyokitazama kile chumba, kilionekana kama mji mkubwa sana, wenye magofu mengi nay a kutisha, masnamu ya wanyama mbalimbali mengine bado yamesimama kwenye nguzo zake na mengine tayari yamekwishaanguka.
Hakukuwa na mmea wenye uhai, yote ilikuwa imekauka kwa ukame uliokithiri. Kwa ujumla ulikuwa mji uliopotea, ukungu ulijaa kila mahali, mvumo wa upepo uliendelea kufanya sauti tamu.
“Hamunaptra!” Amatagaimba akatamka.
Seidon na Anna wakageuka kumtazama, “Hamunaptra?” Anna akauliza.
“Ndiyo, Hamunaptra,” Seidon akaongezea kumjibu Anna kwa ni alionekana kuwa na dukuduku juu ya hilo. Mara baada ya kutaja jina hilo wakasikia sauti hafifu ya kitu kama bembea inayobembea huku na kule na minyororo yake kufanya hiyo sauti kuashiria kuwa ni minyororo mikavu isiyo na kilainishi. Sauti hiyo ilisikika umbali mdogo tu kutoka pale waliposimama. Ukungu mzito uliwafanya wasiweze kuona hata mbele yao kuna nini, kwani hata wao wenyewe walikuwa wakionana kuanzia viunoni kuja juu. Ile sauti ya watu waliokuwa wakifanya ibada iliendelea. Dakika chache baadae walisikia kama mlango ukifunguliwa sehemu Fulani, kisha ukimya ukawakabili.
Ule ukungu uliowazunguka ukaanza kupungua taratibu na wote wakaweza kuona ardhi iliyopo eneo lile, vito vya thamani vya dhahabu, almasi, yaspi, quartz, coral na vingienvingi vilikuwa viking’azwa na mwanga wa jua husio na joto la kuchoma bali la kuburudisha lakini kila walipoangali hawakuliona jua lenyewe isipokuwa mwanga tu.
Mbele yao kulikuwa na kidaraja kidogo sana chini ya kidaraja hicho kulikuwa na mto lakini mto huo uliwashangaza kwani ulionekana kupitisha kitu kama uji wa buluu uliochanganyika na wekundu na weusi, uji huo ulikuwa ukichemka. Nyuma yao wakasikia kishindo cha ajabu, Amatagaimba akageuka na kumwona Sherhazad akija kwa kasi, mkononi mwake amekamata upinde wa ki-jini.
“Tuondokeni haraka!” Amatagaimba aliwaambia Seidon na Anna.
“Tuelekee wapi?” Seidon akauliza huku mkono mmoja ukiwa umemshika Anna na mwingine umekamata lile fuvu.
“Vuka hilo daraja,” Amatagaimba akawaambia.
Seidon akaanza kuliendea lile daraja, lakini kabla hajaanza kulivuka Anna akaponyoka mkononi mwake na kubaki nyuma.
“Anna!” Seidon akaita.
“Naogopa kuvuka, daraja hilo minyororo yake imeoza, tutatumbukia,” kabla hajamaliza kujibu Anna, akajikuta akipigwa kikumbo kikali ambacho kilimsukuma mpaka darajani. Seidon akiwa tayari katikati ya daraja ambalo lilikuwa likinesa vibaya, na minyororo iliyoshika daraja hilo kuanza kushindwa kuhimili uzito, inayoanza kuachia mmoja baada ya mwingine, akamdaka Anna na kukimbia nae kuvuka. Walipokaribia mwisho mnyororo mmoja ukakatika na lile daraja likainama upande mmoja.
“Mamaaaaaaaa!” Anna akapiga kelele na kutereza vibaya, miguu yake ikaliacha daraja, Seidon akawahi kukaza mikono na kumzuia, lakini miguu yake tayari ilikuwa imeacha daraja na sasa ikining’inia chini ya daraja. Anna akalia kwa uchungu sana, akijua kuwa mwisho wake sasa umefika.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni