RANIA (34)
Zephiline F Ezekiel
4 min read
JINA: RANIA
SEHEMU YA THELATHINI NA NNE
ILIPOISHIA...
Mfalme aliamua kukaa kimya.. Suya na watu wake walikua wakisubiri majibu mazuri kutoka kwa Mfalme kwa hamu kubwa.Mars aliona baba yake hasemi kitu akaamua kumfuata ili ajue angalau nini anachowaza baba yake.
SASA ENDELEA..
Mfalme, Mars anahitaji kuonana na wewe... Alisema mtumishi wa Mfalme.Mwambie aingie.. Alisema Mfalme.
Mars aliingia na kukaa karibu na baba yake.
Baba..hivi mbona uko kimya?...ukichelewa sana Mfalme wa Tharia atakushambulia wewe kabla ya wewe kumshambulia.. Alisema Mars.
Najua hilo mwanangu... Nina mpango wangu mwenyewe.. Alisema Mfalme.
Kwanini usishirikiane na malikia suya?..aliuliza Mars.
Mfalme aligeuka na kumwangalia Mars kwa muda mrefu hadi Mars akashituka.
Sitashirikiana na Suya... Nitajua mimi cha kufanya.. Alisema mfalme.
Baba... Kwanini usishirikiane na Suya?.. Aliuliza Mars.
Mars binti yangu... Aliita Mfalme.
Abeee baba..aliitika Mars.
Hebu acha Mara moja hayo mambo unayoyafanya kwa cheo cha bintimfalme... Alisema Mfalme.
Mars aliita Alisema shituka sana ila alijikausha kama hajaelewa.. Mfalme alikua ameshamsoma tu.
Mambo gani baba?..aliuliza Mars.
Kesho nataka twende mimi na wewe Tharia ili nikawakanye tabia yao ya kufanya majaribio ya kukuua...alisema mfalme huku amemkazia macho Mars.
Eee...nini?.. Wapi?.. Tharia... Alisema Mars kwa mshtuko.
Ndio mwanangu... Fanya haraka kujiandaa..alikazia Mfalme.
Hapana baba...mimi siwezi kwenda huko..wataniua..alisema Mars.
Mfalme aliinuka na kumsogelea Mars na kumwambia:
Mars,wewe ni binti yangu wa pekee..sina mtoto wa kike mwingine ambae ametoka kwenye tumbo la malikia wangu ambae ni mama yako.. Siwezi kukubali baya lolote lakini kukute kwa ajili ya faida ya watu wengine.. Alisema Mfalme.
Mars aliogopa.. Alihisi huenda baba yake amejua.
Sitakuruhusu uende Mars wala kwa huyo suya...utakaa hapa..mimi nitajua jinsi ya kuilinda nchi yangu bila kushirikiana na mtu yeyote... Sasa unaweza kwenda... Alisema Mfalme.
Mars kwa hofu iliyochanganyika na woga aliondoka na kurudi chumbani kwake.
Baba anajuaaje?..nani kamwambia?..alijiuliza Mars akiwa peke yake.
Huku suya na Mganga walikua wanasubiri majibu kutoka kwa Mfalme wa Lazi.
Baada ya siku kadhaa alikuja mwakilishi kutoka Lazi na kuleta majibu.
Suya aliposikia kua kuna mtu kutoka Lazi amekuja alifurahi sana na akatoka nje kwa hamu kubwa.
Yule mwakilishi alijitambulisha kukabidhi barua ile kwa suya na akaondoka zake.
Suya kwa hamu na haraka aliifungua ile barua na kuanza kuisoma.
Suya alishtuka baada ya kuisoma..uso wake ulikunjamana kwa hasira kali.
Mganga kuona hivyo alishituka sana.aliona amuulize malikia tatizo ni nini.
Malikia... Kuna tatizo gani?.
Hivi huyu Mfalme anazani ananguvu sana?..sasa nitamkomesha...alisema suya kwa hasira.
Mganga alichukua barua ile na kuisoma yeye mwenyewe.. Alikasirika Vilevile.
Nani atakua ametoboa siri?..au Mars mwenyewe?. Alisema mganga.
Sijali na wala hatuna muda wa kufikiria hilo.. Sasa nitakwenda kuomba msaada kwa maadui zake na tutamwangusha yeye na Tharia kwa pamoja.. Alisema suya.
Wale watu waliomwona Rania na Namadi wakienda Lazi wala hawakumwambia suya kama walimwona Rania maana waliogopa kwakua walishindwa kumkamata.
Suya akiwa anapita mara aliwasikia wanajadili.
Ila tungemtaarifu tu malikia... Alisema mpambe mmoja.
Weweeee... Nenda kaseme wewe na tutakuruka...alisema mpambe mwingine.
Mnaongea nini hapo?..aliuliza suya.
Wote walishtuka na kuogopa sana.
Suya alisogea na kuwaambia: nimewasikia sana... Kwahiyo kwanini mlinificha?..aliuliza suya kwa ukali.
Hakuna aliejibu...suya alikasirika akaamuru wapewe adhabu kali isiyosahaulika.
Ila moyoni mwake alibaki na swali.. Rania na Namadi walijuaje?..alihisi kuna mtu anawazunguka..ila kwa muda huo aliamua kutomtafuta kwanza ili aendelee na mpango wa kuomba msaada kwa Faritha.
Kama alivyosema.. Kesho yake alikwenda kwa Faritha na watu wake kuomba waungane na kuisambaratisha Tharia na Lazi kwa pamoja kisha wao watawale.
Faritha na watu wake walikubaliana na Suya na wakawa kitu kimoja kwa ajili ya uasi wao.
Huku Rai Alikua na maongezi rasmi na Rania.
Rania... Bila shaka hujui ipi halisi ni kazi yako...nilipewa kuhakikisha unakua salama ingawa sikuifanya hiyo kazi kama kamilifu na badala yake umesaidiwa ba Dom na Fasha.
Kwa hilo nilishindwa..lakini kwa sasa natakiwa kufanya kazi yangu.. Alisema Rai.
Rania alikua hajaelewa bado..alikua anakodoa tu macho.
Rania.. Watu wengi hawajui vizuri uhalisia wa malikia suya. Malikia suya ni mtu wa kawaida na pia ni mtu wa ajabu sana.
Hili jambo sijui hata mganga ambae ni mtu wake wa karibu sana kama analijua.
Suya amefanya jambo hili likawa la siri sana... Mimi mwenyewe nimefanya kazi ngumu sana na ya muda mrefu kujua.
Suya ni mtu wa miujiza..kiufupi ni mchawi hasa..hapo alipo anauwezo wa kuwafanya wanajeshi wake wakawa na nguvu za ziada..namaanisha unaweza kumchoma hata upanga tumboni ukatokezea mgongoni ila asife..alisema Rai.
Heeee...kivipi asife??...aliuliza Rania kwa mshtuko.
Hapo unakua umechoma kitu kingine na sio mtu wa kawaida... Mara nyingine unakua hata hupambani na watu wala hauko uwanja wa vita..ila wewe unakua hujui hilo..anashangaa tu wanajeshi hawapungui kumbe unapigana na mashetani halafu watu wako pembeni wanasubiri uchoke ndo upigane nao.
Kiuhalisia hakuna mtu enzi hizi kwenye ufalme huu wa Tharia au lazi anaeweza kupigana na Suya na akamshinda...ila hilo mfalme halijui..suya ni mtu wa ajabu sana.. Alisema Rai.
Mmh..sasa mbona alikua anaomba msaada kwa Mfalme wa Lazi?.. Aliuliza Rania.
Kwakua hapendi kujulikana kua yuko hivyo ndo maana anaomba msaada ili apigane vita ya kawaida ..ila kama kawaida ikishindikana basi atageuza upande wa pili wa shilingi.. Alisema Rai.
Nguvu zote za Suya zimekaa katika pete yake ambayo kamwe haitoi mwillini mwake..pete hiyo huivaa mguuni kwake.
Sasa itakuaje?..aliuliza Rania.
Kuna mtu mmoja tu mwenye uwezo wa kumuua suya..mwenye uwezo wa kuiondoa ile pete mguuni kwa suya.. Na huyo mtu ni wewe...na hiyo ndio maana halisi ya kua NADISH alisema Rai.
Rania alibaki mdomo wazi baada ya kusikia hivyo.
Watu wengi hata mganga mwenyewe hajui kua NADISH ni kitu gani..wanachojua ni kwamba NADISH anauwezo wa kuupindua ufalme huu kwa kuurudisha kwa wazawa wa kelkuni ila hawajui ukweli wenyewe na uhalisia wa NADISH.. Lakini suya anajua sana tu na hajawahi mwambia Mtu.
Sasa Rania muda wako wa kazi umekaribia kufika.. Suya amekaribia kuanzisha vita..amekaribia sana...kua tayari.... Alisema Rai.
Sawa.. Niko tayari kwa lolote utakalonielekeza.
Muda huo suya alikua kwenye chumba chake cha siri ambacho mtu hajawahi kukanyaga tofauti na yeye mwenyewe.
Alikua akifanya mauchawi yake kujiandaa na vita ila vita yake halisi ilikua juu ya Rania.
Ndio alikua mtu wa miujiza..lakini alipofika kwenye NADISH alikwama...hata muda huu yuko anafanya ibaada ya kumwongezea nguvu kupambana na Rania kuliko hata Mfalme.
Suya alijua fika kua Fasha ni wa ukoo wa kelkuni.. Ila alikusudia kumweka Fasha kua mfalme Halafu baada ya hapo amuue Fasha.kumuua Fasha ilikua rahisi maana suya aliamini kua Fasha anajua yey ni mama yake kwahyo kumuua mtu anaekuamini ni rahisi kuliko asie kuamini..na baada ya ya kumuua Fasha alipanga kutawala yeye kama yeye hakuna cha Mfalme wala nini.
Siku zote suya alifanya mambo yake kwa njia za kawaida ili asijulikane kama ni mtu wa miujiza..alijua fika kua mfalme wa Tharia hana uwezo wa kupambana nae ila aliomba msaada kwakua hakutaka ajulikane miujiza yake..Vilevile hizo nguvu alihifadhi kwa ajili ya kupigana na NADISH.
Baada ya ibaada yake ya muda mrefu alitoka na kwenda kuonana na Mganga ili wapange mambo yao.
Baada ya siku mbili majeshi kutoka kwa Faritha na watu wake yalikua yameshafika tayari kwa kupangiwa kazi na vita ianze rasmi.
Mfalme wa Lazi alipata taarifa za Faritha kuungana na Suya kwa ajili ya kumshambulia Lazi na Tharia.
Haraka alimwita mlinzi wake mkuu na baadhi ya watu wanaowaamini.
Haraka alituma mjumbe apeleke taarifa kwa Mfalme wa Tharia kuhusu uasi unaoendelea ili nao waungane..NINI KINAFUATA?
USIKOSE SEHEMU YA THELATHINI NA TANO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni