MY DIARY (2)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: __
SEHEMU YA PILI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Kwa ufupi japo sitaki kueleza historia yake ila kwa sasa ni shoga na teja. Baba yetu alitupenda sana na alihakikisha tunapata elimu nzuri na bora. Mimi na kaka yangu wote tulisoma International school ya hapo Moshi.
TUENDELEE...
Baadaye kaka yangu alianza kuvuta bangi kitu ambacho kilimtia hofu baba yangu na kuamua kumpeleka kusoma nje ya nchi.
Alikosea sana kwani alimpeleka south Afrika katika chuo kimoja maarufu cha mambo ya utalii. Huko aliendelaa na tabia yake ya miadarati na mbaya zaidi alianza kutumia madawa ya kulevya hivyo akawa teja kabisa. Akaenda mbali kabisa na kuwa shoga kabisa, sitaki kukueleza zaidi ya hapo kwani lengo la simulizi hii ni kukupa historia ya maisha yangu. Kama nilivyosema mwanzo familia yetu ni tajiri sana kwani baba yangu alikuwa ni mfanyabiashara maarufu wa madini tena yale ya Tanzanite.
Historia ya baba yangu nayo ni ngumu sana kwani inasemekana chanzo cha yeye kupata utajiri ni ajali ya wazungu iliyotokea huko Mererani hivyo yeye na wenzake waliiba madini mengi sana. Lakini kabla ya hapo alikuwa ni chokoraa asiye na mbele wala nyuma. Kama nilivyosema sitaki kukupa historia ya watu wengine lakini inanibidi ili uweze kujua aina ya familia ninayotoea.
Baba yangu alituambia kuwa yeye alikuwa ni mtoto yatima ambaye baba na mama yake walikufa kwenye ajali mbaya iliyotokea huko Kateshi/mbulu. Hicho ndicho kikawa chanzo cha yeye kuwa chokoraa. Baadaye alikuja Arusha kutafuta maisha ambapo walipelekwa Mererani kama manyoka. Huko aliteseka sana mpaka alipokuwa kijana anayejitambua. Baadaye ndo akapata bahati ya mtende ya kuiba madini.
Tangia hapo akaanza biashara ya kuuza madini na mungu alimjalia sana na baadaye alikuwa anaenda Dubai kuchukua magari.Huko ndipo alipopata bahati ya kukutana na mtoto wa kiharabu ambaye naye alimpata katika hoteli ambayo alikuwa akifikia. Inasemekana msichana huyo alikuwa n imzuri sana kitu ambacho kilimfanya baba yangu atumie gharama kubwa kumpata.
Kwa kuwa binti huyo alikuwa akifanya kazi kwenye hotel hiyo aliyokuwa akifikia hivyo ilikuwa ni rahisi kumwingiza laini. Basi hicho ndo chanzo cha mimi kuzaliwa. Baba yetu alituambia kuwa baada ya mahusiano yao ya mda mrefu na mtoto huyo wa kiarabu huku wakizunguka nchi nyingi na kula raha, baadaye binti huyo aliacha kazi na kuja Tanzania.Baba anasema walipata wakati mgumu sana kwani familia ya binti huyo mrembo alikataa katu katu mwanao kuolewa Afrika na mtu mweusi tena mkristo.
Hivyo basi kutokana na upendo wao wa dhati binti huyo alikubali kutengwa na familia yao na kuja Tanzania n kuishi na baba yangu. Nazani sasa umeanza kupata picha halisi ya uzuri wangu. Huu unene sijui niliupata wapi lakini nahisi ni kwa upande wa baba yangu ambao na wao nasikia walikuwa ni wazuri sana. Hapo ndipo historia ya maisha yangu inapoanzia.
Nimekulia kwenye familia ya kitajiri hali ambayo ilinifanye nisizijue shida mpaka nilipofkisha umri wa kubalehe. Nakumbuka niliwahi sana kubalehe au kuvunja ungo na kipindi hicho nilikuwa standard six(darasa la sita) huko international school mjini Moshi.Basi waswahili husema hujafa hujaumbika na kaka yangu kama nilivyowaeleza alipelekwa nje ya nchi ambapo baada ya miaka mitatu alirudi nchini akiwa katika hali hiyo ya uteja na ushoga.
Kaka yangu huyu alikuwa ni wa mama mwingine ambaye baba alizaa nae kabla ya kukutana na mama yangu.Najua unasubiri kwa hamu na jamu kujua nini kilitokea katika maisha yangu mpaka mimi kuharibikiwa na kuwa malaya, kahaba maarufu ndani na nje ya nchi.Sio mbaya nikaanzia hapa. Ilikuwa ni siku ya
jumapili asubuhi mimi nikiwa likizo nimelala kwenye chumba changu, kipindi hicho najielewa kabisa kwani tayari nilikuwa na umri wa miaka 13 na tayari nilishaanza kusoma sekondari.
Siku hiyo ulitokea ugomvi mkubwa sana baina ya mama yangu na baba yangu.Chanzo kikiwa ni mama ambaye alikuwa akimshinikiza baba waame Tanzania na kwenda kuishi Dubai kwenye moja ya jengo lao la kifahari ambalo walikuwa wamelinunua. Baba alikuwa akikataa kwa madai kuwa asingeweza kuhama Arusha kwani biashara zake zingeyumba sana.
Ugomvi ulikuwa ni mkubwa sana kitu ambacho kilimpelekea mama yangu kuondoka Tanzania na kurudi kwao Dubai.Kiukweli mpaka leo sina uhakika kuwa hiyo ndo ilikuwa sababu ya msingi ya wao kuachana au kulikuwa na kitu kingine nyuma ya pazia.
Tangia siku hiyo sikuwahi kumwona tena mama yangu mpaka leo hii ninapoamua kusimulia historia ya maisha yangu.Tuliendelea kuishi na baba yetu na cha ajabu baba hakutaka kuoa mwanamke mwingine yeyote.Tuliishi vizuri sana na baba yetu ingawa kaka yangu tayari maisha yake yaliharibika na kuugua ukichaa kabisa. Sikushangaa sana kwani tunajua madhara ya madawa ya kulevya.
Lakini kuna kitu kimoja ambacho huwa nakikumbuka sana. Kitu hicho ni kilichosemwa na daktari mmoja wa KCMC ambaye ni bingwa wa saikolojia na magonjwa ya akili. Alitueleza kuwa kaka yangu alikuwa anaugua ugonjwa wa U-SOCIAL huu ni ugonjwa mbaya sana unaosababishwa na mapenzi.Inasemekana kuwa kaka yangu alipokuwa huko chuoni alitokea kumpenda dada mmoja ambaye alikuwa amemzidi mwaka mmoja wa masomo.
Inasemekana pia mapenzi yao yalipita kiasi mpaka wakawa kama ni mwili mmoja. Daktari huyo alitueleza kuwa U-SOCIAL ni ugonjwa hatari sana ambao unafanya watu wengi kuchanganyikiwa na kuwa vichaaa kabisa. Dakatri huyo alisema kuwa huo ni upendo mkubwa sana ambao mtu hawezi kuishi bila ya mwenzie na nakumbuka alitutolea mfano wa nyuki ambao wanakuwa tayari kutoa kizazi chao kwa ajili ya nyuki mmoja ambaye ni malikia.Sijui kama nipo sahihi sana ila mtawauliza wataalam wa ecology.
Basi inasemekana kaka yangu na huyo msichana walifikia hatua hiyo kwani kaka yangu alishawahi kumtolea mpaka figo kuokoa masiha yake. Binti huyo alikuwa anatokea Kampala nchini Uganda na kutokana na hali nzuri ya kiuchumi baiana ya familia zote mbili yaani ya kwao na kwetu penzi lao liliweza kushamiri sana.
Kwa kuwa binti huyo alimtangulia kaka yangu mwaka mmoja wa masomo basi alivyomaliza alirudi nchini kwao Uganda. Hapo ndipo kasheshe ilipoanzia kumbe binti yule alikuwa na mpenzi wake wa mda mrefu na ndiye alimpeleka South Afrika kwa ajili ya masomo. Hivyo alipomaliza tu masomo aliolewa na kibaya zaidi siku ya harusi yake kaka yangu alipewa taarifa na mmoja wa marafiki wa karibu wa msichana huyo.
Kaka yangu akafunga safari mpaka Kampala nchini Uganda kwenye mji mkuu wa nchi hiyo na alifikia Severa Hotel sehemu ambayo shughuli za harusi zilikuwa zikiendelea. Hakuamini macho yake lakini
Sijisifii lakini kiukweli nilikuwa na uwezo mkubwa darasani kitu ambacho kilimfurahisha sana baba yangu na kuwa tayari kuniudumia kwa gharama yeyote ile.
Basi niliendelea kuishi maisha mazuri yale ya kutojua shida, maisha ambayio kila mtu aliyatamani. Nilisoma mpaka nikafika form five hapo ndipo safari yangu ya maisha yalipoanza kuingia doa. Hapa nitasimulia kwa urefu zaidi kwani ndicho chanzo cha mimi kuharibikiwa. Nakumbuka kipindi hicho biashara ya baba zilianza kuyumba, migogoro ya kutokulipa kodi na serikali ilimmalia
Sijui kama ilikuwa ni kweli ni mkwepa kodi au laa lakini nakumbuka baba yangu dakika chache kabla hajafa alinambia kuwa serikali eti imeamua kumfilisi sio kwa sababu eti halipi kodi la hasha bali ni kwa sababu alikuwa na mahusiano wa kimapenzi na msichana mmoja ambaye alikuwa ni kimada wa kigogo mmoja wa serikalini.
Baba alienda mbali sana na kuniambia licha ya kutaka kumfilisi pia walishajaribu mara kibao kumbambikizia kesi ili wamfuge. Nilikuwa simwelewi kwa sababu kila baada ya sentensi mbili alikuwa akinambia “mwanangu dunia sio mbaya bali walimwengu ndio wabaya” Alionekana kama ni mtu ambaye alikuwa akisubiri mda wake wa kukata roho ufike. Niliumia sana kwani uwezekano wa baba yangu kuendelea kuishi ulikuwa ni mdogo sana.
Baba yangu alikuwa akiongea maneno hayo hospitalini ambayo kwangu yalionekana kama ni wosia wa mwisho. Baba yangu alipigwa risasi na watu waliosadikika kuwa ni majambazi, japo taarifa zilikingana kwani wapo waliodai kuwa baba yangu alipigwa risasi na majambazi na wapo waliodai kuwa baba yangu alipigwa risasi na wafanyabiashara wenzake ambao walizulimiana madini. Ukweli haujulikani mpaka leo lakini baba kabla hajafa alinambia kuwa watu wanaomtoa uhai tayari walikuwa wameshaiba hati zote za nyumba zake.
Kauli ambayo hata mimi ilinishangaza na kuniumiza sana. Kitu pekee ambacho baba yangu alinambia ni kwamba katika moja ya shamba lake ambalo lipo huko longoi wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro amefukia kiisanduku ambacho hicho kisanduku ndani yake kulikuwa na madini ya Tanzanite na hicho ndicho kitu pekee ambacho alikihifadhi kama urithi wangu. Baba alinambia kuwa “kwa sasa mwanangu huna nguvu ya kutetea mali zilizoporwa na kutaifishwa na watu wasiopenda maendeleo ya watu wengine lakini hayo madini kama nikiyapata ni zaidi ya utajiri. Kauli hiyo ndio ilikuwa ya mwisho kutoka kwenye kinywa cha baba yangu.
Baba alikata roho kwa mtindo huo na kuniacha njiapanda nisijue ni sehemu gani hasa hayo madini aliyaficha. Nikabaki nimeduwaa nikachanganyikiwa nisijue cha kufanya. Basi taratibu zingine za mazishi ziliendelea na baada ya hapo ndipo mauzauza yalipoanza. Nilibaki mwenyewe nisiye na ndugu kwani kaka yangu alipelekwa huko Milembe kwenye hospitali ya vichaa. Basi baada ya hapo nilirudi shuleni na kuendelaea na masomo yangu huku nikiwa sijui nini hatima ya maisha yangu
Baadaye tulifunga shule na niliporudi likizo nilichoka kabisa kwani ile nyumba niliyokuwa nakaa ilikuwa imevunjwa na kujengwa ghorofa kubwa sana na kwa sasa ni moja ya shoping centre kubwa sana hapo Njiro-Arusha. Nilichanganyikiwa nisijue cha kufanya na kila rafiki wa baba niliyempigai walikana kunijua.
Nilikosa msaada na ikumbukwe kuwa baba yangu pamoja na kujulikanna Mbulu tena kwa jia la Bura lakini ukweli ni kwambaalikuwa ni mkimbizi kutoka
Rwaanda na huyo baba yake Bura alikuwa ni baba wa kumlea tu. Na babada ya wazazi wake hao wa kumlea kufariki kwa ajali yeye alikuaja Arusha na kuishi maisha ya kichokoraa mpaka hapo alipoapata bahati ya mtende.
Nazani sasa unanielewa ninaposema nilikuwa sina ndugu kwani baba yangu hakuwa na ndugu yeyeote zaidi ya marafiki ambao na wao kwa sasa ndio hao wameshagawana mali zote. Nimebaki mimi na dunia yangu hivyo basi nilimwomba rafiki yangu wa kufa na kuzikana kwa jina Joyce anisaidie kunisitiri nyumbani kwao.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni