MY DIARY (28)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: __
SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Sisi tumesomea mambo haya bhana waliendela kuzungumza wale walinzi huku wakishuka ngazi kwa polepole. Hapo na mimi nikawa nimejifunza kitu kuwa kumbe unaweza kuingia na mtu guest akakuzuru kisha akaondoka zake.Sasa sijui kwenye zile guest zetu za uswahilini kama wanalijua hili.
TUENDELEE...
Basi nilala japo usingizi ulikuwa hautaki kuja kwa sababu nilihisi kuwa nilimzulumu sana mwalimu John na pia niliona kuwa nimeizulumu nafsi yangu kwa kuwa hata mimi nilikuwa na hamu sana ya kufanya mapenzi. Mwili ulikuwa ukitamani sana usiku huo kukumbushia enzi lakini nafsi ilikataa na bado nilikuwa nakumbuka machungu yote aliyonisababishia Mwalimu John. WAkati naendela kufikiria mara meseji ikaingia kwenye simu yangu na kuangalia alikuwa ni mwalimu John “asante saana kwa uliyonifanyia mimi nimefika salama”
Sikutaka kuiijibu zaidi ya kuangalia meseji zingine za WhatsApp ambazo nilikuwa sijazisoma. Mmmmh makubwa nilijisemea mara baada ya kuona video moja ya uchafu wa wanafunzi wa chuo kimoja maarufu hapa nchini.
Sikutaka kujipandisha nyege niliamua kuifutilia mbali kisha nikaweka simu silence na kulala zangu. Nilikuja kushituka saa mbili asubuhi na kwa kuwa nilikuwa sina pa kwenda asubuhi hiyo niliamaua kumalizia usingizi wangu mpaka saa nne mda wa kurudisha room.
Ni saa sita mchana nipo stend ya Moshi tayari kwa safari ya kurudi Arusha mara napigiwa simu na rafiki yangu Joyce akanieleza kuwa yupo safarini anakuja moshi. Nikamuuliza kwa hiyo nimsubiri maana mimi nilikuwa zangu stend narudi zangu Chuga. Akanambia nimsubiri na ndo kwanza alikuwa KIA. Sikuwa na jinsi zaidi ya kumsubiri rafiki yangu huyo. Nilienda sehemu moja inaitwa Uhuru Park nikaweka kambi hapo na kumsubiri.
Niliendelea kunywa vinywaji laini lengo likiwa ni kupoteza mda. “ samahani dada naweza kukaa na wewe”? ilikuwa ni sauti ya kijana ambaye nilihisi kuwa namfahamu. Hamna shida karibu nilimjibu kwa sauti ya ukarimu. Bila shaka wewe ni Leah alisema kijana yule mara baada ya kukaa. Hapana utakuwa umenifananisha kwani wewe ni nani ilinibidi nikatae jina langu maaana sikujua nia yake na nilikuwa simkumbuki vizuri.
Mimi ni Bryan miaka mingi iliyopita tulishawahi kukutana Dar es Salaam na tukala bata na ulikuwa narafiki yako mmoja hivi ingawa simkumbuki jina. Nilimkumbuka kuwa ni Yule kijana ambaye nilimpaga namba zangu mombo nikiwa safarini kwenda Dar sehemu niliyokwenda kufuatilia mambo ya mikpo.
Nakumbuka siku ile nilimpa penzi lakini kwa kumtoza hela.Ingawa nilikuwa nimeshamkumbuka lakini nilimwambia “ujue duniani watu wameeumbwa wawili wawili hivyo atakuwa amenifabnanisha”. Hakuwa na jinsi ilimbidi akubaliane na matokeo. Akaniuliza kwa hiyo wewe unaitwa nani? Nikamjibu masogangwe?
Akatabasamu na kuniuliza Masogangwe huyu wa Belle 9. Nikamwambia tusichoshane kwa maswali mengi kwani yeye ni polisi?. Hapo nikawa nimemkata maini akabaki amekaa kimya akitafuta sound ingine ya kuniingilia.
Rafiki yangu alifika na alikuwa amependeza kama vile Rihana Robinson ukilinganisha na hilo wigi nilidata kwa kweli mtoto hachuji kila siku anazidi kuwa mzuri pamoja na kupambana kote huko.Alinipa ishara kuwa tuhame sehemu hiyo tukae sehemu ambayo tuatakuwa wenyewe. Ilibidi nimuage yule kaka ambaye nilikuwa nimekaa naye. “ kwa heri Bryan ngoja niongee na rafiki yangu” Haya bye mrembo japo umekataa kunipa hata namba zako?
Sikutaka kumjibu zaidi ya kuhama sehemu hiyo. “ wewe naye yaaani huku ushapata kampani alinikaribisha Joyce kwa maneno hayo.Alafu kama namfananishe vile yule kaka alisema Joyce kabla hata sijamjibu kitu.Ilibidi nicheke na kwa haraka haraka akaniuiza nacheka nini. Nikamwambia unaongea vitu vingi sana na maswali unayoayauliza yote unayajibu mwenyewe. Akanambia basi tuyaache hayo best maana ushaanza kunishushua mapema.
Joyce akanambia kuwa amepata email ya wale wazungu ambao tulishawahi kufanya nao kazi haramu ya kucheza mikanda ya xxx. Akaniuliza naonaje kama safari hii nikifanya nao kazi mimi kwa sababu wanataka mtu mmoja. Nikamuuliza vipi kuhusu zile dola zetu zilizobakia? Akanambia shoga acha kukumbushia yaliyopita zile hela zilishatokaga nazote nilizitumia katika ile kesi yako.Hapo nikagundua kuwa alishawahi kufanya nao kazi kwa mara ya pili maana wasingeweza kumpa bila kufanya kazi ingine.
Sikutaka kuingia tena kwenye matatizo ya kufanya vitu ambavyo vinaweza kuhatarisha maisha yangu na kuharibu jina langu.
Nilihisi hiyo safari ya pili ambayo Joyce alifanya nao kazi ndio alipata ukimwi. Maana katika stori zake kuna siku alishawahi kuniambia kuwa alikuatna na makaburu akafanya kazi kama ile ambayo tulifanya na wale wafaransa lakini hawakumpa hela. Kuna siku pia alishawahi kunimbia kuwa anahisi hao makaburu ndio walimpa ukimwi kwa sababu wao walikataa katu katu kupima ukimwi kabla ya shughuli.
Kwa harakahaka nilikataa dili hilo kwa madai kuwa yeye alishanambia nisifanye tena dili hizo na pia nilimsihi afanye yeye hilo dili. Joyce kumbe alikuwa akinitega tu maana nilipomuambia hivyo akanijibu kuwa ni jambo zuri maana aliamua kunishirikisha ilia eti nisione kuwa ananibania. Kimoyomoyo nikasema wewe maswala ya kushikishana kifo nani anapenda.? Nakuhaidi rafiki yangu wakitoa hela tunagwana nusu kawa nusu ili na wewe ufungue biashara zako alilisitiza Joyce. Tukakubaliana hivyo na akaniomba niendellee kukaa Moshi kwa sababu wazungu hao watakuja jioni
Tukaamua tuende zetu memoria soko la mitumba kuchagua viwalo viwili vitatu.Tukiwa huko tulijizungushazungusha wee mradi tu mda uende. Tulivyomaliza tulirudi zetu mijini na akaniomba nimsindikize kwa mama yake mdogo. Wakati tuanaenda akanambia ujue mama mdogao anapenda sana zawadi sasa kwenda mikono mitupu sio vizuri. Nikamuuliza sasa tufanyaje? Akawaza kidogo na kuniambia twende supermarket tuchukue mazagazaga tumpelekee. Basi tulifanya kama mawazo yake yalivyomtuma tuliingia supermarket na kuchukua hayo mazaga zaga. Tukiwa hapo supermarket Joyce alinambi tupande sehemu ya juu ili tukaangalie vitu vya electronic kwa sababu alikuwa akitaka kuchukua home theatre mpya.
Tukapanda ngazi na kwenda sehemu hiyo. Wakati sina hili wala lile nipo bize kushangaa vitu vizuri mara Joyce akanishtua na kuniambia kuwa amemuona mtu kama mwalimu John tena yupo na kimwana balaa.Ilibidi nimuulize kwa taharuki umemuona wapi? Akanambia usiwe na papara na wala usigeuke kwa sababu walikuwa wanapanda hizo ngazi. Kwa kweli uvumilivu ulinishinda nikageuka kwa nguvu na tukagongana macho kwa macho.
Kweli kilikuwa ni kimwana ambacho kilijua kudeka maana kilipitisha mikono kiunono kwa Mwalimu John. Mwalimu John aliponiona alitabasamu na kunikonyeza na mimi nilimjibu kwa kumbetuli midomo ishara kuwa nilinfyonza. Kweli huyu mwanaume ni kiboko kwa hiyo jana ningejichanganya na kufanya naye mapenzi ingekuwa nimeliwa bure tu. Kwa ujasiri alikuja kutusalimia na akatutambulisha kuwa huyo ni mke wake mtarajiwa. Basi nilimpa mkono na kumwambia hongera. Hapo Joyce akaropoka na kumuuliza kwa hiyo sa hivi umeamua kutulia nakuoa?
“Yeah umri nao umeenda nimeamua kutulia na kufanya mambo ya maendeleao aliendela kujibu mwalimu John kwa kujiamini”. Basi waliendelea na yao na sisi na yetu huku nikimshukuru mungu kwa kuniepusha na majanga ya jana. Ebu vuta taswira ndugu msomaji kama jana ningelala nae sa hivi ningekuwa kwenye hali gani mara baada ya kumkuta na demu mwingine. Nilimwambia Joyce tuondoke maana nikishakutanaga na huyo mtu nahisi kuharibiwa siku yangu.
Wewe naye husahau tu miaka yote hiyo alisema Joyce kwa kunishushua. Nikamwambia ndo hivyo moyoni mwangu aliniachia kovu ambalo halifutiki. Akacheka na kuniambaia haya bhana twende zetu. Tuliondoka na kupanda magari ya Majengo sehemu ambyo mama yake mdogo alikuwa akiishi. Tulikaribishwa kwa furaha tukapikiwa chakula tukala. Mama yake mdogo hakusita kuniuliza kuwa mbona siku hizi nimepungua sana. Nikamwambia ni kweli ila nimeamua kufanya diet ndo maana nimekuwa model.Mama mdogo alinisifia nakuniambia hata hivi napendeza tu na naonekana mzuri. Ilibidi nishukuru maana ni wachache sana ambao wanaweza kusema kuwa umechukiza hata kama umechukiza.
Basi jioni ilivyofika tulirudi mjini na Joyce akaendelea kuwasubiri hao makaburu ili wafanye hiyo biashara haramu na mimi nikapanda gari na kurudi zangu Arusha. Nilitamni kubaki Moshi lakini sikuwa na la kufanya.Moshi ni mji ambao mimi nilikuwa naupenda sana.Nilifika Arusha salama na nikaendelea na ratiba zangu zingine. Nilifanya yangu na baadaye nilipanda kitandani na kulala. Sikutaka kumpigia Joyce maana nilihisi nitamsumbua na wazungu wake zaidi nilimtumia ujumbe mfupi wa maneno nikimtakia usiku mwema na nilimueleza kuwa nimefika salama.
Kesho yake niliamka kwa kuchelewa na nahisi ni kutokana na uchovu nilio kuwa nao tangia siku hile tupo na yule ticha mkali wa mabinti na wanafunzi. Nilienda saluni kuweka mambo sawa maana hawa wafanyakazi wasiposimamiwa huwa wanafanya utumbo na kutuibia sana hela. Niliendelea na michakato mpaka ikafika mida ya lunch. Nilienda kula huku nikistaajabu kuwa kwa nini Joyce hakunitafuta mpaka mida hiyo. Niliamua kumtafuta lakini hakupatikana kwenye laini yake.
Nilimtumia meseji lakini na yenyewe iliwekwa pending. Niliendelea na michato nai ilifika usiku bado Joyce alikuwa hapatkani.Hapo nilianza kuiliingiwa na hofu.
Nikaanza kuingwa na hofu nisijue cha kufanya.Niliwaza sana lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kusubiri na kila baada ya nusu saa nilikuwa nikipiga simu lakini ilikuwa haipatikani. Siku hiyo nayo iliisha nikalala nikaamka, hapo sasa alamu za hatari zikaanza kupiga kichwani mwangu. Mbaya zaidi sikuwa na hata namba moja ya ndugu zake. Sikutaka kusubiri zaidi nikajikuta nikipanda gari na kuelekea Moshi. Nilivyofika tu Moshi moja kwa moja nilinyoosha kwa mama yake mdogo na bahati mbaya sikumkuta kitu ambacho kilizidi kunichanganya.
Nikaomba namba zake za simu na kwa bahati mbaya na yeye alikuwa hapatikani. Nikamuuliza huyo binti wa kazi mbona namba hiyo aliyonipa haipatikani?.
Alinjibu kwa kifupi kuwa jana usiku luku iliisha hivyo na wewe hakuweza kuchaji simu. Hapo sasa nikazidi kuchanganyikiwa ikabidi nimuulize mama huyo alikuwa akifanyia shughuli zake za kujipatia kipato sehemu gani.? Yule dada akanambia kuwa anafanyia soko la ndizi huko Korongoni. Sikuwa na jinsi nilimuomba anipeleke lakini na yeye alisita sita kwa madai kuwa alikuwa na kazi nyingi za kufanya na bado anatakiwa ampeleke mtoto shule.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni