MY DIARY (31)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: __
SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
“marehemu pia alinieleza kuwa ana miliki duka la vitu vya urembo wa kike ambalo pia Leah analisimamia ila hilo apewe mdogo wake Marry ambaye yupo hapa. Mama mdogo huyo mara baada ya kuyasema hayo alikaa zake chini. Baba mdogo ambaye hakurizika na maelezo hayo alisimama na kusema “kwa hiyo kama marehemu alijua kuwa atakufa hivi karibuni kwani nini hakufuata taratibu za kisheria za kuandika wosia na kurithisha mali.
TUENDELEE...
Mimi binafsi sijarizika na maelezo ya mama mdomo labda kama kuna vielelezo vya maandishi alifafanua baba huyo ambaye alionekana ni mkorofi sana. Akaendelea kusema “ mali za marehemu zinatakiwa ziuzwe na sisi kama ndugu tunufaike nazo, kwanza mnafikiri haya madeni nani atalipa.
Leah ilinibidi nisimame na kusema jamani maisha ya Joyce mimi nayafahamu hakuna mali yoyote ya maana aliyokuwa nayo zaidi ya hicho kisaloon kidogo na kiduka. Hicho kisaluni ni kwamba tupo share mimi na marehemu na hicho kiduka ndo cha kwake na ameshasema apewe mdogo wake.Akaunt ambayo ilikuwa na hela ndo hiyo amesema ni kwa ajili ya akiba ya mwanaye. Kwa hiyo mimi sioni kama kuna haja ya kuendelea na kikao maana hakuna cha kujadili tena nilisema kwa uchungu na kukaa chini.
Baba mdogo mmoja alirizika lakini mmoja hakurizika kabisa na akasema sisi ni ndugu wa marehemu na tupo hapa kwa ajili ya kumwakilisha baba yake hivyo lazima mtoe maelezo ya kutosha lasivyo hatutakubali jasho la mwanetu lipotee bure.Hapo nilisimama kwa jazba na kutaka kuuliza walikuwa wapi wakati marehemu akiwa hai lakini nilibadilsha na kusema “ wewe unatakaje sasa maana maelezo ndo hayo, basi twendeni Arusha mkachukue nguo na vitu vya ndani maana ndio havijazungumziwa hapa. Hapo ilibidi mama mdogo asimaame na kujaribu kutuliza hali ya hewa ambayo ilishaanza kuharibika.
Yaani huyu mzee alinichafua sana sasa sijui alikuwa anazitaka chupi na sidiria za mwanaye au vipi?Nikasema wachukue kila kitu basi maana hasara roho pesa makaratasi. Basi kikao kiliisha kwa staili hiyo mimi nilitoa maneno makali kwa sababu huwa sijui kumkopesha mtu.Ndio ebu fikiria watu hawakuwa na mchango wowote wakati marehemu akiwa hai sasa leo wanataka mali.Yaani sijui walikula maharage ya wapi hawa.Ilibidi kikao kiishe kwa staili hiyo. Mzazi mwenza wa marehemu Joyce aliaga na kuondoka zake. Na hao mababa wadogo pia waliaga na kuondoka zao.
Nilitamani kuondoka na mimi usiku huo huo lakini niliona naweza kumkwaza mama mdogo. Tuliendelea kukaa hapo na kupeana faraja za hapa na pale huku mama mdogo akisisitiza kuwa tuachana na hao watu kwa sababu hawajui A to Z ya Joyce. Kwani kipindi kile anaumwa wewe ukimwangaikia hospitalini zaidi ya miezi mitatu wao walikuwa wapi.Aliendelea kuhoji mama na kunifariji kimtindo mtindo. Ila wakumbuke mimi na Joyce tumetoka mbali sana na tulikuwa tukiishi zaidi ya ndugu na ndio maana biashara zake zote mimi nilikuwa nazisimamia huku yeye akiendelea na mission town.
Yule mdogo wake na marehemu ambaye mda wote alikuwa kimya aliamua kusema jambo “ ujue mimi nimekaa kimya mda mrefu kwa sababu bado nakumbuka mabaya yote waliotutendea hawa wanaojiita ndugu zetu kipindi kile nilipokuwa mjamzito” Cha msingi wewe dada Leah usiwe na wasiwasi wowote sisi tunaelewa milikuwa mkishi vipi wewe na dada Joyce. Aliendelea kueleeza mdogo wa marehemu. “Mimi binafsi sioni haja ya hilo duka la urembo labda uendelee kulisimamia na faida yake utakuwa unamtumia mama mdogo ili aongeze hata chumba kimoja hapa.Mimi kwa sasa siwezi kufanya biashara kwa kuwa nimeamua kurudi shuleni aliendela kufafanua binti huyo kwa jina Marry.
Mimi sikuyaamini sana maneno hayo na kwa kuwa hawajui vibiashara vyenyewe mimi niliwambia cha msingi kesho wote yaani mimi, Marry na mama mdogo tuende Arusha wakazione hizo biashara na vitu ingine vya marehemu vinavyozungumziwa. “ya nini yote hayo mwanangu cha msingi wewe nenda ukaendelee na maisha naamini mimi ni mama yako na tushakuwa ndugu mda mrefu hivyo utakuwa unakuja kunitembelea tu mwanangu. Aliendelea kusisitiza mama huyo. Bado sikurizika nikamwambia hata kama yeye hatoendana Arusha lazima tuende na Marry akachuke vitu vya marehemu avilete huku.
Kwanza naamini kwa mwili wa Marry hauna tofauti sana na mwili wa Joyce hivyo vitu vingi watakuwa wanavaliana. Marry alidakia akasema labda tuende tu nikapajue lakini kuhusu nguo za marehemu kamwe siwezi kuvaa na kwa kweli sina ujasiri huo alifafanua marry. Wewe naye bado hujaachaga imani za kizamani alimuuliza mama mdogo. Basi tuliendelea na stori za hapa na pale na kwa mara ya kwanza nilisikia njaa maana ilikuwa ni siku ya tatu sijala kitu cha maana. Nilimuomba yule dada wa kazi za nyumbani nitengenezee uji mwepesi ili ninyooshe utumbo kabla sijala kitu kizito.
Nilitengezewa uji nikanywa na baadaye nilikuwa chakula vizuri nikashiba na kupanda kitandani kulala. Nililala kama mfu kutokana na uchovu na usingizi kama wa siku tatu hivi. Usiku nikiwa usingizini nilihisi kama tumbo lilikuwa likiniuma.Nilishituka kutoka usingizini na kutoka nje maana nilikuwa naendesha sana. Kwa kweli tumbo lilikuwa linauma sana mpaka nikahisi safari ya kumfuata Joyce ilikuwa imefika.Uvumilivu ulinishinda ikabidi niwaamshe wenyeji ii wanisaidie. Kadri mda uivyozidi kwenda ndivyo hivyo hali ilizidi kuwa mbaya nikawa najinyonganyonga kama nyoka aliyemwagiwa mafuta ya taa. Kila mtu akaingiwa na hofu ikabidi wanikimbize hosptali usiku huo huo.Walinipeleka Mawenzi hospitali na nilipofika nilipokelewa na manesi na wakaanza kuniwekea dripu za maji za kutosha.Kila mtu alibaki akishangaa asijue tatizo ni nini maana nilikuwa naugulia kwa kweli.Mimi binafsi nilihisi labda ni kwa sababu nilikuwa sijala mda mrefu.
Usiku uliisha kwa staili hiyo hiyo na asubuhi palipokucha hali ilizidi kuwa mbaya.Daktari akaja na kuniambia nikachukue vipimo ikiwa ni pamoja na ultra sound. Hali ilizidi kuwa mbaya nikaanza kutapika damu na hata kabla majibu ya vipimo kutoka waliniandikia rufaa nipelekwe hospitali kubwa zaidi na nilipelekwa KCMC.Sikuweza kuelewa kinachoendelea zaidi ya kusikia milio ya ambulance ya gari ya wagonjwa ambalo nilipakiwa.Kila sekeunde moja ilivyopita ndivyo hali yangu ilivyozidi kuwa mbaya nikaanza kuona giza mbee yangu na uwezo wa kusikia ukapungua kabisa nikawa nasiki kwa mbali sana.
Mara nikawa sisikii na kuona kitu tena.Nikajua tu ni giza la mauti lilikuwa limetanda mbele yangu.Hapo nikajua kabisa roho inakacha mwili nikaanza kusali sala zangu za mwisho kimoyomoyo. Mara nikamuona Joyce akinipungia mkono na kuniambia mda wako bado wa kuja huku, utapona ili umlee mwanangu. Hapo nguvu zikaanza kunirudia na kuanza kusikia na kuona kila kitu kilichkuwa kinaendelea. Nikajaribu kujipima kwa kuinuka kitu ambacho kiliwashitua manesi ambao tayari walishajirizisha kuwa nilikuwa nimekata roho na hapo walikuwa wakiniingiza mochwari.
Wote walitimua mbio na kusema hajafa hajafa kumbe bado ni mzima.Sikuelewa kwa nini walikuwa wakinipeleka mochwari badala la chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Nikahisi labda wamechanganyikiwa au mimi ndo nilikuwa ndotoni.Nikajaribu kujiangalia vizuri nikagunduwa nilikuwa nimezungushiwa shuka dizaini ya sanda. Nikainuka kwa nguvu na kuanza kutimua mbio kama vile mwendawazimu. Nilimpamia yule mtunza maiti akadondoka chini na mimi nikaendelea kutimua mbio kuelekea lango kuu la kuingia na kutokea hospitalini hapo.
Nilienda moja kwa moja mpaka kwenye hice ambayo ndo ilikua inaondoka na kuenda mjini.Nilivyoingia tu kwenye gari hilo watu wote waliingiwa na hofu na kuanza kuteremka.Hapo nikajiuliza kwa nini wananikimbia na kabla sijapata jibu nilijitazama kwa kupitia kioo cha gari na kugundua nilikuwa natisha sana kwani nilikuwa nimewekewa pamba puani na masikioni kama zile wanazowekewaga marehemu.
Nikazichimoa zile pamba kwa nguvu na kuanza kupikichapikicha pua zangu.Watu wote walikimbia sio dereva sio konda sio abiria nikabaki mimi mwenyewe kwenye gari. Kuona hivyo na mimi ilinibidi nishuke lakini wazo likanijia kwa nini nisiondoke na lile gari kwa sababu dereva alikua ameondoka na ameacha funguo. Nikashuka ili nizunguke na kuingia kwenye mlango wa dereva. Wakati nashuka watu wote hapo stendi walitimua mbio huku wakisema huyo huyo huyo anakuja. Nikawaona Marry, mama mdogo na manesi wote kwa pamoja wanakuja kwa kasi ili wanishike na kunirudisha hospitalini.
Nikaona hawa watakuwa hawanipendi kabisa yaani walikubali nipelekwe mochwari nikiwa mzima kisa ni vile vimali vya ndugu yao Joyce.Nikasema kwa nguvu hapo mmeshachelewa mtajuata kunifahamu na mtajua kama mimi nilikuwaga mtoto wa kishua au wa kabwela. Mimi ni wa kishua bwana nilifundishwa kuendesha gari tangua nikiwa shule ya msingi. Sikuwapa nafasi ya kunishika maana niliona wamebeba na kamba kabisa kwa ajili ya kunifunga hivyo niliwasha gari na safari ya kwenda mjini ikaanza.
Niliondoka kwa spidi kali sana zilizowafanya watu wote waliokuwepo hapo stendi ya viasi kushangaa. “Yaaani yule binti ana hatari sana na hasipopata ajali ni bahati yake au mikono ya mungu itakua juu yake, hayo yalikuwa ni baadhi wa maneno ya watu walioshuhudia tukio hilo.” Kwa kutumia kioo cha sitemillor nilifanikiwa kuwaona wakinifuata kwa kutumia magari na bodaboda. Dereva na konda wake ndo walionekana kuchanganyikiwa sana. Yaani kwa jinsi msafara wa magari uliokuwa ukinifuatalia ulivyokuwa mkubwa nilichanganyikiwa kwa kweli na badala ya kufuata njia ya mjini mimi nilifuata njia ya kwenda Kibosho Mweka.
Wakati watu wakiniona kama niyechanganyikiwa vile mimi nilijiona nipo sawa a niliamini kuwa nitafika mjini kwa kutumia njia hiyo.Kwa bahati nzuri au mbaya barabara hiyo ilikuwa imejaa matrafiki ambao walikuwa wakisimamia msafara wa Muheshimiwa Raisi ambaye alikuwa akienda Chuo cha wanyamapori mweka alipoenda kama moja ya sehemu ya ziara zake mkoani Kilimanjaro. Kutokana na mwendo kasi niliokuwa nao nilijikuta nashindwa kusimama na kuwapita matrafiki ambao walikuwa wakizuia magari ili yapishe msafara wa muheshimiwa.
Niligundua hatari ambayo ingenikuta mara baada ya kukaidi mikono ya matrafiki kuwa nipaki pembeni.Baada ya kuligundua hilo ilinibidi nichepuke pembeni na kuingia migombani. Lakini kuchepuka kwangu na kuingia mgombani haikumaanisha kuwa sheria ingeniacha hivi hivi.Ilifika mahali ikabidi nizime gari na kutulia tulii kusikilizia nini kitafuata.Tayari nilikuwa nimezungukwa na mapolisi ambao walikuwa wakinifuatilia kwa kutumia pikipiki.Kwa bahati nzuri dereva wa lile gari na yeye alishafika hapo na alishawaambia polisi kuwa mimi naugua ukichaa na nilifufuka kutoka mochwari.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni