Notifications
  • MY DIARY (36)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SITATULIPOISHIA...Sasa wewe fikiria mimi niliyeletewa zawadi sikujua ni zawadi gani lakini yeye tayari alishafungua na kuchungulia na kujua nini kilifungwa huko ndani.Basi nikaendelea kumuhudumia yule mama huku na yeye akiniambia kuwa itabidi nikimmaliza hizo zawadi tusifungue hapo hapo na waniimbie wimbo wa happybirthday.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Tuliendelea na stori mbili…
  • MY DIARY (35)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TANOTULIPOISHIA...Tatu niliambiwa kuwa ndugu zake na wazazi wake walihusika kwenye mipango hiyo hivyo walibariki kabisa huyo binti kuniacha mimi mumewe wa ndoa na kuamua mtoto wao aolewe upya. Nne ni kwamba huyo mzungu amewaamishia wazazi wake mjini na amewajengea nyumba ya kifahari.Kwa hiyo mimi ninavyowapigiana simu na kuwajulia hali kumbe wenzangu huwa wananichora tu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (34)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Hapo nikakumbuka kuwa zile zana zangu za kazi nilikuwa nazo ni vile vifaaa vya kupimia ukimwi ambavyo huwa navitumia kabla ya kukutana na mwanaume yeyote nisiyemfahamu. Nikaamua kumkubalia huku nikiamini kuwa hiyo ndo kinga yangu pekee iliyobaki kama mwanaume huyo atataka kuzini na mimi usiku huo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi tuliondoka na kwenda sehemu…
  • MY DIARY (33)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TATUTULIPOISHIA...Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (32)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MBILITULIPOISHIA...Lakini kuchepuka kwangu na kuingia mgombani haikumaanisha kuwa sheria ingeniacha hivi hivi.Ilifika mahali ikabidi nizime gari na kutulia tulii kusikilizia nini kitafuata.Tayari nilikuwa nimezungukwa na mapolisi ambao walikuwa wakinifuatilia kwa kutumia pikipiki.Kwa bahati nzuri dereva wa lile gari na yeye alishafika hapo na alishawaambia polisi kuwa mimi naugua ukichaa na nilifufuka kutoka mochwari.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA…
  • MY DIARY (31)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MOJATULIPOISHIA...“marehemu pia alinieleza kuwa ana miliki duka la vitu vya urembo wa kike ambalo pia Leah analisimamia ila hilo apewe mdogo wake Marry ambaye yupo hapa. Mama mdogo huyo mara baada ya kuyasema hayo alikaa zake chini. Baba mdogo ambaye hakurizika na maelezo hayo alisimama na kusema “kwa hiyo kama marehemu alijua kuwa atakufa hivi karibuni kwani nini hakufuata taratibu za kisheria za kuandika wosia na kurithisha mali.IKIWA UNASOMA…
  • MY DIARY (30)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINITULIPOISHIA...Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Msiba ni msiba tu na ukitaka kujua binadamu…
  • MY DIARY (29)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TISATULIPOISHIA...Hapo sasa nikazidi kuchanganyikiwa ikabidi nimuulize mama huyo alikuwa akifanyia shughuli zake za kujipatia kipato sehemu gani.? Yule dada akanambia kuwa anafanyia soko la ndizi huko Korongoni. Sikuwa na jinsi nilimuomba anipeleke lakini na yeye alisita sita kwa madai kuwa alikuwa na kazi nyingi za kufanya na bado anatakiwa ampeleke mtoto shule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (28)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NANETULIPOISHIA...Sisi tumesomea mambo haya bhana waliendela kuzungumza wale walinzi huku wakishuka ngazi kwa polepole. Hapo na mimi nikawa nimejifunza kitu kuwa kumbe unaweza kuingia na mtu guest akakuzuru kisha akaondoka zake.Sasa sijui kwenye zile guest zetu za uswahilini kama wanalijua hili.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi nilala japo usingizi ulikuwa hautaki kuja kwa…
  • MY DIARY (27)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SABATULIPOISHIA...Alinamba eti hayo ya mimi kuolewa tuyaeke pembeni na kwa nini siku hiyo nisilale Moshi tukumbushie enzi zetu. Mwalimu John aliendelea kusema kuwa amenimiss sana na anomba nisahu yaliyopita na turudie yale maisha yetu ya zamani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijifanya simwelewi lakini ukweli ni kwamba nyota ya mwanaume huyu ilikuwa ni kali sana zaidi yangu na…

AISEE KUMBE RAHA (14)

Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA KUMI NA NNE
"Na....aaa..m"

"Ujasikia au unafanya kusudi nakuuliza tena je ni wewe ndiye uliyepost picha za utupu za mwanadada catherini na kuziweka hadharani katika mtandao wa facebook naomba unijibu na ukileta ujinga basi pasi hii nitaichomeka vyema katika mbavu zako hizo."....

SASA ENDELEA...
Maneno yale yule jamaa yalizidi kunipagawisha na kunitisha kiasi ambacho nilijikuta nikitokwa na majasho mengi kama nilikuwa nakimbia huku mikono yangu ikiwa inatetemeka kama mgonjwa aliyekuwa akisikia baridi.
"Kijana pablo unanikera maana nakuliza swali ujibu nakuuliza mara ya mwisho na usiponijibu basi ujue kuwa hiyo pasi itakufanya useme yote."yule jamaa akaendelea kuniambia huku akainiangalia mimi niliyekuwa namuangalia yeye huku yeye akiwa amenikazia macho ili kuniogopesha kwa sababu mpaka muda huo alishajua kuwa mimi tayari nimeshaanza kuogopa.

"Pablo je ni wewe uliyepost picha za utupu za mwanadada catherini katika mtandao wa kijamii wa facebook.??"
"H...ha..pana ndio hapana."nikajikuta nikimjibu kigugumizi yule jamaa ambaye baada ya mimi kumjibu kwa hali yeye akaangua kicheko kikubwa ambacho kwangu mimi kilizidi kuniogopesha nikabaki namuangalia tu.
"Sasa hapana ndio hapana ndio nini??"yule polisi akaniuliza tena na safari hii sasa alibadirika kwa sababu kicheko kikageuka na kuwa hasira na yule polisi akanisogelea karibu kabisa nakuangalia na mimi.
"Nipe jibu ni wewe au sio."
"Afande sio mimi na wala picha hizo mimi sijui."hali ikabadilika ghafla mwanaume nikakaza na kumuambia yule polisi ambaye ghafla alishangazwa na hali yangu ile mpya ambayo yeye ilimuacha hoi Mwanaume nikajitutumua nakuanza kumkavia macho nikimuonyesha sasa nilikuwa siogopi hali ambayo ilikuwa sio kabisa na picha ya ndani kwa sababu moyo wangu ulikuwa ukienda sana mbio huku nikimuomba Mungu kimoyomoyo aniondelee balaa lile.

Yule jamaa akaniangalia kwa dharau kisha akaachia tabasamu pana nakutoa hali ile ya mwanzo ya Mshangao baada ya kusikia majibu yangu kuwa sio mimi niliyevujisha picha za catherini mtandaoni na kutabasamu kwake hakika kulizidi kunikatisha tamaa kwa sababu nilikumbuka kale kamsemo kale usimuone mtu anacheka tu.Ukimya ghafla akatalawa yule jamaa ambaye alikuwa polisi akanyanyuka na kuanza kutembea tembea kisha akanifuata mpaka nyuma ya mgongoni wangu kisha akanishika shingoni na mkono wake ambao mkono ule akaupeleka mpaka katika mapigo yangu ya moyo na alipoona yanaenda kasi kuliko kawaida akaanza kucheka.
"Unaogopa nini kijana wangu Pablo halafu nimependa sana jina lako si umesema ujapost wewe mbona moyo wako unadunda kama saa mbovu."yule jamaa akaniambia tena na safari hii aliniambia karibu kabisa kwa sababu mdomo wake aliupeleka Katika sikio langu la kulia na kuniambia maneno yale akiwa kama kwenye ucheshi flani ambao mimi sikuuona ucheshi kama alivyokuwa anafikiria yeye.

"Kudunda kwa mapigo ya moyo ni kawaida hata wewe hapo yanadunda."hakika sikujua nguvu ya kuyajibu maneno yake yalitokea wapi kwa sababu nilivyomwambia vile naye akashangaa sana na kuniangalia tena kwa macho ya kukaza na safari hii akaunyoshe tena ukali wake ambao alinionyesha mwanzo wa kukunja sura yake nakuiweka ya kama mtu aliyekasirika sana.
"Sikia kijana watu hapa wametoa pesa ili wa kufunge kwa sababu wanaushahidi wa kutosha kutoka kwa catherini ambaye yeye anadai kwanza ulimuingilia kimwili bila ya ridhaa yake kisha ukampiga picha za utupu ambazo bila ya wewe kuwa na aibu ukazivujisha mtandano kuonyesha wewe jinsi gani ulivyokuwa shababi si ndio Nakuuliza tena kijana safari hii sitaanii kabisa kijana utajuta kumbuka kuwa watu wanaoingia humu kutoka kwao kunakuwaga sio salama kijana."yule jamaa akaniambia kwa hasira maneno yale ambayo yalisababisha mpaka mwanaume nimeze mate kwa kushushia maneno yale ya vitisho nikabiki kimya nakusubiria swali la yule jamaa ambaye aliamua kwenda kukaa kwenye kiti chake alichokaa mwanzo.Pia na wakati ule ile pasi ilizidi kuchemka na kuweka umoto kila macho yangu nilipoyapepesa na kuiangalia ile pasi ambayo ilikuwa imewekwa kwenye jiko moyo wangu ndio ulizidi kunienda mbio kuliko kawaida.
"Kijana wewe ndio uliyeposti mtandao wa facebook picha za mwanadada catherini akiwa mtupu na kumdhalilisha katika jamii nzima."
"Hapanaa si mimi"

Macho yangu yakashuhudia yule jamaa akinyanyuka taratibu bila ya kusema chochote kutokana na jibu langu kisha akaanza kufungua vifungo vya shati lake bila ya kusema chochote.Taratibu akaenda mpaka katika kabati lililokuwepo mule kisha akafungua moja kati ya droo zilizokuwepo katika kabati lile na kutoa gloves nyeusi ambazo akavaa katika mikono yake huku akiniangalia mimi kwa hasira ya hali ya juu.baada ya kuridhika na uvaaji wake akampa ishara yule jamaa mwingine ambaye alikuwa amesimama tu akaangalia mchezo mzima bila ya kuongea chochote jamaa ambaye ndiye aliyeleta lile jiko la mchina na pasi ambavyo vyote vilikuwa vinazidi kushamiri kwa sababu jiko lilikuwa linawaka kwa nguvu huku pasi ikiwa imewekwa juu kama sufuria vile.ile ishara aliyopewa yule jamaa ambaye naye alikuwa ni polisi pia ilisababisha haraka anisogele na aliponifikia akisimama na kuniangalia.
"Haya vua shati lako hilo."moyo wangu ukaanza sasa kudunda baada ya kusikia yule jamaa akaniambia nivue shati langu hali ya kuunguzwa na pasi sasa nikaiona kabisa inakaribia na jamani sio siri pasi ikapata moyo ikaja kukuunguza basi maumivu yake yanakuaga balaa.
"N...aa....mmm" nikajikuta kama vile sijasikilia kile nilichoambia kwa kujifanya kama naitika tena.
"Pumbavu nimekwambia vua shati hilo."hakika yule jamaa mwingine ndio alikuwa mkali kuliko hata aliyekuwa akinihoji kwa sababu alivyorudia tena kuniambia akaambatanisha na kofi zito la mgongo kofi ambalo mwenyewe lilinifanya nivue shati langu ambalo nilikuwa nimevaa.Baada ya kuvua yule jamaa ambaye aliniambia nivue shati ghafla akanikamata mikono yangu vizuri sana hali iliyosababisha nishindwe hata kutetereka na alinibana kisawasawa.

"Jamanii mnanioneaa tu mimi sina makosa jamanii niacheni kwanini mnakuwa waonevu kiasi hiki mimi sijapost picha hizo mnazozisema kwanza mimi sielewiii jamaniiiii."Mwanaume nikajikuta mwenyewe nikalalamika lakini kwa bahati mbaya hakuna mtu ambaye sasa alikuwa tayari kunishikiliza baada ya yule jamaa kufanikiwa kunikamata vizuri yule polisi aliyekuwa akinihoji taratibu akaenda mpaka katika ile pasi kisha taratibu akaichukua kwa kuishika katika mshikio wake ambao ulimsaidia kutoweza kuungua kutokana na yeye pia kuvaa gloves kisha akanisogelea mimi niliyekuwa nataka kufurukuta lakini yule jamaa alikuwa kweli amenibana sawasawa.Na yule polisi aliponikaribia akaanza kunielekezea pasi pale katika maeneo ya ubavu wangu wa mbavu wa kulia akiwa na lengo la kugusanisha ile pasi na Maeneo yale ya mwili wangu.Macho yakazidi kunitoka yakiambatana na majasho yaliozidi kunitiririka macho yangu yalikuwa yakiangalia ile pasi huku mdomo wangu ukiwa unahema kwa nguvu lakini yule jamaa kabla hata hajaifikisha katika maeneo ya ubavu wa kulia akaibakisha kidogo tu na kusababisha kamvuke cha moto wa ile pasi kuuanza kuniunguza kabla hata pasi ile haijafika.
"Ukweli wake ndio kuponyeka kwako kijana je upo tayari kuniambia ukweli pablo.??"
"Ndioo brazaa ndiooo nakuambia."Yule jamaa akaniuliza swali na mimi nikamjibu huku nikiwa natetemeka nakusababisha yule jamaa aendelee kicheka na kuonyesha kuwa alikuwa na furaha sasa.
"Je wewe ndiye uliyepost picha za mwanadada catherini akiwa mtupu yani bora uniambie ukweli maana hatutoishia hapa na safari hii sasa usiposema utajuta kuzaliwaa"........

Yulee jamaa akaniambia vile na kusababisha mwanaume nibaki kimya huku moyo wangu ukiendela kunienda mbio kuliko mara ya kwanza na kusababisha niendelee kutetemeka huku nikimuangalia Yule jamaa ambaye alikuwa na shauku ya kutaka kujua nitajibu vipi.Hakika kila nilipotaka kujaribu kusema kama mimi ndiye niliyeposti picha zile moyo wangu ulinisita kabisa na kujikuta nikipata mzuka wa haraka na hali ya kujiamini kuwa sitasema.
‘’kama mbwai mbwai tu.’’Nikajikuta nikijisemea maneno yale kimoyomoyo kisha nikabadilisha uso wangu wa kiuoga na kumuangalia Yule jamaa ambaye alikuwa akiniangalia mimi huku mwenzake akiwa kanikamata barabara mikono yangu huku nikiwa nipo tumbo wazi na Yule jamaa polisi aliyekuwa akiniuliza maswali huku mkono wake wa kulia akiwa ameshika pasi ambayo ilikuwa inafuka moshi mkali ikimaanisha kuwa ilikuwa ni ya moto sana na kama ukigushwa nayo tu katika mwili basi ilikuwa inaondoka na ngozi.

‘’kusema ukweli polisi mimi sijafanya chochote na hizo picha wala sijaziposti mimi na wala sielewi kama mnaamua kunifanya chochote nifanyieni lakini mimi sijapost chochote katika mtandao wa kijamii na wala hizo picha mimi sina.’’Nikajikuta nikipata nguvu mpya na kumjibu Yule polisi ambaye hakuamini kile nilichojibu na kujikuta yeye akijishika kichwa chake kuonyesha kabisa kazi kwake ilikuwa ngumu.Taratibu akarudisha pasi yake pale katika jiko ambalo lilikuwa bado linawaka na kumpa ishara Yule mwenzake ambaye baada ya kupata ile ishara akaniachia.
‘’kijana sitaki kukuumiza bila ya hatia lakini ukumbuke kuwa safari hii bado haijaisha kabisa na mguu wako mguu wangu tunaenda makao makuu ya mawasiliano ili kuweza kuchunguza kwa makini ni nani ambaye aliyeposti zile picha na kama ukiwa wewe utajuta hebu kwanza ingia facebook yako sasa hivi kijana.’’yule polisi aliniambia vile kisha akanikabidhi simu yangu aliyoichukua akiwa na lengo la mimi kuingia katika akaunti yangu ya facebook.

‘’afande mimi siwezi kuingia facebook sasa hivi kwa sababu suala la kuingia facebook ni ridhaa yangu mwenyewe.’’Kwa hali ya kujiamini nikamjibu Yule polisi ambaye aliachia tabasamu pana katika uso wake kisha akaniambia tutoke mimi nay eye na bila hiyana wote tukatoka na kuelekea mpaka kwa mama ambaye baada ya kuniona akanikombatia kwa nguvu.
‘’hivi ni kweli mwanangu wewe ndiye uliyempiga Yule dada picha akiwa mtupu??’’Baada ya mama kunikombatia akaniuliza na lile swali ambalo ilipita muda mfupi tu kuulizwa swali ambalo nikajikuta nikimuangalia mama huku hofu ukiendelea kuchukua nafasi yake lakini nikamtoa mama hofu kwa kuachia tabasamu pana ambalo lilimfurahisha sana nay eye.
‘’mama unaniamini kijana wako mimi siwezi kufanya hivyo.’’Nikamwambia mama ambaye akanikombatia tena lakini tukaja kushtuliwa na polisi Yule alinihoji ambaye baada ya kutufikia akiachia mguno wa kukohoa hali ambayo ilisababisha sisi tumuangalie.
‘’kijana samahani kwa usumbufu sisi tunakuachia kwa sababu hakuna ushahidi wa kutosha kwa hilo samahani kwa usumbufu.’’
‘’asante mwanangu.’’maneno ya Yule polisi yakajibiwa na mama ambaye akamuachia na kumpa shukrani juu Yule polisi ambaye hakuna na la kusema tena lakini ghafla mama baada ya pale akamsogelea mama chiku ambaye alikuwa akituangalia kwa macho ya kuibia ibia.
‘’mama chiku tangia niwe na urafiki na wewe mimi sijawai hata siku moja kumuandama mwanao lakini wewe kila tatizo la mwanangu wewe upo basi sasa nakuomba uniachie mwanangu kama alivyo na sitaki sitaki tena kuwa na mazoea na wewe tumekutana kimjini na tutaachana kimjini kwa hiyo nakuomba mimi na wewe kila mtu achukue zake.’’mama akamwambia mama chiku maneno ambayo hata mimi niliyasikia kisha mama taratibu akanisogelea na kunishika mkono nakuanza kuondoka na kuwaacha mama chiku akiwa na binti yake chiku mama catherini na catherini mwenyewe ambaye alikuwa akiangalia chini muda wote kutokana na aibu ambayo imemkuta baada ya mimi kuvujisha picha zake nikiambatanisha na picha zake ambazo nilimpiga wakati nilipomuwekea dawa ya usingizi katika kinywaji chake kisha nikaingia naye gesti nakufanya naye mapenzi bila ya yeye kujitambua.

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA TANO

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
4 Aisee Kumbe Raha Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni